RP Nicodemus Mwakyando akimkaribisha Baba (Dr. Godson) leo kuhubiri ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro |
Utangulizi: Somo la Jumapili ya leo linaitwa “Milima ya Uharibifu”. Neno
mlima lina maana ya sehemu ya nchi iliyoinuka juu. Endapo mtu yupo juu yam lima,
anao uwezo wa kuviona vit vyote vilivyo chini yake kama hivyo vitu ni vya kuonekana.
Wapo waharibifu wengi ambao hupenda kuupanga kazi zao za uhaaribifu na
kutekeleza mipango hiyo maeneno ya chini ya milima hiyo. Wachawi na waganga wanayo
desturi ya kutoa kafara na sadaka zao juu ya milima. Ndiyo maana hata Ibrahimu
alitoa sadaka zake juu ya mlima. Yesu
Kristo vivyo hivyo, alitolewa sadaka juu
ya mlima, ili watu wote wajue na kuioona ile aibu kubwa itakayompata.
Baba (SNP Dr. godson) akifundisha somo: Milima ya Uharibifu, Jumapili 28 Sept. 2014 ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro |
Hata leo hii hali ni ile ile. Wachawi na waganga wa
kienyeji wakishatengeneza mapatano ya uharibifu, hutaka utekelezaji wake ukupate kwa namna ambayo aibu kuu na
udhalilishaji utakaokupata watu wote wataushuhudia. Mfano, badala ya kuitwa ‘baba
au mama fulani’ wachawi watataka waone unaanza kuitwa, “Yule baba/mama asiyezaa
mtaani kwetu”.
2
WAFALME 23:13….[Na mahali pa juu
palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa
uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la
Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni,
mfalme akapanajisi.]… Mahali hapa ambapo mfalme Sulemani alipajenga,
palikuwa ni chukizo kwa wafalme na mataifa mbalimbali, kama yalivyotajwa hapo juu.
YEREMIA
51:25…[Tazama, mimi ni
juu yako, Ee mlima uharibuo, asema Bwana; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha
mkono wangu juu yako, na kukufingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya
kuwa mlima ulioteketezwa.]… Mlima uharibuo umeleta madhara kwa dunia
nzima, na hakuna mtu yeyote mwenye nafuu, kuanzia wakuu wa nchi hata walio
wadogo. Hata hapa kwetu Tanzania, uharibifu upo karibu kila mahali, mashuleni, mahospitalini n.k. kumbe kuna
mlima ambao wanaojikusanya humo hutoa matamko
ili mvua zisiwepo kwenye nchi, kazi zikosekane, magonjwa yaongezeke n.k. wanaokaa katika milima hii ya uharibifu
kuleta matatizo ni wakala wa shetani.
Milima ya uhribifu ni kituo kikuu cha wachawi cha kulaania watu. Inaitwa
laana kwa sababu mara zote laana huleta uharibifu katika maisha ya mtu. Haipo laana
inayomfanya mtu apate maendeleo, au apate gari‼! Laana itakuja kwa mtu ili kwamba avunjike miguu yote, augue, apate
mikosi n.k. haya yote hufanyika katika madhabahu za kichwi kwenye milima ya
uharibifu, ambapo shetani naye hushuka kwenye hizo madhabahu na kusikiliza
kilichotamkwa na wachawi ili shetani akitekeleze.
Katika Biblia,
yupo Balaki ambaye ni Mfalme wa Moabu aliyewaogopa sana wana wa Israeli
na hata akatafuta mchawi wa kuwalaani wana wa Israeli. Ndiyo maana Paulo akasema, “kupigana kwetu
si juu ya mwili na damu…..” (). Yamkini kuna siku unakosa chakula na
ukadhani hiyo ndiyo kusudi la mchawi kwa maisha yako‼! Lahasha, kitendo cha
wewe kuonekana unatembea na kuja
kanisani kinawashangaza hao hao wachawi kwani pengine walikusudia kufikia leo
uwe umekufa lakini bado unaishi na kutembea‼!
Baadhi ya Majeshi ya Bwana - Ufufuo na Uzima Morogoro wakifuatilia kwa makini somo la leo tarehe 28 Sept. 2014. |
HESABU
22:1-7…[Kisha wana wa
Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya
Yordani karibu ya Yeriko. 2 Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo
Israeli wamewatendea Waamori. 3 Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa
walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli. 4 Moabu
akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote
vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe
arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa
Moabu zamani zile. 5 Basi Balaki akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori,
hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu
waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
6 Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda
mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa
maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa. 7
Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga
mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.]…
Balaki alikuwa hajawahi kukutana na wana wa Israeli, ila alikuwa na fununu za yale waliyotendewa na Mungu
kutoka walipotokea Misri. Sifa hizi zilimfanya mfalme wa Moabi kusema ‘Sasa jeshi hili
la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba’
kumaanisha hakipo kitu kitakachosazwa‼! Ngombe akiramba jani hulimeza lote. Kimsingi hivyo vitu si vya
kwao. Wnapojua mtu ameokoka, wachawi hugundua kuwa vile vitu ambavyo
walikuibia utaenda kuviramba, na ndiyo maana huenda kwa waganga wa kienyeji ili
kupata nguvu za kiroho kuupitia laana. Unapokuwa umeokoka usiridhike na maombi
uliyofanyiwa siku moja. Wanaokuwinda hawalali
usingizi hadi wauone uharibifu waliokusudia kwako ukitimia.
