GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
[UFUFUO NA UZIMA MOROGORO]
JUMAPILI: 5 FEBRUARI
2017
MHUBIRI: Dr. GODSON ISSA ZACHARIA
(SNP)
SOMO: KUOMBA KWA BIDII
Maana ya Kuomba ni
kuongea na Mungu aliyetuumba. Maana nyingine ni namna ya kusemezana na Mungu aliyetuumba, na aliyeumba
mbinngu na nchi. Ni namna ya kumsifu na
kumshuukuru kwa mambo mbalimbali
aliyokufanyia. Endpao Unamuomba Mungu kwa habari ya mahitaji yako tu siyo njia
sahihi ya kuomba, bali anza kwanza na kumshukuru kwa mambo yote aliyokufanyia. Hata
wanasiasa katika siasa zao majukwaani, huanza risala zao kwa kuwasifia viongozi wao wa kisiasa na baada ya
hapo huchomekea mahitaji waliyo nayo katika eneo lao. Kama wanadamu wanaweza kufanya haya, je si zaidi kwa Mungu
wetu aliyetuumba?
ZABURI 100:4….(Ingieni
malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini
jina lake;). Malangoni mwake Mungu ni Hekaluni, ni kuingia mahali hapo
kwa shukrani. Hata jinsi Mungu alivyokuumba ni shukrani, kwa sababu pengine
Mungu angekuumba kama nguruwe ungejisikia je?. Hata kwa kuwa na pua nzuri uliyo
nayo, mshukuru Mungu kwa jinsi ulivyo. Usilalamike kwa kuwa na uso mpana, kuna
watu wanaotamani kuwa na uso wa aina yako!
Kumuomba Mungu ni kubadilishana mawazo na Mungu wako. YOHANA 1:12…(Bali wote waliompokea aliwapa
uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;).
Mungu kwetu ni Baba, na sisi ni watoto
wake. Usimfanye Mungu kama jitu kubwa la kutisha sana kiasi kwamba kumwendea
inakuwa ngumu. Kumuomba ni kusemezana naye na kubadilishana mawazo naye kwa habari
ya ndoa yako, maisha yako, taifa lako, na kila kitu kinachokuhusu. Wengine huwaza
kuwa kwa kuwa Mungu hatumuoni, basi kuomba kwao ni kama vile wanajisemesha
wenyewe.
Imeandikwa katika ISAYA 1:18…(Haya, njoni, tusemezane, asema
Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji;
zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.). Kumbe Mungu
mwenyewe anataka kuwapata watu wa kusemezana naye. Maana yake wewe ukimbilie
nyumbani mwa Bwana au nyumbani kwako na kuanza kupeleka maombi yako kwake.
Kuomba ni kupeleka
haja za moyo wako au mahitaji yako. WAFILIPI
4:6 imeandikwa hivi (Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika
kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
Mungu.). Mungu anataka wewe umpelekee haja zako. Unahitaji nini katika
maisha yako? Unahitaji kazi, unahitaji ndoa nzuri, n.k Omba kwa Bidii na vyote
hhivi utavipata.
Katika MITHALI 8:17…imeandikwa hivi (Nawapenda
wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.). Ingawa ni
kweli unampenda Mungu, na amekuona kuwa
unampenda, naye anakupenda, LAKINI ni kwa wale
tu wanaomtafuta kwa BIDII ndiyo pekee
watakaomuona. Mungu wetu siyo mdogo kama sindano, kiasi kwamba itakuiwia
ngumu kumuona
NAMNA 2 ZA KUMTAFUTA MUNGU KWA BIDII:
1. Kufanya
mambo / kazi za Mungu. kama ni kuombea mgonjwa hospitalini unakuwa
upo hapo. Kama ni kuomba na kufunga na wewe hukosekani, n.k. Ni kama Yesu
alivyotoa mfano akisema “Nilikuwa mgonjwa hammkja kuniona, nilikuwa uchi
hamkunivisha nguo, nilikuwa na njaa
hamkunilisha n.k.” Nao walishangaa ni
lini Yesu alikuwa na maisha ya aina hiyo nao hawakumsaidia? Ndipo Yesu atawajibu kuwa kwa namna
mlivyowatendea wadogo katika hawa ndivyo mlinitendea mimi. Yesu anaweza
kuonekana katika maisha yako kwa kufanya
kazi zake.
