Sunday, April 22, 2018

KAFARA YA DAMU


GLORY OF CHRIST TANZANNIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFO NA UZIMA MOROGORO
PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 22 APRILI 2018
MUHUBIRI: MOSES CHAMI (MP)
Mchungaji kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia.

Utangulizi:
Kafara ni aina ya sadaka ya damu. Kwa asili Damu ni uhai. Kafara ni neno lililozoeleka kusikika kwenye maisha ya wanadamu. Kafara ni silaha inayotolewa kwenye madhabahu ya wachawi, waganga wa kienyeji na wale wamtumikiao shetani. Neno Kafara limeandikwa zaidi ya mara 20 katika Biblia. Damu ni uhai na damu inapomwagika mahali popote ujue kuna uhai umetolewa. Neno Damu limeandikwa zaidi ya mara 500 kwenye Biblia.

“Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake;  Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake,  Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.” Kumbukumbu la Torati 32:43

“Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. Ndipo watakapotoa ng'ombe Juu ya madhabahu yako.” Zaburi 51:19
Kafara na damu ni vitu vinavyoendana kwa pamoja. Ili kafara iwepo ni lazima damu imwagike. Iwe ni kafara ya mbuzi, ng’ombe au mtu lazima damu imwegike.

“Nitaingia nyumbani mwako na kafara; Nitaondoa kwako nadhiri zangu.” Zaburi 66:13
Hapa tunaona Daudi anamwambia Mungu ataingia hema mwake kwa kafara. Katika Agano lake watu walikuwa wanaingia na kafara ya wanyama ili kumba msamaha kulingana ukubwa wa dhambi aliyotenda.
Mchungaji Moses Chami akifundisha neno la leo kuhusu kafara ya Damu na namna inavyoweza kufunga maisha ya mtu.

“Kafara za vinono nitakutolea, Pamoja na fukizo la kondoo waume, Nitatoa ng'ombe pamoja na mbuzi.” Zaburi 66:15
Ili kafara iwepo ni lazima damu imwagike.

“Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu;  Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu;  Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.” Muhubiri 5:1
Damu inapomwagika kuna maneno yanazungumzwa. Kafara ya upumbavu ni sadaka inayotolewa na vitu vidhoofu au viwete au vipofu. Unapotoa kafara walitakiwa wapeleke, wanyama ambao hawajawahi kuzaa.

“Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo.” Muhubiri 2:9
Kuna tukio moja limebaki ambalo kwa Yule atoaye kafara na asiyetoa kafara. Kuna baadhi ya watu wanasema hawana haja ya maombi, mwingine anasema hajui kafara. Lakini kuna tukio moja limebaki nalo ni mauti.  Kuna wengine wa upande wa giza wanatoa kafara ili wafanikiwe.

“Lebanoni nayo hautoshi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara.” Isaya 40:16.
Hapa tunajifunza wanyama wanatolewa kama kafara. Unaposikia ujue kuna mnyama, damu au binadamu anaongelewa na kutolewa kama kafara.

“Hukuniletea wanakondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.” Isaya 43:23.
Tunaona neno kafara limeandikwa mara nyingi, leo tutajifunza kwa habari ya kafara ya damu ili tupige hatua tena kwenye maisha yetu. Haitoshi kujua neno kafara bila kujua matumizi na madhara yake.

Damu imeandikwa kwenye Biblia “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]*. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.” Mwanzo 4:8-10. Hapa tunajifunza Abel na Kaini walienda kumtolea Mungu sadaka, sadaka ya Abel Mungu aliitakabili na sadaka ya Kaini Mungu aliikataa. Kaini alimwonea wivu na alimwuua ndugu yake na damu ilimwagika.
Makutano ya Bwana wakijifunza neno la leo kuhusu Kafara ya Damu.

