GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI
TAREHE 02.07.2017
MHUBIRI:
PATOR, GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Yohana 12: 31 Imeandikwa,“Sasa
hukumu ya Ulimwengu huu ipo;sasa mkuu wa Ulimwengu huu atatupwa nje” Kutupwa nje maana yake atupwe nje ya shamba,
ndoa, kazi, shule, huduma, masomo na biashara pia. Mkuu wa ulimwengu huu
anaitwa shetani. Shetani anayo majina mengi. Pengine anaitwa ibilisi, nyoka wa
zamani, baba wa uongo, mshitaki wa ndugu,
na majina mengine anaitwa mwizi.
muuaji tangu zamani, mkuu wa pepo- belzebuli. Na pengine ameitwa mkuu wa
giza katika ulimwengu wa roho. Pengine ameitwa mwarabu ambaye ndiye mkuu wa
uharibifu wote Swali litakuwa ni kwa nini tumtupe wakati hatumwoni? Ijulikane
ya kuwa shetani ni roho na anaweza kukaa mahali popote. Unaweza usimwone kwa
sababu yeye hukaa katika roho.
Imeandikwa Ufunuo 2: 13 “Napajua ukaapo, ndipo penye kiti
cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani
yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa
kati yenu, hapo akaapo Shetani.” Shetani huwa anakaa kokote. Anaitwa Mwarabu
kwa sababu ya uharibifu. Na akiingia mahali basi ujue uharibu umefika. Shetani
huwa anakaa ndani ya watu. Shetani hawezi kufanya kazi isipokuwa amepata mahali
pa kukaa. Asipotupwa utamwona wa faida ila kazi zake zimejaa uharibifu.
Ufunuo 12: 7-21 Imeandikwa “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na
malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na
malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9
Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani,
audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa
pamoja naye. 10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na
nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa
chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na
usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao;
ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu,
nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu
mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Majeshi ya Bwana Yesu yakimwimbia Mungu. |
Shetani alitupwa katika nchi baada ya vita.
Vita hii ilipiganwa kupitia malaika Mikaeli, tena neno linasema ya kuwa malaika wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo.
Neno linasema mbingu ikafurahi baada ya kumtoa shetani kutoka mbinguni ametupwa
katika nchi. Tena ilikuwa nguvu kwa sababu shetani na malaika zake wameondolewa
na kutupwa nje.
Baada ya shetani kutupwa katika
nchi, Mungu alijua hila za ibilisi siku zote huwa ni uharibifu. Baada ya kuona jambo ili ndio Mungu akatoa
matibabu. Silaha ya kumshinda ibilisi ni Damu ya Mwanakondoo. Silaha hii hutumiwa
na watakatifu. Ndio maana neno linasema Kuhani Joshua wakati akiwa kazini,
shetani alisimama pembeni kumpinga. Kwa hiyo
shetani aweza kuwa ndani ya mtu
au nje ya mtu. Lakini ukiwa na utakatifu, malaika wa Bwana atakulinda dhidi ya
mkono wa ibilisi.
Ufunuo 12: 12 Imeandikwa : Kwa
hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa
maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana
wakati mchache tu. Shetani anafanya kazi masaa yote kwa sababu anajua muda
wake ni mchache. Asipoweza biashara atahamia kwenye macho, mikono, shule,
mashamba au kazi. Shetani na wasaidizi wake wana hasira sana ndio maana
wanaweka watu mashimoni. Utaona mtoto aliyekuwa na akili na fahamu nzuri
anabadilika ghafla. Badala ya kuwa namba moja anakuwa wa mwisho, mwenye
magonjwa ya kila namna. Lazima uamue kuchukua hatua ya kupambana kwa nguvu
zote.Mateso haya tunayoyaona kwa watu hayatoki kwa Mungu isipokuwa kwa shetani.
Magonjwa ya ajabu Ukimwi, Kisukari na Pressha na taabu zote havitokani na
Mungu.
Maombolezo 31-33 Imeandikwa: Kwa
kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa
kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.
