Monday, October 6, 2014

SOMO: NAMNA YA KUKATA KAMBA ULIZOFUNGWA NA NDUGU ZAKO WA KARIBU-Na: Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)

JUMAPILI: 05 OCTOBER 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Utangulizi: Somo la Jumapili ya leo linaitwaNamna Ya Kukata Kamba Ulizofungwa Na Ndugu Zako Wa Karibu”. Kamba ni kitu gani? Ni kitu kinachotumika kwa ajili ya kufunga  kitu kingine chochote kile. Lakini kamba katika somo hili inamaanisha mashetani /au majini /au mapepo. Kumbuka imeandikwa MATHAYO 10:36, kwamba “Adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake…..”  Mifano michache ya andiko hili kibiblia ni kama ifuatavyo:-
·        Yesu alisalitiwa na Yuda Iskariote mwanafunzi  wake kabisa
·        Malaika  wa sifa (Lucifer) alitaka na kunuia kumpindua Mungu huko mbinguni
·        Absalomu mwanae  Daudi aliongoza  uasi dhidi ya Baba yake mzazi.
Baba (SNP Dr. Godson) akiombea watu waliofungwa
kamba za mashimoni leo 05/10/2014 Nyumba ya Ufufuo na
Uzima Morogoro wakati ibada inaendelea.


IMEANDIKWA:

2 SAMWELI 22:4-6 …[Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu. 5 Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. 6 Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. 7 Katika shida yangu nalimwita Bwana, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu; Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.  ]… katika andiko hili  yapo  maneno haya ‘Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili’. Kamba zitokazo kuzimu siyo kamba mithili ya hizi zinazofungia vitu hapa duniani.  Kamba zitokazo kuzimu ni mashetani,  majini, mapepo na kadhalika.


ZABURI 18:5…[Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili..]…


ZABURI 129:1-4…[ Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, 2 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza.3 Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao. 4 Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki.]…
Mara kadhaa wamekuwepo ndugu, tena wa karibu ambao  ingawaje siyo wachawi  au waganga wa kienyeji, lakini huenda kutafuta wenye uwezo wa kufunga kamba ili  wakufunge usifanikiwe.


Haipaswi kukaa kwenye mashaka endapo mtu  amekwisha kumwamini Yesu Kristo maishani mwake. Imeandikwa,  “mwenye haki ataishi kwa imani”…. Inapokuwepo  kamba iliyomfunga mtu yeyote, mtu huyo  hukaa katika mashaka na kusitasita kwa kila jambo. Lengo  la wanaofunga kamba ni kumfanya mtu asiendelee,  au asisonge mbele kimaendeleo.


Watu wafuatao hawawezi kukata kamba zilizomfunga mwingine:
·        Endapo mtu ni Mchungaji: Hawezi kukata kamba.
·        Endapo mtu ni Paroko na parokia yake: Hawezi kukata kamba.
·        Endapo mtu ni Shekhe: Hawezi kukata kamba.
·        Endapo mtu ni Askofu: Hawezi kukata kamba.

Showers of Glory wakiruka angani walipokuwa wakimwimbia Bwana

Yupo mtu mmoja tu ambaye anao uwezo wa kuzikata kamba: YESU KRISTO pekee, aliyekufa kifo cha aibu msalabani anao uwezo huo wa kuzikata kamba zilizowafunga watu hapa duniani.


ZABURI 140:5….[Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.]… Kwenye hili  andiko yapo mambo manne yaliyokaa kwa mtindo wa kamba: Mtego, kamba, wavu na matanzi. Kamba iitwayo ‘tanzi’ ni ile ya kusababisha kifo. Ndiyo maana watu wanaojinyonga, hutumia tanzi kwenye shingo zao. Hizi zote ni kamba zitokazo shimoni (kuzimu). Njia iliyoandikwa hapa siyo njia zako za kutembelea hapa duniani. Ni ile njia ya kuelekea kwenye mafanikio yako, kwenye njia ya kuelekea kuolewakwako, kwenye njia ya kufungua mradi wako, kwenye  njia ya Baraka zako. Katika njia hiyo, wapo watu wanaoweka mitego, tanzi, kamba, wavu na tanzi ili mtu asifikie mwisho wa hatima yake.


Matanzi mengine yanahudhuria hata kanisani, wakati mchungaji anaendelea na mahubiri, wengine wanabadilishana namba za simu ili baadae wawasiliane wao kwa wao. Hilo ni tanzi.  Tanzi hukaa shimoni na kazi  yake kuu ni kuua. Tanzi siyo kamba bali ni mashetani. Ipo njia aliyokuandalia Bwana.  Ndugu wa karibu wakeshaifahamu hiyo  njia ya Bwana (kwa kuiona katika ulimwengu wa roho) hufanya mipango ya kuifunga hiyo njia kwa kutumia kamba za rohoni.


Watu walioamua kuzikata kamba kwa kuokoka leo 05/10/2014
katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro.
ATHARI ZA KUWA NA KAMBA:


·        Mtu mwingine amepewa Baraka ya kutoa ushauri (counselor). Ndugu wa karibu wanakifunga kinywa chake kwa kutumia kamba na badala yake kinywa cha bandia kinawekwa ambacho hakiwezi kabisa kuongea au  kutoa ushauri tena.

·      Anakuwepo dada ambaye anasubiria kuoelewa,  lakini sura yake imebadilishwa na kuwekewa sura ya bandia iliyokakamaa.