Tabia ya damu
·         Damu inaweza kulia.
·         Damu ina sauti. Hakuna kulia kama hakuna sauti.
·         Damu inaweza kulaani. Hapa tunajifunza ardhi ililaani kwa kuwa ilifungua kinywa chake na kupokea damu ya Abeli. “Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;” Mwanzo 4:11.
.
·         Damu inalipa kisasi. Tunaona pilato alijua damu inaweza kulipa kisasi alipomuhukumu Yesu yeye alinawa mikono na kusema damu ya mtu huyu haitakuwa juu yangu. Bali watu wa Israeli wakasema Damu yake Yesu iwe juu yao.
“Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.” Mathayo 27:24.

·         Damu inaweza kufuata. Damu ikimfuata huwa inatabia ya kuhukumu. Inamfanya adui ajisikie hatisa moyoni mwake. Petro aliulizwa je hatukuwakataza msifundishe kwa jina hili. Inawezekana unachukiwa ni kwa sababu ya jina ulilobeba ndani yako. Waliwakataza kwa sababu wanakumbuka damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani inauwezo wa kuwafuata. Kwa jina la Yesu naagiza damu ya Yesu ifuate biashara yako,ndoa yako, kazi kwa jina la Yesu.

“Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.” Matendo ya mitume 5:27-28. Yesu Kristo alifanyika kafara akaja uimwenguni kutukomboa wanadamu na dhambi zetu. Yesu alishuka chini na kujinyenyekeza na kuja dunia ili kutukomboa na dhambi zetu.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16.

“na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.” Waebrania 12:24
Damu ya Abili ilikuwa inanena na ndugu yake afe. Lakini damu ya Yesu ni damu ya agano jipya inanena mema. Damu ya Yesu inene mema katika maisha yako, kwenye kazi, familia, ndoa, biashara yako kwa jina la Yesu.

Damu ni uhai, damu inapomwagika mahali popote ujue kuna uhai umetolewa. Unapoona damu inawezekana mnyama ametolewa uhai, au binadamu.
“Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama.” Kumbukumbu la Torati 12:23
Mungu alitoa tahadhari usile damu. Unapokula damu ya mnyama au kituchochote ujue unatembea na uhai wa mnyama au kiumbe hicho. Mfano kama umekunywa damu ya mbuzi, uhai wa mbuzi umeingia ndani yako. Ndio maana unaweza kuona mtu anatenda kama kuku, mbuzi au ng’ombe. Inawezekana unapata shida katika maisha yako ni kwa sababu ulishawahi kunywa damu ya mnyama.

Mungu anakasirika akiona mwanadamu ameuwawa. “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Mwanzo 1:28. Hapa tunajinfunza asili ya mwanadamu ni mavumbini au ardhi. Damu inapomwagika kwenye ardhi damu inaanza kuongea. Inawezekana umeenda kwa mganga wa kienyeji akifanya kafara anafajia katika ardhi. Na damu ikimwagika inaanza kuongea.

“Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.” Mwanzo 9:4
Damu ya mtu ni uhai. Unapomwaga damu ya kitu nawe tarajia kumwaga kwa jina la Yesu. Kama ulishawahi kumwaga damu, leo kuna damu ya mjumbe mpya wa agano jipya itanena mema kwa jina la Yesu. Inawezekana ulishawahi kuchanjwa chale sehemu ya uhai wako upo kwenye madhabahu ikinena uharibikiwe, ushindwe lakini leo tuna damu ya Yesu inayonena mema. Yesu akinyamazisha ya kale yamepita kuna mapya yanaanzishwa tena, kazi mpya, inaanza, ndoa mpya.
Platform Team wakimsifu Mungu katika ibada ya leo.

Aina za damu.
Ø  Damu inayonena mema. Hii ni damu ya Yesu mjumbe wa agano jipya.
Ø  Damu inayonena mabaya, damu ya abili ilikuwa inanena mabaya. Damu zote hizi mbili zina sauti. Damu inapomwagika mahali popote inatengeneza uhai. Na anayepeleka damu anakuwa na dhumuni la kukuharibia maisha yako. Kuna mwingine anamwaga damu ili mambo yako yasiendelee mbele.

