GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
[UFUFUO NA UZIMA MOROGORO]
JUMAPILI: 12 FEBRUARI
2017
MHUBIRI: PASTOR STEVEN NAMPUNJU (RP)
&
PASTOR HAPPINESS GODSON (RP)
Pastor Happiness Godson (RP) akifungua ibada kwa Maombi kabla ya Kumkarabisha Mhubiri wa Leo Jumapili 12/2/217 |
Maana ya ufahamu
ni ule uwezo wa mtu wa kuelewa mambo fulani fulani maishani mwake. Ufahamu na
akili huendana pamoja. Akili ni ule uwezo wa kufikiri na kuamua mambo kwa
ufasaha unaotakiwa. Na endapo mtu amefungwa ufahamu wake, maana yake mtun huyo hatakuwa
na uwezo huo wa kufanya maamuzi. Wapo watu wanaokuwa wamefungwa katika kufanya
maamuzi. Mungu akitaka kumuokoa mtu anamwekea ufahamu ndani yake wa kutaka kuokoka. Ufahamu ni kama ghala la silaha
analotumia Mungu kutunza silaha zake za vita. Mtu akienda shuleni lengo lake ni
kuupata ufahamu wa jambo fulani.
Shetani humwinda
mtu ili kumfanya mtu huyo asiupate ufahamu wake. MITHALI 3:13-17 (Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule
apataye ufahamu. 14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na
faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. 15 Yeye ana thamani kuliko
marijani, Wala vyote uvitamanivyo
havilingani naye. 16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa
kushoto. 17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.). Mtu
apatapo ufahamu mtu huyo huitwa ni “heri”.
MWANZO 41:28-36….(Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao
atakayoyafanya hivi karibu. 29 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi
yote ya Misri. 30 Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile
yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. 31 Wala shibe
ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana
itakuwa nzito sana. 32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa
sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. 33 Basi,
Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. 34
Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya
tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. 35 Na wakusanye
chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa
Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. 36 Na hicho chakula kitakuwa akiba
ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri,
nchi isiharibike kwa njaa.). Yusufu aliliona tatizo la njaa kupitia
ndoto ya Farao, na akatafutia ufumbuzi kwa akili na nchi yote ikaweka akiba ya
chakula kipindi cha miaka saba ya shibe ili ije itumike kwa kipindi cha miaka
saba ya njaa iliyofuata.
Mwenye ufahamu
hahitaji uangalizi wa karibu. Ndiyo
maana watoto wadogo huhitajji mtu wa kuwalinda ili wasidhurike kwa sababu ya kuukosa ufahamu. Ufahamu wa mtu humfanya
afanikiwe ama asifanikiwe. AYUBU 39:17..(Kwa
sababu Mungu amemnyima akili, Wala hakumpa fahamu.). Kumbe kuna
uwezekano wa kunyimwa akili na kuukosa ufahamu vile vile. Je, mtu asiye na
akili au ufahamu huwa anafananishwa na kitu gani? Jibu la swali hili lipo
katika ZABURI 49:12…(Lakini
mwanadamu hadumu katika heshima, Bali amefanana na wanyama wapoteao.).
MAMBO YA KUJIFUNZA KUPITIA UFAHAMU.
1.
Ukiwa na ufahamu unapata hifadhi. Katika MITHALI
2:11 Imeandikwa…(Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi.). Kazi ya ufahamu
maishani mwako ni kukupatia hifadhi.
2.
Njia ya Ufahamu humfanya mtu kuishi. Imeandikwa pia katika MTIHALI 9:6...(Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi,
Mkaende katika njia ya ufahamu.) Ukikosa ufahamu maana yake
umejitengenezea mazingira ya kutoishi.
3.
Ufahamu utakuepusha na mapigo. Imeandikwa pia katika MITHALI 10:13…(Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye
ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo
wake asiye na ufahamu..). Ukiwa na ufahamu unajiepusha na mapigo
mbalimbali (mfano: balaa, magonjwa, umaskini, laana, mikosi n.k). Haya mapigo
yameamriwa kwa mtu asiye na ufahamu. Nikiupata ufahamu maana yake najiepusha na
fimbo na mapigo ya ulimwenguni humu.
