GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
[KANISA LA UFUFUO NA UZIMA]
MOROGORO
JUMAPILI: 12 MARCH 2017
MHUBIRI: PASTOR Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP MOROGORO)
Pastor Dr. Godson Issa Zacharia akihubiri katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro 12/3/2017 |
Imeandikwa katika YOHANA 1:1, 14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye
Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili,
akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye
kwa Baba; amejaa neema na kweli”.
Huyo mwanzo
alikuwako kwa Mungu. Yesu ni Mungu aliyekuja kwa namna ya mwili. Yesu wetu ni
Mungu aliyeamua kuja duniani akaishi kama wanadamu kwa namna zote. Alizaliwa na
Mariamu na akalelewa pamoja na babaye wa kufikia Yusufu. Akalelewa na kukua kwa
kimo na hekima. Na baada ya miaka 33 akaanza kuifanya kazi ya ukombozi.
Bwana Yesu alikuja
mahsusi ili kuwaweka huru mateka, na watu waliofungwa na nguvu za giza. Ndiyo maana
katika utangulizi wa utambulisho wa kazi zake, Yesu alisema yafuatayo kama
ilivyoandikwa katika LUKA 4:16-18 “Akaenda
Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama
ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya,
akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu
yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha
huru waliosetwa,”. Baada ya kusoma maaandiko haya, Yesu alikirudisha
kitabu na kuwaaambia makutano kwamba
maneno haya yametimia baada ya kusikika masikioni mwao. Huwezi kuifanya
kazi ya Bwana kama hauna Roho wa Bwana. Na hii ni saa ya waliotekwa kurudishwa katika Jina la Yesu.
Unapotangaza
kuwaweka huru mateka ujue kuwa umetangaza
vita, na watakuwepo watu wengi wa kukuzuia. Ndivyo ilivyotokea hata kwa Yesu.
Imeandikwa katika LUKA 4:.29-30.. .(Wakaondoka
wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao
umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; 30 lakini yeye alipita katikati yao,
akaenda zake.). Ni wakati wako pia kupita katikati ya wanaukuzuia.
Katika ISAYA 14:12-17 imeandikwa…(Jinsi
ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi
ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako,
Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;
Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano,
Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za
mwisho za shimo. 16 Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana,
wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa
falme; 17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa,
akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? ). Huyu anayeongelewa hapa ni SHETANI. Ulimwengu huu wote umefanywa UKIWA.
Maana yake, kama ni mtu
aliyoea, mwenza wake anapotwaliwa, anabaki na ukiwa. Unaweze kujiuliza, inakuwa
je sasa Biblia kusema ulimwengu umekuwa ukiwa ilhali dunia inao watu wapatao
bilioni saba? UKIWA unoazungumziwa katika maandiko haya ni kwa sababu hao watu
tunaowaona barabarani leo hii, wengi wao HAWAPO. Wengi wa watu tunaowaona leo
hii wameiibiwa na shetani, na kwa maana
hiyo hawapo katika hali ile ya asili ambayo
Mungu aliwaumba ili waishi. Wapo watu wengi sana wapo mashimoni, wametekwa na
muovu shetani. Ndiyo maaana watu
misukule wanapoombewa hapa Kanisani na Kurudishwa, ukiwauliza huko mashimoni ulipokuwa umeacha
watu wengine wangapi, huwa wanajibu kuwa wameaacha watu wengi sana wakiwa humo
mashimoni au pengine misituni au makaburini, watu wasiohesabika.
Watu walioko
kuzimu ni wengi kuliko waliopo hapa
duniani. Kuna mtu anaweza kujjiuliza swali, iweje waliokufa wawe wengi
zaidi yetu wakati katika jamii yake
pengine wapo watu zaidi ya saba na hakuna aliyekufa? Hebu tuanze kwa kusoma
kitabu cha ISAYA 42:22 (Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na
kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa
mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.).
Kwa kuyachambua maandiko haya, utaona kuwa, wanaoitwa watu hapa ni wanadamu
kabisa, ambao kwa lugha nyingine tunawaita MISUKULE
(watu walioibiwa). Msukule Ni tofauti na tunaposema MIZIMU, kwa sababu Mizimu ni roho za mashetani zilizopo ndani ya
watu waliokufa zamani. Yaani endapo shetani alikuwa ndani ya mtu fulani kabla
hajafa, na mtu huyo akifa, zile roho za mashetani zilizokuwa ndani mwake, hujigeuza na kufanya kazi kwa niaba ya huyo
mtu aliyekufa. Majeshi ya Wafu ni roho za hii mizimu.
Kumbe basi, mtu
anaweza KUIBIWA, AKATEKWA na kisha AKANASWA katika mashimo. Ipo tofauti
kati ya kuibiwa na kutekwa. Tukumbuke kuwa Mtu anazo sehemu tatu: Mtu ni ROHO, yenye NAFSI inayokaa kwenye
nyumba, na hiyo nyumba inaitwa MWILI. Ndiyo kusema kuwa Roho ya mtu inaweza
ikaibiwa kutoka ndani ya mwili wake. Inapofanyika hivyo, mwili wa mtu Yule
unaobaki pale unakuwa na mauzauza mengi, mara magonjwa, mara tabia zisizoeleweka.
