GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA → MOROGORO}
JUMAPILI: 09 JULY 2017
MHUBIRI: PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akifundisha katika ibada ya leo kuhusu Ndoa za Kishetani. |
Ndoa ni muungano
wa maisha kati ya watu wawili walioamua kushi pamoja. Mara nyingi ndoa ni mkataba
wa hiari baina ya hao watu wawili, lakini pia kuna nyakatai zingine ndoa hufanyika bila
hiari ya watu wawili. Ndoa ni mktaba pekee ambao, ukishafungwa hauwezi kuvunjwa
tena. Katika kitabu cha MWANZO 2:24 imeandikwa “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba
yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”.
Lakini pia imeandikwa katika MATHAYO19:5
“akasema,
Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao
wawili watakuwa mwili mmoja?” Kwa hiyo ndoa ni hali ya kutoka kwenye
wingi na
kuwa umoja.
Mashetani wapo wengi na
wanajitahidi kuunganisha
uzao wa kijini na uzao wa wanadamu na hatimaye kuzaa watoto.
Tunaposoma katika 1KORINTHO 6:16-17 neno
la Mungu linasema (Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana
asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni
roho moja naye). Shetani anayajua haya maandiko, na hivyo kuwafanya watu
wafunge ndoa za kishetani bila wao kujua. Mume au mke wa kiroho ana uwezo wa
kuoa au kuoelwa na mtu. Lengo la mashetani kufanya haya ni ili kuongeza mawakala wa mashetani kuleta
uharibifu duniani.
Ndoa za kishetani
zilianza muda mrefu sana. Katika MWANZO 6:1-2 Imeandikwa (Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi
usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,2 wana wa Mungu waliwaona hao
binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.)
Katika maandiko haya, wana wa binadamu wanatenganishwa na Wana wa Mungu. Ndivyo
pia tunaposoma katika AYUBU 1:6 “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu
walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.”
Katika kikao hiki cha mbinguni, shetani naye anajihudhurisha kwa sababu naye ni
malaika. Ndivyo pia ilivyoandikwa katika 1WAFALME
22:19-21 (Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi
katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa
mkono wake wa kuume na wa kushoto. 20 Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya
Ahabu, ili akwee RamothGileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi.
21 Akatoka pepo,akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya.).
Tunajifunza kuwa Wana wa Mungu katika maadiko ya AGANO LA KALE ni MALAIKA, bali katika AGANO JIPYA wana
wa Mungu ni wale WATU WALIOKOKA (YOHANA 1:12).
Tunasoma katika
Maandiko EZRA 9:2 “Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi
mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na
mashehe umetangulia katika kosa hili.” Tunasoma pia katika DANIELI 2:43 “Na kama vile ulivyokiona kile
chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu
za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo”.
Tunajifunza kuwa kumbe inwezekana kuwepo na mahusiano ya kindoa kati ya
wanadamu na malaika (aitwae shetani). Kibiblia shetani ni malaika-mchafu, kwa
sababu alimuasi Mungu na kutupwa nje.
Hii ndio sababu siku zote kazi yake ni kuharibu maisha ya wanadamu.
Katika YUDA 1:6 imeandikwa “Na
malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao
yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo
vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.” Na Katika UFUNUO 9:11 imeandikwa “Na
juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni
Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.” Haya majini
yanaweza kukuingia katika ndoto, na pale unapoamka hujikuta umeshajichafua bila
wewe kupenda. Mara nyingine huwajia watu kama binadamu kabisa ndotoni ukadhani
ni watu wa kawaida na hivyo ukajikuta umeoa au kuoelewa nao. Ndoto ni bayana.
Hayupo mtu aliyewahi kuota ndoto na alichoota kisitimie. Wewe unayeota ndoto za
kuvishwa pete usidhani ni ndoto tu za kawaida, unashiriki tendo la ndoa, jua
yapo madhara yatokanayo na aina hizi za ndoto. Ndiyo maana hadi sasa maisha
yako yamekuwa si ya mafanikio.
Malaika wachafu
(fallen angels) na mashetani wanaweza kubadilika na kuwa chochote. Wapo malaika
wachafu wanaweza kujigeuza na kuwa kifuu cha nazi, au gari au mti au chochote
kile. Kwa maneno mengine shetani anaishi kwa kanuni ya rohoni ya kuvaa umbo.
