Sunday, January 14, 2018

KUVUNJA NDOA ZA KISHETANI

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH [GCTC]
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SNP. DR. GODSON ISSSA ZACHARIA
JUMAPILI: 14, JANUARI, 2018

MHUBIRI: SNP. DR. GODSON ISSSA ZACHARIA

Kwa asili Ndoa ni muunganiko wa kudumu kati ya mtu mume na mke na kuwa mke na mume au mwili mmoja.  Mungu alimfunulia mtume Paulo kuhusu ndoa. Mungu alimpa kufundisha na kuonya mengi kwa habari ya ndoa. Mungu anaongelea kwa habari ya mtu kuungwa na mtu mwingine, Kwamba mtu akiungwa na kahaba basi atakuwa mwili mmoja naye. Ndoa za Kishetani ni ndoa zisizoeleweka sana kwa sababu ya watu kutokujua. Lakini ndoa za Kishetani ni ndoa inayofungwa kati ya mwanadamu na mashetani katika ulimwengu wa roho. Imeandikwa, “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.” (1wakorintho 6:16-17) shetani ana uwezo wa kuvaa mwili akamfuata mtu akamtongoza au kumwoa mtu. Ndoa hizi utazijua kwa dalili ya mambo unayoota yakifanyika kana kwamba unafanya mapenzi lakini kwa uhalisia umefanya mapenzi katika ulimwengu  wa roho.
Ndoa ni nini?
Ndoa ni muunganiko wa kudumu kati ya mwanaume na mwanamke na wakawa  mwili mmoja yaani mume na mke. Ndoa ni jambo la kisheria na linatokana na agizo la Mungu kwamba kuwe na ndoa kati ya mume na mke nasivinginevyo. Imeandikwa mwanzo 2:24,“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”  Mungu ndiye mwanzilishi wa jambo la kuwepo kwa ndoa. Neno linaonyesha kwamba Mungu aliona vyema iwepo ndoa. Akasema Adamu awe na msaidizi wake ambaye alikuwa Eva. Ndoa ni taasisi ya muhimu kwa mujibu wa neno la Mungu. Mungu hakusema wawe watu wa jinsia tofauti maana Mungu alikuwa na uwezo wa kusema awe mke kwa mke au mume kwa mume. Kumbe ndoa kati ya watu wa jinsia moja sio ndoa kwa mujibu wa neno la Mungu.  Imeandikwa mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake. Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye. Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.” (Mwanzo 2:18-22)
Baada ya shetani kufukuzwa kutoka mbinguni naye akaanzia jambo la taasisi ya ndoa. Ndoa hizi ni za siri kwa sababu watu hawezi kulisema jambo hili. Hizi ni ndoa za siri kwa sababu tendo la ndoa linafanyika rohoni lakini mtu anajiona kama ndoto.

JE MAMBO HAYA YAPO?
 Neno la Mungu linaonyesha dhahiri kwamba Mungu aliumba wanadamu pamoja na viumbe wengine. Baada ya wanadamu kuongezeka juu ya nchi wana wa Mungu wakaanza kuwaingilia wana wa wanadamu. Wana wa Mungu walianza kuwaingili binti za wanadamu. Neno kuwaingilia maana yake ni kufanya tendo la ndoa kati ya mke na mume. Lakini jambo hili halikuishia kwenye kuwaingilia tu bali walizaa watoto pia. Na watoto wao ndio waliokuwa watu hodari zamani. Imeandikwa mwanzo 6:1-4 “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Nao Wanefili (Wanefili maana yake ni majitu) walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.”  Hawa wanaoitwa wana wa Mungu kwenye agano la Kale ni malaika. Imeandikwa, “wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” (Mwanzo 6:2). Pia neno la Mungu linaonyesha pia katika kitabu cha Ayubu kuwa malaika kwa lugha ya kiebrania ni malaika Imeandikwa “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.” (Ayubu 1:6, 2:1). Kwenye agano jipya wana wa Mungu ni wale waliompokea Yesu. Imeandikwa, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;” (Yohana 1:12)

Kuna malaika wa aina mbili  malaika watakatifu ambao walishangilia wakati wa uumbajii wa Mungu (ayubu38:4-7) na malaika waovu  au walio asi au waliotenda dhambi  na binti  za wanadamu.
Matokeo ya kuingiliana kati ya uzao wa wana wa wandamu na wana wa Mungu ilikuwa ni kuzaa watoto. Watoto hawa ndio watu hodari nyakati hizo.  Malaika Walioasi hawa ndio malaika wa shetani ambao alitupwa nao kutoka mbinguni. Hawa wanawaingilia watu ndotoni ndio malaika wa shetani. Malaika waliotenda dhambi wakati wa Nuhu au walioasi ndio wanaoitwa malaika walioanguka (folen Angels). Imeandikwa Ayubu 38:4-7 “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?  Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?  Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?  Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,  Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,  Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?” (Ayubu 38:4-7)
Malaika wa shetani ndio wale wanaitwa malaika wa giza kwenye neno la Mungu. Neno la Mungu linasema malaika hawa wa giza walifanya uasherati na watu wa Sodoma na Gomora. Kufanya tendo la ndoa kwenye ndoto sio jambo la asili wala halitoki kwa Mungu bali shetani. Basi maneno haya yanaonyesha kuwa ndoa za kishetani zipo.  Ndoa hizi zipo na zinafungwa kwenye ulimwengu wa roho. Imeaandikwa Yuda 1:1-7, “Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo. Mwongezewe rehema na amani na upendano. Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri,  wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini. Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa

Malaika hawa wana tabia ya kujibadilisha maumbo. Malaika aweza kubadilika na kuwa chochote. Malaika waliwahi kumtembelea Ibrahimu lakini wakiwa katika sura au umbo la binadamu. Ibrahimu aliwapokea kama wanadamu lakini walikuwa malaika. Hapa tunaongelea ndoa inayoweza kufungwa na shetani lakini aliyekuja kwako kama mtu kama wewe. Mtu anaweza kukutana na msichana mzuri mpaka kijana anasema mapigo ya moyo yalibadilika ghafla. Anaweza kupendeza kana kwamba hajawai kufanya kazi au hana kovu ni kweli yuko vile lakini zijaribuni roho. Imeandikwa mwanzo 18:1-3 “Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.”

