Sunday, July 6, 2014

USHUHUDA - This is My Story - Mwajuma (Tangeni)

 JUMAPILI  06.07.2014
Mwajuma akihojiwa na SNP Dr. Godson Issa Zacharia,
leo 06 Julai 2014 katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro. 

UTANGULIZI: Siku ya Jumatano (2 Julai 2014) wakati wa ibada, Mwajuma alirudishwa msukuleni, baada ya maombi ya muda mrefu sana kumuita katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima -Morogoro. Mwajuma ni binti wa miaka 24 aliyekuwa anaashi Tangeni. Alikuwepo mtu huko  kijijini alimuoa (katika ulimwengu wa roho) akiitwa Faisari na kuishi naye shimoni kwenye mji ambao upo chini ya ardhi huko Tangeni, maeneo ya Mzumbe – Morogoro. Mwajuma anasema kuwa Ndani ya huo mji kuna watu wengi  sana kupita hata idadi ya waumini wote hapa Kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro. Haya yote yalitokea wakati Mwajuma akiwa darasa la 3. Alizaa naye watoto 25. Watoto 3 walikufa na 22 wapo hai hadi leo.   

Swali: Watoto hao 3 walikufa kufa je? Akielezea kisa cha watoto wake watatu kufa, Mwajuma anasema ilitokea siku ambapo watoto hao 3 walidumbuikia kwenye maji, baada ya yeye kuwadodosha kwenye mto mkubwa alipokuwa anakimbia. Ilikuwa siku ambayo yeye na wenzake walikuwa wanaenda kumchukua mtu mmoja msukule lakini wakashindwa kufanya hivyo, na walipokuwa wanakimbia ndio huo  mkasa ukatokea.

Alivyorudi kule mjini (kuzimu) kwa Mkuu wao, Mwajuma aliulizwa watoto wako wapi? Naye akajitetea lakini hata hivyo akapewa adhabu kwa kitendo kile. Hata hivyo, alijapata mtoto mwingine, huyu alimng’ata ziwa lake ambalo hadi leo lina matatizo na uvimbe. Watoto wake wote kwa sasa wametawanyika baada ya Mwajuma kurudishwa. Mtoto wake wa  kwanza kwa sasa yupo  daraja la Ruvu,  akisababisha ajali na kuzamisha watu/wavuvi  majini eneo lile. Mtoto wa 2 anazunguka maeneo ya stendi ya Msamvu – Morogoro na barabara ya Dodoma kusababisha ajali. Mtoto wa 3 yupo barabara ya Iringa, kabla ya geti la Mikumi. Anapindua magari na kusababisha ajali, ndiyo kazi yake.

Akielezea kuhusiana  na unyonyeshaji maziwa kwa hao watoto, Mwajuma anasema “Maziwa ya mtoto hayatoki kama haya ya kawaida”.

Mwajuma anasema alipokuwa kuzimu alijulikana kama “Mwangili”,  kwani ilikuwa ni lazima kubadilishiwa jina. Chakula kinachoitwa “mbaarato” ndicho walichowalisha hao watoto wao, mfano wake ni mchangagnyiko wa viazi mviringo, damu ya mnyama kama njiwa au paka na mafuta ya watu waliouawa. Mtoto akinywa mchanganyiko huu hukua haraka sana hata kwa siku moja inatosha. Paka wa kule kuzimu huenda mahospitalini kuchukua watoto wachanga kuwafanya supu ya kuzimu. Mwajuma anasema,siyo kila paka unayemuona ni paka,kwani wengine ni wale wanaotaoka kuzimu kwa kazi maalumu.  Anasema “Mama anapojifungua na mwanae akifa, huchukuliwa. Wazazi wake huenda kuzika gogo wakidhani ni mtoto wao kumbe siyo”. Miongoni  mwa ajali ambazo Mwajuma aliwahi kuzisababisha ni ajali ya watu waliokuwa wakienda mashambani hapa Morogoro, njia ya kwenda Dodoma,  na iliua watu wengi sana, lakini anshuhudia leo kuwa siyo kwamba wale wote walikufa, bali wengine walipelekwa kule kule kuzimu.

