GLORY OF CHRIST TANZANIA
CHURCH,
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA
MOROGORO
JUMAPILI -:- 08 JANUARI 2017.
Waraka ni hati yenye habari inayomhusu mtu
fulani. Kwa upande mwingine, hati ni kadi ya umiliki wa jambo fulani. Waraka
waweza kumtambulisha mtu: kwamba ni
nani, anafanya nini n.k. Hapa duniani, zipo nyaraka za aina tofauti.
Waraka ni kama nusu ya kuonana. Mtu akitoka
ofisi moja kwenda nyingine, hutambulishwa kwa njia ya waraka, ikielezea yeye ni nani, anatoka wapi na anatakiwa ahudumiwe
nini kule aendako.
Imeandikwa katika MATHAYO 27:37…(Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake,
yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.). Baaada ya Yesu
kusulubiwa, juu ya kichwa chake waliweka kibao chenye kumtambulisha
Yesu ni nani ili kila ausomaye afahamu Yesu ndiyo yupi!!. Hata leo wapo watu wengi katika
ulimwengu wa roho ambao wanatembea na vibao vinavyowatambulisha. Wengine
hutambulishwa kama tasa, wagonjwa, maskini, n.k. Pale unapokuwa ni mtu wa aina
hii, siyo rahisi kupiga hatua yoyote
kimaisha.
Zipo nyaraka mbali mbali zinazoweza kuandikwa dhidi ya maisha
yako. Mfano, imeandikwa katika KUTOKA
20:3-6…( Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho
juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu
mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha
nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika
amri zangu.). Biblia inasema Mungu
hupatiliza maovu ya baba kwa wanae, hadi kizazi cha tatu na cha
nne.
Kumbe
Mungu naye ameweka waraka wa melekezo, ili kila atendaye kinyume nao apatilizwe
uovu huo hata kizazi cha tatu na nne. Yamkini umezaliwa katika ukoo
uliofanya uovu, na hata sasa shetani
anatumia hicho kama kigezo cha
kukushtaki mbele za Mungu. Yapo maelekezo ambayo unaweza kuwa umeyabeba, na
kila apitaye njani anaweza kuyasoma. Kwamba endapo umeandikiwa kuwa tasa, kibao
cha aina hiyo waweza kutembea nacho kila mahali na waliokitengeneza wakazidi kucheka wanapokiona.
Kila waraka huandaliwa kukiwa na malengo ya kuuandaa. Imeandikwa katika NEHEMIA 2:1-9... (Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta,
na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka
sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wo wote. 2 Basi mfalme akaniambia,
Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya
moyo? Ndipo nikaogopa sana. 3 Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani
uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu,
unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto? 4 Ndipo mfalme
akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa
mbinguni. 5 Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi
wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee
mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. 6 Mfalme akaniuliza, (malkia
naye ameketi karibu naye), Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Nawe utarudi
lini? Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka; nami nikampa muda. 7 Tena
nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio
ng'ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda; nipewe
na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza mwitu wa mfalme, ili anipe miti ya
kufanyizia boriti kwa malango ya ngome ya nyumba, na kwa ukuta wa mji; na kwa
nyumba ile nitakayoingia mimi. Naye mfalme akanipa, kama mkono mwema wa Mungu
wangu ulivyokuwa juu yangu. 9 Ndipo nikafika kwa maliwali walio ng'ambo ya Mto,
nikawapa hizo nyaraka za mfalme. Naye mfalme alikuwa amepeleka maakida wa jeshi
lake na wapanda farasi pamoja nami.).
Nehemia alikuwa akitoka taifa moja ili avuke
kwenda taifa jingine. Kwa kupitia waraka huu,
Nehemia aliweza kuwa na kibali cha kutumia miti ya misitu kwa ajili ya
ujenzi wa Nyumba ya Bwana. Tunajifunza kuwa Ukiwa na waraka, unaweza kuvuka
kwenda nga’mbo ya maisha yako, kwenda nga’mbo ya biashara yako kwenda nga’mbo
ya ndoa yako n.k. Kumbe usipokuwa na waraka, utajikuta ukizuiliwa na walinzi
waliopo ng’ambo ili usiweze kuvuka.
UKIRI
Kuanzia leo mtu yeyote aliyeniwekea viabo
vyenye kuonesha kuwa mimi nina
balaa, au nina mikosi, ninavikamata vibao
hivyo na kuviharibu kwa Jina la Yesu.
|
Yesu alipokuwa hapa duniani alifanya kazi ake
kwa kujiamini kwa sababu alikuwa anajua anacho
kibali. Katika LUKA 13:32 imeandikwa….(Saa
ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende
mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. 32 Akawaambia, Nendeni,
mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa,
siku ya tatu nakamilika.). Yesu anaonekana kujiamini kwa sababu kibali
alicho nacho siyo cha kuisha leo wala kesho. Endapo unacho kibali, na ukazuiliwa
na mtu yeyote, ujue bado utaendelea kujiamini kwa sababu kipo kibali unachokimiliki
wewe.
