JUMAPILI: 06 DECEMBER 2015 –
UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
Na:
DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
AMOS KOMBA (RP)
Utangulizi
wa Somo: Uovu ni mambo yoyote mabaya yanayotendwa na yanayofanywa na watu waovu. Ikumbukwe kuwa 'Waovu ni
Watu'. Anaweza akawa mtu yoyote yule awe ndugu, mama au baba. Hawa watu wanaufanya uovu na siku haiishi bila
kufanya uovu. Furaha ya muovu inaonekana pale anapofanya uovu wake!!.
Imeandikwa katika METHALI 2:14-15… [Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotoe wa waovu;
15 Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.]…kwani
Mungu aliwaumba watu ili wafanye uovu? Jibu ni hapana. Ila kwa sababu ya hila za watu, kupotoka kwa
watu na tamaa za watu wakaamua kumtafuta mfamle wa uovu wakaungana naye ili wafanye uovu.
Imeandikwa katika YEREMIA 5:26… [Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu
wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu..]…
Imeandikwa pia katika 1TIMOTHEO 5:15….[Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.]..
Kinachosababisha ni tamaa za watu na chuki za watu.
Watu wengine huwa wanaamua waende kanisani wakisema
‘nikatafute kiti nikae kanisani, niandae
Bibilia yangu nimsikilize mchungaji nitoke nitakuwa sawa’… Hiyo ni sawa lakini
si sawa sana…Lakini wakati wanaposoma neno na kulitafakari ndipo watakaa sawa. Ni jukumu
la kila mtu kuwa na bidii ya kusikiliza
mahubiri kwa bidii na kuyatafakari. Kwenye
hili, jitihada ya kuingia ndani ya neno
ni ya kila mtu.
Kumbe sio lengo la Mungu kuwaumba watu ili wawe
waovu, watu walipokuja duniani ila kwa hila zao, tamaa zao na chuki zao wakaaamua waungane
na mfalme wa uovu ili waufanye uovu
Kabla ya kutuma uovu wanaanza kwanza kujadili uovu
huu utakuwa upi na nani watakaoupeleka na namna ya kuupeleka wanakotaka uende.
Lazima wanafahamu kwanza huyo mtu
Watu hawa wanaweza wakawa ni ndugu zako, wakati mwingine
wanaweza wasiwe ndugu wa karibu, kama haajamfahamu huyu mtu wanatuma wapelelezi,
wajue unachofanya kila wakati, baada ya hapo
wanarudisha taarifa kwenye vikao vyake, wakati wa bidii, wakati wa kuchoka
na kila maneno wanayooongea, kwa hiyo
wakishafahamu wanaamua kutuma saa
ukiwa na udhaifu.
UKIRI
Baba Mungu katika
jina la Yesu kama kuna wapelelezi wametumwa kwenye maisha yangu nawakataa kwa jina la Yesu. Kwa jina la
Yesu ikiwa kuna wapepelezi wametumwa kutokea katika vikao vya waovu nawasambaratisha
kwa jina la Yesu. Amen
|
Imeandikwa katika injili ya Luka kwamba kulikuwa na
wapelelezi waliokuwa wanamviziavizia Yesu. Nakataa kwa jina la mtu yeyeyote
anayenivizia anayenipekeleza ili anijue
mchana huu wa leo nakataa kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazarethi.
Hawa
wapelelezi hawaleti tukio ila wanatafuta kukujua. Baada ya hapo wanarudi
kwenye kikao chao wanatoa taarifa. Mfano Musa
aliwatuma wapelelezi kwenye nchi ile ni nchi ya namna gani, watu wa
namna gani, wanapigana je n.k. Kati ya hao kulikuwa na makundi mawili ambayo
walirudisha majibu kwa namna ya rohoni na namna ya mwilini.
