GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI: TEREHE 15
JANUARI 2017
MHUBIRI: ADRIANO MAKAZI (RP DAR ES
SALAAM)
Vipo vifungo
kabisa vyenye asili ya kichawi. Na Kwanini vifungo hivi vinaitwa vifungo vya kichawi?
Hii ni kwa sababu kila kifungo cha kichawi ni cha kishetani na kila kifungo cha
kishetani ni cha kichawi. Ukumbuke kuwa Wachawi
wanaweza kumfunga mtu. Akili ya mtu,
maendeleo ya mtu, macho ya mtu, mafanikio ya mtu
Baba (Dr. Godson Issa Zacharia) akiomba kabla ya kumkaribisha Mhubiri RP Adriano Jumapili 15/01/2017 |
Imeandikwa
katika LUKA 13:10-16… (Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika
sinagogi mojawapo. 11 Na tazama,
palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane,
naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. 12 Yesu alipomwona alimwita,
akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. 13 Akaweka mikono yake juu yake, naye
akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. 14 Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa
sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna
siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si
katika siku ya sabato. 15 Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila
mmoja wenu, je! Hamfungui ng'ombe wake au punda wake siku ya sabato katika
zizi, aende naye kumnywesha? 16 Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu,
ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo
hiki siku ya sabato?).
Yesu
alipoingia ndani ya sinagogi alimuona mtu
huyu aliyekuwa na pepo la udhaifu kwa muda wa miaka 18. Mtu huyu alikuwa
anaenda kwenye sinagogi kila siku, na pengine alikuwa anatoa fungu la kumi ,
lakini hapakuwa na mtu wa kumtoa udhaifu huu, na watu waliona kuwa ana kibiongo
tu cha kawaida, kumbe alikuwa na nyuma yake kuna pepo la udhaifu. Kila nyuma ya
tatizo kuna roho nyuma yake. Saa yako
ikifika ya kufunguliwa uwe unajua kuomba au hujui, Yesu atakufungua tu. Yesu
Yule Yule aliyemfungua huyu mama na leo pia atakufungua wewe kwa Jina la Yesu.
Huyu mama alikuwa amefungwa na shetani kwa miaka 18, akiwa na pepo la udhaifu.
MATHAYO 17:14-21…( Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia
magoti, akisema, 15 Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa
vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16 Nikamleta
kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi
kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana
nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka;
yule kijana akapona tangu saa ile. 19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa
faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu
ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha
punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka;
wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21 [Lakini namna hii haitoki ila
kwa kusali na kufunga.] )… Bwana Yesu hapa anakutana na kesi
nyinginne akitokea mlimani, ya kijana mwenye kifafa. Baba wa motto huyu hakujua
kuwa nyuma ya hicho kifafa kuna pepo / jinni la kusababisha tatizo hilo. Na
ndiyo maana pepo huyu humtafuta kijana huyu maeneo ya moto au maji ili siku
akifa watu waseme kilichomuua ni huo moto au maji aliyoangukia huko. Yapo mambo
matatu ya kujifunza hapa:
·
Mwanane
ana kifafa
·
Jinsi
wanafunzi wameshindwa kuleta ufumbuzi
·
Jinsi
gani wanafunzi walivyomwendea Yesu ili kupata utatuzi wa hili tatizo.
Wanafunzi
wanaonekana wakimfuata Yesu kwa faragha na kumwuliza mbona wao wameshindwa
kulitoa hilo pepo? Ina maana kuna mambo kadhaa wa kadhaa ambayo wanafunzi hawa
wallikuwa hawayajui. Yesu aliwaambia sababu kuu ni upungufu wa imani yenu.
Kwamba unapokuwa unashughulika na matatizo Fulani kwanza anagalia imani yako.
biblia inasema imani huja kwa kusikia neno la Kristo (Warumi 17:10). Imani ni mkono wa kupokwa kutoka kwa Mungu. Imani
ndiyo inayodhiirisha kuwa huyu mtu ni wa Mungu au la. Imani inakufanya uwe na ujasiri wa kufanya
mambo yasiyowezekana. Yamkini wanafunzi pia walikuwa na imani bila kuwa na
matendo, kwa kuwa Biblia inasema imani bila matendo imekufa. Imani ina tendo la
imani. Kuna mtu ana imani lakini imani yake imejificha kwenye pochi. Itoe imani
yako nje kwa Jina la Yesu. Wapo watu wanaoogopa kuwa itakuwa je yasipotokea?
