Mch Dr Godson (SNP)
Na Mwandishi Wetu|Morogoro|Jumapili|20/10/2013
SNP Dr Godson |
Utangulizi
Mji wa mauti unaitwa mji wa mauti kwa sababu kazi yake kubwa
ni kusababisha mauti. Na majina mengine unaitwa mji wa damu au mji wa kuzaa
mapoza, na umeandaliwa na shetani mwenyewe, mji huu umefanyika kuwa ni karakana
ya kutengeneza matatizo. Ndani ya huu
mji kuna mauti, kukosa kazi, kuzaa mapoza, kuna magonjwa, kuna umaskini,
kukataliwa.
LUKA 19: 41-43 “ Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia akisema laity ungalijua yata wewe katika siku hii yapasayo amani, lakini sasa yamefichwa machoni pako………….” Hapa Bwana Yesu aliuona ule mji na akawa anaona mauti ndani ya huo mji lakini watu wengine walijua ni amani walizidi kushangilia na kufurahi (mstari wa 37) lakini mafarisayo waliona wivu na walijua kuwa wao na mji wao wako salama hata hawamwitaji Yesu. Hivyo walianza kuwanyamazisha wanafunzi wa Yesu. Bwana Yesu aliwajibu kuwa wajaponyamaza wanafunzi hawa, mawe yatainuka na kushangilia hivyo hivyo. Huu mji wa yerusalemu Bwana Yesu aliuona uharibifu uliokuwa mbele yake na ndivyo ulivyo mji wa uharibifu umejaa damu japokuwa mtu huwezi ukauona kwa macho.
NAHUMU 3:1-4 “Ole
wake mji wa damu, umejaa mambo ya uongo na unyang’anyi, mateka hayaondoki……..
kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa Yule kahaba mzuri, Yule bibi wa mambo ya
uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake. Kwenye
vijiji utakuta kuna mtu mmoja ambaya ni mchawi na kila mtu anajua kabisa kuwa
huyo mtu ni mchawi lakini wanamwogopa kijiji kizima wanamwogopa kwa ajili ya
mambo yake ya uchawi. Hivyo kupitia yeye mji mzima umejaa damu kwa ajili ya
kuwaua watu lakini hiyo miji yote ni lazima iharibiwe kwa Jina la Yesu.
Katika mahubiri yaho mchungaji alizidi kusisitiza kuwa ni
muhimu kufahamu kuwa kuna maisha ambayo watu wanayaishi ni maisha magumu
yamejaa taabu ambazo hata kama rais wan chi angeamua kukussaidia asingeweza. Kwa
mfano kama mtu umechukuliwa msukule, rais wan chi hawezi kukutoa msukuleni,
yeye atakachoweza kufanya atahakikisha kuleta huduma za jamii mfano kujenga
shule, kuleta umeme, kuleta maji, lakini rais wa nchi hawezi kukusaidia wewe
ukiwa unakandamizwa na wachawi, ni mpaka pale ambapo watu wote watakapoamua
kumtegemea Yesu ndipo watakapoweza kuwekwa huru mbali na mji wa mauti. Hivyo ni
muhimu kufahamu kuwa miji ya mauti inaweza kupanga vifo kwa ajili ya watu,
lakini kwa wale ambao ni wana wa ufufuo mji wa mauti hauna nguvu juu yao. HII
NI SAA YA UFUFUO NA UZIMA.
Mch Kiongozi Dr Godson akimfungua mtu leo baada ya huyo dada kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. |