JUMAPILI: 31 MAY 2015 -
UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Ukumbuke
kuwa shetani ni mwindaji, anafanya
jitihada kuwakamata watumishi wa Mungu
na kuwawinda. Shetani hafanyi hii kazi peke yake, bali hushirikiana na
wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota na mawakala wengineo watumiao nguvu
za giza. Leo tunamfuata mwindaji popote alipo. Unapoina ndoa yako au biashara
yako au kazi yako n.k. haviendi vizuri ujue hakika kuwa kuna mwindaji keshaishughulikia.
1SAMWELI
23:25…[Basi Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta. Watu
wakamwambia Daudi; basi kwa hiyo akashuka mpaka mwambani, akakaa nyikani pa
Maoni. Naye Sauli alipopata habari, alimwinda Daudi nyikani pa Maoni.]….
Kama wewe ungekutana na Daudi akikimbilia huko nyikani ungejiuliza maswali ni kwa nini anakimbilia huko nyikani, asitulie?
Bila shaka Daudi angekujibu kuwa kuna mwindaji anauyetaka uhai wake. Ni baada tu ya Daudi kupakwa mafuta ya kuwa
mfalme, ndipo Sauli akaanza kumwinda Daudi. Lengo la Sauli ni kuzuia mpango wa
Mungu kwa Daudi. Hata kazini kwako,
kwenye ndoa, kwenye biashara n.k wapo watu wenye wivu wanaowinda hivyo
ulivyo navyo. Katika vita, mtu hatari sana ni mwindaji, kwani katika Biblia wanajulikana kama watu
mashuhuri. Hawa hujifanya marafiki
lakini kumbe sivyo walivyo. Hata wewe ulivyo okoka tayari ulianza safari
ya kuelekea kwenye ufalme wako. Shetani naye aliaanza papo hapo mipango yake ya kukuwinda,
kwa kila unachokifanya. Usipomwangamiza mwindaji huwezi kufanikiwa. Elewa kuwa
mwindaji ni makini, kwa sababu hataki agundulike kuwa anakuwinda na pia anajua
kuwa mtego alioutega waweza pia kumnasa yeye mwenyewe. Ndiyo maana mwindaji
huwa karibu na wewe ili aifahamu mipango yako.
Sisi kama kanisa lazima kwanza tushinde rohoni.
Kumbuka mfalme yule (Balaki) ambaye aliwaona Waisraeli wakija na akasema hawa watu si rahisi kuwashinda mwilini, lakini endapo
mtu wa kuwalaani atatokezea, basi kuwashinda itawezekana tu. Mtu akikulaani rohoni unakuwa umelaaniwa
kweli kweli. Ilimfanya Mungu amlazimishe punda aongee na Balaam kumwambia
asithubutu kuwalaani wana wa Israeli, kwani angewalaani tu hiyo laana igetokea.
Maisha yako hayajaanza pale ulipozaliwa.
Maisha yako yalianza tokea
ulipotungwa mimba. Hebu jiulize swali, wale mamajusi waliokuwa wakiifuatilia
nyota ya Yesu wakitokea mashariki je, safari yao waliinza lini hadi wakafika
Jerusalemu? Kumbuka nchi walizotoka ni mbali sana. Hili swali ni muhimu kwa
sababu enzi hizo ndege wala meli za kutumia mafuta zilikuwa hazipo. Hii
inamaana kuwa, safari yao waliianza hata kabla Mariamu hajajua kuwa atapata
ujauzito kwa njia ya Roho Mtakatifu.
Kinachonipa nifanikiwe siyo elimu yangu, wala kusoma sana, bali ni kwa sababu yumo anayekaa ndani yangu aliye
msaada wangu. Huyu ni Yesu Kristo, ambaye alikuwa name wakati wa vita. Shujaa
mimi bado nipo hai, ingawa walijitokeza wawindaji wengi toka kuzaliwa kwangu, lakini
Yesu alinipigania na kuvunisha. Tena ninao uwezo wa kumfuatilia Yule aliyetesa maisha yangu. Ewe
adui uliyekaa katika maisha yangu, ukawa unayapindisha,leo nakufuatilia kwa
Jina la Yesu. Sijazaa siyo kwa sababu sitaki kuzaaa, bali ni kwa sababu yupo
aliyekaa kama mwindaji maishani mwangu. Sijasoma siyo kwa sababu sitaki kusoma,
bali ni kwa sababu yupo aliyekaa kama mwindaji maishani mwangu. Kuna jinsi
navyotaka kuvaa, lakini yupo aliyekaa kama mwindaji maishani mwangu.
Imeandikwa ‘Mimi ni rungu la
Bwana na silaha za Bwana za vita”.
Hii ni saa yangu kuanza kuwapiga wote waliokaa ili kuniwinda. Mimi siyo kama wale uliowawinda.
