GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
{KANISA LA UFUFUO NA
UZIMA → MOROGORO}
(SIKU 8 ZA SEMINA YA KURUDISHA KILA KILICHOIBIWA)
WAHUBIRI
1. Mch. Moses Chami - Ufufuo na Uzima Babati
2. Mch. Aaron Ulaya - Ufufuo na Uzima DSM
3. Mch. Kelvin
Mwaipopo - Ufufuo na Uzima Nzega, Tabora
4. Mch. Happiness Godson - RP (Morogoro).
5. Mch. Samson Gwajima - SNP (Mwanza).
6. Mch. Godson Issa Zacharia - SNP(Morogoro).
===========
JUMAPILI: 30 APRIL 2017
SEMINA SIKU YA KWANZA
MHUBIRI: PASTOR SAMSON GWAJIMA (SNP MWANZA)
Pastor Samson Gwajima akifundisha kwa habari ya majeshi yaliyo jipanga Msukule, Jumapili ya Leo 30/04/2017. |
Swali ambalo
tungependa kujiuliza hapa ni: “MSUKULE
NI NINI?” Jibu lake ni kuwa, Msukule
ni mtu kabisa aliyeibiwa / au kuchukuliwa na watu wengine. Yawezekana mtu huyo alikufa
na sisi tukawaza kuwa alikufa kifo cha kawaida tu, lakini kumbe mtu huyo alichukuliwa
na wanadamu waovu na anatumikishwa kazi mbalimbali huko aliko. Katika ISAYA 42:22 imeandikwa “Lakini
watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo,
wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa
mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.” Katika maandiko haya, neno
“Mashimo” linamaanisha mashimo yaliyopo katika ulimwengu wa roho. Inawezekana hata
katika biashara zetu, wapo waliojipanga ili kuiba biashara hiyo, au wengine
wamejipanga kuiba ndoa, masomo yako, afya yako n.k na kuyaweka mashimoni. Leo
tutayaharibu mashimo yote ya rohoni kwa
Damu ya Yesu.
Tukisoma katika ZABURI
27:3-5 Imeandikwa (Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo
wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. 4 Neno Moja
nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana
Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni
mwake.5 Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika
sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.). Leo Neno moja tu ulitake kwa Bwana ili kila kilichoibiwa kirudi kwako tena kwa Jina la Yesu. Neno hili moja
linatafutwa kwa Bwana pekee, siyo kwa waganga wa kienyeji kama wengine
wasiomwamini Yesu wanavyofanya.
Mungu katika kazi ya uumbaji aliumba viumbe wa aina mbili: viumbe vya rohoni na viumbe vya mwilini. Na hata sisi tunapoongelea majeshi yanayojipanga kinyume nasi tunamaanisha yale ya aina mbili: Majeshi ya kiroho na Majeshi ya Kimwili. Ndiyo maana ni vizuri kufahamu leo kuwa MIZIMU siyo ndugu zako bali ni mashetani, na hivyo hupaswi kushirikiana nayo kwa jambo lolote. Mizimu yakikujia ndotoni yafyeke na kuyakemea ili yasikurudie tena kwa Jina la Yesu. Katika WAEFESO 6:12 Imeandikwa “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”. Kumbe Biblia inatufundisha kuwa wakati tunaomba tunakuwa tunashindana na falme. Hatupigani ngumi kwa namna ya mwilini. Shetani anao wafalme wanaomsaidia katika kazi zake za giza. Na hivyo majeshi tunayoshindana nayo ni majeshi ya pepo wabaya. Hakuna mapepo-wazuri kama ambavyo imani zingine zinavyosema. Mapepo yote kihalisia ni mapepo-mabaya na yanafanya kazi zao katika ulimwengu wa roho. Ni majeshi yanayomfanya mtu kuugua na kufa ghafla, na mwishowe wale wasioelewa ukweli wa msukule wanakubaliana na kifo cha aina hii huku wakijifarijjji kwa kusema “Bwana alitoa na Bwana ametwaa”, kumbe siyo kweli. Leo tusikubaliane na vifo vya aina hii kwa Jina la Yesu, bali tutarudisha vyote vilivyoibiwa na mashetani kwa Jina la Yesu.
Maelfu ya washirika na watenda kazi wakifuatilia kwa umakini mafundisho ya neno la Mungu Leo 30/04/2017. |
Mungu katika kazi ya uumbaji aliumba viumbe wa aina mbili: viumbe vya rohoni na viumbe vya mwilini. Na hata sisi tunapoongelea majeshi yanayojipanga kinyume nasi tunamaanisha yale ya aina mbili: Majeshi ya kiroho na Majeshi ya Kimwili. Ndiyo maana ni vizuri kufahamu leo kuwa MIZIMU siyo ndugu zako bali ni mashetani, na hivyo hupaswi kushirikiana nayo kwa jambo lolote. Mizimu yakikujia ndotoni yafyeke na kuyakemea ili yasikurudie tena kwa Jina la Yesu. Katika WAEFESO 6:12 Imeandikwa “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”. Kumbe Biblia inatufundisha kuwa wakati tunaomba tunakuwa tunashindana na falme. Hatupigani ngumi kwa namna ya mwilini. Shetani anao wafalme wanaomsaidia katika kazi zake za giza. Na hivyo majeshi tunayoshindana nayo ni majeshi ya pepo wabaya. Hakuna mapepo-wazuri kama ambavyo imani zingine zinavyosema. Mapepo yote kihalisia ni mapepo-mabaya na yanafanya kazi zao katika ulimwengu wa roho. Ni majeshi yanayomfanya mtu kuugua na kufa ghafla, na mwishowe wale wasioelewa ukweli wa msukule wanakubaliana na kifo cha aina hii huku wakijifarijjji kwa kusema “Bwana alitoa na Bwana ametwaa”, kumbe siyo kweli. Leo tusikubaliane na vifo vya aina hii kwa Jina la Yesu, bali tutarudisha vyote vilivyoibiwa na mashetani kwa Jina la Yesu.