MIFANO  KATIKA BIBLIA ALIYEFUNGWA KAMBA NA NDUGU ZAKE:


WAAMUZI 15:9-13 …[Basi Wafilisti wakapanda wakapiga kambi yao katika Yuda, wakajieneza katika Lehi. 10 Watu wa Yuda wakasema, Mbona mmekuja kupigana nasi? Wakasema, Tumepanda ili kumfunga Samsoni, kumtenda yeye kama alivyotutenda sisi. 11 Ndipo watu elfu tatu wa Yuda wakatelemka hata ule ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia, Kadiri ile walivyonitenda mimi, ndivyo nilivyowatenda wao. 12 Wakamwambia, Tumeshuka ili kukufunga, tupate kukutia katika mikono ya Wafilisti. Samsoni akawaambia, Niapieni ya kwamba ninyi wenyewe hamtaniangukia. 13 Wakamwambia, wakisema, Vema, lakini tutakufunga sana, na kukutia katika mikono yao; lakini hakika hatutakuua. Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya, wakamchukua kutoka huko jabalini.]… Hawa ni ndugu ambao wamemkamata ndugu yao Samsoni  na kuahidi kumfunga sana ili baadae wampeleke kwa adui zake. Hawa ndugu hawajamuua ila wamemfunga sana. Zipo 'kamba mbili mpya' ambazo  yamkini wapo ndugu wamekufunga, na ambazo hata wafunguaji wa hapa dunia wameshindwa kuzifungua.


Ndiyo maana wakaati mwingine, zinapokuwepo kamba mbili mpya, mtu anaweza kuhangaika makanisani, akienda huku na kule, akitaka uponyaji lakini bado uponyaji haupatikani. Yesu Kristo alisema,  “lolote mtakalofungua hapa duniani na mbinguni limefunguliwa”… Kamba mbili mpya ni Kuzimu na Mauti. Hizi kamba mbili  mpya, zinatumiwa na shetani ili  kuwafunga watu.  Ndiyo maana Ufufuo na Uzima wanaposema watu wanafufuliwa,  wengine huanza kupiga kelele‼! Si vyema kuwalaumu  wanaonuna juu yetu kwa sababu hawazifahamu kamba hizi mbili mpya ‘kuzimu na mauti’. Wengi hawajazifahamu  kamba hizi mbili mpya, na ndiyo maana shetani anaendelea kuwatesa wengi kwa kuwafunga na kamba hizi mbili mpya zitokazo kuzimu.


UFUNUO 6:8….[Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.]… Mauti na kuzimu ni  kamba kutoka shimoni na ambazo shetani anazitumia. Hizi kamba mbili  mpya ndizo alizofungwa Samsoni na ndugu zake. Maaskofu au wachungaji wengi hawazijui  hizi kamba mbili mpya. Ndiyo  maana hata madaktari wakati mwingine hawana uwezo  wa kutibu baadhi ya magonjwa, kwa sababu ipo siri ya hizi kamba mbili  mpya zitokazo shimoni.


Pindi ukizikata kamba: Utashangaa, asiyekuwa na kazi anapata kazi. Aliyekuwa amekosa mchumba anapata mchumba na hata kuolewa. Wakati mwingine, ofisini hakuna mtu anayekusifia,  lakni pindi muda wa kustaafu unapowadia, au hata huyo mtu akifa,  watu wanaanza kujitokeza na kumsifia. Hapo ukue hakika kuwa, zilikuwepo kamba zilizomfunnga huyo mtu asionekane wakati akiwa ndani ya ajira yako, ila kwa sababu ajira imekoma, sababu ya zile kamba kumfunga haipo.


MAOMBI:
Kwa jina la Yesu, Leo,  kamba zilizonifunga, zikatike. Kamba za kuzimu, kamba za ndugu nilizofunngwa, zikatike katike, kwa Jina la Yesu. Amen

Dada huyu anombewa na AP Steve (Shati la Bluu),
aliletwa na ndugu zake akiwa kwenye godoro akililalia.


JE, UTAWEZAJE KUZIKATA KAMBA”
Kamba hukatwa na mkata kamba ambaye ni YESU mwenyewe. Wale waliokuletea magonjwa, walifanya hivvyo kwa sababu mkata kamba Yesu Kristo hakuwepo. Yesu siyo wa nadharia, yupo hapa hapa. Yesu yupo tayari kuzikata kamba za mauti maishani mwako. Ukitaka mambo yako yaende salama, mpokee mkata kamba maishani mwako - ambaye ni Yesu Kristo.


Baada ya maombi, matumizi ya godoro kulalia huyu dada
hapa Ufufuo na Uzima hayapo tena, ananyanyuka mweyewe.


Kamba zikeshakatika, asiyeweza kula atakula chakula bila tatizo; asiyeolewa ataolewa; asiyeoa ataoa; asiyeweza kutembea atatembea kwa miguu yake; asiye na kazi atapata kazi  mara moja kwa Jina la Yesu. 










Dada aliyekuwa akilalia godoro siku zote, mara hii anatembea
kwa miguu yake mwenyewe. Utukufu kwa Yesu Kristo.


Leo endapo mtu hujampokea Yesu Krsito maishani mwake, ni vyema kufanya hivyo kwa sababu ni Yesu pekee mwenye kikatio cha kamba za mauti na kuzimu.












© Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Kihonda VETA, Morogoro.
 /or
Contact our Senior Pastor:
 Dr. Godson Issa Zacharia
 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778



Share:
Powered by Blogger.

Pages