UFUFUO NA UZIMA MOROGORO.
wa tatu tokea kulia ni kijana Josephat, wa kwanza toka kulia ni dada yake akidhibitisha. |
Kama maandiko
yasemavyo katika kitabu cha kutoka 22:18 ``usimwache
mwanamke mchawi kuishi”hii ni alama sahihi ya kuonesha hasira ya MUNGU juu
ya wachawi. Hii imedhihirika baada ya kijana Josephat Steven kutoa ushuhuda kuhusu
namna alivyologwa kwa mafanikio aliyoyapata baada ya mda mrefu wa kuhangaika na
maisha yake.kijana huyu alikuwa akiishia maneneo ya Doma mkoani Morogoro,amesimulia
namna alivyologwa baada ya kufanikiwa kujenga nyumba akiwa anafanya kazi yake
ya kukata mkaa na kuuza.
Josephat
akitoa ushuda huo namna alivyologwa anasema``baada ya kuwa nimefanya biashara zangu za kuuza
mkaa,nilifanikiwa kujenga nyumba ambayo ia vyumba viwili na sebule,mara usiku
mmoja nikaota ndoto kuna mtu ananifukuza
na nikawa nakimbia,tangu siku hiyo nikawa nawaogopa watu, na nkawa sitaki
kutoka nje ya nyumba, na hivyo nikawa nakaa uvunguni mwa kitanda changu’’amesema
kijana Josephat. Kijana huyo amesema ,hata alipokuwa akikaa humo ndani ya hiyo
nyumba bila ya kutoka nje hakuwa hata akihisi kuwa na haja kubwa wala ndogo
kiasi cha kujaribu kutoka nje, maana hakuwa anakula chochote. Zaidi saana
alikuwa akiogopa kuonana na watu, hivyo alikaa ndani siku zote chini ya kitanda,
na alikuwa akitoka nje usiku tu ili kukwepa kuonana na watu.
Baada ya
kuonekana kuwa na hali hiyo, ndipo ndugu zake walipoanza kuhangaika kwa waganga
wa kienyeji,amabapo wakiwa wanaelekea kwa mganga wa mwisho maeneo ya kingulwira
mkoani Morogoro ambaye aliwapa utaratibu wa kuleta kuku mwekundu na pesa kiasi
cha shilingi laki moja. Badaye wakiwa katika kujiandaa kuelekea kwa huyo
mganga,mtu mmoja akawaambia nendeni ufufuo na uzima wanaweza kumwombea na akawa
sawa,wakapitia kanisa la ufufuo na uzima Morogoro na kuombewa na kurudia hali
yake ya kawaida kama binadamu wengine.
Kijana Josephat
kwa sasa amekwisha funguliwa na kuwa na akili zake timam kama vijana wengine na anaendela kuabudu na
kujifunza katika kanisa la ufufuo na
uzima Morogoro linaloongozwa na Askofu Dr.Godson Issa Zacharia.
Watu wote
ambao wanapata mateso ya kulogwa na wachawi na kuharibiwa mipango na mifumo ya
maisha, kanisa la ufufuo na uzima lipo kwa ajili ya kushughulika na mambo
hayo,na kudhihirisha ukuu wa Mungu aliye hai. Karibu ufufuo na uzima Morogoro,
eneo la mkundi minara mitatu.