GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA → MOROGORO}
JUMAPILI: 25 JUNE 2017
MHUBIRI: PASTOR JOYCE MAKOGA (SNP-DUMILA)
Yapo mambo ambayo yanatuzuia sisi kutouona Ufalme wa Mungu. Haijalishi umeokoka kwa muda mrefu namna gani. Kitakachotokea ni kuwa, wewe unayetenda mambo ya jinsi hiyo utaonekana tu kama msindikizaji siku ile Yesu atakaporudi kulichukua Kanisa lake. Imeandikwa katika WAGALATIA 5:19-21 (Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu). Haya ni mambo ambayo kwa macho ya kawaida, watu wengi wameanza kuyazoea, lakini neno la Mungu linasema “kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu” Na pia imeandikwa katika 1WAKORINTHO 6:9-10 (Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi).
Siku ya Leo tutayaangalia maneno ya Mungu kuhusiana na dhambi ya Wizi. Katika kanisa, WIZI umezuiliwa, na kila aibaye asitarajie kuuona Ufalme wa Mungu. Endapo unafunga au kuomba yote hayo bado ni mambo mazuri, lakini endapo unamuibia Mungu ujue kuwa hautaweza kuuona Ufalme wa Mungu. Imeandikwa katika MALAKI 3:7-11 (Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? 8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.). Biblia inasema pale ilipo hazina yako ndipo ulipo moyo wako. Kwa lugha nyingine, ukiona mtu anakuwa mgumu sana katika kumtolea Mungu, ujue kuwa moyo wake upo katika hiyo pesa. Je, hazina yako imewekwa wapi? Mungu huuangalia moyo na siyo kiasi cha fedha unayomtolea Mungu. Wapo watu ambao, hazina za mioyo yao zipo katika mavazi, na mtu wa aina hiyo yupo tayari kukopa mkopo ili anunue nguo dukani inayomvutia.
Ndani ya kanisa yapo mambo yaliyopangwa ili kukufanya ujibiwe na Mungu. Mathalani, endapo Jumapili asubuhi ni muda wa maombi, na malaika wa zamu akiwa tayari kuwabariki watu, na kumbe wewe umechelewa kufika, ujue kuwa siyo rahisi upate majibu ya hitaji lako. Mungu anaweza kumtumia hata mtu asiye na sifa kanisani kuutoa ujumbe muhimu kwa maisha yako. Hatuna kitu cha kumhonga Mungu ili atupe afya, au gari au mali. Mungu ameweka ndnai ya mioo yetu kitu kiitwacho “KUMCHA MUNGU”, ambayo ni pamoja na kumtolea Mungu. Kila mmoja wetu anapaswa kuijua ratiba ya Jumapili, kwamba kuanzia saa tatu asubuhi tuwemo hekaluni mwa Mungu ili kukutana na Mungu kwa sababu yamkini Mungu atakuwa amemtuma mtu mmoja kwa ajili ya kuuleta ujumbe wako siku hiyo. Ni bahati mbaya kuwa, baadhi ya watu huiafanya ratiba hiyo ionekane kuwa kama ndefu sana. Siku za Jumapili siyo siku za kufanya biashara. Na si vyema kumsingizia shetani kila unapokosea kwa kusema eti “Shetani amenipitia”, kwa nini kusesmahivyo? Kwani haipo siku utakjayotenda mambo mema ili basi useme “Yesu amenipitia?”. Hatupaswi kutenda dhambi eti kwa sababu NEEMA IPO!!! Kitendo cha kurudia kutenda dhambi kwa kisingizio cha kuitumia Damu ya Yesu basi ujue ni kumrudisha Bwana Yesu Msalabani, na hii ni kuichezea hii neema ya ajabu badala ya kuitunza. Inabidi kuikimbia dhambi na kuionesha kisogo chako kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti.
Hata hivyo Kutenda dhambi ni uamuzi wako, ila ufahamu kuwa endapo Bwana Yesu atarudi ghafla kulichukua kanisa lake ujue kuwa utaachwa na wala huwezi kusingizia kuwa ulikuwa katika kifungo cha dhambi au cha mapepo. Ili kumuona Mungu kuna vitu unapswa kuviacha maishani mwako. Kama tatizo ni hao marafiki ulio nao, achana nao. Usiwe kama nguruwe ambaye hata baada ya kuogeshwa bado hurudia kujilowesha katika uchafu. Tusikubali kupoiteza muda. Yule unayemuona wa maana, pengine ni boyfriend / girlfriend wako ujue ikitokea shida huyo atakukimbia tu. Ni Yesu pekee ambaye ukimfuata kwa asilimia 100% hawezi kukuacha katika shida yako. Ukiwa na Roho Mtakatifu, na endapo dhambi itakunyemelea, utajikuta dhamira ndani yako ikikukataza kutoifanya hiyo dhambi. Hata hivyo, kama mtu haenendi katika roho, dhambi za aina zote zikimnyemelea zitamkamata tu.
