Sunday, September 15, 2013

SOMO: NGUVU YA KABURI


     NA RP ADRIAN

Na mwandishi Wetu|Morogoro|Jumapili| 15/09/2013
Kaburi lina nguvu, ndiyo maana ukiwa unapita kwenye maeneo yenye makaburi unahisi mwili unakusisimka, wakati mwingine watu wengine wanaogopa hata kupita maeneo kama hayo kwa sababu ni  maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine yanaogopesha.

HOSEA 13: 14
“Nitawakomboa na nguvu za kaburi, nitawaokoa na mauti; ewe mauti ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu”
Kuna nguvu ya kaburi ambayo inaweza kumshikilia mtu, ambayo hiyo Yesu Kristo aliishinda. Yesu alikufa akazikwa na siku ya tatu akafufuka nguvu ya kaburi haikuweza kumshikilia aliishinda nguvu ya kaburi. Na ndiyo maana sisi haina haja ya kwenda kwenye kaburi la Yesu kuhiji, maana hayupo kaburini ameshinda mauti. Lakini wale waasisi wa dini nyingine hawajatoka kaburini hata sasa na ndiyo maana watu kila mwaka inawagharimu kwenda kaburini kila mwaka.
Mtu anaweza kuzika masomo ya mtu, kazi ya mtu na pia maisha ya mtu pia yanaweza kuzikwa. Na kuna viashiria ambavyo mtu unaweza kujua kama umezikwa, unaweza kusikia mtu anaota kachimbiwa kaburi na wakiwa wanataka kufukia ukashtuka ndotoni, ukiwa kwenye hali kama hiyo jua upo makaburini. Na sheria kubwa ya kaburi ni kushikilia kile kilichokufa kisipokee uhai tena kibaki katika hali ya kufa.
ZABURI 103:4 “Aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhiri na rehema.

NINI MAANA YA UHAI?
Uhai wa mtu upo ndani ya damu ya mtu na ndiyo maana Mwenyezi Mungu alikataza kabisa watu wasile damu maana damu ni uhai.

MAMBO YA WALAWI 17:11 Inaonyesha kuwa uhai wa mwili u katika damu. Lakini pia damu ina uwezo wa kuongea.
MWANZO 4:10  “……. Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi” unaona, damu ina sauti na inaweza kulia na ndiyo maana hata damu ya Yesu inanena mpaka sasa, inanena uzima, inanena uokolewe, inanena uponywe kwa Jina la Yesu. (WAEBRANIA 12:24).

NINI CHANZO CHA HAYA YOTE?
Chanzo kikubwa huwa ni wivu, watu wamejaa wivu na ndiyo maana watu wanazikana kwenye makaburi. Kwa mfano: Daniel alitupwa kwenye tundu la simba kutokana na wivu wa viongozi wenzake. Wakatafuta sababu ya kumpata wakasema hatuwezi kumpata isipokuwa kwa mambo ya sheria ya Mungu wake. Wakakutana na kukubaliana kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuomba dua kwa Mungu mwingine isipokuwa mfalme tu. Mwishowe mfalme akapiga muhuri ikawa sheria lakini ikimlenga Danieli. Na Danieli aliposikia akawa anaomba kutwa mara tatu akiwa amefungua madirisha ya nyumba yake, akashitakiwa hadi akatupwa kwenye tundu la simba ambao walikuwa na njaa. Lakini Mungu alimlinda na akatoka akiwa mzima. (DANIEL 6: 1-28).
RP Adrian akihubiri leo kwenye ibada
 
Share:
Powered by Blogger.

Pages