Ni vizuri usimwage damu ya kitu chochote bila sababu.
 “Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.” Mwanzo 9:6 Kwa anayemwaga damu na yeye damu yake itamwaga. Inwezekana wewe ni mwanafunzi na ulishawahi kutoa mimba umemwaga damu kwa kukusudia. Leo unatakiwa umwambie Yesu akusamehe na uinyamazishe kwa jina la Yesu.

Kafara ni kutoa kitu chenye damu, ni kutoa uhai wa kiumbe chenye damu ndani yake. Unapoenda kwa mganga wa kienyeji anataka kuku, mbuzi, ng’ombe hivi ni viumbe vyote vina uhai na damu. Mganga wa kienyeji hajawahi kutaka tikiti maji au fanta au kitu chekundu bali wanataka viumbe vyenye uhai na anacholenga ni damu. Mganga anapochinja huwa anaongea maneno kwa lugha za kiarabu, damu inapomwagika  mashetani yanatoka kuzimu kuja kunywa damu na kusikiiza damu inataka nini ili waweze kutekeleza.

Kafara ya damu inaweza kutolewa na;
 Ndugu wa karibu: kafara inaweza kutolewa na ndugu wa karibu anaweza kuwa mama, baba au ndugu ili apata kitu chenye faida kama utajiri. Waganga wa kienyeji huwa wanagiza viumbe vyenye uhai mfano, kuku/mbuzi/ng’ombe au binadamu ili damu imwagike. Inawezekana umeenda kwa mganga wa kienyeji ili akusaidie na akakuambia umtotoe mtoto wako wenye akili sadaka na ulipokataa akakuambia utakufa wewe na wewe umeamua umtoe mwanao. Ndugu yako anajua maisha yako vizuri, unapenda chakula gani, unaongozana na nani, mipango yako ya maisha au maendeleo yako.

 Rafiki wa kaaribu: inawezekana kuna rafiki yako wa karibu anataaka kukutoa kafara.  Lakini leo nakuenga na rafiki yako, naweka uadui na marafiki zako wabaya kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yeu najitenga na marafiki abaya leo kwa jina la Yesu.

Mfanya biashara au mfanya kazi mwenzako: kwenye ofisi zetu za erikalini zinaongoza kutoa kafara. Inawezekana umeenda kwenye ofisi upo karibu na bosi lakini kuna mwingine hafurahi mahusiano yako na boss na anaamu kwenda kwa mganga. Ukiri kwa jina la Yesu nabatilisha kafara iliyologa akili yangu kwa jina la Yesu. Kila aliyetoa kafara mfanyakazi mwenzangu ufyekwe kwa damu ya Yesu. Wafanyakazi wenzako wanatoa kafara ili ushuke cheo na wao wapande.

Bosi au Kiongozi wako kazini: bosi anaweza kukuona unafanya kazi vizuri kuliko wengine. Inawezekana umepata kazi kwingine wanakulipa vizuri ila unakataa ni kwa sababu umetolewa kafara usiondoke.
Watu walikubali kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao ili waipokee damu yake inenayo mema iliyomwagika pale Calvary.

Kwenye Biblia kuna kafara nyingi ziliwahi kutolewa. Kafara ya utawala: ili uweze kutawala ni lazima utoe kafara ya cheo. Mfano viongozi wetu wa serikalini wanatoa kafara. Kuna baadhi ya wabunge wamekaa zaidi ya miaka 20 lakini hawana maendeleo waliyoyaleta kwenye majimbo yao.  

