Sunday, September 8, 2013

MITEGO YA MAUTI

NA MCH. DR GODSON ISSA ZACHARIA


Na mwandishi wetu|Morogoro|Jumapili|08/09/2013

Mauti maana yake ni kuondokewa na uhai. Na shetani amekuwa na silaha nyingi ambazo anatumia kuwatesa watu lakini mpaka sasa silaha zake nyingi zimekwisha kuharibiwa lakini mpaka sasa amebakiwa na silaha moja inayoitwa MAUTI.

1WAKORINTHO 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”

YOHANA 5:25 “Amini amini nawaambia, saa inakuja na saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu na wale waisikiao watakuwa hai”

Kuna mauti ya aina mbili,

1.       Roho ikitengana na mwili

2.       Pale ambapo roho ya mtu inapotupwa jehanum (Ufunuo 20:14-15)

akiendelea  na somo hilo Mchungaji Dr Godson, alieleza matukio matatu ambayo watu katika kukwepa mitego ya mauti walienda kwa waganga wa kienyeji ambao waliambiwa wapeleke vitu vya ajabu sana.

Wa kwanza aliambiwa alikuwa ni bibi ambaye alienda mpaka nyumbani kwa mchungaji akiwa anatafuta maziwa ya nguruwe ili apelike kwa mganga wa kienyeji.

Na mwingine wa pili aliambiwa na mganga wa kienyeji kuwa akatafute mafuta ya kenge jike ya mkiani  aliyetoka kujifungua na awe mwangalifu asije akapewa feki.

Na wa tatu aliambiwa apelike machozi ya samaki la sivyo apelike shilingi laki tano (500,000). Lakini hii yote ni watu katika kufanya juhudi ya kuepuka mauti, lakini Yesu alipokuja duniani alimharibu shetani ambaye alikuwa na nguvu za mauti (WAEBRANIA 2:14)

Yesu alilazimika afe ili kupitia kifo chake aweze kuibatilisha nguvu ya mauti ambayo ibilisi ameiweka ndani ya maisha ya watu. Maana kuna watu wamekaa mahali ili kutega mitego kwenye maisha ya watu wengine maana shetani hawezi kufanya kazi peke yake bila watu kwa sababu yeye ni roho.

Mungu ametuambia kuwa hatutakiwi kuwa na hofu maana Yeye ameshinda mauti (UFUNUO 1:17-18) HIVYO MCHANA WA LEO NI LAZIMA KILA NGUVU YA MAUTI AMBAYO IPO KWENYE MAISHA YA WATU NI LAZIMA TUIHARIBU NA KUITUPILIA MBALI KWA JINA LA YESU.
Share:
Powered by Blogger.

Pages