RP Adriano akifundisha somo la wiki hii "Kukamatwa Uzao" katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Bonde la Maono Morogoro |
Utangulizi: Somo la leo linaitwa “Kukamatwa Uzao”. Katika kitabu cha Mwanzo
3:15 imeandkwa [nami
nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake;
huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.]… Mungu alikuwa anaongea na nyoka. Ukumbuke kuwa nyoka ni ‘mwerevu kuliko wanyama
wote’. Kabla ya tukio hili, nyoka alikuwa
amemdanganya Eva pale bustani ya Edeni.
Ilikuwa ngumu kwa nyoka kumwingia Adamu kwa sababu alijua mwanamke ni mtu
rahisi kuelewa kuliko mwanaume. Kwa
kawaida mwanamke yupo karibu zaidi
katika ulimwengu wa roho kuliko mwanaume. Mwanamke ni chombo
alichotengeneza Mungu kuuleta ufalme
wake duniani, na ndiyo maana Yesu alizaliwa na mwanamke.
Baadhi ya sehemu kubwa ya Majeshi ya Bwana waliokuwa wanafuatilia somo la wiki hii Jumapili 16/11/2014. |
Mungu aliweka uadui kati ya uzao wa nyoka na uzao
wa mwanamke. Je,ni nyoka yupi
ambaye anazungumziwa hapa? Usije ukafikiri nyoka huyu ni sawa na wale
watambaao ardhini. La hasha!!. Huyu 'nyoka' ni 'shetani', ambaye hapo kabla alikuwa
akiitwa Malaika wa Sifa (Lucifer). Watu walimjaza udhalimu Lucifer na akaamua
kuasi, ili naye awe na mbingu yake mwenyewe kama ambavyo Mungu naye ana mbingu yake.
Baada ya uasi huu, vita ilitokea mbinguni, na imeandikwa katika Kitabu cha UFUNUO 12:7-9…[Kulikuwa na vita mbinguni;
Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao
pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena
mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi
na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake
wakatupwa pamoja naye.]…. Lucifer baada ya uasi huu, ndiyo akaingia ndani ya mnyama 'mjanja mjanja na mwerevu', na ambaye ni 'nyoka'. Akiwa
bustani ya Edeni, nyoka huyu kabla ya kuingiwa na roho ya shetani, alikuwa ni nyoka tu
wa kawaida.
YOHANA 4:63…[Roho ndiyo itiayo
uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.]… Maneno ni roho. Eva alifanya kosa la
kuongea na Yule nyoka, bila kujua kuwa ndani ya nyoka yalikuwepo maneno ya roho
la shetani. Wakati huo wa mazungumzo,
Adamu alikuwa hayupo karibu, kiasi kwamba akili ya Eva ilichukuliwa na roho wa
shetani na kumtii shetani zaidi badala ya neno la Mungu.
Showers of Glory wa Bonde la Maono Morogoro hawakuachwa nyuma, kwani nao walikuwa na staili ya kumchezea Bwana |
Uzao wa mwanamke mbele za Mungu ni “kanisa”. Ndiyo maana Yesu
Kristo alipowambwa msalabani, alichomwa mkuki ubavuni, na papo hapo Kanisa
likazaliwa. Kumbuka, Mungu alitumia ubavu wa Adamu ndipo ambapo Eva
alichukuliwa,na hata kanisa lilizaliwa baada ya ubavu wa Adamu wa pili (Yesu
Kristo) ulipochomwa kwa mkuki. Shetani anajua adahabu iliyopo: Kwamba uzao wa
mwanamke utamponda kichwa nyoka (shetani). Mbinu anayoitumia
shetani leo ni kujaribu kuukamata uzao wa mwanamke, yaani kanisa.
Shetani anatumia mbinu na mikakati mbalimbali kudhoofisha uzao wa
mwanamke. Ni kanisa pekee lina uwezo wa
kupatanisha hata wale wasioelewana hapa duniani.
MWANZO 6:1-4….[Ikawa wanadamu
walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu
waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote
waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele,
kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4
Nao Wanefili (Wanefili maana yake ni majitu) walikuwako duniani siku zile;
tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa
nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. 5 Bwana
akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi
analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa
amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.]… Kimsingi ‘Wana wa Mungu’
wanaozungumziwa hapa ni ‘malaika’. Kwa hiyo yalikuja kuwepo kwa mahusiano ya
ndoa kati ya wana wa Mungu na binti za wanadamu, kwamba kingetokea kizazi
kisichokubalika kutokana na ukaidi wake. Waliozaliwa hapa wakawa
mchanganyiko,”nusu shetani, nusu mwanadamu”.
