Tuesday, February 13, 2018

MIMI NA NYUMBA YANGU TUMEHAMA TOKA UFALME UHARIBIFU

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

MHUBIRI:MCHUNGAJI DKT. GODSON ISSA ZACHARIA

Mchungaji Kiongozi Dkt. Godson Issa Zacharia akifundisha kuhama toka ufalme wa uharibifu.
Hakuna shujaa yeyote anaye weza kukaa kwenye ufalme wa uharibifu, ndio maana Mungu anataka leo tuhame toka kwenye ufalme wa uharibifu kwa jina la Yesu.
Hapa duniani kuna falme mbili zinazo fanya kazi pamoja, na falme hizi mbili zinapingana usiku na mchana yaani hazina maelewano.
A. Ufalme wa Mungu
B. Ufalme wa Uharibifu / Ufalme wa giza
Ufalme wa kwanza ni UFALME WA MUNGU, huu ni ufalme halali ambao watu wanakaa ndani yake na hauwezi kutikisika, yaani ni ufalme usio tetemeshwa. Huu ni ufalme halali kabisa na Mungu ndio mwanzilishi wake na yeye ndio alio uleta hapa duniani, maandiko yanatuweka wazi kwenye Luka 11:2, "Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]"
Utaona hapa Yesu anasema Ufalme wako uje hapa duniani, ndio maana nina kila sababu ya kusema ufalme huu wa Mungu upo hapa hapa duniani, hapa sizungumzii ufalme wa Mungu mbinguni hapana maana mbiguni yupo mtawala wake ambaye ni Yehova mwenyewe ambaye ndie Mungu aliye ziumba mbingu na nchi.
Ufalme uliombwa kutoka mbinguni na ukaja kutoka mbinguni. Hapa duniani tunapoishi uraia wetu si hapa bali ni mbinguni ni kwa sababu mtu ni roho na anakaa kwenye nyumba ambayo ni mwili na alipuliziwa pumzi kutoka mbinguni. Wafilipi 3:20 imeandikwa "Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo";
Mfano mzuri ni ubalozi, wa Marekani wanaweza kuja Tanzania na wakaweka ubalozi wake huku na huo ubaolozi unafanya kazi kama vile serikali ya marekani ifanyavyo, hivyo ukiuvamia ubalozi wa malekani ni sawa umevamia nchi ya marekani. Wamarekani wana ufalme wao wakitaka kuja Tanzania wanatengeneza ubalozi. Na sisi ni mabalozi hapa duniani kwenye ufalme wa Mungu wetu, na ufalme wetu haunaga destuli ya kutikisika.

Ufalme wa Mungu ni ufalme usiotetemeshwa (unshakeable kingdom), utaona kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Waebrania 12:28 "Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho"
Lakini ufalme mwingine wa pili uliopo duniani ni UFALME WA UHARIBIFU ambao ni ufalme wa shetani, ufalme huu ni ufalme batili (hauna kibali) yaani mtu amejiapisha mwenyewe tofauti na katiba ya ufalme yaani ufalme hauna kibali. Shetani yeye anajiita mfalme lakini ufalme wake ni wa kuzimu. Ni ufalme ambao haujaruhusiwa na aliyeumba mbingu na nchi. Ni ufalme unaofanya kazi hapa duniani. Ufalme huu ni wa wizi. Mfano wa kibinadamu; huko Kenya kuna raisi aliyepishwa kihalali na amethibitishwa kuongoza nchi hiyo, lakini akijitokeza mwengine aliyejiapisha naye akajiita raisi hajathibitishwa wala hana kibali cha kuongoza ni sawa na ufalme huu wa uharibifu.
Tena ufalme huu batili una weza ukawa na washirika wengi kwa sasa kwa sababu ile njia ya kuelekea uzimani ni nyembamba lakini ile ya kuelekea uharibifu, uzinzi, kuiba ni njia pana sana, na watu wengi wanaipita pasipo kujua ila leo lazima tuhame kwa jina la Yesu..Mathayo 7:13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Kila ufalme unaye mfalme, huwezi kuwa na ufalme bila kuwa na mfalme, Yohana 10:10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. hapa utaona falme hizi mbili, mmoja ni mwizi yaani mwaribifu lakini mwingine yeye anataka watu wawe na uzima kisha wawe nao tele, uta gundua maneno haya hayajasemwa na mtu mwingine ila ni Yesu mwenyewe ndio aliye yasema haya maneno. Yesu anatoa mchanganuo hapa kuwa duniani kuna falme mbili mmoja ni mwaribifu lakini na mwingine ni wa uzima, hivyo shetani ndie mfalme wa uharibifu na Yesu ndie mfalme wa uzima.
