GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA → MOROGORO}
JUMAPILI: 16 JULY 2017
MHUBIRI: PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Mch. Godson Issa Zacharia akifundisha katika ibada ya leo. |
Kuanzia Jumapili
iliyopita, tumekuwa tukichambua dalili, vyanzo na sababu mbalimbali za kuwepo
kwa ndoa za kiroho za kishetani. Yapo
madhara mabalimbali yawapatayo watu walioingia katika ndoa hizi ikiwemo. Leo
tena tutamalizia somo hili kwa upana zaidi na hakika Bwana Yesu atakuweka huru
kwa Jina la Yesu.
Kwa nini
tunazungumzia uwepo wa hizi ndoa za kiroho za kishetani? Hii ni kwa sababu,
tunaposoma katika MWANZO 6:1-4,
Biblia inasema hivi (Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa
nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za
wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana
akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni
nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 Nao Wanefili (Wanefili
maana yake ni majitu) walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana
wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio
waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.). Tunaona katikamaandiko
haya uwepo wa watu wa aina mbili: Wana wa Mungu (ambao ni malaika) na binti za wanadamu (ni mabinti
kweli wa wanadamu kama sisi). Biblia inasema wana wa makundi
haya mawili waliingiliana (kwa maana ya kujamiiana), na hivyo walizaa
watoto ambao ni mchanganyiko wa mbegu za kibinadamu na malaika (majini) ambao walikuwa hodari sana,
wakaitwa wanefili.
Pia tunasoma
katika EZRA 9:2 (Maana
wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu
wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe
umetangulia katika kosa hili.). Mungu ameliona hili jambo kuwa ni
kosa,na ndiyo maana katika Mwanzo 6 Mungu alisema roho yake haiwezi kushindana
na mwanadamu. Malaikawapo wa
aina mbili: Malaika watakatifu
(hawa ndiyo tunaowatumia) na Malaika wachafu (hawa ndiyo waharibifu, wanaoingiliawatu kuwaletea
magonjwa, umaskini n.k). Ndiyo maana katika YUDA 1:9 imeandikwa hivi (Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe,
lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele
chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. 7
Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati
kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili,
imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.) Kundi hili la
malaika waasi walitaka kumpindua Mungu katika kiti chake cha enzi. Malaika hawa
walifuata uasherati kwajinsi moja kama vile Sodoma na Gomora, wakijichanganya
kwa kufanya mambo yasiyo ya asili (sodomization).
Inawezekana hata
wewe kwa kujua au kutokujua umeunganishwa na ndoa za aina hii, kati ya wanadamu
na malaika waasi (majini). Leo tutaiangalia milango inayo ruhusu mume au mke wa
kiroho na kufunga ndoa za aina hii na kisha tutaifunga yote kwa Jina la Yesu
Kristo.
MILANGO INAYORUHUSU MUME AU MKE WA KIROHO KUINGIA NA
KUFUNGA NDOA ZA KIROHO ZA KISHETANI.
1.
Ulinzi wa Kichawi:
Hii hutokea tu
endapo mtu aliwahi kwenda kwa waganga wa kienyeji kuomba ulinzi wa kumfunga
mwenza wake au mchumba wake ili asimkimbie. Ndoa hailindwi kwa madawa bali kwa
Jina la Yesu Kristo. Mtu huyu hupewa masharti magumu sana na waganga wa aina
hii, pengine kumwagiwa maji ya maiti au hata kuamriwa kuvua nguo zote na kulala
nao. Kupitia madawa haya, mume au mke wa kiroho hupatikana. Mwisho wa watu kama
hawa ni kukosa furaha, ndoa kuvunjika na ugomvi wa kila mara kutokea.
2.
Damu ya Hedhi
Hii ni ile damu ya
kila mwezi kwa akina mama. Damu hizi zinapaswa kutupwa kwa uangalifu
sana, hivyo ni vyema damu hizi zihifadhiwe kwa umakini sana ili
zisifikie mikono ya wachawi au
waganga wa kienyeji. Biblia inatukataza ”usile nyama na damu yake kwa
sababu katika damu kuna uhai”. Kupitia damu za hedhi, wanawake wengi
wamejikuta wakifungwa kutozaa watoto baada ya waganga wa kienyeji kuzitumia damun
hizi kuwaloga. Damu hizi ni muhimu sana kwa sababu zinahusisha mambo ya uzazi
(idadi ya watoto na taarifa zinginezo za ndoa). Endapo damu hii ikifika mikonoi
mwa waganga wa kienyeji, uchumba utaharibika, maumivu ya tumbo la uzazi, ndoa
kuvunjika, damu kutoonekana kwa miezi kadhaa kwa mtu asiye mjamzito n.k. Dalili
nyingine ni mume wa mwanamke aliyefungwa kupitia alama hii kuwa na mahusiano
nje ya ndoa (michepuko).