MAOMBI:
Enyi mashetani wa aina mizimu,majoka,minugu, achia uzao kwa Jina
la Yesu, achia uzao wa mwanamke kwa Jina la
Yesu. Amen.
|
Children Ministry wa Bonde la Maono,wanakiri kuwa Yesus Kristo yupo mioyooni mwao, na hawatamuacha kamwe. |
Wana wa Mungu ni malaika. Ni viumbe wasio na miili, kwa sababu ni roho. Hata hapa Kanisani,malaika wapo,ingawa si rahisi kuwaona kwa macho. Katika Biblia MWANZO 18:1-2 [Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. 2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,]… Mwanzoni, tunaambiwa ni Bwana ndiyo aliyemtokea,lakini katika mstari wa 2, Biblia inasema watu watatu‼! Hivi inakuwa je Bwana amegeuka kuwa mtu?
Kitendo cha Ibrahimu kuwasujudia hawa watu,ni ishara kuwa alijua kati yao yupo Mungu. Katika tamaduni za Wayahudi, si rahisi kumwinamia mtu ovyo ovyo. Ndiyo maana Mordekai akagoma kumwinamia Hamani. Hatuwezi kuwasujudia malaika. Ukiona katika Biblia, malaika amesujudiwa, ujue huyo siyo malaika, bali ni Yesu mwenyewe, na hiyo hali ya kusujudu haiombwi, bali ni mawasiliano yaliyopo kati ya roho na roho. Tofauti ni kuwa, shetani hulazimisha watu wamwabudu au kumsujudia. Katika wale malaika watatu, mmoja wao alikuwa ni Yesu mwenyewe, na ndiyo maana Ibrahimu alisujudu.
MWANZO 18:3-14 …[akasema, Bwana wangu,
kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. 4
Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. 5 Nami
nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia
mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. 6 Basi Ibrahimu akaenda
hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande,
ufanye mikate. 7 Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe
aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. 8 Akatwaa siagi na
maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao
chini ya mti, nao wakala. 9 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo
hemani. 10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama,
Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo
nyuma yake. 11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na
Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12 Kwa hiyo Sara akacheka
moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? 13
Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa
mwana, nami ni mzee? 14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa
muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.]…. Ibrahimu alifikiria anawanawisha miguu
watu wa kawaida, kumbe walikuwa malaika.
Je tunajua je kuwa hawa walikuwa malaika? Tusome MWANZO 18:16-17 …[Kisha
watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja
nao awasindikize. 17 Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,]….
MWANZO 19:1…[Basi, wale malaika
wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu
akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.]… Ukumbuke walikuwa watatu, kati yao,
mmoja ni BWANA na wawili ni malaika. Wanaonekana ni watu, lakini kumbe
malaika. Unaweza kuwaona na kuvutiwa nao kwa sababu ya mavazi yao. Siyo kila
unayemuona barabarani ni mtu.lazima uwe mjanja kama nyoka na mpole kama njiwa.
Ni muhimu kuzijaribu kila roho kwa Jina
la Yesu. lutu alikuwa na maarifa ya rohoni,
na ndiyo maana akaweza kuwabaini hawa watu wawili (malaika) na
kwasujudia.
MWANZO 19:4-5..[Hata kabla hawajalala,
watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote
waliotoka pande zote. 5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu
waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.]… Watu wa ile nchi walidhani hawa wageni wa Lutu ni
watu tu wa kawaida, na si malaika. Kitendo cha wenyeji kutaka ‘kuwajua’ hawa watu ni kitendo cha kutaka ‘kujamiiana’ nao‼!
MWANZO 19:6-9..[Lutu akawatokea
mlangoni, akafunga mlango nyuma yake. 7 Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu,
msitende vibaya hivi. 8 Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume,
nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu
hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu. 9 Wakasema Ondoka
hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye
kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga
sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.]… Hiki kizazi kinaonesha jinsi ambavyo
kilikuwa jeuri, kwa sababu walitaka kufanya jambo hili hata kwa Lutu mwenyewe.
MAOMBI:
Kwa Jina la Yesu, Ninaagiza kuanzia sasa, maadui zako wapigwe kwa upofu kwa Jina
laYesu. Naagiza malaika wa Bwana waawpige upofu wanaoitafuta biashara yako,
masomo yako, kazi yako, wakutafute na hata wachoke wasikuone tena kwa Jina la Yesu. Amen
|
Unaona hao ni malaika
lakini wamevaa miili ya wanadamu. Lakini kwa sababu wanadamu na tamaa zao,
wakataka kufanya nao mahusiano ya kindoa.