Pia utaona shetani ni mfalme wa kuzimu, Ufunuo 9:11 "Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni".
Kuna watu wapo kanisani kwa ajili ya kupokea tu na kuruka ruka tu hii haikusaidii sana ndio maana nataka uijue kweli kwanza ili kweli ikuweke huru kwa jina la Yesu. Unaweza ukawa bado unaegelea na ku-operate kwenye ufalme wa uharibifu bila wewe kujua ni bora upate kuijua kweli leo kwa jina la Yesu. Yohana 8:32 "tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru".
1. UFALME WA UHARIBIFU
Shetani ndio ibilisi na ana majina mengi, Abadoni maana yake mwarabu, destroyer, hivyo shetani mfalme wa uharibifu, ndio maana leo nataka uhame kwenye ufalme huu, na anaye weza kukuhamisha kwenye ufalme huu ni Yesu pekee sio mimi Mchungaji wala mama mchungaji ila ni Yesu anaye weza kukuhamisha kupitia kinywa changu au cha watumishi wa Mungu wengine, na mimi kama kuhani wa mahala hapa lazima uhame kwa jina la Yesu.
Hapa maandiko yanasema mimi na wewe tuliye amini tumepita toka mautini, yaani unaye umwa nakutangazia leo umepita kutoka mautini na kuingia uzimani kwa jina la Yesu. 1Yohana 3:14 imeandikwa "Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti".
UKIRI
KWAJINA LA YESU MIMI NIMEPITA TOKA MAUTINI NA KUINGIA UZIMANI, BIASHARA YANGU, NDOA YANGU, KAZI YANGU, AFYA YANGU, WATOTO WANGU, FAMILIA YANGU IMEPITA TOKA MAUITI NA KUINGIA UZIMANI KWA JINA LA YESU.
Mtu yeyote lazima akiri maneno hayo, sasa kwenye kuhama pale utamsikia mtu anasema mimi sio mgonjwa, nina amani yaani niko vizuri kwa hiyo siko kwenye ufalme wa uharibifu au giza au kishetani, unajindanganya wewe mwenyewe, kuna vitu vinaendelea katika ulimwengu wa roho ambavyo wewe huvioni, kuna mambo yametengenezwa, kuna mauti juu ya kazi, watoto, ndoa yako, kibali chako, miradi yako, hilo duka lako n.k, ndio maana ni muhimu kuhama kila mtu kwa jina la Yesu.
Utawaona wana wa Israeli walikaa Misri miaka mingi 430 lakini Mungu alipo amua kuwatoa walitoka, lakini Mungu akawaambia waambieni Farao na wamisri wawape mali, msiondoke mpaka mpewe bali, kumbe unapo amua kuhama kutoka mautini ni lazima uhame na mali zako, fedha yako, watoto wako kwa jina la Yesu.
Kuna mtu ninamwona biashara yake ipo mautini, kazi yake ipo mautini, ndoa yake ipo mautini, familia ipo mautini lakini leo nina hihamisha itoke mautini kwa jina Yesu.
Utaona maandiko matakatifu yanasema "Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani."Yohana 5:24 .
Aliye mpelekaYesu ni Mungu Baba wa Mbinguni, nini maana yake, ni kwamba ukisikiliza neno lake na kuliamini na aliyempeleka hakika utapita kutoka mautini na kungia uzima. Kuna binadamu wapo duniani ambao maisha yao yamekwisha kufa na wana enjoy lakini bila wao kujua na hawajui kama maisha yao yamekufa. Unaweza ukawa unatembea lakini umekufa, ndio maana bibilia inasema tumekuwa wafu kwa wingi wa makosa yetu. Efeso 2:1-2 imeandikwa "Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi"
Yesu anasema umepita au umevuka, maana yake kama ni mtu umepanda boti au ndege ndivyo ilivyo na kwa wale ambao wapo kwenye ufalme wa giza leo Yesu anataka akuvukishe utoke huko kwenye mauti na uingie kwenye uzima kwa jina la Yesu.