2. Kuomba. Hii ni silaha madhubuti ya kumshinda shetani, kwa kuwa
kwa njia ya kuomba unakuwa unasemezana na Mungu na kubadilishana mawazo.
Namna zote mbili
za kunmtafuta Mungu kwa Bidii hata kumuona zinaendana pamoja (yaani kuifanya kazi ya Mungu na Kuomba).
Katika YAKOBO 5:16 imeandikwa…(Ungameni
dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye
haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.).
Tunaomba kwa bidii ili tumuone Yesu maishani mwetu. Utajuaje kuwa
unavyoomba unaomba kwa Bidii? Tukisoma katika YOHANA 1:3 (Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye
hakikufanyika cho chote kilichofanyika.) na YOHANA 1:14…(Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi
tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa
neema na kweli.). Endapo utamtafuta Yesu unapata vyote. Siyo kupata viwili
au vitatu au ishirini, ni vyote!! Kama unahitajji maji, Yesu anakuwa maji, kama
unahitaji mshahara, Yesu anageuka na kuwa mshahara, kama unahitaji watoto, Yesu
anageuka na kuwa watoto, n.k. Hi ni kwa
sababu pale mlimani Musa alipotaka kujua Jina la Mungu ni lipi, Mungu alimjibu
“MIMI
NIPO AMBAYE NIPO”
Pia imeandikwa
katika YAKOBO 5:17….(Eliya
alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe,
na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.). Eliya alikuwa na tabia kama zako ulizo nazo
wewe, lakini alipoamua kuomba kwa bidii alijibiwa.
HEZEKIA naye
alifikia umri ambao Mungu alitaka kumtwaa. 2
WAFALME 20:1-6… (Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika
hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema
hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. 2 Basi
Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema, 3
Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na
kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana
sana. 4 Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia,
kusema, 5 Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi
baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama,
nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana. 6 Tena, nitazizidisha
siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na
mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa
ajili ya Daudi, mtumishi wangu.)
Kwa nini Hezekia
aligeuzia kichwa chake ukutani na kuomba? Ni
kwa sababu ni njia ya kujitenga na mambo
mengine yote ya dunia hii, na ya nyumbani mwake. Faida mojawapo ya
kuomba tena kwa machozi, ni kuwa maombi yako yanasikiwa. Endapo Hezekia
asingeomba kwa bidii hakika angekufa kama alivyopewa taarifa hii na Nabii Isaya. Hiki kilikuwa kifo ambacho
Mungu mwenyewe alishakiruhusu lakini kwa kuwa Hezekia aliomba kwa bidii, kifo hiki kilibatilishwa. Yamkini hata
mashetani nao wamekupangia kifo katika ulimwengu wa roho. Ni juu yak oleo
kung’ng’ana na kumsihi Mungu wetu uovu
wa aina hiyo usitokee kwako kwa Jina la Yesu.
YESU
mwenyewe aliomba, ingawa ni Mungu kwa 100%. WAEBRANIA 5:7 (Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea
yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia
sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;). Hebu
waza, ingawa Yesu ni Mungu lakini aliomba. Kumbomoa shetani katika maombi ya kushindani ni njia tu ya
kutumia silaha kumpiga shetani. Wewe u nani kama hauombi? Yesu pamoja na kuwa
na mamlaka yote ya kimungu, lakini
aliomba. LUKA 22:44…( Naye kwa vile
alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya
damu yakidondoka nchini.]).