Vita vinaendelea,kwa sababu bado napumua,
na kupitia pumzi hii, nitaimaliza kazi aliyonipa ya kukomesha wawindaji
wa maisha yangu. Namwambia Bwana kwa kuwa uliniweka hapa duniani kama silaha,
basi niwezeshe nipambane na hao maadui waliojipanga kinyume na maisha yangu kwa
Jina la Yesu. Maisha yako hayawezi kuwa
sawa kama Yule mwindaji hujamwondoa. Lazima usimame kinyume naye. Hapa nilipo
siyo sawa na hatima ambayo Bwana alitaka niwe. Leo lazima mwindaji huyu
aangamie kwa Jina la Yesu.
MIKA
7:2…[Mtu amchaye Mungu
ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika
wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.]….
Kumbe wanaowinda wengine ili kuwaangamiza wanawawinda hata ndugu zao. Hata
makanisani watu wa aina hii wapo.
HOSEA
9:8…[Efraimu alikuwa
mlinzi pamoja na Mungu wangu; na huyo nabii, mtego wa mwinda ndege u katika
njia zake zote; katika nyumba ya Mungu wake umo uadui.]…. Bado
mpendwa au mchungaji waliopo nyumbani mwa Bwana wanawawinda watu. Wapo
wachungaji na waazee wa makanisa waliojificha makanisani, wakiwa na ngozi za
kondoo lakini ndani ni mbwa - mwitu. Ndiyo maana si vyema kujidaganya eti huyu
mpendwa tunasali naye mchana. Hawa ni wale huenda kanisani siyo kwa miniajili
ya kusali, bali ni kwa ajili ya kujua
afya yako inaendelea je, hasa baada ya kukupitia usiku wake ulipokuwa umelala. Ni sawa, mnakuwa wote
kanisani mchana, lakini je, usiku unajua anachokifanya? Ndiyo maana tunasema wapo maadui
hata makanisani.
Si ajabu kwa Tanzania kuwaona wachungaji wakiwasifia
waganga wa kienyeji. Siyo ajabu kusikia kuwa kuna mchungaji ameenda kupata
nguvu kwa waganga wa kienyeji. Si ajabu kuona vibao vya wagamga wa kienyeji
ni vingi kuliko vibao vya makanisa.
HESBAU
23:22….[Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu
za nyati.]…
Huyu ndiye Mungu tunayemtumikia, nanguvu zake ni kama za nyati. Kama ulifikiri
Mungu wangu ni yule anayekaa msalabani hapo umekosea. Kama ulidhani Mungu wangu ni yule aliye mikononi mwa Mariamu ujue
umekosea sana. Mungu wa maisha yangu aliyeniweka hai mpaka sasa anaongea na
mimi sasa. Hii ni saa ya kuwafuatilia wale waliojikusanya kupambana na wewe kwa
Jina la Yesu. mungu hakupanga niwe kama nilivyo. Nilazima nirudi kama
ambavyoBwana alivyotaka niwe. Ewe adui uliyepambana nami katika ujana wangu
sikubaliani na wewe. Leo tunalifuatilia
jeshi la mwindaji wanaowinda maisha yangu, na lazima apigwe kwa Jina la Yesu.
Vipo vitu
viwili tu: Aidha unaokoka au unakufa kwa
Jina la Yesu. Biblia inasema “na alaaniwe mtu yule asiyutumia upanga wake kumwaga damu”.
Mimi ni nani nisiue kama nabii mkuu kama Eliya aliwakata vichwa manabii wa
Baali 450 (mia nne hamsini)? Sitaki kujua mwindaji ni nani. Pale nitakapopata
taarifa ya msiba, uwe wa kazini au biasharani kwangu, nitafahamu tu ni kuwa huyu
ni yuleyule aliyekuwa anawinda maisha yangu. Wapo wawindaji wengine wanaowinda
huduma zetu. Hawa hufanya juhudi ili watu wasifike kanisani au kusababisha mtu
akose nauli ya kuja kanisani. Kama ni elimu, uliipindisha. Kama ni ndoa yangu,
ni kweli uliiharibu. Cha muhimu siyo kile nilichopoteza, bali ni kinachofuata
baada ya hapa. Ni saa ya mimi kuongelea
yule Mungu mkuu kuliko miungu yote.
Kinachofuata
sasa: Endapo hujaokoka, sirahisi kuwashinda wawindaji wa
maisha yako. Ni vyema leo kufanya maamuzi
ya kuokoka ili uwe na uwezo wa kupokea nguvu kutoka kwa Yesu Kristo kupigana na
wawindaji wa maisha yako.
WIKI HII NI MFUNGO RASMI WA KUMSHUGHULIKIA KILA ALIYEWINDA
MAISHA YETU. NI OPERESHENI “FUATILIA MWINDAJI”
UKIRI:
Kwa Jina la Yesu, mimi
ni rungu la Bwana, na silaha
za Bwana za vita, leo ninataka kuwakomesha walioniwinda kwa Jina la
Yesu. Bwana Yesu kwa kuwa mimi ni silaha nigeuze niwe moto ili niwateketeze
walioniwinda kwa Jina la Yesu.
Amen
|
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: +255 765 979866 / (+255) 713 459545.