MAOMBI:
Enyi mashetani mliokamata uzao wangu achia kwa Jina la Yesu. Navunja mikataba yote, navunja
makubaliano yote kwa Jina la Yesu. Ninanyausha miti yenu, matunda yenu, kwa
Jina la Yesu. Amen.
|
Hata sasa, wapo mashetani
waliovaa miili ya wanadamu na wewe bila kujua unahisi ni wanandamu wenzako. Wapo
watu wanaosumbuliwa na majini, na
wanakuwa na mahusiano ya kukutana kimwili na aina hii ya majini mahaba.
Mashetani yanapenda sana kufanya mapenzi na wanadamu, ili kuweza kuwa level moja na wanadamu. Kawaida,
katika ngazi za kiungu, Yupo MUNGU,
halafu WANADAMU waliookoka, halafu MALAIKA, halafu MASHETANI.
Kitu cha kuweza kuwaunganisha watu wawilli ni NDOA… Katika kitabu cha MWANZO 2:24…[ 24 Kwa hiyo mwanamume
atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili
mmoja.]… Ndiyo maana
Mungu amekataza kitendo cha kufanya ndoa nje ya asiye mume/mke wako. Maana yake, katika tendo hilo, wengine wanakutana na kufanya ndoa na majini
bila kujua, na kufanyika kuwa mwili
mmoja nao!!.
1 KORINTHO 6:15-16…[Je! Hamjui ya kuwa
miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya
viungo vya kahaba? Hasha! 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni
mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.]…. Mashetani yanataka kuwa mwili mmoja na wanadamu pale wanapooana nao au
kufanya nao mapenzi. Hapo ndio mwanzo wa uzao kukamatwa. Mtu anapoota ndoto za yeye kufanya tendo la ndoa na mtu/watu asiowajua,
na kujikuta kweli amejichafua, ni kuwa anakuwa amekwisha unganishwa na huyo mtu/jini
katika ulimwengu wa roho. Ujue kuwa mwisho wa yote ni kuzaa watoto katika ulimwengu wa roho.
1 KORINTHO 7:4…[Mke
hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya
mwili wake, bali mkewe.]..
Mashetani wanajua kuwa, yanapopata fursa ya
kuwa mwili mmoja na mwanadamu, yanaweza kuharibu chochote anachokifanya
huyu mwanadamu: Kuharibu biashara,
kuharibu kazi, kuharibu afya, kuharibu masomo na kingine chochote mwanandamu anachokifanya.
Kinachofanya haya yatokee ni kwa sababu mashetani yanaitambua hii kanuni ya kiroho. Jini anapokuwa anammiliki mtu,
anataka kuharibu kila alicho nacho huyo mtu.
Baraka za mtu zipo
ndani ya mtu. Muujiza wa mtu upo ndani ya mtu. Inamaanisha kuwa, huwezi kupata maendeleo
bila kuhitaji wanadamu wenzako. Ni kwa
Kupitia kwa hao wanadamu, unaweza kuinuliwa au kuangushwa chini. Imeandikwa katika
LUKA 2:34….[Simeoni
akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka
na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.]….Ni kuwa Yesu aliwekwa kwa ajili ya
watu kuinuka na watu wengine kuangushwa
chini. Kwa hiyo, kupitia kwa Yesu, wengi
wanainuliwa na wengi wanaendelea kushushwa
hadi leo.
Ibrahimu alipoenda Misri, alimshawishi mke wake asije kumuita ni
mumewe, bali 'mtu na kaka yake', ili asije
kuuawa na Mfalme wa Misri - aitwae Abimeleki. Mungu alimtokea Abimeleki katika ndoto
na kumzuia asifanye jambo lolote na Sara. Hii ni kuonesha kuwa ndoto ni
bayana, na kwamba Mungu anaweza kuzungumza na mtu kwa njia ya ndoto.
MAOMBI:
Enyi mashetani mliokamata uzao wangu, nawatoa nje kwa Jina la
Yesu. Naharibu nguvu zenu kwa Jina la Yesu. Enyi majini mahaba, naharibu
mtandao wenu kwa Jina la Yesu. kwa maana imeandikwa 'tokeni katikati
yao, mkajitenge nao', leo najitenga nanyi kwa Jina la Yesu. Leo
nawapiga mashetani wote na kuwaangamiza,
napiga ndoa za kiroho, kwa Damu ya Mwanakondoo, Kwa Jina la Yesu.
Amen.
|
Endapo wewe hujaokoka, ni
vyema kufanya maamuzi hayo kwa sababu huwezi kuangamiza uzao wa shetani wakati wewe upo mikononi mwake
shetani. Maamuzi ya kuokoka ni maamuzi ya kukuweka salama, ili
uweze kuungamiza uzao wa shetani ukiwa mikononi mwa Yesu Kristo.
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi (Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778