UKIRI
Kuanzia leo,
nakjuanzia sasa, endapo ipo taabu iliyokaa maishani mwangu kwa sababu ya kuukosa
ufahamu leo nakataa kwa Jina la Yesu. Ewe uliyeshika ufahamu wangu rudisha
kwa Jina la Yesu. Amen.
|
4.
Ukikosa ufahamu unaweza kufa. Imeandikwa katika MITHALI
10:21… (Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi; Bali wapumbavu hufa kwa kuwa
hawana ufahamu.). Kumbe Chanzo cha vifo vya watu wengi hutokana na ukosefu
wa ufahamu. Kupitia ufahamu, hutaogopa chochocte kwa sababu ufahamu utakuwa
unatembea na wewe.
5.
Ufahamu huleta upendeleo. Imeandikwa katika MITHALI
13:15…(Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya haini huparuza.). Kumbe
ukiwa kazini na ukaona upendeleo ukiwa juu ya mtu fulani ni kwa sababu ya
jufahamua alio nao huo mtu. Ufahamu mwema kama unaleta upendeleo, maana yake
ufahamu mbaya hauwezi kuleta upendeleo
wowote. Upendeleo katika afya njema, maisha mazuri n,k hupatikana tu kwa kuwa
na ufahamu mwema. Ndiyo maana shetani huiba ufahamu ili kusababisha mtu asipate
upendeleo mahali popote pale. Hata kwenye biashara, utakuta duka moja lina
wateja wengi zaidi ya maduka mengine ni kwa sababu ya tofauti za ufahamu.
Yamkini mwenye duka mwenye fahamu zake ameweka TV ya kuonesha habari na kwa
hivyo wateja hupendelea kupata huduma mahali hapo kwa sababu wakati wa kuapata
huduma zao pia wanazijua pia habari mbalimbali za dunia hii.
6.
Mwenendo wa mtu huvyoonshwa kwa njia ya ufahamu. Imeandikwa katika MITHALI
15:21…(Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu
huunyosha mwenendo wake.). Kumbe mtu mwenye ufahamu anaweza kuunyoosha
mwenendo wake. Biblia inasema kuwa Ufahamu
ni chemchemi ya uzima. MITHALI 16: 22 …(Ufahamu
ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao;
Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao). Kanisani
tunafundishwa maarifa mbalimbali ili yawe chemchemi ya uzima kwa uzao wetu,
familia zetu n.k. Katika MITHALI 19:8 Imeandikwa….(Apataye
hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye
ufahamu atapata mema.). Kumbe ufahamu unaweza kukamatwa ama kushikwa. Leo tutaita
fahamu zetu ili popote zinaposhikiliwa ziachiliwe kwa Jina la Yesu.
Ili uweze
kumsaidia mtu aliyefungwa katika ufahamu wake, kwanza umsaidie kwa kuufungua
ufahamu wake umrudie. Ili kumkabili mwenye nguvu yeyyote, kwanza ni kwa
kumfunga kisha kunnyng’anya silaha zake. Imeandikwa katika 2TIMTHEO 2:26.. (wapate tena fahamu zao, na kutoka katika
mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake).
Tunjaifunza kuwa kumbe kuna uwezekano wa ufahamu wa mtu kuchukuliwa, na
anayeuchukua ufahamu wa mtu ni ibilisi shetani.
Kwa wewe ambaye hujaokoka
leo mpe Yesu maisha yako, ili Mungu aweze kukusaidia tena na kuupata ufahamu
wako kwa Jina la Yesu. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU
32:29…(Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya, Ili watafakari mwisho wao.) pengine unaweza
kuwa uliokoka hapo awali kisha ukarudi nyuma, leo hii Mungu akupe akili na
ufahamu tena na kumpokjea upya Yesu kuwa
Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Amen.
========== M W I S H O ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NA NASI KIPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM:
pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE:
pastor:dr.godson
SIMU: 0719 798778 (Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro
http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/?m=0
http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/?m=0
© Media and Information Ministry
GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +255719612874 / +255713459545
|