Sunday, September 21, 2014

SOMO: MAPATANO YA DAMU-Na: Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)


JUMAPILI: 21 SEPTEMBER 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

Utangulizi: Somo la Jumapili ya leo linaitwaMapatano ya Damu”. Ukisikia watu wamefanya mapatano, ujue  kuna makubaliano yanayoafikiwa kati ya watu/familia/ukoo/nchi n.k na mwishowe kuingia mkataba. Katika mapatano, pande  mbili huhusishwa.   Mapatano ya Damu hufanyika kwa kutumia damu. Hata katika  muungano  wa Jamhuri ya Tanzania,  mchanga ulitumika kwa kuchanganya mchanga wa upande huu na upande wa pili. Miungano au mapatano  yanakuwa na jambo la rohoni ndani yake.

 

Baba (SNP Dr. Godson) akihubiri somo liitwalo
"Mapatano ya Damu" leo Jumapili 21/09/2014.
Katika Biblia,  Damu ina tabia kama 5 hivi:

         1.    Damu inayo sauti:             MWANZO 4:10…. [Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.]…. Mungu hapa alikuwa anamuuliza Kaini  kwa nini amemuua ndugu yake.

 
         2.      Damu ina uwezo wa kulia: Siyo  kila chenye sauti kinalia. Damu  yaweza kulia na Mungu akiwa mbinguni akasikia (MWANZO 4:10).

 

         3.     Damu inweza kuleta laana, kwa mtu au familia au nchi. Imeandikwa ‘Alaaniwe mtu  yule amwagaye damu ya mtu’.

 

         4.    Damu ina uhai: KUMBUKUMBU 12:23….[Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama.]… Ndiyo maana Yesu alipokuja aliutoa uhai wake kwa kusulubiwa msalabani badala ya  kulala na kufa akiwa  usingizini.

 

         5.     Damu  inaweza kuongea/kunena: Kumbuka kuwa kutoa sauti siyo kunena.  Ufafanuzi wake ni sawa na kuona mtoto mchanga azaliwapo, yeye hutoa sauti lakini siyo kunena. Maana ya kunena ni kutamka kitu chenye maana, kwa kupangilia sentensi. Kwa hiyo,  damu yaweza kunena  mema au kunena mabaya.

 

EBRANIA 12:24…[na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.]…. Kumbuka ile damu ya Habili ilikuwa ikimhimiza Mungu alipize kisasi kwa kitendo cha kuuawa na Kaini bila hatia yoyote.
Kulia ni Baba (SNP Dr. Godson) akiombea mmoja wa watu
waliokuwa wanasumbuliwa na "mapatano ya damu" leo 21/09/2014.

 

WALAWI 17:10-12…[Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake. 11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. 12 Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu.]…Kwa hiyo damu ni nyenzo pekee ya kupatanisha makundi mawili.

Kama mjuavyo, zipo  aina mbili za ulimwengu. Ulimwengu  wa mwili na ulimwengu  wa roho. Ulimwengu wa mwili hukaa viumbe ambavyo ni rahisi kuviona kwa macho ya mwilini. Ulimwengu wa roho ni ulimwengu ambao  siyo rahisi kuona viumbe wake kwa macho haya ya mwilini, bali  huonekana vizuri tu kwa kutumia macho ya kiroho. Katika  ulimwengu wa roho,  wapo wakazi wa aina mbili:

·        Viumbe wa rohoni Watakatifu (Mungu, malaika wema, makerubi, maserafi, watakatifu)

·        Viumbe wa rohoni Wachafu: Shetani mwenyewe na malaika zake,

Yesu alimwaga damu  yake kuleta upatanisho kati yetu sisi wanadamu (wenye dhambi) na Mungu. Shetani naye kwa kugundua hili,  naye amewekeza katika kumwaga damu ili yale anayotaka yaafanyike yaweze kufanyika.

 
Majeshi ya Bwana yakifuatilia somo la leo tarehe 21/09/2014
katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro.