Kwani ingetokea au istokee, utukufu unamrudia nani? Ni saa ya mtu wa Mungu
kurudi katika asili yake. Itoe imani yako uliyoiweka kwenye boksi. Akina
Shedraki, Meshaki na Abednego waliitoa imani yao nje, bila kumuogopa mtu
yeyote. Hawa walikataaa kuiabudu sanamu
ya mfalme, wakiwa tayari kufa kwa imani yao. Ikumbukwe kuwa imeandikwa katika WAEBRANIA 11:1 (Basi imani ni kuwa na hakika ya
mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.), na hivyo
Unatakiwa kuamini kwanza kana kwamba yameshatokea.
Watendakazi wakiombea watu waliofungwa na Vifungo vya Kichawi Jumapili 15/01/2017 |
MARKO 5:25-34… (Na mwanamke mmoja mwenye kutoka
damu muda wa miaka kumi na miwili, 26 na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu
wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali
yake ilizidi kuwa mbaya 27 aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano
kwa nyuma, akaligusa vazi lake; 28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu,
nitapona. 29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake
kwamba amepona msiba ule. 30 Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba
nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi
yangu? 31 Wanafunzi wake akamwambia, Je!
Wawaona makutano wanavyokusongasonga, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa? 32
Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo. 33 Na yule
mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia,
akamweleza kweli yote. 34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako
kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.).
Tatizo la
huyu mama liliongezeka siku hadi siku. Kwa kusikia habari za Yesu, huyu mama
alijenga imani na kuweka mkakati wa jinsi ya kumfikia Yesu kwa uponyaji wake. Yawezekana
mwanamke huyu alitangatanga sana kutafuta upenyto wa kumuona Yesu kwa muda
mrefu. Inawezekana huyu mama amemwendea Yesu siku ya kwanza, nay a pili na hata
wiki nzima lakini akashindwa kumpata. Unajua kumtafuta Yesu siyo kazi ya kuamka
na kumwendea. Mimi nakushangaa wewe ambaye umetafuta uponyaji kwa siku mbili au
tatu na umeanza kukata tamaa. Imeandikwa katika WAGALATIA 4:4 (Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu
alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,)
Hata kama zipo tatratibu zilizowekwa na ulimwengu huu, au na wagganga wa
kienyeji, lakini siku au saa yako ikifika imefika na hakuna wa kuweza kuizuia
kwa Jina la Yesu.
Elisha
alipokuwa anaambatana na Eliya, wale wana wa manabii walikuwa wakimtahadharisha
kuhusu kutwaliwa kwa bwana wake, lakini akawajibu kuwa anajua wanyamaze. Wapo
watu walipokuona umeanguka walishangilia wakijua utabakia hapo hapo. Cha
kufanya simamam tena na uanze safari yako tena hata ufike unapoelekea kwa Jina
la Yesu.
UKIRI
Ninaamuru kuanzia vifungo vyote vya
kichawi ninavikata, naviharibu vifungo vya umaskini, vifungo vya utasa, leo
naviharibu vyote kwa Jina la Yesu. Amen
|
Watendakazi wakifuatilia kwa makini Maandiko ya Biblia Jumapili 15/01/2017 |
Kwa habari
za Hamani, jemedari mkuu wa jeshi la Syria, alimwendea Elisha akitaka uponyaji.
Hata alipomfikia Gehazi na kumweleza shida zake, Gehazi alimwendea Elisha na
kupata maelekezo kuwa aende kujichovya katika mto Yordani mara 7. Jambo hili
lilimuudhi sana Hamani, kwa sababu alikuja na misimamo yake. Ukiwa na ukoma hupaswi
kuwa na hasira, unapswa kuwa mtulivu na kutii maelekezo. Hamani aliingia na tarratibu zake, lakini
akaambiwa hatufanyi hivyo. Kila nyumba ina taratibu zake, usitumie taratibu za
nyumba yako kuzileta kwa nyumba ya watu wengine. Inawezekana hata wewe una
tatizo lakini unaliwekea taratibu za jinsi ya kulitoa. Ukiendelea hivyo Mungu
atakuacha ubaki hivyo hivyo, na wala hata kusemesha.