Wala kuwahuzunisha. Si mapenzi ya Mungu kuona tukiwa na huzuni. Huzuni
ya ndoa, kazi, shule, njaa au hali ya uchumi. Haya yanatokana na shetani na
mawakala wake waliotupwa nje.
Platform ministry wakiongoza sifa na kuabudu. |
Mapepo hawapendi kukaa hewani.
Kumbe siku zote wanapenda kukaa ndani ya watu. Ndio maana wakati wa Yesu walipo
mwona walisema tuna nini nawe mwana wa Mungu. wakauliza kwanini anataka kuwatoa
kabla ya muhula wao. Leo ndio siku au muhula wa kuwatupa nje mashetani waliokaa
ndani yako siku zote. Silaha yetu ni kwenda kwa damu ya Yesu maana ndio iletayo
ushindi katika maisha yetu. Ukiwapiga
USHAHIDI WA KUWA SHETANI YUPO DUNIANI.
Yohana 14:30 Imeandikwa, “Mimi
sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala
hana kitu kwangu.” Ukikaa vizuri
na Yesu, shetani hawezi kufanya chochote kwako. Si mchawi wala mganga
atakayeweza kutenda lolote juu yako. Luka 4:1 Imeandikwa, “Na Yesu, hali amejaa Roho
Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,
2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia,
aliona njaa. 3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe
hili liwe mkate. 4 Yesu akamjibu,
Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.
5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika
moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa
kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe
ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.
8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako,
umwabudu yeye peke yake. 9 Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara
cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; 10 kwa maana
imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba, Mikononi mwao
watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12 Yesu akajibu
akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 13 Basi alipomaliza kila
jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.” Shetani yupo hapa hapa duniani. Hapa
alimjaribu Yesu mwana wa Mungu, je wewe? Watu hawaamini lakini yako matukio
yanayowapata watu lakini hayatokani na Mungu. Mtu akiombewa leo kesho anavamiwa
tena, kwa sababu shetani anapenda kukaa ndani ya mwanadamu.
2 Korintho 4:4 Imeandikwa, “ambao
ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru
ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Mbinu ya
shetani ni kupofusha fikra za wanadamu ili wasijue hila zake. Yohana 16:11
Imeandikwa, “kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha
kuhukumiwa”… shetani yupo na alikwisha kuhukumiwa. Makao yake ni
kuzimu. U nani wewe usikubaliane na neno la Mungu, kama Yesu anamwita Mungu
muovu wa dunia hii, utakataaje kwamba shetani yupo duniani.
Ayubu 1:6-9 Imeandikwa, “Ilikuwa, siku moja ambayo hao
wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda
kati yao. 7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu
Bwana, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea
huku na huku humo. 8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo
mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu
mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. 9 Ndipo
Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure.” Hapa
ina maana kabla shetani hajasema kwa Mungu, alikuwa ameishajaribu kuharibu mali
za Ayubu ila akashindwa. Kumbe shetani ni roho inayoweza kuyachunguza maisha ya
wanadamu na kuwajua kwa undani zaidi. Mali, kazi, biashara, mashamba, mifugo na
ustawi wako shetani anajua. Pambana kwa jina na damu ya Yesu ili kumtupa nje
ibilisi. Ibilisi akitupwa nje furaha urudi katika maisha ya wanadamu.
Utarudishiwa vyote shatani akaiondolewa ndani yako. Ustawi, afya, upendo,
maendeleo na kicheko kitasikika tena kama mbingu ilivyoshangilia baada ya
shetani kutupwa nje.
Maombi:
Kwa mamlaka ya jina la Yesu
namtupa nje adui wa maisha yangu,kila kilichofunga maisha yangu nakitupa nje
kwa damu ya mwanakondoo,nakamata roho zote zilizofunga maisha yangu,ndoa
yangu,biashara yangu maanikio yangu nazitupa nje kwa jina la Yesu.namkamata
mkuu wa ulimwengu aliyeshikilia maisha yangu aliyezuia hatua zangu namtupa nje
kwa jina la Yesu.
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KIPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG:UfufuonaUzimaMorogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/