JUMAPILI:
04 MAY 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo la leo ni Damu ya Yesu juu ya Watesi wangu. Tangia Agano la Kale, kila aina ya kafara iliyofanyika Damu
ilitumika. Ndiyo maana hata sasa, wachawi na waganga wa kienyeji wakitaka kufanya kazi zao za uharibifu huhitaji
damu, aidha ya wanyama kama kondoo, mbuzi, kuku n.k.
WAEBRANIA 9:22….[Na katika Torati karibu vitu vyote
husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.]… Pasipo
kumwaga damu hakuna ondoleo lolote. Katika damu ndio kuna ukombozi wote. Damu inatakiwa
imwagike ili mtu awe salama. Adamu na Eva walipotenda dhambi, Mungu mwenyewe alimchinja
mnyama na kufanya ile ngozi ya yule mnyama iwe vazi kwa ajili yao.
Makuhani waliagizwa pia kuchinja wanyama kwa ajili ya kuwapatansiha watu na Mungu baada ya watu kutenda dhambi. Damu ilipomwagika, iliwapa uwezo wa kusogea mbele za Bwana. Jambo hili endapo lingeendelea, si ajabu leo hii wanyama wasingekuwepo tena, kwani wanadamu wanatenda dhambi mara kwa mara. Ndiyo maana Yesu alimwaga damu yake mara moja tu ili kafara zote za kumwaga damu za wanyama zikome mara moja.
Katika
dunia hii wanasayansi wamekuwa na uwezo mkubwa sana kufantaya tafiti na
kugundua mambo mengi sana. Hata hivyo
hayuop hata mmoja aliyeweza kugundua DAMU au kutengeneza DAMU.
TABIA ZA DAMU
- Damu ina uhai ndani yake. WALAWI 17:11….[Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami
nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa
ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya
nafsi.]…. MWANZO 9:4…
[Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake,
msile. 5 Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila
mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu
nitataka uhai wa mwanadamu.]… Hii ina maanisha kwamba, kwa kuwa
uhai u ndani ya damu, ndiyo maana
wanasayansi wameshindwa kutengeneza damu, la sivyo wangeweza kutengeneza uhai pia.
- Damu ina Sauti.
- Damu inanena / au
ina uwezo wa kuongea. WAEBRANIA
12:24…[na
Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko
ile ya Habili.]
- Damu inaweza kulia…. MWANZO 4:10…[Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako
inanililia kutoka katika ardhi.]… Kwa hiyo Mungu alisikia sauti
ya damu ya Habili ikilalamika, “Mungu nimeuawa bila sababu”. Yawezekana uliwahi
kumwaga damu ya mtu, kwa kujua au kujua. Damu hiyo inalia hata sasa. Yawezekana
uliwahi kutoa ujauzito kipindi Fulani. Yawezekana ulishiriki kumpa binti
ujauzito na wewe ukatoa fedha ili afanye abortion (kutoa mimba). Damu zote
hizo zinalia hata leo. Yawezekana ulikuwa
na cheo na ukakitumi hicho cheo kwa naman ambayo mtu fualni
alipoteza maisha yake kwa sababu yake.m damu ile inalia hata leo. Kwa sababu
ulimwaga damu ambayo Mungu alisema nitaitaka.
- Damu inaweza kutamka laana. MWANZO 4:11…[Basi sasa,
umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya
ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake;
utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.]… Yamkini zipo
laana zinaendelea kukupata wewe kwa sababu ya damu za aina hii. Au ipo
damu iliyomwagwa na wachawi ili
kukulaani wewe.
- Damu ina uwezo wa kufuata. Damu yaweza kufuatilia
kutoka ukoo mmoja hadi mwingineie,
familia moja hadi nyingine, kizazi
kimoja hadi kingine au hata taifa moja
hadi jingine. MATHAYO 27:24….[Basi Pilato
alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji,
akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu
ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.]…
Katika
Biblia zimetajwa damu za aina kubwa mbili tu (WAEBRANIA 12:24):-
(a)DAMU INENAYO MABAYA…. Hii
hulinganishwa na ile damu ya Habili. Ni damu
inayomwagika pasipo haki. Inatamka mambo mabaya. Damu ya aina hii inmmwagwa na
wandamu katika madhabahu za kichawi. Jina la kitu ni kiyu chenyewe. Endapo hii damu inaitwa damu ineneayo mabaya
basi ujkue kuwa ni damu iletayo mabaya. Mteja wa mganga wa kienyeji akienda na
shitaka lake, huambiwa atoe kafara ya
mnyama. Damu ya mnyama huyu ikeshamwagika mashetani huitumia kutimiza dhamira
ya kumwagika kwake (Labda, Fulani asizae/asiolewe/akataliwe/asipate kazi n.k).
Katika Biblia, adui wa mtu ni wale wa nyumbani kwake. Kumbuka Yesu alisalitiwa
na Yuda Iskariote. Daudi alisalitiwa na Absalom mtoto wake wa kuzaa. Mungu alisalitiwa
na Lucifer, aliyekuwa mwimbaji wa sifa maarufu
mbinguni.
(b)
DAMU INENAYO MEMA…..
Hii ni damu ya Yesu iliyomwagika kwa ajili yako na mimi.
