GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
[KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO]
JUMAPILI: 26 FEBRUARI
2017
MHUBIRI: Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)
Duniani hapa yapo
mateso mengi sana ya aina tofauti tofauti. Kila mmoja wetu kuna wakati aliwahi
kupata mojawapo ya mateso haya kwa namna moja au nyingine. Yesu Kristo mwenyewe aliwahi kupata mateso hata
akasulubiwa msalabani. Tukisoma katika KUTOKA 3:7 neno la Mungu linasema hivi...”Bwana
akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia
kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;”.
Kwa maandiko haya, Mungu anasema “ameona
na kusikia” mateso ya wana wa Israeli waliokuwa wakiteswa huko Misri. Hata
kwa wewe uliyeokoka, ujue kuwa mateso bado yapo, tena siyo machache. Ndiyo
maana katika ZABURI 34:19 imeandikwa
hivi…(Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.).
Kumbe ukiwa mwenye haki mateso yapo pale pale, tena siyo moja wala mawili wala
matatu; ni mateso mengi. Cha kufurahia ni kwamba, Mungu ameahidi kutuponya na mateso haya yote. Kwa nini
atuponye? Ni kwa sababu mateso haya pamoja na wingi wake, hayajatoka kwa Mungu.
Kwa hiyo Mungu anakuja kutuponya na mateso haya yatokayo kwa yule muovu shetani,
na kutuweka huru.
Katika MAOMBOLEZO 3:33 imeandikwa hivi “Maana
moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.” Ni dhahiri
kuwa, Mungu wetu hapendi kutuona tukiwa katika mateso na huzuni. Siyo kweli ktuiana
moo na kusema ni mapenzi ya Mungu kwa mtu afukuzwaye kazi, ambayo alimuomba
Mungu ampatie!! Siyo sahihi pale unapopata ujauzito na baadae mimba kuharibika kusema
eti hayo ni mapenzi ya Mungu. Fahamu kuwa, mateso yote ya aina hii hayatoki kwa
Mungu, kwa kuwa Mungu wetu hapendi kutuhuzunisha.
Watoto wa Showers of Glory Morogoro wakiimba na kucheza mbele za Bwana 26/2/2017 |
Wapo watu wanaojiliwaza kwa kusema “mwenzenu
nimeiningia katika majaribu” au “mwenzenu
nimeingia katika madeni” au mwingine “mwenzenu
nimeingia katika masteso” na mwingine pia “mwenzenu nimeingia katika magonjwa”.. Usikiapo kauli za watu wa
aina hii ujue kuwa, kuna mlango wa mateso na shida wa kishetani uliofunguliwa,
na mtu akaingia katika huo mlango bila kujua. Ni rahisi sana kuingia katika mlango
wa mateso wa kishetani. Kwa kawaida, mlango wa kuingia katika raha, au utajiri
na mafanikio ni mwembamba sana, na wachache sana wanaweza kuuona na kuingia
ndani mwake. Lakini ule mlango wa mateso wa kishetani, ni mpana sana kiasi
kwamba watu wengi wanaingia na kujikuta tayari wamenaswa na mambo ya dunia yaliyomo
mle ndani. Wapo walinzi wanaozuia watu kuingia katika mlango wa baraka. Lengo lao
ni kuachilia watu wasiuone na waingie ule mlango mpana wa kishetani na kukaa
katika mateso siku zote. Sio rahisi upatapo mateso kuwapata watu wa kukushauri
uende kanisani, sanasana wengi watakushauri ubaki na dini yako au uende kwa waganga wa kienyeji n.k.
Umati wa Waumini na Watendakazi wa Ufufuo na Uzima Morogoro wakifuatilia kwa makini Mahubiri ibadani 26/2/2017 |
Kwa kawaida mlango
ni mahali pa kuingilia. Mlango wa kishetani humfanya mtu kuingia katika ngome
ya mateso, na siyo rahisi kutoka humo labda apatikane mpakwa mafuta wa Bwana
aliyeandaliwa maalumu ili akutoe humo. Yesu mwenyewe aliwahi kutangaza kazi
yake ya kuja hapa duniani, tunaposoma katika LUKA 4:18…”Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana
amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa”.
