Wednesday, August 23, 2017

KIJANA RIZIKI ARUDISHWA KUTOKA MSUKULENI (TOKA ZIWA NYASA) BAADA YA KUOMBEWA.

                                        UFUFUO NA UZIMA MOROGORO.
Katikati ni kijana Riziki akishhudia namna alivyoteseka msukuleni, na jinsi alivyopona.

Akieleza anasema nilikuwa anafanya biashara ya kusambaza na kuuza malimao maeneo  ya dumila, baadaye nikaona ni vema nipeleke mkoani Morogoro ili nipate faida zaidi. Siku moja nikapeleka malimao elf tatu na mia nane, pale sokoni mawenzi, nikutana na mnunuzi yaani tajiri wa jumla. Yule mnunuzi akayaangalia malimao akamwambia mbona umeleta malimao yameoza? ndipo nikamwambia malimao yangu nimevuna mwenyewe ni mabichi na hakuna lililooza hata moja, yule jamaa akasisitiza malimao yote yameoza, nikasema malimao yangu ni mazuri hayajaoza. Yule mnunuzi akaniambia wewe una ugonjwa wa akili.


Kumdhibitishi nikamwita mtu aliekuwa karibu adhibitishe kauli yangu, ndipo naye alipoangalia malimao akasema malimao yameoza, akatokea mama mmoja akasema mbona malimao yote ni mazima mbona mnabishana, na hakuna lililooza hata moja. yule mnunuzi akasema malimao yameoza na ni ya kupeleka jalalani maana yanaharibu mazingira. Basi yule jamaa akatoa elfu kumi na tano, akaniambia chukua hii maana mzigo wako umeoza ni wa kutupa.


Nikazipokea zile hela, nikapiga hesabu ya kununua na kusafirisha nikaona ni hasara kubwa, na nimepoteza mtaji wote. kijana Riziki anaeleza baada ya kupokea zile elfu kumi na tano na kuona nimeshapata hasara, nikachanganyikiwa nikaondoka pale sokoni nikaanza kuutembea kuelekea njia ya Dar es salaam tokea Morogoro, hadi nikafika Kingulwira nkaendelea hadi nikafika njia kuna reli, nikakutana na babu mmoja akanishika mkono akaniambia twende huku, nilikuwa nakusubiria muda mrefu, nilijua unakuja. nilikuwa nakuona wewe katika chuo changu unakuja mtu wangu, yale malimao ungeuza ungerudi maana gari ilikuwa inakusubiri, ndio maana nilikuwa nafanya yale malimao usiuze,yaonekane yameoza, twende huku.



Riziki anasema akanipeleka katika shamba lake la migomba, nikaanza kupalizi migomba, baadaye akatokea mama mmoja mnene akasema mtu wetu huyu nitaondoka naye kwenda nyasa akatusaidie mizigo.Nikawa nafanya kazi ya kubeba mizigo, wakati huo sikuwa na akili ya kuuliza nitalipwa shilingi ngapi. Akiendelea kueleza anasema nikaendelea na kazi ya kubeba mizigo, nikashindwa kutembea peku, pia nilishindwa suala la mavazi anayotaka nivae. yaani nivae kikokoro yaani nguo nyeupe juu na chini nijifunge kitambaa cheupe mithili ya uvaaji wa kisukuma, nikamwambia bosi wangu mimi siwezi kuvaa hivyo maana nilikotoka sikuwahi kuvaa hivi.Hivyo basi suala la kutembea peku haitawezekana na kuvaa mavazi yale halitawezekana.


Nilipofika kule nikapewa chakula, nilipokiangalia ni ''ndizi na pumba'' zimekorogwa pamoja,nikambwambia kwangu haiwezekani kula pumba na ndizi, sijawahi kula chakula hiki,nikakikataa. Walipoona mimi ni mbishi sana wakanipuliza nikawa kama zuzu, zezeta, ikawa kila wanachoniamrisha nafuata, natii amri. Baadaye nikiwa ndani na wenzangu maana tulikuwa wengi, mimi nilikuwa kama mtu wa sabini na tatu(73), nikaanza fujo mle ndani, nikaanza kupigana, baada ya kuona mimi ni mkali sana wakanipulizia dawa ya usingizi, ikawa kila nikifanya kazi hakuna usingizi, nikiingia ndani napata usingizi mzito nalala sana.


Misukule wangine niliokuwa nao wakasema maisha haya tumeyachoka, tukakubaliana huyo mzee akiingia humu ndani tumfinye, yaani tumpige asitoke ndani, na kila atakaeingia ndani tumpige. Basi wakasahau kupaka madawa yao kabla ya kuingia ndani, wakaingia,tukawapiga hadi kuzimia wasiweze kutoka nje. wakashituka mbona kila anaeingia hatoki? mmoja akachungulia akaona misukule wamekuwa wakali sana, mmoja akatoa ushauri akasema hao wengine hawawezi kuondoka, ila huyu yaani mimi wanipige usingizi halafu waniache niondoke. Wakanipulizia dawa ya usingizi wakanitoa.Nikatoka pale nina usingizi mzito hadi nilitaka kugongwa na gari. Nikaondoka nikatembea nisijue ninakoelekea,baadae nikapata wazo la kufanya kibarua nipate nauli ya kurudi nyumbani.


 Ndipo nikakutana na kijana mmoja wa hapa kanisani nikamweleza shida yangu ya kutaka kazi, baada ya kuniangalia vizuri akanikuta siko sawa, akanipa msaada wa chakula.Akanipa chai na maandazi, kutokana na ule usingizi niliokwa nao mzito nikajikuta badala ya kula maandazi na chai, natafuna magazeti yaliyokuwa yamefungia maandazi. ndipo yule kijana wa kanisani alipoona hali niliyonayo sio ya kawaida akanileta kanisani Ufufuo na Uzima Morogoro, nikafanyiwa maombi,na ndipo  kumbukumbu zangu zote zilirudi,nikakumbuka tangu siku nilipopeleka malimao sokoni sikurudi nyumbani na hapo ndipo waliponichukua msukule.. Kwa sasa niko katika kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro naendelea na mafundisho, Namshukuru Mungu kwa kunitoa katika shimo la misukule.
wa pili kushoto ni kijana aliyekutana naye na kumleta kanisani ufufuo na uzima Morogoro.
wa pili kulia ni kijana Riziki.
Karibu katika kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro, Mungu anatenda mambo makuu kwa utukufu wake. Huduma ya ufufuo na Uzima ni ya masaa 24. Pia tuna ibada kila siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa saa kumi jioni na Jumapili kuanzia saa tatu asubuhi. Wote mnakaribishwa. Amen.

















Share:
Powered by Blogger.

Pages