Hata wapelelezi wanachaguliwa wenye akili ya kuona
mbali, nani ana uwezo wa kugeuka akaja kwako kama rafiki, au mtu wa karibu…
wana akili sana. Na hawa wapelelezi wanaotumwa huwa wanalipwa. Mfano pepo
unaweza ukaliambia toka likakataa kwa sababu
limeahidiwa malipo baada ya kazi hiyo.
Hawa
Wapelelezi wanatafuta kukufahamu. Mfano Hamani alikuwa na shida na Mordekai hivyo
Hamani akatafuta watu akawalipa ili wampekeleze Mordekai.
Immeandikwa katika ESTA3:1-5..[Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha,
Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo
pamoja naye. 2 Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme,
wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari
zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia. 3 Basi watumishi wa mfalme
walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya
mfalme? 4 Ikawa, waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani,
ili kuona kama mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa
yeye ni Myahudi. 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala
kumsujudia, alighadhibika sana.]… Kumbuka Hata shetani alitaka
Yesu amuainamie. Hamani alipelekewa
taarifa kuwa Mordekai huwa hainami kila
anapopita. Hamani akajaribu kupita wote waliinama lakini Mordekai hakuinama na
Hamani akajua kuwa huyu Mordekai hayupo peke yake.
Wana wa Israel wametolewa Misri wanapekwa Kaanani
wapetishwa jangwani nguo walizovaa hazikuisha wala kuchafuka wala viatu. Mungu
huyu ni wa ajabu. Hamani aliamua ili
ainamiwe vizuri alimua na kupanga kuwaangamiza Wayahudi pamoja na Mordekai.
Alifanya haya yote kwa sababu ya wivu na
kupenda sifa. Kumbuka kuwa anayesimamisha
mambo siyo Mordekai bali anayesimamisha mambo ni aliye nyuma ya Mordekai (Mzee wa siku.)
Wapo wale walioesema “tuone kama ataolewa”, “kama
biashara yake itaendelea”, “kama atamaliza chuo” n.k….. Kumbbuka kuwa kuona
wataona lakini hawatapata. Ni kweli utaona lakini sio yale unayoyawaza; ila
utaona kivingine..
ESTA
3:5-13…[ 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia,
alighadhibika sana. 6 Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana
wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza
Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani,
watu wake Mordekai. 7 Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi
na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku
kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.
8 Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na
kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme
wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki
amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao. 9 Basi, mfalme
akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za
fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya
mfalme. 10 Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin
Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi. 11 Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo
fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema. 12 Basi, waandishi wa mfalme
wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama
vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu
ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila
taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa
muhuri kwa pete yake. 13 Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka
majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha,
vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya
kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali
yao kuwa nyara.]…
Hawa wapelelezi huwa wanalipwa. Unaona Hamani alikuwa tayari kulipa
watakaochaguliwa na mfamle Ahusuero kuwangamiza Wayuhudi…
Sio kila mtu huwa anakuwa katika vikao vya uovu…ila
anachagua walio karibu na mkeo. Je Una mke bingwa wa kutoa mawazo.? Je yote
huwa uanayafanyia kazi?
UKIRI
Kwa jina la Yesu ninaugeza mauovu waliyoyachilia
kwangu urudi kwao walioutuma. Marafiki waliokusanya kwa ajili yangu wakakaa ili kuniharibia kikao
hicho nakisambaratisha kwa Jina la Yesu. Amen
|
Tunapoungumzia vikao
kuna vikao vya aina mbili vya
kiroho na kimwili.
UKIRI
Kwa mamlaka ya jina la Yesu nasambaratisha vikao
vyote vya uovu kwa jina la Yesu na yote
yaliopangwa yawapate wao. Kwa jina la yesu kila aliye
kaa kwenye kikao mabaya yote ywapate wao kwa jina la YESU. Amen
|
=== © Information & Media Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadership:
Bishop Dr. Godson Issa
Zacharia
(Glory of Christ
(Tanzania) Church in Morogoro).
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545.