Kwa hiyo wafungwa waliopo ndani ya magereza wataachiwa tu na aliyetumwa
kuifanya kazi hiyo, yaani Yesu Kristo pekee. Yesu mwenyewe ndiye mlango wa
baraka zetu. Imeandikwa katika YOHANA
10:1 “Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni
katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni
mnyang'anyi”.
UKIRI
Nakataa kuingia
katika mlango wa mateso kwa Jina la Yesu. Ewe mlango mpana wa kishetani
ulioandaliwa ili mimi niingie humo nakataa mimi na nyumba yangu kuingia
mlango huo kuanzia sasa kwa Jina la Yesu. Nakataa kupanda farasi
aliyeandaliwa kunipeleka kwenye mateso, kwa Jina la Yesu. Amen
|
Katika kipindi cha
zamani, miji ilijengwa kwa kuta kuizunguka na kujweka mlanjgo wa kuingilia.
Ndivyo ilivyofanyika katika mijikama Yeriko na hata Yerusalemu. Lengo la
kufanya ote haayo ni kuismarisha ulinzi, kujilinda. Hata hivyo, katika
nyakati zetu hizi, ulinzi wetu siyo
wakimwili bali kupambjana na maadui katika ulimwengu wa roho. Imeandikwa katika
EFESO 6:12…”Kwa maana kushindana kwetu sisi
si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza
hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” na pia
katika 2KORINTHO 10:3-4 imeandikwa
hivi “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya
mwili; 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu
hata kuangusha ngome;)”. Malango ni
mashetani, na walinzi wake ni
mashetani na ngome yenyewe ni ya kishetani, ila wanaoingizwa mle ndani na
wanadamu.
Kila penye mlango
pana mlinzi wa kuruhusu watu kuingia au kutoruhusu waliomo ndani kutoka. Ndivyo
ilivyoandikwa katika YOSHUA 2:1-3 (Yoshua,
mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza,
akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani
kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. 2 Mfalme wa Yeriko
akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo
usiku, ili kuipeleleza nchi. 3 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu,
akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako,
maana wamekuja ili kuipeleleza nchi.). Jambo la kujiuliza hapa ni, Mfalme
alijuaje kwamba kuna wapelelezi walioingia humo mjini?. Ni kwa sababu walinzi
wa kutazama kutokea juu ya ukuta walikuwepo na ndio waliowaona wale wapelelezi
waliotumwa na Yoshua.
Mlango wa Mateso wa
Kishetani unao walinzi ambao nao ni mashetani, wanaokaa mlangoni mwa ngome za
mashetani. Unapoyaona mateso katika mwili wako, ujue kuwa mateso hayo
yalishatengenezwa katika ulimwengu wa roho kabla ya kudhihirishwa katika mwili.
Unaweza kuwa tayari umeshakamatwa, na ndiyo maana unakiri kuwa umeingia katika
mateso!!. Anayetaka kukuingiza katika mateso anakaa katika mlango, na ujue kuwa milango hii ni ya kiroho.
Mashetani
yanayolinda malango yapo katika idara kuu tatu:
1.
Idara ya Kukamata (Arresting Department).
Hawa hufanya kazi
ya kuwinda watu, kisha kuwakamata na kuwaingiza mle kwenye lango la mateso. Kwa hiyo ukiona mtu yupo mwenye
mateso (mfano: mwenye magonjwa, dhiki, uzinzi, ulevi n.k), ujue aliwahi
kuwindwa, akakmatwa na kuingizwa mle kwenye ngome hiyo ya mateso. Imeandikwa
katika 1PETRO 1:8 “Mwe
na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,
huzungukazunguka, akitafuta mtu ammeze.” Watu wanapokamatwa na kuingizwa humo ngomeni,
huteswa sana. Mateso ya magonjwa, hasara, kukataliwa, kuachwa, ndoa kuharibika
n.k. Endapo teso moja likiisha hutokea teso lingine. Mungu mwenyewe anayajua haya, na ndiyo maana
akasema “Mateso ya mwenye haki ni mengi
sana” Misukule wengi wanakamatwa katika idara hii. Na wengi wa watu
waliowahi kukaa msukuleni utakuta wakihadithia mateso ya aina hii (kulishwa
pumba, damu za watu n.k). Mashetani wanaotesa watu waliomo humu langoni ni wenye
wivu sana. Ukionekana unakula vizuri, watakuwinda na kukuingiza katika hayo
mateso ili usiweze kula vizuri tena.
