Sunday, July 6, 2014

SOMO: KUWARUDISHA TOKA NYUMBA ZA KUFUNGWA - Na: Pastor Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)

JUMAPILI: 06 JULY 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

Utangulizi: Somo la leo  linaitwa “Kuwarudisha toka Nyumba za Kufungwa”. Zipo nyumba zinaitwa nyumba za kufungwa. Haya ni majumba na magereza yaliyopo hapahapa duniani, pahali pa kuzimu. Kwenye nyumba hizi utawakuta akina mungu Artemi na Mpinga Kristo. Wateja wa nyumba hizi huweza kuonekana mara mbili: hapa duniani anaonekana lakini wakati huo huo huonekana upande wa pili akiwa katika hizi nyumba za kufungwa.

ISAYA 42:6-7 … [Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; 7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.].. Shetani anaiba watu na kuwakodisha kwenda kulima mashamba ya watu wake nyakati za usiku.


MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, nakataa kukaa kwenye nyumba za kufungwa. Amen.


ISAYA 42:22...[Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]… Haya mashimo ni zile nyumba ninazoziongelea.


Wachawi humpeleka mtu kwenye nyumba za kufungwa kwa kutumia njia 3 za kupata wafungwa:-

1.      Huweza kumchukua  mtu wa ndani (roho) na kumbadilisha na mwingine. Wakifanya hivyo huweka roho ya kitu kingine mle ndani (mfano nyoka),  ili mwili ule uendelee kuwepo ukionekana. Njia hii humfanya Yule mtu wa kawaida apelekwe shimoni (nyumba za kufungwa). Yule anayebaki duniani, siyo halisi, na ndiyo maana anaweza kuwa na magonjwa ya ajabu ajabu au tabia zisizo za kawaida. Imeandikwa, “roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu”.  Anayewafunga ni shetani mwenyewe na hataki wafungwa warudi kwao. 

    YEREMIA 50:33… [Bwana wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda, wameonewa pamoja; na wote waliowachukua mateka wanawashika sana; wanakataa kuwaacha.]…

2.      Mtu hubebwa mzima mzima. Mtu huyu hutafutwa kila mahali na vyombo vya habari hutangaza tukio hilo,  lakini hawezi kupatikana. Mito ya maji na bahari huchunguzwaili angalau kuuona mwili wa mtu  huyo, lakini hata hivyo hawezi kupatikana. Wachawi humpeleka mtu huyu mahali pa mbali, kiasi kwamba siyo rahisi watu kumbaini. Watu hudhani pengine mnyama mkali amemla,  na ndipo hufanya taratibu zingine za kimila, mara watanyoa nywele na kuzizika wakiashiria ndiyo mazishi ya  huyo mtu. Kumbe kimsingi mtu huyo yupo mahali fulani amefichwa.

3.      Kufa kabisa na kuzikwa kabisa. Sababu hii itafundishwa siku nyingine.


SABABU ZINAZOSABABISHA MTU ABEBEKE HADI NYUMBA ZA KUFUNGWA (MSUKULE)

Zipo kama sababu 3 ambazo husababisha ubebeke:

1.0 WIVU.

Wachawi hukasirika na kuona wivu kwa nini wewe: una mume, mke, mali, biashara, elimu n.k. wivu ukijaa wachawi hupeleka jina lako kwenye madhabahu zao kuulizia kwa nini wewe upate vyote lakini  yey asiwe navyo. Huomba kwenye hiyo madhabahu ili kwamba utengenezwe, nao humwaga damu za wanyama ili kwamba wewe uchukuliwe.


MAOMBI: Kwa Jina la Yesu ninalifuta Jina langu lililoandikwa kwenye madhabahu za kichawi ili kwamba mimi nichukuliwe. Naliondoa Jina langu kwenye list ya watakaochukuliwa kwa Jina la Yesu.


MATENDO 5:17-18…[Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu, 18 wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;]… Kwa hiyo hii ni sababu ya kwanza,  siyo kwamba umewakosea watu la hapana.


MAOMBI: Leo ninageuka na kuwa mzito kama container,nisiweze kubebeka. Yeyote aliyenishtatki kwa wachawi, na amenijia ili anibebe ninakuwa mzito na sitabebeka, kwa Jina la Yesu. Sibebwi. Nakataaa kubebeka. Walionibeba wako njiani  na mimi, nakataa kufa kwa Jina la Yesu. Leo nakataa kubebeka, niachieni kwa Damu ya Yesu.


2.0 KUKOSA MAARIFA

Watu wengi duniani kote hawana maarifa / elimu ya mambo haya. Information is power. Kukosa taarifa ni kukosa nguvu.

ISAYA 5:13 … [Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.]…

HOSEA 4:6… [Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.].


Kwa Jina la Yesu, popote waliponificha, kwa kukosa maarifa. Nakataa kubaki mashimmoni. Nimetumikia wachawi na waganga kwa kukosa maarifa, leo nakataa. Kwa Jina la Yesu. Nakataa kuzaa watoto baharini kwa kukosa maarifa. Nakataa kwa Jina la Yesu.

Maarifa ni neno la Kristo. Imeandikwa,matiajua kweli, nayo kweli itawaweka huru. Unatakiwa kujua maarifa ya Krsito, hata kama utasikia sauti uweze kuikataa.

3.0 DHAMBI

a)     Maana ya kwanza ya dhambi ni kutotenda yale ambayo Mungu amesema tuyatende. Mfano, Mungu amesema wewe uokoke lakini unakataa. Mungu amesema utoe fungu la kumi lakini unakataa. Yote hayo ni dhambi.

b)     Aina nyingine ya dhambi, ni kufanya vile ambavyo Mungu amekukataza usifanye. Mfano imeandikwa usiibe, lakini wewe unaiba. Usiue,  lakini kila mara unafanya abortion (kutoa mimba). Zote hizo ni dhambi.


EZRA 9:6-7… [nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni. 7 Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo.]…


MAOMBI: Nakataa kukaa kwenye njia ya shetani kwa Jina la Yesu. Sitapitiwa tena na shetani, nakataa kufanya dhambi tena kwa Jina la Yesu.


EZRA 5:12… [Lakini hapo baba zetu walipomkasirisha Mungu wa mbingu na nchi, hata akaghadhibika, akawatia katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Mkaldayo, naye ndiye aliyeiharibu nyumba hii, akawachukua watu mateka mpaka Babeli.]… Sabau kuu hapa ya watu kupelekwa mateka hadi Babeli ni  DHAMBI. Unapotenda dhambi, Mungu anakuacha peke yako, akiondoa ule wigo na papo hapo wachawi huwa rahisi kukuchukua.


ISAYA 42:24… [24 Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, Bwana? Yeye tuliyemkosa, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.]… Mungu akiondoa ulinzi wake, unabebwa haraka.


MAOMBOLEZO 1:5… [Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa Bwana amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.]… Maadui wanafanikiwa kukuteka na kukutesa endapo utakuwa unayo makosa.


MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, Ninakataa makosa na uovu wa ukoo, wa nchi, wa nyumba yangu kwa Jina la Yesu.


==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==

==(Cellphone: (+255) 713 45 95 45)==
Share:
Powered by Blogger.

Pages