GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI: 22, OKTOBA, 2017
MHUBIRI: MCHUNGAJI.
Dr. GODSON ISSA ZACHARIA
Utangulizi: Tunaposoma maandiko katika Yohana 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa
kumwabudu katika roho na kweli.” Mungu
wetu ni Roho, kwa hiyo hana mwili. Hata
hivyo, ni Mungu mwenye mikono, vidole, macho ana pua ana akili ambayo haichunguziki kwa mujibu wa
neno lake!!!! Musa alimuona Mungu mgongoni, ikimaanisha kuwa kumbe Mungu anao
mgongo. Mungu wetu ambaye ni roho bado neno lake linatufundisha kwamba
ana akili, macho, mgongo, mikono na miguu.
Zaburi 80:15
Imeandikwa, “Na mche ule ulioupanda Kwa mkono wako wa kuume; Na tawi lile
ulilolifanya Kuwa imara kwa nafsi yako.” Hapa tunaona Mungu anatumia
mkono wake kupanda mbegu. Zaburi 88:5 Imeandikwa, “Miongoni mwao waliokufa
nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena,
Wametengwa mbali na mkono wako.”… wametengwa mbali na mkono wako Luka 11: 20 Imeandikwa, “Lakini,
ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha
kuwajilia.” Mitume wa Yesu wanasema wao walitoa pepo kwa kidole cha
Mungu. Zaburi 29:11 Imeandikwa, “Bwana
atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.” Mungu
atawapa watu wake nguvu za roho mtakatifu kwa ajili ya kazi yake.
Mkono wa Kichawi au kishetani, kama
vilevile Mungu alivyo na mikono wakati yeye ni roho vilelvile na shetani ana mikono pia. Kwa
kawaida shetani hakuumba chochote bali anachukua nakala ya uumbaji wa Mungu. Kama
Mungu anaweza kuokoa kwa mkono na shetani naye anaweza kuangamiza kwa mkono.
Kuna mwanadamu ambaye ni mchawi ambaye
akigusa kitu kwa mikono yake, lazima uharibikiwe. Pili anaweza kuwa shetani
akagusa mali zako na ukaharibikiwa. Kuna watu akigusa shamba, biashara au ofisi
yako lazima ukose wateja. Habakuki 2:9 Imeandikwa,
“Ole
wake yeye aipatiaye nyumba yake mapato mabaya, ili apate kukiweka kioto chake
juu, apate kujiepusha na mkono wa uovu!” Mkono wa uovu ndio mkono wa shetani
na mawakala wake mchawi na waganga. Anaweza
kuwa mtu wa kawaida lakini amevuviwa na nguvu za kishetani. Wapo baadhi ya watu
ambao wakikusalimia au wakigusana na wewe kwa kutumia mikono yao basi kuanzia
hapo mambo yako huanza kuharibikiwa. Unaweza
kuwa umeajiriwa ofisi fulani, mfanya kazi mwenzako akaamua kwa mkono wake
akachomoa nyaraka muhimu kwa ajili ya kazi yako ili kazi yako iharibike. Pengine
kuna mtu ambaye ulikutana naye siku moja na akakusalimia kwa kukupa mkono, na tangu
siku hiyo mambo yako yakaanza kuharibika.
Mkono wa shetani au mchawi waweza
kunyooshwa kwenye kazi, biashara, familia au afya n.k. Ndio maaana utaona mtu
anafanya biashara lakini analia kwa sababu hajawai kupata faida. Wengine ameolewa
lakini hajawai kupata mtoto ni kwa sababu kuna mtu alimgusa au amenyoosha mkono
wa kishetani juu ya uzazi wake. Kama Mungu anasema kila tutakapokanyaga ametupa.
Kwa hiyo shetani naye akikanyaga jua kazi, biashara, uchumba, miradi au ujenzi
jua huwezi kufanikiwa.
Majeshi ya Bwana wakisikiliza Neno la Mungu katika ibada ya leo. |
1. MIKONO YA WACHAWI AU WANADAMU
Wanadamu hawa wachawi wanaweza
kukugusa moja kwa moja au kupitia bidhaa. Yawezekana ikawa ni nguo, wigi,
kitenge au suti Fulani lakini kumbe iemenuiziwa manuizo ya kichawi nyuma yake.
Matendo ya Mitume 12: 1-6 Imeandikwa, “Panapo
majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya
watu wa kanisa. Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga. Na akiona ya
kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa
siku za mikate isiyochachwa. Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia
mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na
kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu
kwa juhudi kwa ajili yake. Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule
Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili;
walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza”.
Herode alikuwa ni mwanadamu lakini
alitumia mkono wake kuwatenda mabaya watu wa kanisa. Huyu alikuwa mfalme lakini alinyoosha mkono
ili watu wa Mungu wauwawe. Anaweza kuwa Rais, Waziri, Mbunge, Kaka, dada au
rafiki lakini wakanyosha mkono ili wewe uharibikiwe. Pengine anaweza kuwa ni
mwanadamu lakini akaiandika barua ya wewe kuachishwa kazi, au kufunga biashara
au kusitisha mkataba. Wakati mwingine ukoo au familia wanaweza wakaandika
maagano ambayo baadae yanageuka kuwa matatizo ya kiukoo au familia husika. Pengine
yawezekana ilikuwa ni kwa sababu tu kwa mkono wako ulibeba kuku kwenda kwa
mganga wa kienyeji kipindi kile kabla hujaokoka!!. Wapo watu ambao ukiwapa kubeba
watoto lazima walie sana, ukiona hayo jua kuwa watu kama hao mikono yao ina
uovu ndani yake.