Ni wajibu wetu
tuliookoka kuingia magotini na kuomba kwa bidii ili kuwatoa watu walionaswa katika
hizi ngome za mateso za mashetani. Kuna watu leo hii ni wezi sugu na hata wakiaambiwa
waache wizi wanashindwa kabisa. Watu wengine wana tabia ya ukahaba, na imekuwa
ngumu kwao kuiacha tabia hii. Wengine ni watumiaji wa dawa za kulevya, tena hata
wanajidunda sindano za dawa hizi, pamoja na maumivu ya kujjidunda sindano
yalivo lakini bado wapo tayari kuvumilia tu!!. Mateso yote haya husababishwa na
mashetani wanaotesa watu wakiwa katika hizi ngome za mateso. Leo tuanze kwa
kumpiga huyu anayekamata watu (Arrester)
yaani shetani na kumlazimisha kutachia kwa Jina la Yesu.
Vijana wa Showers wakionesha umahiri na vipaji vyao namna ya kucheza mbele za Bwana Jumapili 26/2/2017. |
UKIRI
Leo wale wote
wanaowinda maisha ninawaponda, ninakushinda ewe mzimu, ewe joka, imeandikwa kila silaha ya uwindaji iliyopangwa inipate
haitafanikiwa, imeandikwa nao wakamshinda kwa Damu ya Mwanakondoo, nami
nawashinda wawindaji wote wa maisha yangu kwa Damu Ya Mwanakondoo. Mashetani
wa mateso leo ninawaponda kwa Jina la Yesu. Amen
|
Hata hivyo katika idara hii, mtu anaweza kuteswa kwa kitambo kidogo tu, pengine siku au wiki moja au hata mwezi au mwaka. Wanaweza kumuacjhim mtu na baadae wakaja tena kumwinda upya.
2.
Idara ya Kulinda Mtu abaki katika mateso aliyo nayo milele
Hawa hawataki
kabisa aliyekamatwa aachiliwe au kuwekwa huru. Katika idara hii, mashetani wake
hawaachi mtu kuwa huru. Imeandikwa katika ISAYA
14:17… “Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua
wafungwa wake waende kwao? ”. Mtu akeshaingizwa kwenye idara hii,
asitarajie kuwa huru, ni sawa na kifungo cha maisha. Mashetani haya hukasirika
yanapoona kuna watu wanaofanya juhudi ili mtu wawekwe huru. Ndiyo maana, utaona
baadhi ya ndugu wakizuia mgonjwa asipelekwe kanisani ili kuombewa. Uonapo watu wazuiaji
wa aina hii, ujue ni wale ambao wanafanya kazi na mashetani katika idara hii ya
kuzuia, na hufanya kazi ya kumfanya mtu abaki katika mateso yake.
Katika ZABURI 24:7-10 Imeandikwa hivi “Inueni
vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu
apate kuingia.8 Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana
hodari wa vita.9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi
malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. 10 Ni nani huyu Mfalme wa
utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.”. katika hili,
utaona kuwa zipo familia au koo zenye mateso ya jkufana fanana. Mfano ni pale Sara mke wa
Ibrahimu alikuwa tasa, na hakuzaa kwa muda tarajiwa, na hata alipompata Isaka
uzeeni, shida hii ilijirudia kwa kumpata Rebeka mke wa Isaka kwa kutopata mtoto
kwa wakati, na baadae shida hii ikampata pia Leah mke wa Yakobo. Hayo ni mashetani
yazuiayo, na hata katika familia na koo mbalimbali yanakuwepo ili kusababisha
mateso ya kufanana.