MIFANO YA KIBIBLIA KUHUSU MALAIKA KATIKA UMBO LA
WANADAMU
1. Ibarahimu aliwahi kuwapokea wageni vijana waliokuwa
malaika bila yeye kujua, akawaandalia chakula, wakala na kunywa.
Kitabu cha MWANZO 18:1-8 “Bwana akamtokea Ibrahimu karibu
na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa
hari. 2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele
yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama
mpaka nchi, 3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba
usinipite sasa mimi mtumwa wako. 4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu,
mkapumzike chini ya mti huu. 5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo,
baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama
ulivyosema. 6 Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza
vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. 7 Ibrahimu akapiga mbio
kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi,
naye akahimiza kuiandaa. 8 Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa,
akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.”
Tunajifunza kuwa mgeni anaweza kuja kwako na ukamsaidia lakini kumbe siyo mtu
bali ni malaika. Kwa hiyo kumbe malaika anaweza kuja kwako na kula chakula au kunywa,
lakini kumbe siyo mtu. Kwa hiyo, malaika wazuri au malaika wachafu wanaweza
kuingia nyumbani mwako, na kwa maana hiyo siyo kila chenye umbile la binadamu ukakidhania
ni mwanadamu mwenzako!!
2. Mfano mwingine ni wa Lutu, ambaye pia katika Biblia
alikutana na malaika. MWANZO 19:1-5 “Basi,
wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa
Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. 2
Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu,
mkalale, mkanawe miguu yenu, hata
asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa
uwanjani usiku kucha. 3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake.
Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. 4 Hata kabla
hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa
wazee, watu wote waliotoka pande zote. 5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi
wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.” Tunajifunza
kuwa Lutu aliwajua hawa si wanadamu bali ni malaika, pengine kwa sababu walitokea
kwa Ibarahimu, nduguye. Malaika wanaweza kukaa ndani ya nyumba, wakalala, wakapiga
hata mswaki. Tujifunze kuwa hata unapopokea mgeni mtendee vizuri na endapo ni malaika
mchafu anaweza kukuletea uharibifu. Katika mstari wa 5 tunajifunza kuwa watu wa
mji wanaweza kuwaona malaika na kuwapenda kwa uzuri wao, na hata wakataka
kuingilia nao kimwili (kuwajua). Kama basi wanadamu wanaweza kuwajua majini,
inamaanisha kuwa ndoa za wanadamu na majini zipo.
3. Katika kitabu cha YOSHUA, tunajifunza eneo lingine
ambalo malaika walikutana na wanadamu. Katika YOSHUA 5:13-15 “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa
Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili
mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na
kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? 14 Akasema, La,
lakini nimekuja sasa, niliamiri wa jeshi la Bwana. Yoshua akapomoka kiusouso
hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi
wake? 15 Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako
miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya
vivyo.” Kumbe tunajifunza kuwa, kama malaika wa Bwana anaweza kuuvaa
mwili na kushika silaha, basi hata malaika wachafu wanaweza kufanya vivyo
hivyo. Kwa hiyo majoka na majini yanaweza kufunga ndoa baada ya kuvaa mwili wa
kibinadamu. Wapo watu wanaoota ndoto za kunyonyesha watoto, wakati bado
hawajaolewa au kuwa na mume.
JINSI GANI
MAJINI HAYA HUWAINGIA WANADAMU?
Wake au waume wa
rohoni ni wa hatari sana. Ni bora kuoelwa na mume wa kibinadamu hata kama
atakuwa anakutesa kimwili kuliko hao wa kiroho. Ili kuwaepuka unapaswa kuzijua
njia anazotumia shetani kukutegahadi kujikuta umefunga naye ndoa za rohoni.
Mara zote shetani hupenda sana kuwaingia watu kuendana na vile vitu ambavyo mtu
husika anavyopendelea maishani mwake, Mfano:-
1. Pengine mtu ni mpenzi sana na maua fulani fulani, na
hivyo akipita njiani aweza kuokota ua la aina hivyo kumbe ni mtego, na papo
hapo jini huyu hupata nafasi ya kumuingia huyo
mtu.