Katika maombi ya
wiki hii tokea Jumatatu hadi leo, tulikuwa tukijifunza staili mbalimbali za Kuomba kwa Bidii hadi majibu yapatikane.
Kwa ufupi, tulijjifunza kuwa zipo staili tofauti tofauti za kuomba kwa bidii,
na mojawapo ni:-
1.
STAILI YA ELIYA. Utaona Eliya alipoomba kwa bidii ili mvua inyeshe, kuna mkao wake
aliokuwa nao wakati huo. Maandiko yanasema "..........Naye Eliya akapanda juu mpaka
kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini”
(1 WAFALME 18:42). Akajitupa chini,
akainama uso mpaka magotini, akaanza kuomba kwa bidii mpaka mvua ikanyesha.
Aliendelea kuomba na akamwambia mtumishi wake nenda hata mara saba kuangalia
dalili ya mvua.
2.
STAILI YA YESU
(Ni njia ya kulia na kutoa machozi). Kama ilivyoandikwa katika WAEBRANIA 5:7 (Yeye, siku hizo za mwili wake,
alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja
na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;),
na pia imeandikwa katika LUKA 22:44…(
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana
kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]). Ni maombi ya kuomba kwa bidii dhidi yay a dhiki
yako hadi jibu litokee kwa Jina la Yesu.
3.
MAOMBI YA STAILI YA HANA. Huu ni mfano dhahiri wa staili ya kuomba kwa bidii ya
mtu aliyeomba kwa hisia na shauku kwa ajili ya kumpata mtoto Samweli. Hapa haikuwepo
kuomboleza kwa kulia wala kupiga kelele Katika 1SAMWELI 1:10-13 ..(Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni
mwake, akamwomba Bwana akalia sana. 11 Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa
majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala
usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo
mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe
hautamfikilia kichwani kamwe. 12 Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za Bwana,
Eli akamwangalia kinywa chake.13 Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo
yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli
alimdhania kuwa amelewa.)
4.
STAILI YA YAKOBO. Huyu aliomba usiku kucha na kukutana na malaika na kung’ang’ana ilia
pate baraka zake. Imeandikwa katika MWANZO
32:24-26…. (Yakobo akakaa
peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. 25 Naye
alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka
uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. 26 Akasema, Niache,
niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.). Leo katika staili ya Yakobo tutadai haki zetu hadi
tuzipate kwa Jina la Yesu.
5.
MAOMBI YA STAILI YA DAUDI. Daudi na jeshi lake walipotoka vitani walikuta mji
wao umechomwa na wake na watoto zao wametekwa na kuondoka na maadui zao. Jeshi
lake lote lilitaka kumpiga Daudi mawe. Hata hivyo Daudi aliomba kuletewa
NAIVERA, na kisha akamsihi Bwana akitaka jibu la ama alifuate jeshi la
adui zake au la!! Ni aina ya maombi ya
kumuuliza Mungu ukiwa na uchungu moyoni, kwa ajili ya kurudisha kile
kilichoibiwa. Leo katika Staili yaMaombi ya Daudi tutaenda kuomba hadi
kurudishiwa tena vile vyote vilivyoibiwa kwa Jina la Yesu.
6.
MAOMBI YA KUMTEGEMEZA KUHANI. Kwamba Kuhani anapokuwa amechoka mnamtegemeza na
hatimaye unawashinda maadui zote kwa Jina la Yesu. KUTOKA 17: 11-13.. (Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli
walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. 12 Lakini mikono ya
Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia.
Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu;
mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. 13 Yoshua akawaangamiza Amaleki
na watu wake kwa ukali wa upanga.)
=====================MWISHO===================
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NA NASI KIPITIA:
FACEBOOK:
Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
SIMU: 0719
798778 (Sms only)
BLOG: Ufufuo
na Uzima Morogoro
http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/?m=0
http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/?m=0
© Media and Information Ministry
GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +255719612874 / +255713459545
|