Mmoja wa watu waliokuwa na Mapepo akipewa huduma ya maombezi Jumapili 26/2/2017 Ufufuo na Uzima Morogoro |
3. Idara ya Kufunga Mlango wa Baraka
Haya ni mashetani
yatakayomzuia mtu kuingia katika baraka zake. Mashetani haya yanajua kuwa mtu
huyu ni mwaminifu na kwamba yameshindwa kuingia ndani yake au hata kumkamata
kwenye mateso. Mashetani haya yatakaa mlango wa baraka za mtu na kufanya kazi
ya kumzuia mtu huyu, kwa sababu yanajua kuwa akipenya hapo basi maisha ya mtu
huyu syatakuwa mazuri mno kupindukia. Mathalani mtu akitaka kuoa, au kufanya
bishara fulani nzuri au fursa nzuri ya kujiendeleza kimasomo, mashetani haya
yatahakikisha kuwa mtu wa aina hiyo hawezi kupenya hapo. Mashetani haya ni ya
kuzuia mtu asifikie ufanisi wa anachokifanya.
Yesu na wanafunzi
wake waliwahi kuzuiliwa kuuingia Mji wa Wagerasi. Tukisoma katika MATHAYO 8: 28-34 imeandikwa “Naye
alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana
naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. 29
Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je!
Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? 30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la
nguruwe wengi wakilisha. 31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache
twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe. 32 Akawaambia, Nendeni.
Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi
gengeni hata baharini, wakafa majini. 33 Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda
zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia. 34 Na
tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi
aondoke mipakani mwao). Huu mji wa Wagerasi uliitwa pia Decapolis (maana
yake ni miji 10 iliyoungana pamoja). Ndani ya watu hawa wazuiaji yalikuwepo
mapepo yaliyoweza kuingia ndani ya kundi la nguruwe 2,000 nao wakakimbilia
baharini na kuangamia wote. Mji wa Wagerasi
ulikuwa umezuiliwa watu
kutouingia, na wazuiaji wake walikuwa ni
wakali mno. Ndivyo ilivyo hata kwako
leo hii, kwamba unapotaka kuingia katika eneo la baraka zako,
watajitokeza wazuiajjji ili usifanikiwe.
Hata hivyo
wazuiaji hawa hawana shida ya kuwazuia watu wale wasiomwamini Yesu, kwa sababu
watu wa aina hiyo wepesi kumsujudia shetani katika muda wowote ule. Ndiyo maana
shetani alimjaribu Yesu ili eti amsujudie kama sharti la kumpatia fahari za
dunia hii. Imeandikwa LUKA 4:5-7 “Akampandisha
juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi
akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi
mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu
yote yatakuwa yako). Ndiyo kusema, wapo watu waliotajirika leo hii
lakini kupitia njia za kumsujudia shetani na mawakala wake (waganga wa kienyeji,
wachawi, wasoma nyota n.k).
Kwa wewe
uliyeokoka unachopaswa kufanya kinyume na mashetani yanayozuia mlango wa baraka
zako ni kuamka kama shujaa wa Bwana na kuyang’oa hayo malango na kisha
kuwapiga walinzi wake kwa Jina la Yesu. Amua leo kuingia katika baraka zako kwa
kuomba kwa Bidii kwa Jina la Yesu. Kumbuka alichokifanya mnadhiri wa Mungu
Samsoni pale alipozuiliwa na lango la mji ule wa Gaza, alichokifanya ni kuling’oa
lile lango na kuondoka nalo. Yesu Kristo anayetuponya na mateso yupo hapa leo
kwa ajili yako. Leo tutayang’oa malango yanayozuia baraka zetu na kisha
kumiliki yale Bwana aliyokusudia kwetu kwa Jina la Yesu.
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KIPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
SIMU: 0719 798778 (Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/
ENGLISH
© Media and Information Ministry
GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +255719612874 / +255713459545
|