2. Wakati mwingine kuna mtu anakuwa anapenda sana pete au
mikufu, na hivyo akiokota vitu vya aina hiyo alivyotegeshewa, basi jini huyu
humwingia huyo mtu.
3. Unaweza kuwa na jirani mchawi au pengine ni ndugu au
mtu unayesoma naye au kufanya naye kazi.
Endapo kila siku mtu wa aina hii utakuwa unamuota ndotoni
akikuingilia mwilini, ujue siyo kwamba uliota ndoto bali ni
hakika uliingiliwa.
DALILI KWA WENYE
WAKE / WAUME WA ROHONI KABLA YA NDOA:
Kwa mtu ambaye
kimwili hajaoa au kuolewa, zifuatazo ni dalili kufahamu kuwa una mume au mke wa rohoni:
1. Endapo utakuwa unaota ndoto za kuwa umeolewa au kuoa,
ujue hiyo ni mojawapo ya ndoto.
2. Kama wewe ni binti utakuwa huwapendi wanaume. Na kama
wewe ni mwanaume, unakuwa huna muda
wowote wa kusalimiana na watu wa jinsi
ya kike. Ndiyo aina ya watu ambao hujiita ni WAGUMU!!
3. Dalili nyingine na hasa kwa wadada, mathalani ni pale
kila baada ya kuchumbiwa uchumba huo huharibika kwa sababu kadhaa wa kadhaa
zisizo za msingi. Hii ni kwa sababu mume wa rohoni aliye naye hataki kuruhusu
uolewe na huyo mume mpya.
4. Dalili nyingine ni kuwa, mtu huharibu mwenyewe kile
kitu alichokianzisha. Pengine unalo gari lako mwenyewe na unaliharibu bila kulitunza.
Hii ni kwa sababu wale wanaokumiliki kiroho wanataka usipate msaada kokote ili
baadae uwafuate wao.
5. Dalili nyingine ni kuwa hakuna kitu chochote
kitakachokaa au kudumu. Hata kama watoto watazaliwa hawataishi muda mrefu.
6. Dalili nyingine ni kuwa hata ukiota ndoto nzuri namna
gani, ndoto hiyo husahaulika mara moja uamkapo. Hii ni kwa sababu wanaomiliki
huiiba hiyo ndoto ili mtu huyo asifanikiwe.
7. Kwa wadada wakiwa
kwenye siku zao (hedhi), husikia maumivu makali sana. Na mbaya zaidi
hukaa zaidi ya muda wa kawaida.
8. Wakati mwingine mtu anakuwa akiishi kivyake vyake tu, anakuwa na mpangilio fulani
wa kuweka mambo yake vizuri kwa utaratibu chumbani mwake, na endapo mtu mwingine
akivuruga chochote atakuwa mkali sana kama
pilipili akitaka alichokipanga kibaki vile vile tu.
DALILI KWA
WANANDOA WENYE WAKE / WAUME WA ROHONI:
Kwa walioolewa au kuoa,
zifuatazo ni dalili za watu wenye waume au wake wa rohoni:
1. Dalili ya kwanza nikukosa furaha ya mahusiano yao. Mke
huona karaha kumuona mume anapotokezea.
2. Watu wa aina hii usiku ukifika mke atalala na jeans
kitandani. Na kama ni mume mwenye mke wa rohoni, kuna wakati mume atakuwa analala
sebuleni au kwenye kochi.
3. Wakati mwingine mke au mume wa aina hii hafurahii tendo
la ndoa, baada ya kujikuta wote kama vile wanalazimishana.
4. Wanakuwa na Ugumu wa kuzaa au kupata watoto. Mke anapata
wakati mgumu sana kupata mtoto na pia ugumu wa kujifungaua pale anapokuwa
anajifungua. Wakati mwingine mimba huharibika.
Kama wewe haumjui
Yesu wala hujawahi kumpokea kuwa BWANA NA MWOKOZI wa maisha yako,leo ufanye
hivyo ili maombi yetu ya siku ya leo
yaweze kuleta suluhisho la kudumu
kuwatimua waume na wake wa kirho
wanaosumbua maisha yako.
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KIPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG:
Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/