Na Mwandishi wetu |Morogoro |Alhamisi |01/08/2013
Mchawi mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara
moja alikutwa akiwa amedondoka eneo la nanenane mjini morogoro.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea usiku wa kuamkia alhamisi
mara baada ya Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima tawi la Morogoro
mjini Dr Godson Issa Zacharia kuongoza majeshi siku ya jumatano kwenye ibada
kuliteka anga la morogoro na kuweka msimamo kuwa mchawi yeyote atakayeruka
kwenye anga la morogoro usiku huo anaswe.
Katika tukio hilo kijana huyo ambaye umri wake unakadiriwa
miaka 17 na 18, baada ya kudondoka hali akiwa uchi wa kuzaliwa, alichukuliwa na
askari polisi na kumpeleka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro. Mara baada
ya kufika hospitalini hapo, taarifa zilimfikia Mchungaji Kiongozi wa kanisa la
Ufufuo na uzima Dr Godson ambaye akawasiliana na mtendakazi wake ngazi ya Shepherd Dr Gershom ambaye ni daktari katika hospitali hiyo alikwenda
kufanya mahojiano na huyo mchawi.
Alisema kuwa yeye ni mwenyeji wa Shinyanga, usiku huo
alitoka pamoja na babu mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake pia kulikuwa na
wachawi wengine wengi walitoka pamoja kwenda mpaka mkoani mbeya, na walipotoka
mbeya wakaenda hadi baharini na walipotoka baharini iliwabidi waje mkoani
morogoro kuhudhuria kikao. Anadai kuwa walipofika eneo la morogoro walikumbana
na shida (ambayo hakutaka kuitaja) alidai kuwa ililazimu yeye adondoke ili
awanusuru wengine lasivyo kungekuwa na madhara makubwa kwenye kundi zima, hivyo
kiongozi wa msafara huo alimshurutisha awe kafara ili wenzake wapone.
Aidha alipoulizwa daktari wa wodi hiyo kuwa mwanga huyo wao
wanamhudumia kama mgonjwa mwenye shida Gani? Daktari huyo (jina lake
tumelihifadhi) alisema wanamtibu kama mgonjwa mwenye tatizo la akili la muda
mfupi (Acute Psychotic Disorder).
kijana mchawi akiwa wodi namba 9 ya hospitali ya mkoa morogoro baada ya kuletwa na askari. hicho kinguo kafunikwa kwa ajili ya kumhifadhi ila alidondoka akiwa uchi wa mnyama |
Wachawi wapigweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee………………………………………………………..
UFUFUO NA UZIMA-MOROGORO