Unaweza kumwona kama mwanaume au mwanamke  mzuri kumbe ni shetani katika mwili. Anaonekana kama mtu na anazo sifa zote. Anaonekana kama mwanaume mwenye mali na anao moyo wa kujali sana. Anaweza anafanya hayo yote lakini si kwamba ni mtu bali ndani yake ni joka. Ndoa za kishetani ni janga la watu wote wa mataifa yote.
DALILI AU ATHARI ZA NDOA ZA KISHETANI.
MADHARA KWA MTU AMBAYE HAJAOA AU HAJAOLEWA
i)             Kama ni mwanamke hapendi wanaume hata mara moja. Akitokea mwanaume anataka kumchumbia binti, utasikia maneno ya huyu binti haijuzu dunia kuyasikia. Hawezi kukaa au kufanya kazi na wanaume. Wadada wanakuwa na maneno ya kutisha, mfano mdada mmoja alikuwa akisema yeye mwanaume akimsumbua lazima atammwagia maji ya moto. Mdada Mzuri lakini haolewi. Maana yake huyu amevalishwa vazi la uzee ili mashetani waweze kumtumia kimapenzi. Haya yote yanatendeka kwa sababu ya ndoa za kishetani
ii)            Kama ni mwanaume, hapendi kukaa na wanawake. Huyu tayari ana jini jike wa ndotoni. Majini haya yanasababisha cijana wengi kuchelewa kuoa. Kwa hiyo kijana huyu hawezi kuoa. Hata akichumbia lazima baadae atakuwa na sababu ya kufanaya uchumba uvunjike.
iii)           Kama ni Mwanamke, anakuwa na maumivu makali wakati wa Hedhi. Mwanamke anasikia maumivu kabla na wakati wa hedhi kiasi ambacho dawa zote haziwezi kumfanya apone. Hii ni kwa sababu yapo majini yanasimamia ndoa.
iv)           Kuvunja Uchumba. Kijana ipo ndoa na cheti cha ndoa kwenye ulimwengu wa roho, akianzisha uchumba lazima uvunjike. Na utakuta anayevunja ni Kijana mwenyewe. Hii ni kwa sababu yupo mume au mke wa kiroho anayehakikisha ndoa yake ya rohoni haiwezi kuingiliwa na mtu mwingine.
v)            Anavunja au kuharibu vitu vyake mwenyewe. Awe mke au mume lazima awe na tabia ya kuharibu vitu au mali zake mwenyewe bila sababu. Hii ni kwa sababu kuna mke au mume wa rohoni. Hata ni mashetani yanayosabaisha vurugu kwenye familia. Ni kazi ya shetani kuharibu vitu vya watu. Anaweza kuwa mfanyakazi mzuri na mwenye umahili katika kazi hiyo lakini anaamua kuacha. Imeandikwa,Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
vi)           Anatabia ya kuacha vitu. Anaweza kuwa kijana mahili wa ushonaji  lakinianaamua kuacha bial sababu za msingi. Mtu huyu anaacha kazi ili Yule mume au mke wa rohoni amfanye huyu kuwa mtegemezi wake.

KWA WALE WENYE NDOA.
i)             Huwa Anakosa Furaha wakati wa Tendo la Ndoa.  Awe mke au mume lazima ajisikie maumivu makali sana wakati wa tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu yupo mke wa rohoni anayezuia isiwepo furaha kati ya wanandoa ili yeye ammiliki vizuri kwenye ulimwengu wa roho. Na utakuta mke au mume anaota anafanya tendo la ndoa na afurahia sana.
ii)            Unahisi kumpenda mwenzio akiwa mbali. Mtu mwenye ndoa anakuwa na hasira mwenzi wake akirudi nyumbani. Lakini mume au mke akiwa mbali ndo ulalamika kumhitaji. Hii yote ni mifumo ya ibilisi ambayo Yesu alikuja ili kuivunja. Imeandikwa, “atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” (1 Yohana 3:8)
iii)           Anakuwa Mlevi. Mwnaume anapandikizwa roho ya ulevi ili apoteze ule moyo wa uwajibikaji katika fsmilia yake. Lakini pia mtu akilewa sana na pombe ikawa sehemu ya maisha yake hawezi kufanya tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu kuna mwanamke au mume wa rohoni.  Kumbuka lengo la ndoa za kishetani ni kutaka kuvunja ndoa za mwilini.
iv)           Roho ya kushindwa. Huwezi kufanya jambo ukafanikiwa. Kila unachoanza lazima kiishie njiani, iwe kazi, biashara, shule lazima hawezi kufanikiwa. Ukipata mtu wa kukusaidia lazima aondoke kabala hajakusaidia au anakufa kabla msaada wako haujawa timilifu.  

KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: Pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro       http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/


Share:
Powered by Blogger.

Pages