UKIRI
Kwa Jina la
Yesu, Ninamfukuza jini aliyeingilia ndoa kwa njia ya Damu ya Hedhi. Ewe
shetani ninakufukuza kwa Jina la Yesu. Ewe shetani uliyenifunga kwenye ndoa
ya kiroho nakufyeka kwa Jina la Yesu.
Amen
|
3.
Uvaaji wa Nguo Mbaya za Kimahaba
Njia hii humfanya
mtu aliyevaa nguo kuonekana amevaa lakini viungo vyote vya mwili na sehemu za
siri zinakuwa zinaonekana. Uvaaji wa nguo za aina hii huyafanya majini
yamgundue haraka kuwa wewe ni mwenzao. Kwa
njia hii, mashetani haya hupata upenyo wa kumuingilia mtu anayevaa mavazi ya
aina hii. Kwa wanaume ni pale mtu anavaa shati kwa kuachakifua wazi au kama ni
wanawake ni wale wavaao nguo fupi sana au zinazoonesha maumbile yake.
4.
Ngoma za Asili
Hizi ni ngoma za
asili zinazochezwa na baadhi ya makabila (kama vile Waluguru). Aina ya ngoma
hizi ni VIGODORO na MDUNDIKO. Uchezaji wa ngoma hizi
huambatana na uchezaji usio na staha, wakati mwingine uchezaji-nusu uchi.
Mashetatni hupata nafasi kuwaingia wafuasi wa hizi ngoma na kuoana nao. Ngoma nyingine
ni ile ya CHAKULAGA (kwa Wasukuma) ambayo
huchezwa na watu kuchaguana wakati wa uchezaji. Majini nayo hujipatia watu wa
kuwachagua na kufunga naao ndoa za kishetani.
5.
Mlango kupitia Uzinzi au Ukahaba au Uasherati
Imeandikwa katika 1WAKORINTHO 6:15 (Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae
viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!). Unapofanya ukahaba
unajiungamanisha na mtu usiyemjua, na hatimaye mashetani kjukutamia wewe kama
mume aumke wa ndotoni.
6.
Mlango kupitia Mbegu za Uzazi za Kiume
Kwa mtu ambaye hujaoa
au hujaolewa, na kutenda tendo la ndoa (uasherati)
au kama umeoa na una mke na kufanya tendo la ndoa nje ya mke wako (uzinzi), unakuwa umejichimbia kaburi
lako mwenyewe. Biblia inasema ikimbieni zinaa. Imeandikwa katika 1WAKORINTHO 6:15-16 (Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae
viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!16 Au hamjui ya kuwa
yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili
watakuwa mwili mmoja.) Mara nyingi mashetani yanakuwa yanakusanya mbegu
hizi nakwenda nazo baharini ili kuzalisha watoto wa kijini. Wengi wetu tuliwahi
kusikia habari za uwepo wa mashetani yakiitwa POPO-BAWA ambayo huwaingilia watu
usiku na kutoa sharti la mtu aliyeingiliwa kujitangaza rasmi kwamba
umeshaingiliwala sivyo yaendelee kukujia usiku.
Kama ambavyo damu
ya hedhi inatumika na mashetani, vivyo hivyo mbegu za kiume ni njia ya
kumuunganisha mwanaume na majini, na kumfanya aolewe na wanawake wa kijini.
Yapo maeneo ambayo ni hatari, yanatumika kwa shughuli za ukahaba. Hata
mahotelini pia uvaajji wa nguozakikahaba upo
na lengo ni kuwavuta wateja wa ukahaba na wakeshalala pamoja mbegu hizi
hukusanywa na mashetani na kuolewa na majini.
MADHARA YANAYOMPATA MTU MWANAUME WA AINA HII NI:
·
Mambo ya kifedha
huharibika ghafla (miradi kufa, biashaara kuyumba)
·
Kukosa hamu ya
tendo la ndoa na mke wake wa ndoa.
·
Mwanaume kuchanganyikiwa
kila anapomuona mwanamke au binti amekatisha mbele yake.
·
Mwanaume anakuwa
hapati ujauzito kwa sababu mwanaume anakuwa hana mbegu za kutosha (low sperm
count) baada ya mashetani kuzigema na kuzipeleka baharini.
7.
Kuirithi Mikoba ya Ukoo
Katika Bara la
Afrika, zaidi ya miaka 100iliyopita wengi wa wazee wetu walikuwa siyo Wakristo.
