GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA → MOROGORO}
JUMAPILI: 30 JULY 2017
MHUBIRI: PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Mch. Godson Issa Zacharia akifundisha katika ibada ya leo Jumapili. |
Katika Biblia maana ya neno UPAKO humaanisha ule uwezo katika Roho Mtakatifu wa kufanya vitu au mambo mbalimbali yaliyo juu sana nje ya milango mitano ya fahamu: Maana yake ni kuwa penye mambo ya upako - ngozi haiwezi kuyagusa, sikio haliwezi kusikia, macho hayawezi kuamini yakionacho, ulimi hauwezi kuyaonja n.k. Upako ni ule uwezo wa kufanya mambo ambayo tayari dunia yote walishasema kuwa imefikia mwisho. Upako ni ule uwezo utendao kazi ng’ambo ya mawazo na akili za wanadamu. Endapo dunia imesema HAIWEZEKANI, upako huingilia kati na kusema kwamba INAWEZEKANA.
Kwa upande
mwingine, Mkoma ni mtu aliyetengwa na jamii. Katika Agano la Kale, mtu mwenye
ukoma alipawswa kutengwa kabisa na kukaa nje ya makazi ya wandamu wengine. Tunaposoma
Kitabu cha HESSABU 12:10-12 (Kisha
hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye
ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye
ukoma. 11 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee
dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.). Tofauti
na zamani, kwa sasa watu wenye ukoma hawatengwi tena, wala kutolewa nje ya miji
yao. Pia katika WALAWI 13:45-46 imeandikwa
(Kisha
mwenye ukoma aliye na pigo ndani yake, nguo zake zitararuliwa, na nywele za
kichwa chake zitaachwa wazi, naye atafunika mdomo wake wa juu, naye atapiga
kelele, Ni najisi, ni najisi. 46 Siku zote ambazo pigo li ndani yake, yeye
atakuwa mwenye unajisi; yeye yu najisi; atakaa peke yake; makazi yake yatakuwa
nje ya marago.).
Ndugu zako wanaweza
kukutupa nje, wakakukataa, wakakutenga. Pengine hata wewe kuna watu wanakuona
haufai, wakisema ya kuwa wewe u najisi. Usimtumainie mwandamu kwa kuwa muda
wowote mwanadamu huyo anaweza kukuacha. Weka tegemeo lako kwa Yesu Kristo pekee. Imeandikwa katika 2WAFALME 6:24-30 kusema “Ikawa baada ya hayo, Benhadadi mfalme wa
Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria. Njaa ikawa kuu
huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa
vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya
fedha. Ikawa mfalme wa Israeli alipokuwa akipita ukutani, mwanamke mmoja
akamwita akisema, Unisaidie, bwana wangu, mfalme. Akasema, Bwana asipokusaidia,
nikusaidieje mimi? Ya sakafuni, au ya shinikizoni? Mfalme akamwambia, Una nini?
Akajibu, Mwanamke huyu aliniambia, Mtoe mtoto wako, tumle leo, na mtoto wangu
tutamla kesho. Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya
pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake. Ikawa, mfalme
alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa
akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani
mwilini mwake.” Katika Samaria njaa ilikuwa imeuma sana na Mfalme wake
akawa hana msaada. Hata katika miji yetu hapa kwetu, na nchi za duniani leo hii
kuna NJAA KALI sana, nayo ni NJAA YA WOKOVU. Mtu akimpata Yesu
amepata chakula kwa kuwa Yesu alisema yeye ni Chakula cha Uzima. Njaa kali tuliyo
nayo ni ya kiroho, na hasa watu kutomwamini Yesu Kristo, na hivyo huu ni muda
wa kumsihi Bwana Yesu akalete upako wa
kuiponya nchi yetu na miji yake.
Majeshi ya ufufuo na uzima Morogoro wakimsifu Mungu. |
Pamoja na njaa kuendelea kule mjini Samaria, hata hivyo nje ya mji walikuwepo watu wanne wenye ukoma. Inahitajika Eliya Mtishbi ili aweze kutabiri tena kwa habari ya mvua ya baraka kunyesha, ili chakula kipatikane na njaa itoweke kwa Jina la Yesu. Imeandikwa katika 2WAFALME 7:1-18 “Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. 2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.
7 Kwa hiyo
wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao,
na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate
kujiponya nafsi zao. 8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo,
waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na
mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile
vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. 9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya
tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja
hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa
nyumba ya mfalme. 10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia,
Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya
mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziach.” Swali la kujiuliza: Je, hawa wakoma ni nani aliwatakasa hata kuweza kuingia mjini kutoa
taarifa ya kuwepo chakula na nyara?
