Sunday, January 21, 2018

MAOMBI YA KUVUNJA NDOA ZA KISHETANI

GROLY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO

SNP DR. GODSON ISSA ZACHARIA

JUMAPILI: 21 JANUARI 2018

MHUBIRI: MCHUNGAJI: JOYCE GABRIEL (SNP DUMILA)

(MILANGO INAYOMPA NAFASI MME AU MKE WA KIROHO)

Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akisisitiza jambo kabla hajamkaribisha Mchungaji Joyce Gbriel.
Ndoa ni muunganiko wa maisha yote kati ya mwanaume na mwanamke unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii. Ndoa huwa inawafanya waliokuwa wawili kuwa mtu mmoja. Ndoa huwa inampa mtu uwezo wa kumiliki kile ambacho hakikuwa haki yake kabla ya ndoa. Lakini shetani naye bado anaweza kuwa na ndoa na wanadamu. Ndoa za kishetani ni jambo linalowapata watu wa dini na kabila zote. Lakini ijulikane kuwa shetani hawezi kummiliki mtu isipokuwa mtu amefungua mlango fulani. Ipo milango ambayo inamfanya shetani aanzishe ndoa za kishetani kati yake na wanadamu. Ifuatayo ni baadhi MILANGO;
i)                   Kupitia Ulinzi kwa waganga wa kienyeji. Kuna wakati watu wanapokwenda kwa waganga wa kienyeji kupewa ulinzi. Lakini kinachoitwa ulinzi huwa ni malaika wa shetani ambao kwa mujibu wa neno la Mungu hawa ndio walioamua kuwaingilia wana wa wanadamu. Kwa hiyo anakuja kama mlinzi lakini anaamua kujimilikisha kama mke au mme wa kiroho.
Mchungaji Joyce Gabriel akiwa katika uwepo wa Bwana
ii)                 Kucheza ngoma za Kimila.  Kila kabila lina taratibu zake. Mfano kwa watu wa Pwani wana taratibu za kumtoa mwali. Kwa hiyo kupitia sherehe hizo kuna mambo fulani yanafanyika kwenye ulimwengu wa roho. Kuna sadaka zinatolewa ambazo zinasababisha watu kuungamanishwa na mashetani. Katika sherehe hizi watu wanatoa kafara ya damu ambayo inasababisha mashambulizi . kupitia vyakula na vinywaji katika sherehe  vinawaungamanisha watu na  mashetani  pasipo kujua. Matukio haya yanampa shetani kuwamiliki watu kama mke na mme kwenye ulimwengu wa roho. Imeandikwa 1Wakorintho 10:20-21Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.”   
iii)                Matendo ya Uzinzi na Uasherati. Jambo hili limekuwa jambo la kawaida hata kwa waliookoka. Anaweza kuwa ni kijana lakini ana wapenzi au mke au mme wa mtu lakini anamiliki nyumba ndogo.  Miili yetu ni hekalu la Mungu na Roho Mtakatifu. Kwa kufanya uzinzi na uasherati ni mlango ambao shetani anawamiliki watu kwa kasi sana. Kumbuka Mungu anatuonya kwamba zinaa haikemewi bali sharti uikimbie.  Si wote wazinio walitaka kwa hiari yao, bali wengi kwa sababu ya roho ya uzinzi walijikuta wameungana na mashetani. Mashetani yanatengeneza ndoa ili waweza kuzaa kwa ajili ya kuzimu. Ndio maana ndoa zilizokumbana na mashetani hawa lazima ziwe na ugomvi siku zote.  Wanagombana kwa sababu kisa mmoja wao ana wapangaji kutoka kuzimu ndani yao. Imeandikwa 1Wakorintho 6:15 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!”.
Baadhi ya Makutano wakisikiliza neno la Mungu wakati wa Ibada ya leo.