ISAYA 28:15…[Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi;]…. Ili watu wapatane na kuzimu, nyenzo ya kufanya hivyo lazima ipatikane. Damu  nyinginezo  zote ISPOKUWA DAMU YA YESU,  hunena mabaya. Kuzimu ni  karakana ya matatizo yote unayoyaona hapa duniani.  Shetani ndiye aliyefanya maagano na kuzimu.

 

WALAWI 19:26-28…[Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi. 27 Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu. 28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.]…. Pale  pale ambapo Mungu ameongelea watu wasinywe damu, ni hapo hapo pia alikataza uchawi. Ndiyo maana hata kwa waganga wa kienyeji,  haijawahi kutokea akahitaji sadaka ya matikiti, au mkungu wa ndizi,  au kitu kisichokuwa na damu. Mara zote mganga wa kienyeji atahitaji kuku, mbuzi n.k ili baaadae amwage damu  katika madhabahu zake. Wachawi wote, waganga wote huomba  damu. Mungu alizuia watu kuchanjwa chale kwa sababu kitendo hicho huwapa fursa mashetani kuondoka na uhai wako na kuishia kukaa kwenye madhabahu zao.

 

Kitakwimu,  zaidi ya 95% ya watanzania wamechanjwa chale. Na kwa sababu  ya umuhimu wake katika madhababhu za kishetani, alama za chale mara zotet hazifutiki. Unapotoa damu yako, hiyo si sawa na damu ya kuku au mnyama yoyote. Kwa hiyo,  damu yako mwenyewe ikiwa  kwenye meza za waganga wa kienyeji,husema kana kwamba ni wewe mwenyewe. Unapoona mtu  anaamua kujiua,  ujue si kwamba alitaka kweli kujiua, bali ni kwa sababu damu yake iliyo kwenye madhabahu Fulani, inalazimishwa kusema ‘nataka kujiua’.

 

MAOMBI: Kwa jna la Yesu, mahali popote ilipo damu yangu, mahali popote damu yangu iliyomwagwa kwenye madhabahu za kichawi, mahali popote nilipochanjwa chale, damu yangu iliyomwagwa kwenye madhabahu makaburini, leo kwa Jina la Yesu, naiyeyusha kwa Damu ya Yesu. Damu yangu iliyoshikiliwa na wasoma nyota, naiyeyusha kwa Damu  ya  Yesu. Ewe damu unayeongea mimi nipaate mikosi, nisipate kazi, nisizae, nisifanikiwe,  leo nakueyeusha kwa Damu ya Yesu. Amen.

 

Wachawi wanafahamu  jinsi ambavyo damu ina uwezo wa kunena. Wachawi hupenda kuleta mapingo kwa mtu kupitia damu. Mapatano na kuzimu  hufanywa na damu za wanyama mbali mbali au hata damu ya mtu. Waweza kuona watu wana matatizo ya kufanana lalkini kufunuguliwa kwao huchukua sura tofauti.  Endapo njiwa ndiye alitumika kwenye kafara, mtu huyo akiombewa hufunguliwa mapema kwa sababu hata kajini  kanakomshikilia ni kadogodogo hivyo  hivyo. Mtu mwingine yamkni damu iliyomwagika ni ya ng’om,be, kwa hiyo kufunguliwa kwake huchukua muda mrefu kidogo, na kwa kuongezea nguvu za rohoni za huyo mwonaji, basi mtu wa aina hii hufunguliwa ingawa muda mrefu kidogo.

 

Endapo mtu amemwaga damu ya mtototo wake nmwenyewe, ujue kufunguliwa kwake kunachakua muda mrefu sana kulinganisha na wenye vifungo wengineo.