Kazi uliyonayo leo hii ni kuuvunja
mkono wa kichawi kwa jina la Yesu. Leo waendee wachawi kwa nguvu ya jina la
Yesu, Damu ya Yesu na Roho Mtakatifu. Kumbuka kuwa Wewe ni silaha za Bwana za
vita na kwa wewe Bwana atavunja wachawi wazee kwa vijana. Wachawi wamepanda
uovu, mabaya, ajali, magonjwa kama Ukimwi, Kisukari na mengine lakini tumepewa
mamlaka ya kung’oa yote na kuyaharibu kwa jina la Yesu.
2.
MIKONO
YA KISHETANI
Hii ni mikono ya mashetani kama
mizimu, majoka na majini n.k. Ayubu 1:1-3 Imeandikwa, “Palikuwa na mtu katika nchi ya
Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu,
ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana
saba, na binti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia
elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa
nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote
wa upande wa mashariki.” Ayubu alikuwa mtu aliyebarikiwa na Yehova kwa
mali na vitu vingi. Kwa maandiko haya tunauona wasifu wa rohoni wa Ayubu (kwamba
ni mkamilifun na mwelekevu), na wasifu
wake wa wa mwilini (kuwa na mali nyingi, watoto 10 n.k.).
Hata hivyo shetani aliziona Baraka zote
juu ya Ayubu akashikwa na wivu. Ayubu 1:6- Imenadikwa, “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana
wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati
yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana,
na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na
huku humo. Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu
Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na
mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu
Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa
ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za
mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha
mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso
wako”.
Mungu alimzuia shetani asinyooshe mkono
wake juu ya roho yake. Lakini alimruhusu shetani anyooshe mkono wake na kugusa
mali na ustawi wa Ayubu. Kumbe shetani kwa kuwa anayo mikono anaweza kunyoosha
mkono wake juu ya kazi, biashara, shamba au mali ulizonazo na kukuletea
matatizo.
MADHARA YA KUNYOOSHEWA MKONO NA SHETANI.
Ni yapi madhara ya shetani kunyoosha mkono wake na kugusa maisha
yako? Hebu tumuangalie mgusaji (shetani), ambaye anaweza kuingia hata katika
familiayakona kuleta madhara mbalimbali!! Tunaposoma katika AYUBU 1:13-20,
tunaona kwamba:
a) DHARA LA KWANZA: Katika
AYUBU 1:13-15 imeandikwa (Ilitukia
siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika
nyumba ya ndugu yao mkubwa, 14 mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao
ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; 15 mara
Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi
kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.).
Je, huyu mjumbe namba moja wa kuleta taarifa alikuwa kajificha wapi kwa
nini yeye asishambuliwe na hao Waseba? Inawezekana kuwa hata huyu mleta taarifa
ni miongoni mwao.
b) DHARA LA PILI: Katika
AYUBU 1:16 imeandikwa (Huyo
alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu
umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na
kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.). Swali
la kujiuliza: Huyu mjumbe namba 2 naye alijuaje kuwa huo moto ulitoka mbinguni?
Ni lini alienda mbinguni na kuukuta huo moto? Lazima watoa taarifa kama hawa
tuwahoji, kwa sababu yumkini ni miongoni mwa wajumbe wa kishetani wanaowekwa
ili kutoa taarifa mbaya.
c) DHARA LA TATU: Katika
AYUBU 1:17 imeandikwa (Huyo
alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya
vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale
watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea
habari.). Huyu mjumbe namba 3 wa kuleta taarifa naye ni wale wale, kwamba haiwezekani aweze kuliona tukio lote
kuanzia linapoanza hadi kumalizika, na mwishowe apate nafasi ya kupeleka taarifa.
d)
DHARA
LA NNE: Katika AYUBU 1:18 imeandikwa
(Huyo
alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako
walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa;).
Huyu mjumbe namba 4 naye kama walivyokuwa watangulizi wengine, huyu naye siyo mtu, bali
ni wakala wa kishetani. Kwa nini tuseme hivyo? Ni kwa sababu
tunajiuliza, Aliwezaje kujua upepo ulikotokea, na mambo yaliyokuwa mle ndani
kwenye karamu, na je, alijua je kule ndani kwamba hakuna aliyesalimika? Lazima
tugutuke na kuwaaibisha watu wa aina hii, kwa kuwa watu wa aina hii nao ni
sehemu ya hao mashetani.
Showers of Glory Morogoro wakisifu na kumchezea Mungu wakati wa Ibada ya Leo |
Tunajifunza kuwa shetani aliuvaa mwili na kutengeneza matukio
katika nyumba ya Ayubu. Kwa kuitumia
mikono yake, shetani aliweza kugusa vitu vya Ayubu na kuleta uharibifu mkubwa.
Leo tukatae kuguswa na mkono wa shetani, tumkaribie Mungu wetu ili yeye ndiye
ayaguse maisha yetu. Pengine wewe ni mwanandoa, nasasa maisha unayopitia nis
tofauti na maisha uliyoanza wakati mnaanza ndoa. Leo tutaikata mikono ya
wachawi waliogusa ndoa au maisha yako na
kusababisha balaa na migogoro isiyoisha kwa Jina la Yesu.
Leo kupitia sadaka zetu tunamsihi Mungu kwa Agano kwamba Bwana akayazuie
matukio kama yale ya kishetani yasitokee kwetu. Leo tutashambulia mikono ya
akina Herode (wanadamu), na ile mikono ya mashetani wanaotuzuia na kuleta
uharibifu maishani mwetu. Hata hivyo, ni sharti ukubali kuokoka kwanza kwa
maana ya kumpokea Yesu Kristo maishani
mwako.
KWA MSAADA ZAIDI NA
MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/