GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA → MOROGORO}
JUMAPILI: 23 JULY 2017
MHUBIRI: PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Mch. Godson Issa Zacharia akifundisha katika ibada ya leo. |
Leo ni siku ya
kutoroka kutoka kwenye gereza la kidiplomasia na kwenda kwenye usalamawetu kwa
Jina la Yesu. Maana yaKutoroka ni kuondoka bila ruhusa. Gereza la kidiplomasia ni gereza kama yalivyo
maferza mengine.ulimwenguni kote kazi kuu ya gereza ni kumnyima mfungwa uhuru
wa kufanya yale anayotaka kufanya. Mfano, ukiwa gerezani muda wa
kulalautapangiwa, ratiba ya kula chakula unapangiwa n.k. Kwa kawaida mfungwa
huwekwa gerezani kwa sababu ya makosa aliyofanya. Hata hivyo, shetani humtupa
mtu gerezani siyo kwa sababu aliiba au kufanya kosa kubwa namna gani la hasha!!
Shetani huwaweka watu gerezani kwakosa tu la wao kumufata Yesu.
Upo muda wa
mfungwa kukaa gerezani na kutumikia kifungo fulani. Wafungwa wengine hutumikia
kifungo kwa mwaka mmoja,miaka miwili,wengine 30 na wengine kifungo cha maisha
yao yote. Anayeamua utendewe nini ni mkuu wa gereza, ambaye huitwa Bwana Jela.
Gereza tunalozungumzia hapasiyo yale ya kimwili kama lilivyo Ukonga, au
Kingulwira au Kilakala-Morogoro. Tunazungumzia gereza la Kiroho na ambalo kismingi
hufanya kazi kama yalivyomagereza ya kimwili. Tunaposoma katika ISAYA 14:17, neno
laMungu linasema hivi “Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji
yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? ” Tunajifunza kuwa
wanadamu wanawezamkufungwa na ibilisi na kuwekwa jela, na baadae kukosa uhuru wa kuishi maisha ya
uhuru.
1. Ulikuwa zamani unapenda kula vyakula fulani, lakini leo
hii ibilisi amekuweka kwenye jela ya kisukari, na sasa unachagua chakula.
2. Ulikuwa zamani unapenda kusuka nywele lakini leo hii
ibilisi amekuletea ugonjwa wakansa na nywele hazioti tena!!
Imeandikwa katika ISAYA 42:22 “Lakini watu hawa ni watu
walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana
asemaye, Rudisha.”. Kwa hiyo mtu aingiapo kwenye haya magereza hawezi
kuachiliwa tena, hadi pale atakapotokea mtu
wa kusema “Rudisha”.
Kwa kawaida
wafungwa wa magereza mengine hupata mateso ya viboko na chakula cha shida
magerezani. Gereza la Kidiplomasia (Diplomatic
prison) ni gereza la tofauti kidogo na pengine ni maalumu. Gereza la
Kidiplomasia ni gereza la starehe. Mtu anakuwa amefungwa lakini bado zile anasa
za kidunia mtu huyo anaendelea nazo. Ni kifungo kwa watu walioheshimika sana. Chumba
cha gereza hili kina vitu vyote muhimu kama vile godoro, TV, AC, simu, chakula
cha starehe n.k. Hata walinzi wanaolinda wafungwa wa kidiplomasia ni walinzi
maalumu. Pamoja na starehe zake, mfungwa
wa kidiplomasia anakosa ule uhuru wa kufanya baadhi ya mambo aliyotaka
kuyafanya binafsi. Mbaya zaidi, mfungwa wa kidiplomasia huwa hajitambui kuwa
yupo gerezani. Mara zote mtu anayesababisha wewe kufungwa katika gereza la aina
hii anakuwa ni ndugu au jamaa wa
karibu.
Majeshi ya Ufufuo na Uzima Morogoro wakisikiliza mafundisho ya leo. |
Mtu anaweza kuwa
na mali na kila anasa anayoitaka. Watu wa aina hii wanatumia hela hiyo hiyo
kuwafanya wawe walevi, au waasherati, kuwa na nyumba ndogo mitaani, kuambukizwa
maradhi yasiyotibika, kuwa watumiaji dawa za kulevya n.k. Wewe uonapo watu wa aina hii ufahamu kuwa ni watu
waliopo katika magereza ya kidiplomasia.
Tunasoma katika UFUNUO 2:10 “Usiogope mambo yatakayokupata;
tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi
mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya
uzima.”. Kwanza tujue kuwa kuna kifungo, anayeweka watu gerezani ni
ibilisi, mateso yatakuwepo uwapo gerezani,
nnekuna muda wa siku kumi kukaa gerezani na tano atakayevumilia hadi mwishjo
atapata taji ya uzima. Kumbe upo muda fulani ambao mtu anaweza kuwepo katika
gereza la kidiplomasia, na ni pale tu mtu atakapovumilia hadi mwisho atakuja
kupewa taji.
UKIRI
Ewe ibilisi
uliyejipanga kuniwekea kifungo cha kidiplomasia kwa muda maalumu leo na
kushambulia kwa Jina la Yesu. Mimi leo ninatoroka kwenye gereza hilo kwa Jina
la Yesu. Amen
|
Kwa kawaida Mungu wetu
anakuwa amekusudia mambo mazuri sana katika maisha ya watu mbalimbali.