Baba (SNP) Dr. Godson Issa Zacharia akihubiri Jumapili hii tarehe 4/5/2014 katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima-Morogoro. |
YOHANA
15:5-6. [Mimi
ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa
sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa
ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa
motoni yakateketea.]…
MAOMBI: Kwa Damu ya Yesu, ewe damu yoyote iliyomwagwa kwa ajili yangu, damu inayotaja uharibifu na mabaya juu yangu, leo nakushinda kwa
Damu ya Yesu.
WARUMI 8:19…[ Kwa maana viumbe
vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa
maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa
sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; 21 kwa kuwa viumbe vyenyewe
navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie
katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. 22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe
vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa.]…
Damu za wanyama hata kama ni kuku, mbuzi n.k ikimwagwa katika madhabahu za
kichawi, huendelea kulia kwa sababu ilimwagwa BILA HATIA. Ndiyo maana Mungu mwenyewe akateremka duniani na kumwaga damu
yake mwenyewe. Hii ndiyo inaitwa Damu ya Agano Jipya / Damu ya Mwanakondoo. Ilimwagika
msalabani na inanena mema. Damu hii hata leo
itamwagika kwa ajili yako kwa Jina la Yesu. Ni damu inayosikia, inaishi, inanenna mema,
inafuata, ni kiboko wa Ibilisi na inanyamazisha damu zingine zote.
UFUNUO 12:11… [Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na
kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.]..
i. Damu ilimwagika pale Gethsemane. Damu
hii huwashinda mashetani yote yanayopindisha mapenzi ya Mungu ili yatimie
maishani mwako.
ii. Damu ilimwagika mgongoni mwake. Ina uwezo wa kushinda aina zote za magonjwa
yote yaliyopo duniani, yale ya kuambukiza na yasiyoambukiza, familia na yasiyo
ya kifamilia.
iii. Damu iliyomwagika mikononi
mwake. Kupitia damu hii unaweza kuweka mikono yako mwahali popote na
afya iaktoea.
iv.Damu iliyomwagika
miguuni mwa Yesu. Damu humfanya mtu awakanyage majoka na nge kwa kuwa tunao
uwezo na mamlaka hiyo tulikabidhiwa.
v. Damu iliyomwagika kichwani mwa Yesu. MWANZO 3:16… [Akamwambia
mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa
watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 17 Akamwambia Adamu,
Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao
nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu
utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia,
nawe utakula mboga za kondeni; 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata
utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe,
nawe mavumbini utarudi.]… Laana
ya kukosa, uchungu, umaskini n.k.
ilianzia hapa. Laana ya uchungu ilianzia hapa. Ndiyo maana akina mama
wanapata uchungu kila wakati. Ikumbukwe
kuwa siyo ule uchungu wa kuzaa (labour
pain). Yesu ilibidi avalishwe taji ya miiba ili kuifuta laana hii.
vi. Damu ya Yesu iliyotoka ubavuni mwake na maji. Ni damu pekee ya Yesu
iliyomwagika baada ya Yesu kufa msalabani. Damu hii ilishinda mauti. Imeandikwa "Ku wapi kushinda kwako ewe mauti".
MATHAYO 27:24-25…[Basi Pilato
alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa
mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu
mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe. 25 Watu wote wakajibu wakasema,
Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.]… Pilato tofauti
na watesi wa Bwana Yesu, alijua kuwa damu yamtu ina uwezo wa kufuata. Ndiyo maana
alinawa mikono yake, ili damu hii isiyo
na hatia isimfuate yeye wala watoto wake.
MATENDO 4:1-2…[ Hata walipokuwa
wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, 2
wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo
wa wafu. 3 Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha
kuwa jioni. 4 Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu
ya watu waume ikawa kama elfu tano. 5 Hata asubuhi wakubwa na wazee na
waandishi wakakusanyika Yerusalemu, 6 na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na
Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu. 7
Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi
mmefanya haya? 8 Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu,
akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, 9 kama tukiulizwa leo
habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, 10 jueni
ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa
Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina
hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. 11 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na
ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. 12 Wala hakuna wokovu
katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu
walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. 13
Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na
elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja
na Yesu. 14 Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno
la kujibu. 15 Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao,
16
wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao
Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana. 17
Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu
awaye yote kwa jina hili. 18 Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala
kufundisha kwa jina la Yesu. 19 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba
ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
20 maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.]… Ndiyo maana Nyumba
ya Ufufuo na Uzima tunaamini katika ufufuo wa wafu hata sasa. Kwamba aliyekufa
na kuzikwa au kabla ya ya kuzikwa anafufuliwa mahali hapa katika Jina la Yesu.
MATENDO 5:28…[akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu,
msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho
yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.]…Utaona kuwa, wachawi, wasoma
nyota, waganga wa kienyeji wanaogopa sana kulitaja Jina la Yesu. Haikuwepo sababu ya kuuliza “kwa
jina hili?” bila kulitaja ni jina la nani.
Leo tunalipeleka
Jina la Yesu kokote kwenye madhabahu za kichawi, wasoma nyota, waganga wa
kienyeji n.k ambako damu ya wanyama iliwahi
kumwagwa kwa ajili yako ili kukulaani.
==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==