Joshua alisema na alaaniwe yeye atakainuka na kuujenga ukuta wa Yeriko na afiwe na mzaliwa wake wa kwanza na wa mwisho aliye mdogo. Inawezekana kuna watu wamekujengea ukuta wa Yeriko kwenye maisha yako, ukuta wa magonjwa, ukuta wa umaskini kwa laana ileile na atakayeinuka kukujengea ukuta tena apatwe na laana ile kwa jina la Yesu. Baada ya miaka mingi kuna mfalme aliinuka na kuutaka mji wa Yeriko na akasema yupo tayari kutoa kafara kwa ajili ya utawala wake.
“Naye Joshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.” Joshua 6:26

Mfalme Hieli Mbetheli, alifiwa na mwanawe Abiramu mzaliwa wa kwanzakwa kujenga msingi wa Yeriko. Na aliweka malango yake kwa kufiwa na mzaliwa wake wa mwisho Segubu. Kuna watu wanaweza kutoa kafara ya mbuzi ili aanze kujenga msingi wa magonjwa. Yeyote atakaanza kujenga msingi wa magonjwa afiliwe na mzaliwa wa kwanza.
 “Naye Joshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.” 1 Wafalme 16:34.

“Basi Wamoabi wote waliposikia ya kuwa wafalme hao wamekwea ili kupigana nao, walijikusanya pamoja, wote wawezao kuvaa silaha, na wenye umri zaidi, wakasimama mpakani. Wakaamka asubuhi na mapema, na hilo jua likametameta juu ya maji, na Wamoabi wakayaona yale maji yaliyowaelekea kuwa ni mekundu kama damu. Wakasema, Ndiyo damu hii; bila shaka hao wafalme wameharibika, wamepigana kila mtu na mwenziwe; basi sasa, enyi Wamoabi, nyara hizo! Hata walipokuja matuoni kwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata wakakimbia mbele yao; wakaendelea wakiwapigapiga Wamoabi hata kwao. Wakaibomoa ile miji; wakatupa katika kila mahali palipo pema kila mtu jiwe lake, wakapajaza; wakaziziba chemchemi zote za maji, wakaikata miti yote iliyo mizuri; mpaka katika Kirharesethi tu wakayasaza mawe yake; ila wenye kombeo wakauzunguka wakaupiga. Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.”  2 Wafalme 3:21-27.
Mchungaji wa Mungu akimfungua mtu aliyekua amefungwa katika vifungo vya kafara ya damu

Huyu ni mfalme wa Moabu alikuwa anapigana vita na wana waisaerli. Waizrael wakawakata wanyama na kuweka damu kwenye maji. Wakapanda ili kupigana nao lakini walipopanda kupigana na wana wa Israeli wakapigwa wakakimbia. Ndipo mfalme wa Edomu akamtoa mzaliwa wake wa kwanza sadaka juu ya ukuta. Wana wa Izraeli wakapatwa na hasira kuu wakondoka. Kafara ilipotolewa vita ikaisha.

Kuna nguvu nyuma ya kafara yoyote inapotoewa. Nguvu hiyo itatenda kazi kulingana na malengo aidha kwa wema au kwa ubaya. Kama kafara imetolewa kwenye madhabahu ya giza ni lazima wafanikiwe kwa sababu mashetani yanamfanikisha haraka sana. Inawezekana umehangaika sana kutuma maombi ya kazi hujafanikiwa kwa bahati nzuri umefanikiwa kuitwa kazini lakini wewe unajisikia kuacha. Kuna kafara imetolewa ili ikulaze usingizi.
Showers of Glory wakicheza na kumsifu Mungu baada ya kafara ya damu kuny'amazishwa kwa jina la Yesu 

Kafara ya Damu inatolewa wapi?
·         Kafara inatolewa kwenye madhabahu. Madhabahu inawezekana ni ya waganga wa kienyeji au wachawi. Kafara inaweza kutolewa kwenye maingilio ya kuzimu, malango ya kuzimu yanaweza yakawa baharini, kwenye mito mikubwa au kwenye makutano ya maji au kwenye misutu minene.
·         Kafara hizi zinatolewa kwenye milima mirefu, mfano mlima Kilimanjaro, mlima Uluguru.

KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro


Share:
Powered by Blogger.

Pages