JUMAPILI: 07 JUNE 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi:Tunaposema
silaha, wengi wetu wanawaza sime,
bunduki, mishale n.k. Mwindaji anapokuja kwako, huja akiwa na silaha. Imani yake
mwindaji ni kuwa, kwa silaha aliyoibeba, wewe hutapita. Hata hivyo, Mungu wetu naye ameandaa silaha. Tatizo kubwa hapa
ni kuwa, silaha ya Mungu haionekani, kwa sababu Mungu wetu hubadilisha kitu
kulingana na matumizi. Mungu akimaua
kugeuka sime,anafanya hivyo.
AMOSI
3:5..[Je!
Ndege ataanguka mtegoni juu ya nchi, mahali asipotegewa tanzi? Mtego utafyatuka
juu ya nchi, bila kunasa kitu cho chote?]…. Hii ina maana kuwa, umuonapo ndege
kanaswa katika mtego, ujue kuna aliyeutega. Kila kitu na mtego wake, na kila
silaha na mtu wake. Mtego wa ndege haumasni swala, na mtego wa swala haumnasi
nyani.
Katika maisha
ya kawaida, ipo mitego na pia wapo wawindaji.
Katika Biblia, shetani anaonekana akizuia Ibrahimu asipate uzao kupitia
Sarah, kwa kuwa alishajua kupitia uzao wa Ibrahimu Baraka za Mungu zitafuatana
na uzao wake. Shetani alitengeneza silaha za kumzuia Ibrahimu kupata motto, bila
yeye na mkewe kujua. Mwishowe, baada ya
kukata tama kwa muda mrefu, hatimaye alipata mtotoo aitwae Isaka. Hata hivyo
Isaka naye alipitia kipindi kigumu kama hiki cha Ibrahimu, kwa sababu tumbo la
mkewe nalo lilifungwa asizae.
Hata uhai ulio
nao ni sehemu ya miujiza. Kumbuka kuwa, Bwana amekupitisha katika nyakati usizozijua na kukuepusha na mitego
mingi sana ya wawindaji. Kila jambo
ulionalo maishani mwako lina sababu yake. Kwa kadiri unavyopiga hatua za maisha
yako, ujue kuna ………….
Kupitia Isaka,
shetani aliwachonganisha Yakobo na Esau. Kupitia Yakobo, shetani alisababisha
asimuoe Raheli kwa sababu alishaona ndani
ya tumbo la Raheli angepatikana Yusufu, yaani mkombozi wa wana wa
Israeli, atakayewaokoa wasife kwa njaa. Hata baada ya Yusufu kuzaliwa, shetani alitengeneza mipango mibaya ili
Yusufu asifikie ndoto zake. Yusufu alitengenezewa mipango mibaya, pale ndugu
zake walipomuuza kwa wafanyabiashara wa Kimisri. Kumbuka lengo la shetani
siyo Yusufu auzwe Misri bali auae na afe. Hata Yusufu alipokuwa Misri,
bado shetani aliendelea kuandamwa na shetani kiasi kwamba alitupwa gerezani, na
hapo ikawa ndio mwisho wa ndoto zake.
Yusufu akiwa
gerezani, ndiposa Farao akota ndoto ambayo haikupata mtafsiri bali kwa kupitia
kwa Yusufu peke yake. Yusufu alipotoka gerezani alienda moja kwa moja kuwa
mtawala wa nchi ya Misri. Bwana atafungua mlango kwako
Baada ya
Yusufu kuimaliza kazi yake ya ukombozi, alilala na baba zake. Mwanzoni mwa
Kitabu cha Kutoka, habari za Mfalme mpya wa Misri asiyemjua Yusufu zinaelezwa. Kila vita husimama kwenye kila hatua. Wazalishaji wa Kimisri
wanaelekezwa wasiachie Waisrael kujifungua salama, na ikitokea hivyo,
watoto wa kiume wote wauae‼ Kumbe
aliyekuwa anawindwa hapa ni Musa,
ili Israeli wasipate mtu wa
kuwaongoza watoke utumwani. Hata wazazi wa Musa nao walishindwa jinsi ya kumlinda, na kuazimia kumweka kando ya
mto na papo hapo Bwana akatengeneza njia
ya kumuokoa. Kumbe basi, wanaddamu hufika mwisho na wakawa hawawezi. Lakini ugumu wa wanadamu siyo ugumu wa Mungu Baba.
Usikate tamaa.