Kwa upande wa sadaka, Mungu hajawahi kutupangia kiwango cha sadaka cha kumtolea wala haangalii kiasi cha fedha yako ulicho nacho. Imeandikwa katika MWANZO 22:9-12 (Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. 10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. 11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. 12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee).
Kumbe Mungu hakuwa anamhitaji Isaka, bali alitaka kuijua ilipo hazina ya Ibrahimu ili kuuona moyo wake upo je.!! Ni kweli kuwa Ibrahimu alimpenda sana mwanae Isaka. Lakini kumbe huwezi kumcha Mungu hadi Mungu atakapokigusa kitu kilichoko ndani ya moyo wako na baada ya hapo atakubariki. Tunajifunza kuwa pale tunapompa Mungu sadaka, hiyo ni njia ya kudhihirisha kuwa tunamcha Mungu. Biblia inasema “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;” (ISAYA 1:19). Endapo tutamwamini Mungu kwa mioyo yetu yote, Mungu atafanya yale yote tusiyoyaweza. Uchaji ni kitu cha msingi katika moyo wa mwanadamu kuliko kiwango cha sadaka zetu tutowazo. Hakuna kitu utakachokifanya na ambacho hautakivuna. Ukitenda mema utakula mema ya nchi, lakini ukitenda dhambi ujue mshahara wake ni mauti.
Showers of Glory Morogoro wakicheza mbele za Mungu katika Ibada ya leo. |
Kumbe Mungu hakuwa anamhitaji Isaka, bali alitaka kuijua ilipo hazina ya Ibrahimu ili kuuona moyo wake upo je.!! Ni kweli kuwa Ibrahimu alimpenda sana mwanae Isaka. Lakini kumbe huwezi kumcha Mungu hadi Mungu atakapokigusa kitu kilichoko ndani ya moyo wako na baada ya hapo atakubariki. Tunajifunza kuwa pale tunapompa Mungu sadaka, hiyo ni njia ya kudhihirisha kuwa tunamcha Mungu. Biblia inasema “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;” (ISAYA 1:19). Endapo tutamwamini Mungu kwa mioyo yetu yote, Mungu atafanya yale yote tusiyoyaweza. Uchaji ni kitu cha msingi katika moyo wa mwanadamu kuliko kiwango cha sadaka zetu tutowazo. Hakuna kitu utakachokifanya na ambacho hautakivuna. Ukitenda mema utakula mema ya nchi, lakini ukitenda dhambi ujue mshahara wake ni mauti.
Wakristo wengi leo hii wanapoteza muda mwingi kuomba kwa habari ya magari na mali na ambayo siyo mambo ya msingi. Ndicho kinachosababisha Wakristo hao kuifuata miujiza kanisa moja hadi jingine. Endapo tungemuomba Mungu atuoneshe kazi za kuleta uharibifu anazofanya shetani, ni hakika kuwa tungeingia kazini mara moja na kuanza kumshambulia shetani. Ndiyo maana Biblia inasema “mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache”. Ni muda wa kuwaza kusudi la Mungu maishani mwetu kwanza. Hivi utaupataje utajiri endapo hujaugusa moyo wa Mungu? Mungu anatengeneza maisha yetu kupitia mioyo yetu. Tunapaswa kumdhihirisha Mungu machoni pa watu wengine, hata wasiookaoka. Nyakati zingine hata majirani zako pengine wanashindwa kumwaminiYesu kwa sababu ya matendo uliyo nayo huko mitaani kwako. Endapo tutaishi vizuri, kila mtu atatamani kuishi kwa mfano wa maisha yetu tuliyo nayo.
Kuna Wakristo leo hii wanawadharau watu wengine, huku wakiwa na kiburi cha uzima, wakiacha kumtolea Mungu sadaka zao. Siku ya Leo tunaenda kumtolea Mungu sadaka zetu, na kumfanya Mungu aiguse mioyo yetu tena. Kupitia maombi ya leo, tumsihi Mungu atuguse, na kumtolea sadaka tofauti na mazoea yetu. Hata kama sadaka yako inayoambatana na moyo wako ni kidogo kwa siku ya leo, amini kuwa bado utamuona Bwana. Katika MATENDO 3:19 imeandikwa hivi “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;” Kumbe mara baada ya watu kuzitubu dhambi zao, kinachofuata ni kuja zile nyakati za kuburudika. Leo tuzitubu dhgambi zetu na kuahidi kutozirejea tena ili uje wakati wa kuburudika maishani mwetu.
========== AMEN ========
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KIPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/