JUMAPILI: 13 DECEMBER 2015 –
UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
Na:
STEVEN NAMPUNJU. (RP) &
DR.
GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi
wa Somo: Imeandikwa katika EZEKIELI 37:-1-10…[Mkono wa Bwana ulikuwa juu
yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya
bonde; nalo limejaa mifupa; 2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama,
palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.
3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana
MUNGU, wajua wewe. 4 Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie,
Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. 5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii
maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. 6 Nami nitatia
mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na
kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 7
Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii,
palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa
ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. 8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na
mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini
haikuwamo pumzi ndani yake. 9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo,
mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo
nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. 10 Basi nikatabiri
kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi
kubwa mno.]…Mungu alimuuliza Ezekiel je mifupa hii yaweza
kuishi? Mungu akamwambia Ezekiel
aitabirie, aiambie isikie sauti ya Bwana.
Tunajifunza
kwamba kumbe kilicho kikavu kinawweza kusikia
sauti ya Bwana. Alipotoa utabiri
mtikisiko ukatokea na mtikisiko huo ukaanza kuunga mfupa . Nyama na
ngozi vikawa juu ya mifupa ile. Baadae
upepo ukavuma na upepo huo ukaleta uhai
ndani ya watu. Ezekieli
aliamuru upepo ukaleta uhai.
UPEPO UNA MAJINA:
Tunasoma katika MATENDO YA MITUME 27:9-13..[Na wakati mwingi ulipokwisha
kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa
zimekwisha kupita, Paulo akawaonya, 10 akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari
hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na
ya maisha yetu pia. 11 Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye
merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paulo. 12 Na kwa sababu bandari ile ilikuwa
haifai kukaa wakati wa baridi, wengi wao wakatoa shauri la kutweka kutoka huko
ili wapate kufika Foinike, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi;
nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazinimashariki na kusinimashariki. 13
Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata
waliyoazimu kupata, wakang'oa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.].. Upepo wa kusi ulileta matumaini kwenye
safari yao. Baada ya upepo wa kusi
ukavuma upepo mwingine ulo kuwa
mbaya ambao uliondoa matumaini.
MATUKIO YANAOWEZA KUTOKEA BAADA
YA UPEPO KUVUMA.
- Upepo wa Kusi
Imeandikwa katika MITHALI 25:23 kwamba [Upepo wa kusi huleta mvua; Vile
vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.]. Upepo huu una matokeo
mawili makubwa.
Ø
Upepo
wa kusi huleta mvua.
Ø
Asinziae
huleta uso wa ghadhabu.
- Upepo wa Mashariki
Imeandikwa katika MWANZO 41:23…[Na tazama, masuke saba membamba, dhaifu, yamekaushwa na
upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.]… Upepo
wa mashariki ukivuma unaweza kukausha na kufanya dhaifu na vyembamba. Leo umwamini Mungu atuondeee upepo uliovuma
katika maisha yako. Hivyo ulivyo leo sio vile ambavyo Mungu alivyokuumba baada ya kuvuma kwa upepo wa mashariki. Mchawi
anaweza kuuamua akutumie upepo gani ili akukamate. Upepo ukivuma unakuja na matokeo
yake. Kwenye nnchi yetu upo upepo unavumishwa ili nchi yetu ibaki katika hali
ililyo nayo.
Imeandikwa
katika HOSEA 13:14-15…[Nitawakomboa na nguvu za kaburi;
nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi
kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu. 15 Ajapokuwa yeye ni mwenye
kuzaa sana kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja, hiyo pumzi ya Bwana
itokayo upande wa nyikani, na kijito chake cha maji kitakauka, na chemchemi
yake itakaushwa; yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.]…
Kukumbuka
upepo wa mashariki una nguvu na unavuma
kwa nguvu na kwa bidii. Unaweza ukaa na Baraka zako lakini upepo wa mashariki
ukavuma ukakausha kila kitu. Inawezekana wewe unaonekana kuwa ni mkame. Yaani
huwezi kusaidika yaani huwezi kuanza chochote, lakini leo utaisikia sauti ya Bwana.
Imeandikwa
katika YONA 4:8 [Basi ikawa, jua lilipopanda juu,
Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona
kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi
kuliko kuishi.]… Upepo wa mashariki wenye hari nyingi ukampiga
Yona mpaka yona akazimia.
Imeandikwa
katika KUTOKA 10:12-15...[Bwana akamwambia Musa, Nyosha
mkono wako juu ya nchi ya Misri kwa hao nzige, ili wakwee juu ya nchi ya Misri,
waile mimea yote ya nchi, yaani, vyote vilivyosazwa na ile mvua ya mawe.13 Basi
Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka
mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo
wa mashariki ukawaleta nzige. 14 Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya
Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo
nzige kama hao majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo. 15
Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea
yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; hapakusalia
hata jani moja, mti wala mmea wa mashamba, katika nchi yote ya Misri.]…
Farao
alipozidi kuwazuia Mungu akawaletea upepo wa mashariki ambao ulileta nzige
waile kila kitu kilichosazwa. Tunajifunza kuwa Upepo wa masharki unaweza kumtoa
mtu kwenye nafasi yake.
Kama ilivyoandikwa katika AYUBU 27:21 [Upepo wa mashariki humchukua, naye
huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake.]..
Upepo
huu ni kana kwamba huu upepo una mikono.
Ni kwamba unaweza kumchukua mtu kutoka kwenye nafasi yake aliyopo. Leo tunae
Bwana mtenda miujiza atavumisha upepo mwingine wenye Baraka nao utazirudisha Baraka zetu na kwenye nafasi
zetu katika Jina la Yesu.
UKIRI
Ee upepo a masharki ulievumma ili unitoe mahala
pangu, leo nakataa kwa jina la Yesu. Nakataa leo kuchukuliwa na upepo wa kila
aina. Amen
|
Upepo wa Mashariki waweza kuwa jini, au pepo au
mashetani au mchawi kwamba likija kwenye maisha yako na kukutoa kwenye nafasi
yako.
UKIRI
Kuanzia leo ee upepo na alie ndani ya upepo leo nakushinda kwa
nguvu ya msalaba kwa jina la Yesu. Amen
|
Mungu ametazama watu leo na ameona kuwa tumekuwa
wakame. Ziko familia ambazo hazina matumaini, mtu mmoja mmoja amepoteza matumaini
kabisa, wapo watu ambao wamekaushwa, tumeona upepo wa mashariki unaweza
kukaausha na kumeza na kubaki kilicho kinyonge. Lakini pia tabia zinaweza
kukukausha.
Tunasoma katika ISAYA
43:6… [nitaiambia
kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti
zangu kutoka miisho ya dunia.]. Mungu anataka watu waletwe toka mbali…kusini toa na
kaskazini usizuie.
Magharibi naweza kuotoa upepo wa kutoa nzige, kama
ilivyoandikwa katika KUTOKA 10:19 [Bwana akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa
wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja
ndani ya mipaka yote ya Misri.]
=== © Information & Media Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa
Zacharia
(Glory of Christ
(Tanzania) Church in Morogoro).
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545.