Imeandikwa katika 2 SAMWELI 11:14-15….( Hata
ikawa asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu waraka, akaupeleka kwa mkono wa Uria.
15 Akaandika katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita
vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe.) Ingawa Uria ndiye aliubeba huu wa
waraka, lakini hakuwa na taarifa kuwa ni waraka wa kumwangamiza
yeye binafsi. Maandishi ya waraka yanakuwa ndani. Kuna watu leo hii wanaishi
lakini wamebeba hati / nyaraka zilizoandikwa na zenye kuwahusu, na zimekaa
ndani yao kama alivyofanya Uria.
Mwaka wa 2017 ni mwaka ambao macho ya Bwana
yapo juu yetu. Hata hivyo ni lazima
ziwepo sababu za kufanya macho ya Mungu kuwa juu yetu. Lazima kiwepo kitu cha
kushawishi macho ya Mungu kuweza kuwa juu yako.
Mungu aliwahi kukiandika kibali/waraka kwa
ajili ya Kaini. Hata hivyo, Kaini aligundua kuwa asingekuwa na makazi duniani kupitia
waraka huo wa Mungu, na alipomuomba Mungu, kile kibali kilifutwa na Mungu
akazuia watu mahali popote pale duniani wasimdhuru Kaini. Hata leo wapo watu
ambao wanatembea na waraka unaowafanya wasiwe na makazi hapa duniani, na kila mtaa
watu wa aina hii huingia kukaa nyumba moja na kuhamia nyumba nyingine mtaa kwa
mtaa kwa visingizio mbali mbali: Mtaa wa Mafiga, Kihonda, Mazimbu n.k. kama
namna ya kuwafanya kukosa makazi hapa duniani.
UKIRI
Haati yoyote iliyandikwa kwa majina yangu,
majina ya mume, majina mke, majina ya
watoto, leo nazikataa kwa Jina la Yesu. Kila hati iliyoandikwa kifo, leo nazikusanya, nakuziharibu, niachieni kwa
Jina la Yesu, na kwa Damu ya Yesu. Leo nazichana hati zote nilizoandsikiwa
kwa Jina la Yesu.
|
Yawezekana katika kazi unayoifanya, zipo
hasara/shoti unazozipata na ambazo unalazimika kuzilipa ili kufidia. Ukiwa na
waraka utakuwa na uwezo wa kukemea wafalme wa giza. Ukiwa na waraka hautasumbuliwa
kamwe na majini mahaba. Leo uanze
kushughulikia kila waraka uliaoandikwa mabaya kwa mwaka 2017, kwa Jina la Yesu.
Ukiwa na waraka utapata haki zako zote. Kibali au nyaraka iliyoandikwa na
mfalme, hufanya hata maadui zako washindwe kukuzuilia.
Imeandikwa katika ESTA 3:8-15…..(Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna
taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko
katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za
kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme
kuchukuliana nao. 9 Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe;
nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli
hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. 10 Ndipo mfalme alipoivua pete yake
mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi. 11 Kisha
mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo
vema.12 Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu y a mwezi wa
kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa
mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila
jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la
mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake. 13 Barua zikapelekwa kwa
mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na
kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku
moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa
Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara. 14 Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu
katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile. 15
Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko
Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa
Shushani ukafadhaika.). Wayahudi walitakiwa waangamizwe kwa sababu tamaduni
zao hazichangamiani na za makabila ya watu wengine, na Hamani ndiye aliandaa
waraka wa maangamizo hayo. Yamkini hata wewe Hamani wa maisha yako ameandaa
waraka wa maangamizi yako kwa mwaka huu 2017. Leo ni siku ya kushughulika na watu wa aina hii
katika Jina la Yesu.
Ili upate kibali cha kuandikiwa waraka wa
kuhudumiwa na Mungu kwa mwaka 2017, ni vyema leo ujulikane na Mungu, kwa sababu
hata katika maisha yetu ya kawaida, mtu haandikiwi waraka kama hajulikani
kabisa. Cha kufanya leo ni kumwamini Yesu Kristo kwa kukubali kuokoka.
Tembelea Facebook Yetu:
Somo: Waraka wa Kifo
Tembelea Facebook Yetu:
Somo: Waraka wa Kifo
© Media and Information
Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +25571765979866 / +255713459545
|
© Media and Information
Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +25571765979866 / +255713459545
|