Unaweza ukawa umeokoka lakini upo kwenye ufalme wa magonjwa, umaskini, shida, mikosi, balaa nuksi ndio maana Mungu amenituma leo nikutoe kwenye ufalme huu kwa jina la Yesu.
Huyu mfalme wa giza ni mvuvi mwovu, anavua mpaka mimba za watu, watoto wachanga, anavua vijana kuwa wazinzi, ndio maana mimi nataka wewe uwe shujaa ili tupige kwa pamoja kwa jina la Yesu, mimi simpendi kabisa huyu maana ndiye anaye wachukua watu mashimoni, mashambani, kuzimu ila mimi leo nawaita kwa jina la Yesu njoooooo kwa jina la Yesu.
Utaona katika Isaya 42:22. "Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha"
Mfalme huyu haitaji makubaliono ya aina yeyote, haitaji negotiation wala mapatano kwa habari ya kuwarudisha watu, bali ukigundua yupo wewe anza kumpiga kwa jina la Yesu, shetani alipigwa mbinguni na akatoka (Ufunuo 12:7-9), na wewe unatakiwa uombe mpaka kieleweke. Ndiyo maana sisi tunasema PUSH (yaani PUSH- PRAY UNTIL SOMETHING HAPPENS) usikubali kuacha kuomba hata kama unaona unaumwa, ndoa imevunjika, watoto hawana ada wewe undelea kuomba mpaka Bwana akujibu kwa jina la Yesu.
"Ufunuo 12:7-9 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye".
Shetani huwa haridhiki kabisa, Nchi ya Tanzania ni nchi iliyo barikiwa sana, madini yapo, mbuga za wanyama zipo, mashamba yapo, rasiliamali watu wapo lakini bado nchi inaomba misaada, mimi sishangai maana nyuma yupo mwaribifu amekaa hapo, ili tufanikiwe lazima tumpige huyu kwa jina la Yesu. Ndio maana kuna sababu ya kuwaombea hawa viongozi wetu tokea Rais mpaka mjumbe wa nyumba kumi ili Mungu awape maarifa ili waamke na walete maendeleo kwa mkoa wetu na Tanzania kwa ujumla kwa jina la Yesu.
Tumuagalie huyu mfalme wa uharibifu asiyependa kuwaacha wafugwa wake kwenda kwao, yaani kwenda kwenye baraka zao, mitaji yao, ndoa zao kwa jina la Yesu, imeandikwa Isaya 14:17 "Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwmmoja UKIRI
SEMA KWA JINA LA YESU, WEWE SHETANI ULIYE PANGA VITA JUU YA RAIS WETU, MAWAZIRI, MKUU WA MKOA, WAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI, NA VIONGOZI EOTE, LEO NASAMBRATISHA KILA KAZI ZA KUZIMU KWA JINA LA YESU, ACHIA VIONGOZI WETU KWA JINA LA YESU, NAFUNGA KILA SILAHA ZILIZO FANYIKA JUU YAO SILAHA ZA MAUTI, AJALI, MAGONJWA KW JINA LA YESU.
Ufalme wa uharibifu una makao makuu matatu, Baharini, nchi kavu, na angani, zote hizi ni kuzimu, na huko kuna vitengo mbalimbali, hivyo lazima leo tuzipige kuzimu zote hizi kwa jina la Yesu, kuzimu hizi zina magereza ,na ndani ya ufalme huu kuna master plan iliyo tengenezwa na mfalme wa kuzimu au mfalme wa uharibifu, nani asiolewe au asioe, nani afe, nani avunjike mguu, nani waachane au nani achukuliwe msukule.
Kuna miji iliyo jaa damu, ambayo mfalme wa uharibifu ameijenga, na ndani ya miji hiyo kuna mijeledi, mizoga, mateso mengi, ndio maana nataka leo tufanye vita kwa nguvu kwa jina la Yesu. Ndani kuna mateso mengi, ndani ya ufalme huu kuna uchawi, magonjwa kila aina ya mateso yamejaa, Mungu hapendi kuona watu wanateseka ndio maana amenituma leo nikutoe kwenye miji hii ya mateso kwa jina la Yesu.
