Sunday, January 28, 2018

VIUMBE WA KIROHO NA MATUKIO YA KICHAWI

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH [GCTC]

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

SNP. DR. GODSON ISSSA ZACHARIA

JUMAPILI: 28, JANUARI, 2018

MHUBIRI: MCHUNGAJI, AMOS KOMBA (SNP MTWARA)

Mchungaji Kiongozi Dkt. Godson Zacharia akisikiliza neno la Mungu.

Uchawi ni roho chafu inayotokana na shetani. Kwenye Biblia neno mchawi limeandikwa mara nyingi. Mchawi ni mtu au watu wenye roho za uchawi ndani yao. Wanaitwa wachawi kwa sababu ndani yao kuna roho ya uchawi ndani yao. Mchawi akiona, akitembea, akikaa na kila anachokifanya nyuma yake kuna roho ya uchawi. Wanadamu wote ni roho ambao wanakaa ndani ya nyumba inaitwa mwili. Chochote anachokifanya ndani yake kuna roho inamsukumiza kufanya hivyo. Ndio maana Mungu anasema usimwache mwanamke mchawi kuishi.

“Usimwache mwanamke mchawi kuishi.”   Imeandikwa Kutoka 22:18.

 “Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.” Imeandikwa, Mambo ya Walawi 20:27

Mungu anasisitiza wachawi hawatakiwi kusamehewa wala kuwaonea huruma. Na hutakiwi kubebea jiwe katika ulimwengu wa mwili bali utumie upanga wa rohoni. Hii ni vita ya rohoni wala si vita ya mwilini. Inawezekana umefika hatua ya kuolewa lakini mchawi akasema hutapenya (ukafika Pafo). Inawezekana kuna matukio yanakupata kumbe ni matukio ya kichawi. Kuna hatua uliyotakiwa kuifikia ila hujafika kwa sababu kuna wachawi wametuma upepo wa kukurudisha nyuma.

Mchungaji Amos Komba akifundisha neno la Mungu.
Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.”  Imeandikwa, Matendo ya Mitumi 13:6-11

Hapa tunaona BarYesu alikuwa akishindana na akitaka kutia imani ya kuicha ile imani. Mtume Paulo alikuwa amejawa na Roho Mtakatifu ili apate uwezo wa kushindana na BarYesu akamkazia macho. Inawezekana kuna mtu au rafiki anatembea na wewe lakini akawa na roho ya uchawi anapotosha njia ya haki.

Viumbe na matukio ya kichawi. Hakuna uchawi kama hakuna viumbe wachafu. Wachawi wanapata nguvu kutoka kwa shetani kwa sababu kuna viumbe wachafu.

“Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Imeandikwa, Wakolosai 1:16

Hapa Biblia inatudhihirishia kwamba kuna viumbe mbinguni na dunia vipo pia. Kuna viumbe vinavyoonekana na visivyoonekana. Viumbe visivyoonekana ni pamoja na Mungu, Roho Mtakatifu havionekani ni kwa sababu ya asili yake. Pia shetani ni kiumbe asiyeonekana ingawa hakuwa shetani hapo mwanzo alikuwa malaika baada ya kuasi ndipo akatupwa shimoni.
baadhi ya Makutano wakifuatilia neno la Mungu wakati wa Ibada.
Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.” Imeandikwa, Ufunuo wa Yohana 20:1-3

Sehemu ya shetani ni kuzimu. Ulimwengu wa roho na mwilini una kanuni. Na ndio maana ikifika jioni watu wanaenda kulala na s kazini. Na ulimwengu wa roho una kanuni pia. Makao ya shetani ni kuzimu wala sio ndani ya mwili wa mtu au kazini kwako.

“Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.”  Imeandikwa, Isaya 14:9

Inawezekanaje shetani yupo nyumbani kwako, au tumbo unatakiwa umwambie shetani mahali pake ni shimoni. Kuna wakati mwingine anahama kuzimu anakuja kwenye ulimwengu wa mwili. Kwenye Biblia tunasoma Mungu huwafanya malaika zake kuwa pepo (upepo). Maana yake malaika awe wa nuru au wa giza anaweza kujigeuza na kuwa upepo. Si kila upepo ni upepo, na si kila kimbunga ni kimbunga.
Maana yake ni kwamba upepo wa shetani uambatana na laana, mikosi na balaa zote. Na upepo wa Mungu uambatana na Baraka, mafanikio, kuongezeka, afya na ustawi.

Platform Ministry wakiongoza  nyimbo za sifa na kuabudu katika ibada ya leo.
“Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali.” Imeandikwa, Zaburi 104:4

“Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.” Imeandikwa, 2 Samweli 22:10-11

Mungu aliruka kama mabawa ya upepo. Kumbe Mungu anaweza na aliwai kuufanya upepo kuwa mbawa na kwazo akaruka.

Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya nchi ya Misri kwa hao nzige, ili wakwee juu ya nchi ya Misri, waile mimea yote ya nchi, yaani, vyote vilivyosazwa na ile mvua ya mawe.  Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige. Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo.”   Kutoka 10:12-14
Upepo huu ulileta nzige, hapa tunajifunza kuna upepo unavuma kuleta ugonjwa, au kuleta vitu katika ulimwengu wa mwili. Ndani ya upepo unaweza kuleta vitu.
“Kisha upepo ukavuma kutoka kwa Bwana, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao ukawaacha wakaanguka karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, na kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, kuizunguka, nao wakafikilia kiasi cha dhiraa mbili juu ya uso wa nchi.” Hesabu 11:1
kila upepo unamahali unapotokea, upepo huu ulivuma ukaleta kware pande za baharini walianguka karibu na kambi kwa mwendo wa siku moja. Huu upepo ulileta chakula. Unawezaa kuamuru upepo ulete amani kwenye ndoa yako, maisha yako. Inawzekana unafanya biashara lakini unapata hasara kumbe kuna pepo imevuma.
“1. Ikawa, hapo Bwana alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha. 11. Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.2 Wafalme 2:1,11
Upepo ulivuma kama gari la moto, kama farasi, upepo wa kisulisuli ulimbeba Eliya mpaka mbinguni. Tunajifunza kwamba upepo unaweza kuwatenganisha watu na watu wao. Wachawi wanaweza kutuma upepo uje kukubeba ukakutupe kwenye matatizo.  Upepo unaweza ukabeba nyota ya mafanikio na hatima yako.
“Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari. Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari. Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakaamka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?Luka 8:22-25
Kuna mahali unatakiwa kuvuka ila huwezi kwenda kwa sababu kuna Baraka zako kule. Yesu na wanafunzi wake walikuwa wanavuka kwenda ng’ambo walipanda chomboni Yesu alilala usingizi, wakiwa wanavuka upepo ukavuma wanafunzi walimwamsha Yesu. Kilichokuwa kinataabishwa ni chombo, chombo hicho kilitakiwa kikuvushe mpaka ng’ambo. Chombo ni kifaa kinachoweza kukuvusha wewe. Inawezekana ndoa yako ndio chombo, shule ndio inataabishwa, ndio inayotakiwa ikufiishe ng’ambo.
Ukiri: Kuanzia leo kwa jina la Yesu kila pepo iliyotumwa kwangu kunitaabisha, kunikwamisha, kunipindisha, kunichelewesha, leo nakunyamazisha kwa jina la Yesu. Ewe mwongozaji wa upepo, unayeongeza mwendo wa upepo nakuapisha kwa jina la Yesu.
Mchungaji Amos Komba akimwokoa mtu kutoka nguvu ya upepo wa kishetani.
“Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukingo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.” Ayubu 1:6-12
Shetani alituma matukio, lakini alipogusa nyumba yake alianguka na kurarua mavazi yake.
“Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.” Ayubu 1:18-19
Upepo ulivuma wa nguvu na umetokea jangwani, na kwani nini jangwani ni kwa sababu jangwani ni shimoni. Jangwa lina nguvu ya kuzuia/kutatanishwa vitu vya rohoni. Wacahawi kwa nanmana ya kafara wanaouweza wa kuita mapepo na kuyageuza yakawa upepo wakayatuma kwenye maisha yako. Haya ni matukio ya kichawi, leo sema na upepo, upepo una akili na masikio nao utatii.
NAMANA YA KUSHINDA MATUKIO YA KICHAWI
1.       Kuokoka; ni kwa sababu ukiokoka unapewa uwezo (unapewa mamlaka) wa kufanyika kuwa watoto wa Mungu. Ukiwa mtoto wa Mungu unapata sifa ya kulindwa na malaika wa Mungu. Zaidi unakuwa na nguvu ya kuyaamuru mashetani na yakakutii.

“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.” Yohana 1: 12-13.

“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;” Marko 16:15-17

2.       Mamlaka; Ni ile hali ya kuwa na uwezo na nguvu ya kutenda. Unaweza ukaamini usiwe na mamlaka, wanafunzi wa Yesu walikuwa wameokoka. Neno la Mungu linasema naye Yesu aliwaita wale Thenashara akawapa amri (mamlaka). Tembea, omba na ongea kwa mamlaka nao upepo utakutii kwa jina la Yesu.
Mchungaji Dkt. Godson Issa Zacharia akiwafungua kutoka matukio ya kishetani.
“Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” Mathayo 10: 1

Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; ” Marko 6:7
Kuitwa ni kuokolewa, na hii amri ni mamlaka. Ukiomba tumia mamlaka. Omba kwa mamlaka maana wewe ni mwana wa Mungu.

3.       Maombi ya Kushindana; haya ni maombi ambayo ni vita ya rohoni. Wewe unatakiwa uombe ushindane na ule upepo. Upepo wa usaliti ulishavuma mbinguni mpaka nao wakashindana wakamtupa shetani nje. Na wewe ili kushinda unatakiwa kushindana na vita inaanzia kwenye ulimwengu war oho na hatimaye utashinda na mwilini.
“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;” Ufunuo wa Yohana 12:7
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro       http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/


Share:
Powered by Blogger.

Pages