LUKA 8:29-30 imeandikwa
(Kwa
kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara
nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile
vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. 30 Yesu akamwuliza, Jina
lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia.).
Tunajifunza kuwa kumbe Mungu anataka
uende mahali fulani lakini wapo waliojipanga kukuzuia usipafikie. Yesu alimuuliza Yule mtu, jina lake ni nani naye akajibu ni “JESHI”. Ina maana kuwa unaweza kumuona mtu anazo tabia za ajabu
ajabu lakini kumbe tabia hizo zimesababishwa na majeshi ya pepo wabaya yaliyokaa
ndani mwake.
Katika MARKO 5:9 Imeandikwa “Akamwuliza,
Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.”. Kumbe
kuna watu wana shida au mambo yao fulani hayaendi vizuri, lakini ni kwa sababu
yapo mashetani mengi ndani yake yanayomzuia. Tukisoma katika MARKO 5:15 neno la Mungu linasema “Wakamwendea
Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye
ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.” Kumbe basi mtu akiwa na mashetani
haoni hata umuhimu wa kuvaa nguo.!! Tunajifunza pia kuwa ukiwa umechukuliwa msukule
/ au umeibiwa unakuwa “hauna akili”. Ni vizuri kujua mambo kadhaa kadhaa
yaliyopo katika ukoo wako au familia yako na kurudisha akili zote zilizoibiwa kwao
kwa Jina la Yesu.
KWA NINI NI MUHIMU MTU ARUDISHWE KUTOKA MSUKULENI?
Katika 1WAFALME 22:20-22 imeandikwa (Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee RamothGileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi.21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. 22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo.). Tunajifunza kuwa kumbe mashetani yanaweza kutumwa na kupepesa uongo kila mahali na watu wakadhani ni uongo ule ni ukweli. Pengine Utmuona dada ni muongo au baba fulani ni muongo sana, lakini ni kwa sababu ya kuingiwa na mashetani haya ya uongo ndani mwao. Endapo hauchukii kitu fulani hicho kitu hakiwezi kuondoka. Leo ni siku ya kukataa kukumbatia mapepo ya uongo kwa Jina la Yesu.
Katika MARKO 5:1-21 Tunaisoma ile habari ya
mtu aliyepaswa kuwa mchungaji na mhubri wa Injili lakini majeshi ya pepo
wachafu yalimuingia na kumzuia kwa kumfanya akae makaburini muda wote. Kila jambo
lako lililokuzuia lazima leo likuachie kwa Jina la Yesu. Yamkni ni katika
biashara yako, au ndoa yako, au masomo au afya yako, leo KILA KILICHOIBIWA LAZIMA KIRUDI KWAKO TENA kwa Damu ya Yesu. Sisi hatuhitaji
kujua jina la huyo shetani kwa sababu shetani mara zote ni muongo, ila
tunachotaka ni kuona kila kilichoibiwa kinarudishwa kwako kwa Jina la Yesu.
MWANZO 32:1-2 imeandikwa (Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye. 2 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu.). Kwa kawaida malaika ni watumishi wetu. Tunao uwezo wa kuwatuma malaika na kwenda kupambana na majeshi yaliyojipanga kinyume nasi kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Kila majeshi
yaliyoniibia ninayawashia moto kwa Jina la Yesu. Amen
|
Resident Pastor Happiness Godson akimwombea mmoja wa watu waliokuwa wamechukuliwa msukuleni leo 30/04/2017 |
Kwa kawaida Majeshi
ya pepo wabaya yanakuwa na walinzi wanaosimamia shida ya mtu. Wanaweza kuwa ni
walinzi wa kusimamia mtu asiwe na afya, asiwe na ndoa nzuri, asiwe na biashara
au kipato n.k. Biblia inasema kuwa “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;
Na wao waupendao watakula matunda yake.” (MITHALI 18:21). Kadiri unavyokiri kinyume ndivyo utakavyopokea kile
ulichokikiri kwa ulimi wako. Jambo lolote utakalotamka kwa kinywa chako linakuwa
lenye mamlaka na lazima litakuwa. Ndiyo maana imeandikwa katika MATHAYO 18:18 kuwa “Amin,
nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo
yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni”. Leo lazima
turudishe vyote vilivyoinbiwa kwa Damu
ya Yesu. Kuanzia leo tunawafunga kila majeshi waliojipanga kinyume nasi, na
kuuwasha moto kwa Damu ya Yesu dhidi ya majeshi ya pepo wabaya waliojipanga kinyume
nasi kwa Jina la Yesu.
Hata hivyo hauwezi kumpinga shetani wakati yeye bado ni baba yako. Ni lazima kuhama kwanza kutoka katika ulimwengu wa mashetani na kumjia YESU ili kuwa rahisi kumshinda huyu muovu shetani. Endapo katikati yetu leo yupo mtu ambaye hajaokoka, ni fursa pekee kwako kumpa Yesu maisha yako.
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KIPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/