Kuna wabibi huwaita wajukuu zao wakiume kuwa ni wachumba zao. Au kuna wababu au
wanaume watu wazima katika ukoo huwaita binti wadogo kuwa ni wachumba zao.
Maneno kama haya huumbika katika ulimwengu wa roho.
SHETANI HUWEZAJE KUMUINGIA MTU?
Kama tulivyosoma
katika MWANZO 6:1-3, zipo alama ambazo mashetani humwekea mtu mwilini au rohoni
na kuwezakumuingia mtu. Katika kitabu cha MWANZO, Mungu alimwekea alama Kaini
ili watu watakaomuona wasimdhuru. Kwa hiyo zipoalama zakuwafanya mashetani
wamuingilie mtu:
Platform ministry wakiongoza sifa na kuabudu. |
Imeandikwa katika UFUNUO 3:16-18 (Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na
walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika
vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza,
isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama
huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na
sita.) Hizi ni alama za kimwili kabisa ambazo mpinga Kristo anaweza
kumwekea mtu.
1.
Alama katika Paji la Uso
Alama hii huweza
kuwa ya kuonekana au kutoonekana. Majini huwa rahisi kuiona alamahii wanayomwekea
mtu. Wakati mwingine hata katika
magariau daladala, unaweza kuziona alama au maandishi yaliyowekwa ndani mle kumbe
ni alama inayotumiwa na majini kuwasiliana.
2.
Alama katika Viungo vya Uzazi
Kwa wanawake, alama
za aina hii huwekwa kifuani karibu na maziwa, au katika magotini, au chale shingoni
n.k. Pengine mtu anakuwa anajua au hajui. Majini humuingia mtu kwa sababu wanapoiona hiyo alama inakuwa
rahisi kukutambua.
UKIRI
Ewe jinni
unayenimiliki, niachie kwa Jina la Yesu Kristo. Hizo alama futikaleo kwa Jina
la Yesu. Ewe jinni unayeingia ndani yangu kwa sababu ya alama leo naifuta kwa
Jina la Yesu. Amen
|
3.
Alama kwenye Miguu
Shida hii huwapata
sana wanawake kwa sababu miguu yao huwa wazi na kuonekana. Baadhi ya akinamama
huvaa chain wakidhani ni fasheni kumbe tayari wanakuwa wamemilikiwa. Chain hii huvaliwa zaidi mguu wa kushoto.
Kuna wanawake wengine huvaa pete miguuni wakidhani ni urembo lakini kumbe ni
alama za kishetani za kumfutailia. Mtu wa aina hii atakapotembea popote majini
husema ni mtu wao, na nyakati za usiku majini haya humuingilia mtu huyu
kimapenzi.
4.
Alama inayowekwa kwenye kiuno
Kuna wanawake
wanaofundishwa namna ya uvaaji wa shanga kiunoni kwa matumizi ya unyumba.
Mashetani humuingilia mwanamke wa aina hii kwa sababu ya kuiona hiyo alama
kiunuoni. Kwanza jiulize swali: Kwa nini
shanga hizi hutengenezwa na jamii ya aina moja? Wale wale wanaotengeneza shanga
hizi ni wale wale wanaouza dawa za kuongeza
nguvu za kiume.
5.
Alama ya vazi la Hijabu
Alama hii ya
Hijabu hata kuanzia utotoni kwa wenye utamaduni huu huanza kuvaliwa na kuyafanya
mashetani yapate upenyo wa kumuingilia huyu mttoot na kukaa naye hadi ukubwani
mwake.
KWA NINI MTU UWEKEWE ALAMA HIZI?
Shetani huziweka
hizi alama ili kazi yake iwe rahisi. Biblia inaasema katika WARUMI 12:2 (Wala msiifuatishe namna ya dunia
hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya
Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu). Kwa hiyo hatupaswi
kufuatisha kila kitu kinachofanywa na watu wa dunia hii. Zipo taratibu za dunia
hii ambazo ukizifuatisha utajikuta unapata madhara.
UKIRI
Kwa Jina laYesu,
kama Damu yangu imechukuliwa kwa mimi kukubaliana na waganga wa kienyejji,
leo nayakataa makubaliano. Alama ya damu kwenye vidole vangu, alama ya damu
usoni mwangu, leo nazifuta kwa Jina la Yesu. Amen
|
Ili kuwa salama,
yapo mambo mawili ya kufanya:
Jambo la kwanza ni kumpa Yesu maisha yako (kwa maana ya kukubali kuokoka), pili
ni kufanya maombi ya kujifungua viungo vyako vilivyowekewa alama na tatu ni
kutoa talaka na kuachana na hizo ndoa za
kiroho za kishetani na mwisho ni
kuifunga milango yote iliyoruhuhsu wewe kuingiliwa kirahisi.
========== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/