Nahumu 3:1-4 "Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki. Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka; mpanda farasi akipanda, na upanga ukimeta-meta, na mkuki ukimemetuka; na wingi wa waliouawa, na chungu kubwa ya mizoga; mizoga haina mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao. Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake".
Ufalme wa uharibifu umejaa hila, hila ni udanganyifu, mtu una pata ujauzito kabla huja jifungua mtoto anakufa, au amezaliwa lakini baada ya mwezi mmoja unasikia degedege mara anakufa, hizo ni hila za ibilisi, anapanga maovu juu ya familia yako, mitaji yako inaliwa, ndoa inaliwa, mahusiano yanaliwa, au unazalishwa kabla ya ndoa kupia hizo hila mambo yako yaka haribika, lakini leo Yesu atakusaidia kwa jina la Yesu.
Matendo ya mitume 7:18-19 imeandikwa "hata mfalme mwingine akainuka juu ya Misri, asiyemfahamu Yusufu. Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi."
Unakura unalala na kuota ndota za ajabu ajabu na ndoto hizo zikaharibu maisha yako, umejaribu kuuliza kwa watu lakini watu hawajakusaidia, ndugu hawajakusaidia, mwangalie Hana alikuwa na shida ya mtoto yeye hakuamua kukimbilia kwa ndugu ila akakimbilia Shilo na alipo fika akamimina moyo wake kwa Bwana na Bwana akamjibu hitaji la Moyo wake, wewe, acha kukimbilia kwa watu kimbilia kwa Yesu naye atakusaidia kwa jina la Yesu.
Ufalme huu wa uharibifu baba yao ni muongo, huyu ibilisi ni muuaji ndio anachinja maisha ya watu, usiwalaumu bodaboda eti wanapata ajali sana la hasha, mfalme huyu anaweza kuingia ndani yao na mwaribifu huyu kuanza kutengeneza mauti. Yohana 8:44 "Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo."
Mchungaji Kiongozi Dkt. Godson Issa Zacharia akifundisha katika nyumba ya Ufufuo na Uzima

Inawezekana upo hapa lakini hauna furaha, mke na mume hamna furaha, masomo yana yumba yumba lakini nakutangazia uhuru wako leo kwa jina la Yesu. Ndani ya ufalme huu kuna wizi, misuko suko, taabu, shida na kila aina ya mateso, Kuna watu wana fukuzwa kazi lakini ufalme wa giza umetengeneza, ufalme huu ndio unao iba akili kumbe kuna mfalme wa uharibifu yupo ametulia mahali fulani leo nakutoa kwa jina la Yesu.
WAKAZI WA UFALME WA GIZA/UHARIBIFU
Wakazi wa ufalme huu wamejwaa na baadhi ya mambo kama yafuatayo:
- Magonjwa, hii ni kwasababu huyu anahari afya za watu, hapendi watu wawe na uzima
- Wamejawa na taabu, mtu ametaabika bila sababu, anapata nafuu leo kesho taabu ipo palepale
- Wamejawa na umaskini, mtu unamkuta ame okoka lakini ni maskini na kusema nataabika kwa jiili ya Yesu, huu ni uongo maana Mungu hapendi tuwe maskini, Mungu wetu ni nitajiri sasa huu umaskini umetokawapi?
- Wakaazi wa ufalme huu wamejawa na majuto, mtu anajuta kwa nini amezaa watoto wavuta bangi, kwanini mimi nimeolewa
- Wakazi wa falme huu wamejaa kukatailiwa.
- Wamejaa mikosi, kila kitu kwao ni mikosi tu, ukianza jambo halifanikiwi
- Wamejawa na kuchukuliwa misukule, watu wana kufa bila sababu yoyote ile, mimba zinatoka bila sababu
- Wakazi wa ufalme huu wamejawa na vifo vya gafla
- Wamejawa na huzuni, humwoni mtu akicheka hata mara moja, ni mtu wa huzuni kila siku hana furaha. Isaya 53:4 imeandikwa, "Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa'
- Wakazi wake wana chuki sana, utamsikia mtu anasema hata nikifa sitaki aje kwenye kaburi langu, yaani chuki imetawala ndani ya moyo wake, Yaani ndani ya ufalme huu ukianza jambo halifanikiwi
2. UFALME WA MUNGU
Huu ndio ufalme halisi ambao Bwana aliuleta toka mbinguni, huu ndio ufalme tulioubwa toka mbinguni, na ufalme huu ni ufalme ambao hautikisiki kwa jambo lolote lile, ndani ya ufalme huu ukienda sawasawa na kanuni, sheria na tamaduni za ufalme basi;
- hakuna kufilisika,
- hakuna kiu wala njaa maana mtawala wake ni Mungu mwenyewe
- Kwenye ufalme huu kuna uzima wa milele. Waebrania 12:28 imeanikwa, "Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;"
WAKAZI WA UFALME WA MUNGU USIOTETEMESHWA.