Na ROHO ile iliyobiwa inakuwa imetekwa na kulindwa na mashetani kiasi kwamba
roho hii haiwezi tena kuurudia ule mwili wake. Hata hivyo, mtu aliyeibiwa aina hii akiletwa
kanisani, na watu wakianza kuomba maombi ya kushindana, na kumuita NJOO mtu huyu
hurudi tena katika asili yake ya awali.
Umati wa Watendakazi na Waumini wa Ufufuo na Uzima Morogoro wakimwabudu Bwana katika Roho na Kweli Jumapili 12/3/2017. |
Zipo aina kama tatu za watu walioibiwa
(misukule):-
1. Mtu anakuwa amechukuliwa mzima mzima na kufichwa.
Inawezekana akaletewa ugonjwa wa kumfanya aonekane amekufa ghafla. Watu wakienda
kuzika mtu huyu inakuwa kuwa wamezika kitu mithili ya gogo tu, waa siyo Yule
Mtu. Na wachawi wakeshaona lile gogo limezikwa, huondoka na ule mtu waliyemeka
na kumficha na kwenda kumtumia kwa kazi mablimbali akiwa msukule.
2. Aina nyingine ya mtu aliyeibiwa (msukule) ni ile
ambayo mtu anaibiwa akiwa mzima mzima na kupotea kwa mazingira tata. Mtu huyu hutafutwa
na watu kwa njia zote, ziwe za kipolisi na vyombo vya habari lakini mtu huyo
hapatikani kamwe. Hata hivyo, wakiwepo majeshi ya Bwana wakianza kuomba, mtu wa
aina hii hurudi tena kwa Jina la Yesu, na hata kuweza kusimuliwa mahali alipokuwa ametekwa na kuwekwa.
3. Aina ya tatu ni ya kitaaalamu zaidi. Hii ni ile ambayo
watu huiba roho na kwenda kuziuza. Kwa kuwa mtu ni roho, na maandiko yanasema “Roho
ndiyo itiayo uzima na mwili haufai kitu”, humaanisha kuwa mtu wa aina hii roho yake
hutolewa ndani na kuipanda roho ya kitu kingine, ili asionekane amekufa na watu
wa pembeni wasifahamu kuwa alishaibiwa.
Mtu ambaye roho yake ilishaibiwa na kuwekewa roho ingine (iwe ya majini,
mapepo, majoka n.k). Na mtu wa aina hii anakuwa na mikosi, balaa, magonjwa na
matatizo yasioyisha. Tabia zake pia hubadiliaka ghafla. Pengine Mtu alikuwa na
bidii sana lakini kwa sasa hawzi tena
kuwa kama mtu yule wa zamani. Hii ni kwa sababu mtu aliyeko ndani mwake siyo
Yule roho wake wa asili. Endapo utakutana na mtu wa aina hii, maombi yako yawe
ya kumuita NJOO KWA JINA LA YESU, naye atarudi katika asili yake tena kwa Jina la Yesu.
Je, una uhakika
mume unayeishi naye leo bado ni yuleyule uliyeoana naye miaka kadhaa iliyopita
aliyekuwa anakupenda sana na kukuita majina yote mazuri? Je, una uhakika dereva
wa daladala aliyekuendesha na basi lake leo YUMO au ni mtu wa kawaida?
Imeandikwa katika YEREMIA 50:33 33 “Bwana wa majeshi asema hivi, Wana
wa Israeli, na wana wa Yuda, wameonewa pamoja; na wote waliowachukua mateka
wanawashika sana; wanakataa kuwaacha”. Maelfu ya watu wameonewa sana,
na ndiyo maana Biblia inasema dunia imkeuwa ukiwa. Na mbaya zaidi ni kwamba huyo aliyewachukua mateka (shetani)
hataki kuwaachia.
UKIRI
Walionishikilia makaburini,
mashimoni au magerezani waniachie kwa Jina la Yesu. Achia ndoa, achia afya,
kwa Jina la Yesu. Leo ninaamuru kwa mamlaka ya Jina la Yesu, leo achia vyote kwa
Jina la Yesu.
|
Platform wa Ufufuo na Uzima Morogoro, wakiwa na furaha wakiimba na Kumsifu Bwana Yesu Jumapili 12/3/2017. |
Tunaposoma katika AYUBU 33:29 imeandikwa hivi (Tazama,
hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu).
Roho ya mtu inaweza kutoka ndani yamwili wa huyo mtu. Imeandikwa katika 2 KORINTHO 12:2-4…(Namjua mtu mmoja katika Kristo,
yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba
alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu
ya tatu. 3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa
nje ya mwili sijui; Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia
maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.). Kumbe unaweza
kumuona mtu lakini mtu huyo akawa ndani au nje ya mwili wake (HAYUMO).
