Sunday, September 22, 2013

SOMO: IMEKWISHA


 
Snp. Dr Godson Issa Zacharia akihubiri leo katika ibada
Na Mch: Dr Godson Issa Zacharia
Mwandishi wetu|Morogoro|Jumapili|22/09/2013

NENO LA MSINGI: YOHANA 19:28-30

"……….. lakini Yesu alipokwisha kuipokea ile siki alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”
Hili ni neno la mwisho alilolitoa Yesu kabla ya kuitoa roho yake, aada tu ya kusema hili neno, akaitoa roho yake. Neno la mwisho la marehemu lina uzito wake, ndiyo maana hata kwenye jamii ya watu ambao hwajamjua Mungu nao wanaogopa sana neno la mwisho wakati mtu anaelekea kufa. Hata kama mtu ni mwongo au mwizi anapoelekea kufa anaongea pointi tu hana muda wa kuweza kudanganya na hana muda wa kuleta utani, anaongea maneno yaliyochujwa tu.

MATHAYO 27:50 “Na Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake”
MARKO 15: 37 “naye Yesu aakatoa sauti kuu, akakata roho.”
Kuna watu wengi hawajui maana halisi ya neno “ imekwisha”, shetani alijua kuwa Yesu alimaanisha kuwa amekwisha, Lakini haikuwa hivyo, Yesu alikuwa anamaanisha kuwa amemaliza kazi ya kumkomboa mwanadamu. Kuna kazi ambayo Yesu alitumwa na Baba yake. (Yohana 4:34, 17:4),

Bwana Yesu alikuja duniani alikuja kwa kazi maalum na kabla ya yote alitoa muhtasari wa kazi yake ili dunia ijue kwamba alikuja kufanya nini.

LUKA 4:16-21………. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa  “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri masikini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika…….. akaanza kuwaambiwa, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” Hapa ndipo Yesu alitangaza kazi yake. Na baadae akaendelea kufanya kazi yake kwa waaminifu, alikuwa mwaminifu mpaka akaenda mautini, akiwa anataka kukata roho ndipo alitangaza kuwa IMEKWISHA, na ghafla tetemeko kuu likatokea na makaburi yakapasuka na pazua la hekalu likapasuka katikati toka chini hata juu.

Yesu akiwa msalabani alipiga keleleakisema imekwisha,magonjwa, laana taabu, mikosi, imekwishaa. Kila kazi ya shetani imekwisha, kila kifungo cha shetani kimekwisha kwa Jina la Yesu. KWA KUWA IMEKWISHA, NAMI NINAAMURU UKUE NA KUONGEZEKA, UMILIKI NA UTAWALE, UJENGE NYUMBA UKUE KATIKA USTAWI MAANA IMEKWISHAAAAAAAAAAAA.
Share:
Powered by Blogger.

Pages