1. Mathalani ulikuwa binti mzuri, na Mungu alikusudia
uolewe na upate watoto watakaokuwa mawaziri, wabunge, majaji, Wakurugenzi au
Katibu Mkuu wa baadae. Hata hivyo, katika kipindi kile cha umri wa miaka 18-35 binti
huyu akaringia kila kijana aliyekuja kwake akitaka kumuoa. Maana yeke ni kuwa shetani
alikuweka katika gereza la kidiplomasia, na sasa hawapo vijana wanaokufuata tena
wakitaka kukuoa. Miaka imepita na sasa umri wako ni miaka 40 muda wa kukaa katika
gereza la kidiplomasia umeisha na wanaotaka kukuposa ndiyo wameanza kukujia
tena. Ni kweli kuwa utaolewa lakini hautafaidi matunda ya uzao wako, hata kama utazaa watoto
mawaziri wa baadae kwa sababu upo nje ya
muda wa Mungu wa baraka zako.
2. Mfano mwingine ni pale ambapo mtu anaitwa kwa ajili ya
usaili wa kazi fulani lakini siku moja kabla ya usaili huo anavitafuta vyeti
vyake na havipati, mtu huyu anakuwa amefungwa katika gereza la kidiplomasia.
Baada ya siku ile ya usaili, mfungwa huyu anavikuta vyeti vyake vikiwa sehemu
ya wazi kabisa, viko chini ya Biblia na kumshangaza mbona hakuviona? Uonapo mtu
wa aina hii jua walikuwepo walinzi wa gereza la kidiplomasia ili mtu uyo
asipewe kazi iyo na hatimaye kufanikiwa. Na ukimwona mtu asiyejua kabisa kusoma
au kuandika wala usimlaumu kwa sababu ni mashetani yalitumika kumfunga katika
gereza la kidiplomasia. Na mtu fungwa kwa sababu ya ile hatima iliyo ndani
yake.
Imeandikwa katika YEREMIA 1:4-6 “Neno la Bwana lilinijia, kusema, 5
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni,
nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. 6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana
MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni motto”. Mungu
anatuhakikishia kuwa alitujua kabla ya kutuumba katika matumbo ya mama zetu.
Tena Mungu alitutakasa hata kabla ya kututoa ndani ya matumbo ya mama zetu. Ni
sawa na kusema, Mungu alituwekea UHESHIMIWA
ndani yetu kabla ya kutuumba. Yeremia katika utoto wake alitaka kukataa
lakiniMungu akamsisitiza kuwa. Kumbe watu wengi ni waheshimiwa lakini hawatambui
hilo. Ndiyo maana Mungu anasema katika ISAYA
43:4 “Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami
nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa
ajili ya maisha yako”. Kumbe Mungu anatutambua sisi kama waheshimiwa,
na zaidi sana Mungu ametupenda.
Lipo jambo la
ajabu sana na halivumiliki ambalo mtunzi wa Kitabu cha Mhubiri aliliona
kwamacho yake likifanyika duniani. Katika MHUBIRI
10:5-7 imeandikwa “Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni
kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; 6 ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa
juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. 7 Mimi nimeona watumwa wamepanda
farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa”. Tunajifunza
kuwa wapo watu wasiostahili kabisa lakini ndiyo wanaendesha magari ya kifahari,
na wapo watu waliookoka, wenye kuheshimiwa na Mungu lakini wanatembea kwa miguu
mabarabarani!!!! Wewe uliyeokoka unakaa nyumba ya kupanga tena isiyo na umeme na
wale wasiostahili wanakaa kwenye nyumba za kifahari!!! Leo hii tukatae kuishi
katika magereza ya kidiplomasia kwa Jina la Yesu.
Katika ZABURI 8:4-8 neno la Mungu linasema
hivi “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5
Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6
Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani,
na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini”. Yawezekana
wewe unajiona ni mtumwa, kwa kuwa bado unatembea kwa miguu. Kumbe tunajifunza
kuwa Mungu huwa anawaangalia wanadamu. Mtunga Zaburi anasema “Umemfanya
mdogo punde kuliko Mungu” kumaanisha kuwa Mungu amemfanya Mwanadamu
kuwa kidogo sawa naye, na ndiyo maana “tukitamka
mambo kwa vinywa vyetu lazima mambo hayo yatokee”. Wewe siyo mtu wa
kawaida. Kutokujua kwako ndiyo kunamfanya ibilisi akuweke kwenye magereza ya
kidiplomasia. Leo lazima tutoroke kwenye magereza ya biashara, miradi, elimu, ndoa
n.k. Katika Biblia, Danieli alikuwa hana
kosa lolote lenye kuweza kumfanya
afungwe gereza la kidiplomasia. Maadui zake walipokosa sababu ya kumfunga,
wakatafuta namna ya kumshitaki kwa habari za Mungu wake na ndipo akatupwa
kwenye gereza lenye samba wakali.
Leo tutatoroka
kutoka kwenye magereza yote ya kidiplomasia ambayo shetani alituweka. Ili
kufanya haya, lazima apatikane mtu wa
kukusaidia ili utoroke. ISAYA 42:6-7 “Mimi, Bwana, nimekuita katika
haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na
nuru ya mataifa; 7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa,
kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa”. Leo lazima
tuhame kutoka vifungo hivi vya
kidilomasia kwa Jina la Yesu.
Mfungwa yeyote anapotaka
kutoroka hapaswi kuomba ruhusa au kumuaga mtu yeyote. Ni muda wa mfungwa
kuchungulia walinzi wa gereza walivyokaa na kuwaruka walinzi hawa bila wao kufahamu.
Jambo la muhimu la kufanya ni kumpa Yesu Kristo maisha yako (kwa maana ya
kukubali kuokoka). Baada ya leo kumpa Yesu maisha yako kila neno utakalotamka
kwa kinywa chako litatokea vilevile kwa Jina la Yesu.
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/