Swali: Wewe umesema una umri wa miaka 24, iweje  useme ulipata watoto 25? Uliwazaa je? Mwajuma anasema “Watoto wa kule kuzimu huzaliwa hata ndani ya wiki moja, siyo miezi 9 kama wanandamu wa kawaida. Hawa watoto hawaafanani na wanadamu, kwani upande wa usoni huwa sehemu ya kisogoni”.

Swali: Mauaji hufanywa je hadi kuipata hiyo damu? Mwajuma anasema “Mtu wa kule akitaka kuua huivaa sura ya mwanadamu (jambazi Fulani anayejulikana na watu) na kufanya mauaji, kisha hurudi kuzimu”.
Mama mzazi wa Mwajuma akihojiwa na SNP Dr. Godson Issa Zacharia
kuhusu alivyokuwa akiishi na mwanane huko nyumbani kwake Tangeni.

Mama mzazi ambaye pia siku ya leo alikuwepo kanisani, ameshuhudia kusema kuwa,  alikuwa na mwanane, lakini nyakati nyingine mwanane anaanguka na kuzimia. Mwajuma anajitetea kuwa kisa cha yeye kuanguka kulisababishwa na kuiona picha yake wakati alipokuwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro, na wakati  huo huo alipaswa apeleke damu kule kuzimu. Hivyo kitendo cha kujiona mara mbili kilimshtua na kumfanya azimie

Hadi  leo hii, Mwajuma anayo alama  yao ya kule kuzimu. Hii alama ipo mguuni pake na imekuwa ikifanya mashetani ya kule kuzimu yamtokee kila usiku yakidai alama  yao. Mwajuma aliyebaki duniani, alikuwa anaishi na mama yake na tena alikuja kuolewa, na hivi leo Mwajuma ni mjamzito. Hata hivyo, kutokana na kupata ujauzito wa kibinadamu, kuzimu iltaharuki na kutaka kuzidi kumpa adhabu yule Mwajuma wa kule Kuzimu kwa kitendo cha kukubali fotokopi yake kuchukua mimba ya kawaida duniani. 

Swali: Ni  yupi basi aliyeolewa hapa duniani? Alipoulizwa kuhusu ndoa, Mwajuma anasema “Alieyeolewa ni ile fotokopi yangu. Ndiyo maana hata nikiziangalia picha zangu za harusi hazifanani na mimi binafsi”

Swali: Chakula cha kule ni nini? Mwajuma anasema ni damu za wanyama na wanadamu. Mkubwa wa kule shimoni huitunza hiyo damu. Mojawapo ya adhabu aliyowahi kupewa ni yeye kumkatakata mtu mzima hadi ammalize. Aliona hiyo  adhabu kali mno, lakini hata hivyo alifanikiwa kumuua huyo mtu, ingawa kwa taabu akianzia na viganjani hadi alipomaliza kumkatakata hadi mwisho. Yule aliyemkatakata aliwahi kusoma naye shule ya Msingi Msamvu. Anasema, aliambiwa na kuzimu kuwa hatasoma zaidi ya darasa la 7, na hata alipokuwa darasani alikuwa hawezi kuona daftari lake,  kwani macho yalikuwa yanakataa.

Swali: Je ana ushauri gani kwa watu wasioamini  kuhusu uwepo wa “misukule?” Mwajuma amesema “Ni kwa vile haya mambo hayajamtokea mtu huyo asiyeamini. Lakini ukweli wa mambo ndio huo, kwamba watu wanachukuliwa, na mashimo ni mengi wala siyo moja”. Mwishowe, Mwajuma ameahidi kumtumikia Bwana Yesu maisha yake yote, na hatamuacha.

============END OF STORY============
Share:
Powered by Blogger.

Pages