Yamkini upo mahali ambapo madaktari wamekuambia ugonjwa ulio nao hauna tiba, lakini Bwana Yesu yupo kwa ajili ya shida
yako, naye atafanya safina katika mito ya Misri. Kumbuka mwisho wa wanadamu
ni mwanzo wa Mungu. Katikati ya maadui,
Musa alikuzwa na kukua. Musa alikula mbele ya Farao, na kukulia ndani ya nyumba ya Farao. Mbinguni
Mungu alikuwa akijua huyu ndiyo mbabbe wa Farao. Musa akakua katikati ya adui zake. Daudi
akasema, “Bwana huandaa meza mbele
zangu, machoni pa watesi wangu”. Ambacho Wamisiri hawakukijua ni kuwa,
Musa ni kutoka juu na yupo kwa kazi maalumu. Kuku ni kuku,hawezi kuwa tai hata
siku moja.
Musa
alikimbilia jangwani ili kujifunza mbinu
za kuishi jangwani. Shetani alidhani kuwa Musa akiwa jangwani hatoweza tena
kuwakomboa Israeli. Hata hivyo
ndani ya jangwa alikokimbilia kwa
kuitwa muuaji, ndiko huko huko alipokutana na kichaka chenye kutoa sauti. Musa alipotoka jangwani, kwenda kwa Farao kwa
kazi maalumu, hakwenda kama yule Musa wa
zamani, bali alikuwa kama jemedari aliyepata mafunzo.
Muda
usingetosha ningekuletea habari za Joshua,
Esta, Gideon, Samsoni na Waamuzi mbalimbali wa Israeli. Cha kujua hapa
ni kuwa, Bwana kwa kila mmoja wao,
alifanya njia pasipo njia. Daudi mathalani, katika wana wa familia ya Yese, hakuonekana
wa maana, na ndiyo maana wakati Samweli
anasubiri ampake mafuta, Yese alikuwa kasahau kabisa kuwa yupo mwanane
mwingine ambaye hajatokezea. Ndiposa Bwana akamwambia Samweli, kuwa asimpake
mafuta Eliabu wala wana wengine wa Yese kwa sababu Mungu haangalii kama
vile wanadamu wanavyoangalia. Usiogope upitapo katika bonde la uvuli wa mauti, kwa
sababu Bwana yupo ili akupiganie. Hutakufa
wala hutaangamia,bali utaishi katika
ushindi wote.
ISAYA 49:1-2..[Nisikilizeni, enyi
visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana
ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. 2 Naye
anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake
amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake
amenificha;]….
Kumbe jina nililo nalo, hakunipa baba au
mama yangu. Hili ni jina alilonipa
Bwana, na wazazi wakatumika tu kukamilisha mpango wa Bwana. Wengine wananiona
mimi kama mshale, na gari la vita la Bwana. Kumbe yale magumu adui zangu
mnayoileta kwangu ni kutetemeka kwenu. Mimi
sikujua adui zangu wanatetemeka wanionapo. Kumbe adui wanapokuja na silaha zao
kwangu ni kwa sababu wanaziona silaha nilizo nazo mimi. Kumbe mimi ni silaha za
Bwana, ndiyo maana adui zangu wanatetemeka na kufuatilia maisha yangu
wanaponiona. Kama ulifikiri ndoa yangu
ilianzia hapa duniani ujue umekosea, kwa sababu tangu nikiwa tumboni nilishafanywa
silaha za Bwana za vita. Mwenye nyundo au rungu ndiye anayeibeba na kuichomoa
ili apige maadui zake. Imeandikwa “mimi ni rungu la Bwana na silaha za Bwana za vita”. Kwa hiyo Bwana mwenyewe
hukutumia wewe kuwapiga wachawi na wanaotumia
nguvu za giza kutawala. Bwana amesema “Bwana ni mtu wa vita,
Bwana ndilo Jina lake”.
Ni saa ya
kuwapiga walioharibu maisha yako. Usimuogope yule aliyekuja kufanya vita na wewe.
Ukiona unapigwa vita ujue tayari umemzidi adui yako. Jua kuwa kama ungekuwa
hujamzidi asingefanya vita na wewe. Hata
hivyo ili uweze kupigana ni lazima Yesu Kristo awe ndani ya moyo wako.
Endapo wewe hujaokoka, leo ni sikumuhimu kwako kufanya maamuzi ya kuokoa na ndipo uewze kupigana na adui wanaowinda maisha yako na kuwa mshindi katika Jina la Yesu.
Endapo wewe hujaokoka, leo ni sikumuhimu kwako kufanya maamuzi ya kuokoa na ndipo uewze kupigana na adui wanaowinda maisha yako na kuwa mshindi katika Jina la Yesu.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 765979866
/or +255 713459545