Kwa kuwa mtu mwenye
ukoma alikuwa ametengwa, ni sawa sawa na kile ambacho ndugu au majirani
wamefanya kwako. Yamkini umetengwa nao, wanakuonea n.k Tunajifunza kuwa
unapokuwa unaonewa, chukua hatua, usikae kimya. Huwezi kufanikiwa kwa kukaa tu bila kuchuka hatua
yoyote. Wakoma wanne (4) katika Biblia
waliamua kwenda na kuliendea Jeshi.
Taabu iliyoopo mbele yako ni sawa na jeshi. Muujiza wa kuleta ukombozi
unatokana na wewe kuanza kuchukua hatua: Usiwaze kusema eti unasubiria uwe na
mtaji mkubwa wa milioni moja ndiyo upige hatua!! Hapana. Hicho kiasi cha fedha
ulicho nacho kinatosha kukufanya kuleta ukombozi maishani mwako. Hatua za wakoma zilileta ukombozi.
Vivyo hivyo na wewe pale ulipo piga hatua zako binafsi na Mungu atakuletea
muujiza wa ukombozi maishani mwako. Huwezi kuanza kuhesabu milioni moja bila kuanza
na Shilingi moja. Ushindi huanza kwa kujihatarisha.
Platform ministry wakiongaza sifa na kuabudu. |
Mungu anapenda kuziona
hatua ulizochukua ili akuletee ukombozi. Pengine ni kiwanja chako unacho mahali
fulani, chukua hatua kwa kupeleka hapo matofali kiasi kadhaa, ili hata wachawi
waliokuwa wanakizuia kisijengejke wakimbie wote kwa Jina la Yesu. Kumbuka
Biblia inasema kuwa MITHALI 28:1
Imeandikwa, “Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.”
Pia Imeandikwa katika WALAWI 26:36 “Tena
hao wa kwenu watakaobaki, nitawatilia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za
adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama
mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.” Ukipiga hatua Mungu atasababisha uwoga kwa adui
zako waliokufanya uonekane kama mkoma. Ni kwa hatua yako tu maadui zako
watahama njiani kwako kwa jina la Yesu. Katika UFUNUO 6:15-16 imeandikwa “Na wafalme wa dunia, na wakuu, na
majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana,
wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na
miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha
enzi, na hasira ya MwanaKondoo.” Utakapoanza kupiga hatua, utasababisha
wote waliokaa mbele yako kukuzuia wajifiche kwenye pango, na chini ya miamba ya
milima kwa Jina la Yesu. Leo Bwana atasabisha uwezo wa rohoni ambao binadamu
hawezi kuuona ili waliokuzuia wakimbie kwa Jina la Yesu.
UKOMA KATIKA ULIMWENGU WA LEO.
Je, katika kizazi
cha leo, wenye ukoma ni akina nani? Mkoma katika nyakati za leo ni mtu
aliyetengwa na watu, mtu aliyeachwa, asiyependwa na jamii. Mtu aliyeamua kumwamini
Yesu anakuwa ametengwa na dunia, nap engine utaitwa majina ya ajabu ajabu.
Wengine huwaita waliookoka ni makafiri. Ndiyo maaana ukipanga nyumba mahali
popote utafukuzwa tu. Pamoja na wewe kutengwa, lakini wewe ndiyo suluhisho lao
la kuwapatia chakula. Ndiyo maana Biblia inasema “Wala msiifuatishe namna ya dunia
hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya
Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” (WARUMI 12:2). Watu wa dunia hii wanatamani kuona kuwa wewe siyo
muombaji, kwa sababu kila unapoomba unaharibu nguvu za giza. Ndiyo maana wapo
wenye nyumba wanaowafukuza wapangaji wanaopiga majeshi kwa maombi ya kushindana
usiku. Wenye nyumbe hawa hufanya hivyo kwa sababu kupitia maomni haya nguvu zao
za giza huangamizwa kwa Jina la Yesu.
Mch. Godson Issa Zacharia akimfungua mtu aliyefungwa na shetani. |
UKIRI
Enye mizimu,
mashetani nawafyekwa kwa Jina la Yesu. Nawafuatia Washami wa maisha yangu,
wanaonizuia na kuwafanya wakimbie kwa Jina la Yesu.
|
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/