TABIA ZA MTU AMBAYE HAYUMO KATIKA MWILI WAKE WA ASILI:
1. Mtu anakuwa hawezi kufanya maamuzi. Ni mtu ambaye hata ukimpa ushauri kuwa kwa
umri alio nao akaoe, anashindwa kufanya maamuzi ya maisha yake mwenyewe.
2. Mtu anayefanya mambo mengine ambayo binadamu mwingine
hawezi kuyafanya. Mathalani, waweza kuzisoma taarifa za kushangaza kwenye
magezeti kama vile “kijana kumuoa mama
yake mzazi”, au taarifa kama “baba wa miaka 70 kambaka mtoto wa miaka 8”.
Tabia zingine ni kama zile za kusikia kuwa “Daktari kuacha kutoa huduma kwa mgonjwa mwenye shida ya kujifungua, na kwenda
kustarehe kwenye mabaa”.
3. Mtu ambaye anasongwa na magonjwa mengi. Yaani mtu huyu
anapata ugonjwa wa aina hii na huu
ugonjwa ukiondoka unatokea ugonjwa mwingine na mengine bila kukoma.
4. Mtu anayesongwa na mikosi na balaa nyingi mfululizo. Mtu
huyu anaweza kuomba maombi mengi sana, akitokea kanisa moja hadi jingine. Kwa
kuwa mtu ni roho, basi endapo ndani yake imewekwa Roho ya mashetani, maana yake
ni kuwa wachungaji wanapomuombea mtu wa aina hii ambaye hayumo, baraka wanazomuombea
zinaelekea kwa ile roho iliyopandwa ndani mwake. Shetani aliyeko ndani mwake
hufurahia sana kwa sababu kilichomo ndani ni roho za mashetani. Ni wajibu wa
wachungaji kuwa makini sana, siyo kila mtu kumuombea baraka, bali kabla ya
kjufanya hivyo ni kung’oa roho zilizopo ndani mwa mtu mwenye kuhitaji maombi. Ukiwa
mchungaji unaweza kubariki lakini kumbe uliyembariki ni joka liliko ndani mwa
mtu husika.
NB: Dalili zinginezo za mtu ambaye hayumo katika mwili wake wa asili
tutazichambua katika Ibada za katikati ya Wiki Ijayo, kuanzia kesho Jumatatu.
Watendakazi na Waumini wa Ufufuo na Uzima Morogoro wakifuatilia Somo "Amekuja Kuwaweka Huru Mateka" 12/3/2017 |
UKIRI
Ninakataa kukaa
kwenye kundi la shimoni kwa Jina lka Yesu.
|
Katika UFUNUO 18:9-13 Imeandikwa (Na
hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na
kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake; 10 wakisimama mbali kwa hofu ya
maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na
nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. 11 Nao wafanya biashara wa
nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; 12
bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri,
na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi,
na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha
shaba, na cha chuma, na cha marimari; 13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na
marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano,
na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.).
Kwa hiyo kumbe wapo “WAFANYABIASHARA WA
MIILI NA ROHO ZA WANADAMU”. Hawa
kwa lugha nyinigne ni wafanyabiashara wa
kichawi.
Imeandikwa katika EZEKIELI
13:18-19…(useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi
katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili
wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai
roho zenu wenyewe? 19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya
makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao
haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa
kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.). Leo tutashughulika na
watu wanoiba roho za watu wengine kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Kwa jJIna la
Yesu, Leso na hirizi za wachawi leo nazichana chana kwa Jina la Yesu. Bwana
Yesu naomba leo unigeuze niwe kisu cha Bwana ili niwafuatie wote walioniteka.
Yamkini akili zangu zimetekwa, au mwili wangu umetekwa. Najua kwamba Bwana
Yesu ni mkombozi wangu uliyekuja kuniweka huru kwa Jina la Yesu. Ninauruka ukuta
kwa Jina la Yesu. Walionifunga na kunizuia kizuizini, au kwenye mashimo leo
ninawafyeka. Leo nalaegeza kamba za mauti
zilizoniweka shimoni kwa Jina la Yesu. Imeandikwa “Nao wakamshinda kwa Damu ya
Yesu”, Wewe uliyenilinda mashimoni, niachieni leo kwa kuwa
nimewashinda kwa Jina la Yesu. Amen
|
Inawezekana kuwa
mtu uliyesikia habari hizi hujaokoka,
nakushauri fanya maamuzi yako leo ya kuokoka. Cha kufanya leo ni kumkubali Yesu
maishani mwako kwa maana ya kuokoka ili ukiwa upande wa Yesu ufanyike kiumbe
kipya na YESU atakuweka huru wala hutakuwa
mateka tena kwa Jina la Yesu.
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KIPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
SIMU: 0719 798778 (Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/
© Media and Information Ministry
GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +255719612874 / +255713459545
|