Wachawi
wanapotaka kumtesa mtu, wanaiologa hata akili yake. Ndiyo maana katika WAGALATIA 3:1 Imeandikwa (Enyi
Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa
wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?), ikiwa na maana kuwa
hata akili za watu zinaweza kulogwa. Katika nchi ya Tanzania, kuna kila aina ya
fursa za kuwezesha watu kupata pesa. Kinachokosekana na akili ya kuzipata hizo
fursa. Unachopaswa kufanya ni kumuomba Mungu ili akupe akili. Farao aliota
ndoto na kukosa mtu wa kuitafsiri, lakini baadae aliletewa Yusufu akitokea
gerezani, ambaye alimpa majibu ya ndoto zile. Farao baadae alimpa uongozi
Yusufu kwa sababu katika utawala wake hakumuona mtu mwenye akili ya kuleta
majibu kwa Taifa lake. Akili ni kila kitu, hata kwa wanaume Biblia inasema “Enyi
wanaume ishini na wake zenu kwa Akili”, ikimaanisha kama yupo mwanaume
anayeshindwa kuishi vizuri na mke wake ni dhahiri kuwa amelogwa na hana akili. Katika
Biblia tunamuona Danieli akisoma vitabu na kugundua kuwa muda wa kurudi kutoka
utumwani umewadia. Imeandikwa katika DANIELI 9:22..(Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.). Kumbe hata Mungu alimpa Danieli
akili.
Wapo watu ambao wana matatizo yanayofanana na matatizo ya wazazi wao. Kwamba kijana ana tatizo lenye kufanana na la mzazi wake. Hii inaonesha kuwa kwenye familia kuna vitu vinapitishwa mle. Shetani aliliona tumbo la Elizabeth na kulifunga kwa sababu ndani yake angezaliwa Yohana Mbatizaji wa kuisafisha njia ya Bwana. Ukimwangalia Hanna, naye alikuwa tasa, lakini lengo la shetani kulifunga tumbo la Hanna lilikuwa kumzuia Samweli asizaliwe. Hanna alipoenda Shilo, na kumlilia Bwana, baadae Mungu alimjibu. Ili upate ufumbuzi wa shida yako nenda nyumbani kwa Bwana. Hata hivyo katika kumtafuta Bwana, wapo wavunja moyo. Hanna alikumbana na Eli (Kuhani wa Bwana), ambaye alimuona kama mama mlevi. Yupo mmoja tu aliyekufa kwa ajili yako, Yesu Kristo. Akina Martha na Maria walipokuwa pale kaburini mwa Lazaro walimwambia Yesu kuwa ndugu yao amkeaa kaburini kwa siku nne na ananuka sasa!! Kuna nyakati nyingne matatizo yako yanakuwa mengi, yananuka na hata kuwakera ndugu zako.
Yesu aliutoa
mfano wa Msamaria Mwema, ambaye alimsaidia yule mtu aliyejerushiwa na majambazi.
Walipopita Kuhani na Mlawi hakuna hata mmoja wao aliyekuwa tayari kwa ajili ya
kutoa msaada. Ndivyo ilivyo asili ya mwanadamu, kwamba unapokuwa na maisha mazuri
watakuwa karibu na wewe. Yamkini hata wewe wapo wanadamu walipokuona kuwa una
maisha mazuri, wakaja kwako na kukusalimia kwa heshima zote. Lakini leo hii kwa
kuwa umejeruhiwa, na maisha yamekwenda mrama na matokeo yake wote wamekukimbia
na hawapo karibu na wewe tena.
Kwa wewe
ambaye hujaokoka, maneno kama haya hayana maana kwako, kwa sababu hujapata
kibali cha kuitwa “Mwana wa Mungu”.
Hii ni kwa sababu endapo mtu hajaokoka, shetani na mtu wa aina hiyo wako kitu
kimoja.
Vifungo vya Kichawi
© Media and Information Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +255719612874 / +255713459545
|