Friday, August 18, 2017

SEMINA YA SIKU NANE UFUFUO NA UZIMA MOROGORO YAWAVUTIA WAKUU WA VYUO


·     Wasema ufufuo na uzima ni mahali sahihi kwa huduma za kiroho.

Semina ya neno la Mungu ya siku nane ambayo imefanyika ndani ya kanisa la Ufufuo na Uzima mkundi minara mitatu Morogoro,imegubikwa na matendo makuu ya Mungu. Wanawake na waume waume wameponywa na wengine wamerudishwa kutoka msukuleni,pia imewagusa watu mbali mbali mashuhuri mkoani Morogoro.

Semina hiyo ambayo imehudumiwa na Askofu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima mkoa wa shinyanga Snp. Godfrey Mwakyusa, akiwa sanjari na mkewe mchungaji Yuka Yamada,pamoja na waimbaji mbali mbali lukuki akiwepo  mwimbaji maarufu kutoka jijini Dare s salaam anayefahamika kwa jina la Super Bukuku.
Askofu Mch. Godfrey Mwakyusa(Shinyanga)
Katika ibada ya semina ya siku ya nane ambayo ilianza mapema saa tatu asubuhi katika kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro lililoko eneo la Mkundi minara  mitatu,wakuu wa vyuo viwili vya mkoani  morogoro walihudhuria ibada hiyo,ambapo walitambulishwa na Askofu wa ufufuo na uzima Morogoro Dr.Godson Issa Zacharia.
Kulia ni Mkuu wa chuo Saint Joseph Morogoro Bwana Seif Chomoka,
Kushoto ni Askofu, Mch.Dr. Godson Issa Zacharia (Morogoro).
Askofu Dr.Godson alianza kumtambulisha mkuu wa chuo cha Saint Joseph Morogoro Bw.Seif Chomoka,licha ya kuwa ni mara yake ya kwanza kufika katika ibada za makanisa ya ufufuo na uzima,zaidi alioneshwa kufurahishwa na namna ibada za ufufuo na uzima zinavyoendeshwa huku zikiwa zimejaa ngu vu za Mungu.

Kulia ni Mkuu wa chuo cha habari Morogoro, Bwana .Agustine Nongwe,
Kushoto ni Askofu Mch. Dr, Godson Issa Zacharia (Morogoro).
  Baadaye askofu Dr.Godson Issa Zacharia alimtambulisha  mkuu wa chuo cha uandishi wa habari Morogoro Bw.Agustine Nongwe,upande wake mkuu huyo wa chuo alieleza namna alivyouona utofauti mkubwa wa kihuduma za kiroho katika makanisa ya ufufuo na uzima,na kusema kuwa kwa kweli kanisa la ufufuo na uzima Morogoro ni mahali sahihi ambapo watu wanaweza kufunguliwa, na kurudishiwa vitu vyao na si pengine.
Share:
Powered by Blogger.

Pages