GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO
JUMAPILI:
20 AUGUST, 2017
MHUBIRI:
PASTOR, Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (Snp)
Biashara
ni shughuli inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuuza au kununua bidhaaa
fulani ili mtu apate faida. Kwenye biashara kuna mfanya biashara, bidhaa, na
lengo lake ni kupata faida. Kwa hiyo biashara ya kichawi ni ile biashara
inayofanywa na mawakala wa kishetani. Wafanya biashara wake ni wachawi ambao ni
wanadamu. Siku zote wanawadanganya watu na kuwapokonya mali zao. Kwenye
biashara hii kuna taaaluma nyingi, mfano: Afisa usafirishaji, Afisa
mawasiliano, wataalam wa udanganyifu na wachumi wanaoangalia kipi kifanyike ili
wapate fedha. Wapo wataalam wa kuteka na kuhakikisha wapate watu wa kuwateka.
Wachawi
kupitia wataalam wa uchawi, watu wanakuwa masikini, fukara, wenye taabu na
mateso ili wao watumie nyota zao. Biashara ya kichawi huwa inalenga kuleta
mauti katika maisha ya watu. Mchawi ni mtu mwenye roho ya uchawi ndani yake.
Wachawi ndio wachuuzi katika biashara hii.
Habakuki
2:5 Imeandikwa, Naam,
pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani
mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi
kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu
chungu.
Kutoka
22:18 Imeandikwa, Usimwache mwanamke mchawi kuishi. Hii ni biashara inayovuviwa
lakini ina wasimamamizi. Divai ndio mchumi mdanganyifu. Uchami watu wengi
uharibikia kwenye ulevi.
Ufunuo
wa Yohana 18:11:13 Imeandikwa, ‘Nao
wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye
bidhaa yao tena; 12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na
lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo
nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti
wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; 13 na
mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya
mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari,
na miili na roho za wanadamu.’ Hapa neno la Mungu linataja baadhi ya
bidhaa katika biashara, zaidi unaweza kujifunza kuwa mtu anaweza kuibiwa na
kuuzwa ama mwili wake au roho yake. Watu waliokufa katika mazingira tata
wanaweza kuuzwa kutoka kwa mchawi mmoja na kwenda kwa mwingine.
Baadhi ya makutano wakifuatilia mafundisho ya neno la Mungu katika nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro. |
Wachawi
siku zote wana waloga watu kwa sababu ya Wivu
tu.kwahiyo hapa tunajifunza kuwa chanzo cha wachawi kumloga mtu ni wivu.
Kwa kawaida kila taarifa njema unayowapa marafiki zako, si wote wanaofurahia.
Kumbuka taarifa zako za kushinda, faida katika biashara zako, mavuno na ustawi,
tangu ulipozitoa ndipo matatizo yalipo anza. Mateso na shida unazoziona
zinatoka kwa wachawi.
Kumbukumbu
la Torati 18:10-11 Imeandikwa, ‘Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au
binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye
nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa
kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye
wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu
ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.’ Mungu hapendi mambo
ya uchawi na wasoma nyota. Uchawi una madhara kuliko ambavyo tunaweza kuwaza.
Mfano, mtu alikuwa mwenye miguu iliyojaa Baraka lakini ghafla anaugua miguu.
Mtu akisha ugua basi hawezi kutembea na kukutana na Baraka zake.
Kuchukua
watu Misukule. Hii ni madhara ya biashara za kichawi. Uchawi unaweza kusababisha
nyota, kazi, fursa zikapotea na hatimaye mtu anakua masikini. Mtu anaibiwa eneo moja na kuuzwa eneo
lingine,
Nahumu
3:1-4 Imeandikwa, ‘Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka
hayaondoki. 2 Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na
farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka; 3 mpanda farasi
akipanda, na upanga ukimeta-meta, na mkuki ukimemetuka; na wingi wa waliouawa,
na chungu kubwa ya mizoga; mizoga haina mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yaoKwa
sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi,
auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake..’
Kuna watu leo wametekwa na wanapigwa mijeledi na wachawi. Misiba na machozi
imekuwa mingi katika miji kwa sababu ya biashara ya uchawi. Watu wanalia na
kuomboleza kwa sababu ya uchawi. Watoto hawawezi kusoma tena, vijana wamependa
anasa kuliko Mungu kwa sababu ya uchawi. Mchawi anaweza kuuza taifa moja kwa
nchi nyingine. Kama mchawi anaweza kuuza mtu mwingine au taifa, basi mchawi
anaweza kuuza nyota, miguu na mikono yenye Baraka, uso au kinywa chenye kibali.
Macho yanaweza kuuzwa ndio maana una matatizo ya macho.
Biashara
ni
kubadilishana. Kwa baishara za kichawi, wakiiba uso au nyota lazima waweke pepo
wa balaa na mikosi. Wanaweza kuuza kibali cha mtu na ukawekewa roho ya
kukataliwa. Ezekieli 13:18-19 Imeandkiwa,’ useme,
Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo
vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za
watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?
19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na
vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi
hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu
wasikilizao uongo. 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha
hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa
katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama
ndege. 21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono
yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa
mimi ndimi Bwana.’
Wachawi wanawinda roho za watu. Mtu akiwa na nyota nzuri au kibali, akiwindwa
utaona anaanza kuchanganyikiwa. Kumbe kuna mambo yaliyokupata kwa sababu ya
nyota, kibali au Baraka ulizopewa na Mungu. Wasimamizi wa biashara ya kichawi
wanauza kilicho bora ili kitumike kuzalisha katika ufalme wa shetani.
MAOMBI
Katika
jina la Yesu Imeandikwa hapana uchawi juu ya Yakobo wala uganga juu ya Israeli
nakufuata ewe mchawi uliyeshikilia nyota yangu,akili yangu ya biashara,miguu
yangu,mikono yangu,kibali changu, nakufuata popote ulipo nakupiga kwa jina la
Yesu ,nawashambulia kwa mawe achia akili yangu,leta nyota, leta mikono yangu ya
kufanya biashara.
Leo
ni siku ya kushambulia biashara za kichawi na kufuta kabisa nguvu zao kwa Jina
la Yesu. Endapo kuna mtu ambaye hajampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa
Maisha yake binafsi, leo ni muhimu kufanya maamuzi hayo ya kuokoka ili
kufanyika kiumbe kipya.
© MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T)
CHURCH
MOROGORO CHURCH
|