Tabia za uzinzi na uasherati ni chanzo cha migogoro katika ndoa. Kila mtu kabla ya ndoa aliyonayo leo alikuwa na wapenzi wengi na wote aliungwa pamoja naye.  Chunga  sana tabia zako na mienendo yako. “Amani ya ndoa yako itategemea sana namna ambavyo wewe ulianza. Kwa hiyo namna ya kumaliza kwako itategemea sana na namna ulivyoanza. Kumbe ni heri uanze na Bwana na umalize na Bwana”.  Kataa kuwa kahaba kwa jina la Yesu. Amua kujikana leo na ujitie bidii kumtafuta Mungu, nawe utakuwa imara kwa jina la Yesu. Maana kwa kumtafuta Mungu utaishinda roho ya ukahaba. Imeandikwa ``Ufunuo wa Yohana 17:1-2 “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.”
Watu walio kwenye ndoa za kishetani hawawezi kufanikiwa katika maisha yao. Watu hawa ni msukule katika ulimwengu wa roho. Nndio maana talaka ni nyingi katika dunia ya sasa. Kumbe wengi waliovunja ndoa zao si kwamba walitaka, bali ni kwa sababu yapo mashetani walio sababisha ugomvi kati yao. Watu hawa hawajawai kufanya kazi na ikazaa matunda. Akianza biashara, kazi, mradi au shule hawezi kufikia mwisho wa jambo hilo.  
Mama huyu akifunguliwa kutoka vifungo vya Ndoa za Kishetani.
iv)              Kurithi Mikoba ya Uchawi ya Ukoo. Kila aliyerithi huwa anapata haki juu ya mambo yote. Kila aliyerithi mambo ya familia au ukoo huwa anarithi na miungu ya familia na koo husika. Mtu anaweza kuwa anaonekana kama mwanadamu lakini ndani yake ni mashetani. Ndio maana mtu alioa kwa tamaa zake, lakini baada ya kuanza ndoa ni vita kubwa. Hii ni kwa sababu ndani hao wanaoonekana ni wazuri lakini ndani yao wamejawa mashetani. Imeandikwa 2 Wakorintho 12:2 “Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.”
v)                 Zawadi. Kuna vitu unaweza kupewa na vikageuka na kuwa mlango wa kukuletea matatizo, hasa chanzo cha ndoa za kishetani. Tabia ya kupenda vitu vya kupewapewa mara nyingi vinagharimu sana maisha ya watu. Yawezekana ilionekana kama zawadi lakini ndani yake imebeba mauti. Kuna mtu aliwai kupewa ua zuri na usiku wake akaota mtu anakuja na ni mzuri kama lile ua alilopewa asubuhi. Mwangalie Bwana awezaye kukupa vyote vya mwilini na rohoni. Achana na tabia ya kujipenda kuliko Mungu. Maana watu wengi wameibiwa na kuolewa kwa sababu ya kupenda vitu vya duniani. Litumikieni kusudi la Bwana lililo ndani yako.
vi)               Mavazi. Wengine wametekwa kwa sababu ya mavazi na stahili za kuvaa. Mavazi yanachukua sehemu kubwa ya kuwafanya watu wamjue au wamkatae Mungu. Wengine wametekwa kwa sababu ya kuomba au kuazima nguo za wenzao. Nguo nyingine zina manuizo ya mashetani ndani yao. Mwingine amepatwa na mabaya kwa sababu nguo aliyovaa imezoelewa na mashetani na kila wakimwona usababisha mabaya kwake. Kumbe kwenye nguo za kuazima unaweza kuazima na matatizo ya mmiliki wa nguo. 
Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akimfungua mtu kutoka ndoa za kishetani
Chunguza maisha yako ni wapi ulifungua mlango mpaka shetani akakuingilia. Mabaya huja kwa sababu ya kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Shetani hawezi kukuvamia isipokuwa umemfungulia mlango. Amua kumrudia Mungu maadamu anapatikana.  Tengeneza na Bwana, tubu maana Mungu anapenda roho ya toba na hapendezwi na kiburi cha uzima.   
                                    ======== AMINA ========
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/




Share:
Powered by Blogger.

Pages