MAOMBI: yeyote anayetamka laana kwako,
laana hiyo imkute mwenyewe, kwa Jina la Yesu. Amen
|
Yesu vivyo hivyo aliwahi kupelekwa na shetani mlimani
na kuoneshwa miliki zote za dunia. (LUKA 4:1-7… [Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za
ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote,
na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama
nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako] ). Kwa nini Yesu apelekwe mlimani? Ni ili
aweze kuona watu wote, na vile wanavyomiliki.
HESABU
22:41 …[Ikawa asubuhi
Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hata mahali pa juu pa Baali; na kutoka
huko akawaona watu, hata pande zao za mwisho.]…. Baali ni shetani mwenyewe. Juu ya
milima hii ya uharibifu, kila kitu huonekana.
HESABU
23:1-6 …[Balaamu
akamwambia Balaki, Nijengee hapa madhabahu saba, ukaniandalie hapa ng'ombe
waume saba, na kondoo waume saba. 2 Balaki akafanya kama Balaamu alivyonena.
Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng'ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu
ya kila madhabahu. 3 Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako,
nami nitakwenda, labda Bwana atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia.
Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima. 4 Mungu akakutana na Balaamu; naye
Balaamu akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng'ombe mume mmoja na
kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. 5 Bwana akatia neno katika kinywa
chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno haya. 6 Akarudi kwake,
na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote
wa Moabu pamoja naye. 7 Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka
Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo!
Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli. 8 Nimlaanije, yeye ambaye Mungu
hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye
Bwana hakumshutumu?]… Balaam alikuwa amelipwa fedha ya kichawi, lakini Mungu alikuwa amekwisha kumuonya
assitamke laana yoyote kwa Israeli. Unaona hapa kwamba, Balaam amepelekwa mlimani, lakini Bwana akawa amekikamata kinywa chake. Kumbe unapokuwa
na Bwana Yesu, wachawi hawataweza kabisa kukulaani.
MAOMBI: Tunavigeuza vinywa vyote vya wachawi badala ya kutoa
laana vinywa hivyo vighafirike na kutamka Baraka kwa Jina la Yesu. Amen.
|
HESABU
23:11-6 …[Balaki
akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na
tazama, umewabariki kabisa kabisa. 12 Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi
kuangalia, niseme neno lile Bwana atialo kinywani mwangu? 13 Balaki akamwambia,
Haya! Njoo, tafadhali, hata mahali pengine, na kutoka huko utaweza kuwaona;
utaona upande wa mwisho wao tu, wala hutawaona wote, ukanilaanie hao kutoka
huko.]… Yamkini wapo watu
walikutamkia laana kwenye kilima cha kwanza, lakini mara hii tunataka wanapokutanika badala ya laana
wakatamke Baraka kwako kwa Jina la Yesu.
Hata baada ya hapa, Bwana aliendelea kukikamata kinywa
cha Balaam tena. Kama ilivyoandikwa:-
HESABU
23:14-6…[Akamchukua mpaka
shamba la Sofimu, hata kilele cha Pisga, akajenga madhabahu saba, akatoa sadaka
ng'ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu. 15 Akamwambia
Balaki, Simama hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami nitaonana na
Bwana kule.]…
HESABU
23:18-19 …[Naye akatunga
mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize; Nisikilize, Ee mwana wa
Sipori; 19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute;Iwapo amesema,
hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?20 Tazama, nimepewa amri kubariki,
Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.]…
HESABU
23:23… [Hakika hapana uchawi
juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na
Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!]… Mtu
anapookoka, anakuwa na hii sifa: Kwamba hapana uganga wala uchawi unaoweza
kumpata tena kwa Jina la Yesu. Lakini pia anakuwa sawa na malaika na kwa kuwa
ni mwana
wa ufufuo, LUKA 20:36 ….[wala hawawezi
kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile
walivyo wana wa ufufuo.].
