MCH. DR GODSON ISSA ZACHARIA
Na Mwandishi Wetu| Morogoro|Jumapili|06/10/2013
Kila kitu duniani lina chanzo chake, ukiangalia duniani kote
kuna matatizo marekani wana matatizo yao urusi korea japan na mataifa mengine
yoote yana matatizo. Kitu chochote ulicho nacho kina chanzo chake.
MITHALI 1:7 “KuMCHA Bwana ni chanzo cha maarifa………” hata
maarifa nayo yana chanzo chake kwa hiyo kila tatizo lina chanzo chake, na
ukitaka kuondoa tatizo ni lazima uende kwenye chanzo cha tatizo husika. Ni muhimu kutambua kuwa maisha yoote yanaanzia kwenye ulimwengu war oho, kabla mtu hujapata tatizo kwenye ulimwengu wa mwili, tatizo hilo linakupata kwenye ulimwengu wa roho kwanza, kushinda kwako au kushindwa kwako kunaanzia kwenye ulimwengu war oho. Na ndio maana Mtume Paulo alisema “kwa maana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wagiza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (WAEFESO6:12). Kwa hiyo ni muhimu kugundua kuwa kuna vita inaendelea kwenye ulimwengu wa roho na ndiyo inaleta matukio unayoyaona kwenye ulimwengu wa mwili.
TUNASHINDANA NA NANI?
Ufunuo 12:7-12. Hapa tunaona shetana pamoja na malaika wake
ambao ni mapepo na hao ndiyo wakala wa matatizo na uharibifu. Na hawa ndiyo
majeshi ya pepo wabaya ambao ndiyo chanzo cha matatizo, na mahali popote walipo
wanasababisha matatizo ambayo mengine yana ushahidi wa kidaktari, mwingine
anaweza kuwa bubu lakini chanzo chake kipo ambacho cha weza kuwa ni mapepo. Mfano: MARKO 9:17-29 “Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako ana pepo bubu, na kila ampagaapo humbwaga chini naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda. Nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze……. Akamwambia ewe pepo bubu na kiziwi mimi ninakuamuru umtoke mtu huyu wala usimwingie tena. Unaona, mara baada ya Yule pepo kutolewa mtu Yule akanena na akaendelea kusikia vizuri, wakati mwingine unaweza ukawa unakula chakula halafu unakonda pasipo kujua chanzo cha kukonda kwako, fahamu ya kuwa mapepo yanaweza kukufanya ukonde.
2WAFALME 22:22 Hapa tunaona pepo anajitokeza na kusema nitakwenda nakugeuka kuwa pepo wa uongo kwenye vinywa vya manabii wake Mfalme Ahabu ili wamtabirie uongo halafu aende vitani ili auawe huko. Hivyo pepo anaweza kumuingia mtu na kugeuka kuwa tayizo Fulani wanaweza kugeuka na kuwa kisukari, kansa, shinikizo la damu, wanaweza kugeuka na kuwa laana. Pepo akikuingia anaweza kukutia vitu ambavyo vinaweza kuhatarisha maisha yako. Mfano, shetani alimwingia Yuda aitwaye Iskariote naye akapata kumsaliti Yesu. Unaona! Hapa shetani anaweza akakuingia na kukushawishi uweze kumsaliti mwenzako au umsaliti baba yako, au mkeo, au mumeo au wanao, hii inadhihirisha kuwa vyanzo vya matatizo vinatokana na mapepo, na majini.
NINI KIFANYIKE KUONDOA HAYA MATATIZO???
majeshi ya Bwana wakisikiliza somo la leo kwa umakini ili waweze kubaini vyanzo vya matatizo yao |
majeshi ya Bwana wamenyoosha mikono ili kumruhusu Yesu atimue vyanzo vya matatizo maishani mwao |
showers of Glory wakimsifu Mungu leo ndani ya nyumba ya ufufuo na uzima |
mwimbaji wa nyimbo za injili Emmanuel Mwaitege akimsifu Mungu leo ndani ya nyumba ya ufufuo na uzima na wimbo wake ULINZI WA MUNGU UMENIZUNGUKA |