2 WAFALME 3:21-27 [Basi Wamoabi wote waliposikia ya kuwa wafalme hao wamekwea ili kupigana nao, walijikusanya pamoja, wote wawezao kuvaa silaha, na wenye umri zaidi, wakasimama mpakani. 22 Wakaamka asubuhi na mapema, na hilo jua likametameta juu ya maji, na Wamoabi wakayaona yale maji yaliyowaelekea kuwa ni mekundu kama damu.23 Wakasema, Ndiyo damu hii; bila shaka hao wafalme wameharibika, wamepigana kila mtu na mwenziwe; basi sasa, enyi Wamoabi, nyara hizo! 24 Hata walipokuja matuoni kwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata wakakimbia mbele yao; wakaendelea wakiwapigapiga Wamoabi hata kwao. 25 Wakaibomoa ile miji; wakatupa katika kila mahali palipo pema kila mtu jiwe lake, wakapajaza; wakaziziba chemchemi zote za maji, wakaikata miti yote iliyo mizuri; mpaka katika Kirharesethi tu wakayasaza mawe yake; ila wenye kombeo wakauzunguka wakaupiga. 26 Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 27 Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.]… Baada ya kuona kuwa Wamoabi wamepigwa, ndipo alipopatana na kuzimu ili kupata wanajeshi  wengine wa rohoni. Kumbe mtu akiona ameshhindwa huweza kupatana na kuzimu kwa kutoa kafara kwa kumwaga damu ya mtu kabisa.  Wanadamu hutoa kafara ya wanyama au ya mtu kabisa. Wanapotoa kafara za wanadamu wenzao, mashetani  hunywa hiyo damu na kusema ‘kwa damu hii,  mtu huyu awe hivi  na hivi’. Kumbuka imeandikwa, “kushindana kwetu si juu ya mwili na damu, bali ni….. (EFESO 6:12). Ndiyo maana Yesu akamwaga damu yake mwenyewe,  damu yenye kunena mema.

 

MAOMBI: Ewe alama unayetumiwa na wachawi kama tochi ili kunifuatilia, leo nakufuta kwa Jina la Yesu. Alama za kichawi nilizowekewa kupitia chale nazifuta kwa Damu  ya Yesu.

 

Yamkini yupo ndugu yako sasa hivi ambaye ameona wivu kwa maendeleo kidogo tu uliyopata, na amekusudia kukushtaki  katika  madhabahu za kichawi kwa kumwaga damu. Ndiyo maana nyakati nyingine waweza kushangazwa kwa kuona ajali mbaya ya gari imetokeaa, na gari lote limeharibika vibaya sana, lakini aliyekufa kwenye hiyo ajali ni mtu mmoja tu ambaye alikuwa amewindwa afe kwenye hiyo ajali, na wengine wote hawana hata jeraha!!!!. 


Sauti ya Kristo ya Msalabani ilisema “Imekwisha”, na baada ya pale, makaburi yakapasuka, miili mingi ya watu ikatoka makaburini, dunia ikawayawaya, na miamba ikatetemeshwa.

Damu inapomwagwa na wachawi, mashetani yanayotumwa hupewa maelekezo ya mtu aliyekuuusdiwa balaa zimpate na kipi kimkute.  Damu haiwezi kumwagwa kwa mtu ‘A’ na balaa likamkuta mtu ‘B’.

 

MAOMBI: Kuanzia leo ninanyamazisha damu zote kwenye madhabahu za kichawi,  kwa Jina la Yesu.

 

Utaona kuwa hata wanyama wenyewe wanaugua mioyoni mwao kwa kukosa uhuru wa kujitetea dhidi ya wale wanaowaua kwa njia ya kafara.

 
WARUMI 8:19-20.. [Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;]… Wanyama wanaochinjwa kwa ajili ya kfara, hawawezi kusema hawataki. Wanakusubiria wewe uokoke ili wana wa Mungu wakeshaokoka watawapatia hao viumbe uhuru wao dhidi ya watoa kafara (wachawi na washirikina wote).



Baadhi ya watu waliompa Yesu Maisha yao Leo kwa
Kuokoka ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro. 
 Wachawi wanapopatana na kuzimu (mfano: tunataka mtu huyu afukuzwe kazi), damu iliyomwagwa hukaa ndani ya huyo  mtu, au familia yake, au tumbo lake au ofisini mwake na kumfanya huyo mtu afanye maamuzi magumu yasiyokuwa yake, na kuamua kuacha hiyo kazi anayoifanya  ghafla‼!!.





 

© Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)

Kihonda VETA, Morogoro.

 /or

Contact our Senior Pastor:

 Dr. Godson Issa Zacharia

 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

Email: godson.issa@yahoo.co.uk 

 

 
Share:
Powered by Blogger.

Pages