HESABU
23:25-26…[Balaki akamwambia
Balaamu, Basi usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa. 26 Lakini Balaamu
akajibu akamwambia Balaki, Je! Sikukuambia ya kwamba, Kila neno Bwana
atakalolisema sina budi kulitenda? 27 Kisha Balaki akamwambia Balaamu, Haya,
njoo sasa, nikupeleke mahali pengine; labda Mungu ataridhia kwamba unilaanie
watu hao huko. 28 Basi Balaki akamchukua Balaamu akaenda naye mpaka kilele cha
mlima Peori, mahali paelekeapo upande wa nyika iliyo chini yake. 29 Balaamu
akamwambia Balaki, Haya, unijengee hapa madhabahu saba, kisha uniandalie
ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba. 30 Basi Balaki akafanya kama Balaamu
alivyosema, akasongeza sadaka ng'ombe mume na kondoo mume juu ya kila
madhabahu.]…. Unaona jinsi ambavyo wachawi hawakati tamaa hata
kama laana zao hazitokei, au wakiona
wanachelewa kuona uharibifu ukitokea, bado hawakati tamaa.
MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, enyi wachawi, nazigeuza laana zenu igeuke ziwe
Baraka, na laana mliyoandaa juu yangu iwapate waliowatuma kwa Jina la Yesu. Amen
|
NINI
HUWA KINAFANYIKA WACHAWI WANAPOKUWA MILIMA YA UHARIBIFU?
Baadhi ya watu waliookoka siku ya leo |
Wachawi hutoa kafara, na mashetani hupanda hapo milimani, na kunywa ile damu ya hiyo kafara. Kwa sababu mambo haya yamefanyika milmani, mashetani haya hufanya mlima wa kiroho ili kuusimamisha kati yako wewe na hatima yako. Mlima huu wa rohoni hukuzuia usifikie kile kitu ulichokusudia kukiendea. Mlima wa rohoni hukuzuia usione mambo mazuri ambayo hapo awali ulikusudia kuyaona. Mfano;
·
mlima huwa
kati yako na afya yako na ndiyo maana unakuwa mgonjwa kila mara‼!
·
Wachawi hujenga
mlima mkubwa wa uharibifu kati yako na
ndoa ya mtu. Hii humfanya mtu asimjue mwenza wake wa maisha yake, na hivyo kumfanya asioe au asiolewe‼!
·
Mtu mwingine
amewekewa mlima kati yake na Kanisa la Ufufuo na Uzima, ili mtu huyo
asiweze kufika hapa kanisani kuupata uponyaji wake au wa watu wa nyumbani kwake‼!
·
Endapo mwanaume
anachepuka na kutafuta nyumba ndogo,
ujue tayari kuna mlima ambao umekaa mbele ya mke wake kumziba na kumtenga
kati yake na mume wake, ili kwamba mumewe
asimuone kama ambavyo anaweza kuiona hiyo nyumba ndogo‼!
·
Pengine unalo
duka zuri, lakini watejea hhuwaoni, kwa sababu
upo mlima mkubwa ambao unaawafanya wateja wasiweze kulifikia duka lako‼!
·
Watu wengine
wanakaa kwenye ndoa lakini wanakosa furaha
ya ndoa yao. Furaha inakosekana kwa sababu upo mlima kati ya hiyo ndoa na
furaha ya ndoa yao‼!
MAOMBI: Kwa jina la Yesu, ewe mlima
uliyekaa kati yangu na biashara yangu, ewe mlima uliyekaa kati yangu na kazi
yangu, ewe mlima uliyekaa kati yangu na mume wangu, ewe mlima uliyekaa kati
yangu na mke wangu, ewe mlima leo nakuteketeza kwa Jina la Yesu. Amen
|
NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MLIMA WA UHARIBIFU
Mtoto huyu alikuwa amechukuliwa msukule na babu yake, lakini leo amerudishwa na Bwana Yesu kutoka utumwani. |
Cha kwanza na muhimu ni mtu kugeuka na kuwa mwana wa Mungu, ili Bwana akutumie wewe kama mtu wake.
YEREMIA 51:20 …[Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe
nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;]…
YEREMIA 51:25…[Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima uharibuo, asema Bwana; wewe uiharibuye
dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukufingirisha chini
toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa.]… Mungu
anaongea na huu mlima kana kwamba huo mlima una masikio‼! Kinachoonekana hapa
kama mlima si mlima wa kawaida bali ni mashetani yaliyojibadilisha na kuwa
makubwa kama mlima‼!.
Biblia inasema “kama vile milima iizunukavyo Yerusalem, ndivyo Bwana
awazungukavyo watu wake”…. Wachawi vivyo hivyo huweka milima ya
uharibifu mbele za mtu ili mtu huyo asipate
hatima ya kusudi la Mungu maishani mwake.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Kihonda VETA, Morogoro.
or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778
Email: godson.issa@yahoo.co.uk