Kwenye ufalme huu kuna Mungu Baba, Malaika watakatifu, mkutano mkuu wa kanisa la kwanza walio tangulia, Roho za watu walio tangulia, Yesu mjumbe wa agano jipya. Hawa ndi wajumbe wa ufalme usio tikisika au kutetemeshwaa kama ilivyo andikwa kwenye
WAEBRANIA 12:22~28 "Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni; ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia. Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae. Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho"
- Ufalme huu kanuni yake hakutakiwi watu wake na wakazi wake wawe na magonjwa Kutoka 23:25 imeandikwa "Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako."
- Ufalme huu hakutakiwi kuwa na mateso wala huzuni Maombolezo 3:33 "Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha".
- Kwenye ufalme huu hakuna taabu na mikosi
- Ndani ya ufalme huu kuna hatma zetu zote
- Ndani ya ufalme huu Mungu ameshatuwekea Master plan hata kabla ya sisi hatujazaliwa, Yeremia 1:5 "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa".
- Ufalme huu unapanga mipaka ya kumiliki kwako,
Mwanzo 12:1-3 "Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa'.
- Ndani ya falme kuna Baraka nyingi Kumbukumbu 11:26 imeandikwa, "Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana."
- Ndani ya ufalme huu kuna utajiri, hapa sio utajiri wa kiroho ila ni utajiri wa kimwili,kuna mwingine anasema uwe maskini ili uingie mbinguni, lakini mtume Paulo anasema 2 Wakoritho 8:9 "Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake"
- Ndani ya ufalme huu watu wake ni baraka kwa watu, yaani ukifanikiwa wewe jamii yako imefanikiwa pia, Ibrahimu baba yetu wa Imani alikuwa na mali nyingi sana hivyo na sisi lazima tumiliki mali na kizazi chetu kibarikiwe kupitia sisi lakini sasa hatuna mali kwasababu shetani amefunga na kujimilikisha leo.
Wagalatia 3:14 imeandikwa " ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani"
Sasa inawezekana umeokoka lakini unaishi ndani ya ubalozi wa uharibifu badala ya kuishi ndani ya ubalozi wa ufalme wa Mungu, ndio maana nataka leo tuhame ndani ya ubalozi huu wa giza au wa kishetani kwa jina la Yesu. Ufunuo 5:9-10 imeandikwa "Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi". Kumbe wewe ni uzao wa kifalme.
1Petro 2:9 imeandikwa "Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu"
Dunia hii kama tulivyoona kuwa shetani ni mungu wa duniahii, sasa shetani anaweza akakuhamisha toka kwenye umiliki wako na kukuingiza kwenye madeni, ambapo mtu anatakiwa akaishi Marekani lakini leo mtu anaishi manzesekwa mfuga mbwa, yaani anaishi maisha duni kwasababu shetani amefunga na kupindisha maisha ya mtu, ndio maana leo nataka tuhame kwa nguvu kwenye ufalme wa giza kwa jina la Yesu.
2Wakoritho 4:4 imeandikwa, ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Kwenye kuhama hapa hahuitaji majadiliano na mke au mume, baba, au mama, au watoto lazima uamue wewe mwenyewe na kwa ujasiri wote kwa jna la Yesu.
Wakolosai 1:13 imeandikwa Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.
SASA KIRI MANENO HAYA
Baba Mungu katika jina la Yesu kristo wa Nazareth, nakupokea ndani ya Moyo wangu uwe Bwana na mwokozi wa maisha yangu, kuanzia leo namkataa shetani na wafalme wake wote kuyatawala maisha yangu kwa jina la Yesu.
Pastor Dr. Godson Issa Zacharia
Ufufuo na Uzima - Morogoro
Share na watu wengine !
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogorohttp://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/
Share:
Powered by Blogger.

Pages