Sunday, August 10, 2014

SOMO: VIUMBE VISIVYOONEKANA - Na: RP Adriano

Baba (SNP) Dr. Godson Issa Zacharia (Kushoto) akimkaribisha RP Adriano
(Kulia) ili afundishe leo 10.08.2014  Nyumba Ya Ufufuo na Uzima Morogoro
Utangulizi: Somo la Jumapili ya leo  linaitwa “Viumbe Visivyoonekana”. Katika dunia yetu hii yapo  mambo yanayotokea kutokana na visababishi. Viumbe hapa duniani vipo  vya aina mbili: 

  • Vile viumbe vinavyoonekana na 
  • Vile viumbe visivyoonekana. 


Viumbe wale wasioonekana katika somo letu hili  siyo vile visivyoonekana kwa sababu ya udogo wake (mathalani, bacteria, virus n.k). Hapa tunavilenga viumbe visivyoonekana vya rohoni. Vile viumbe vya rohoni  visivyoonekana si  kwa sababu ya udogo wake, la sivyo; bali ni kwa kuwa ni viumbe vya rohoni, kama vile malaika, mapepo, Mungu n.k. katika Ulimwengu wa Roho.


YOHANA 1:14….[Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.]…


YOHANA 4:24…[Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.]…. Roho huwezi kuiona kwa macho. Katika ulimwengu wa roho wanaishi viumbe wasioonekana, kama vile viumbe watakatifu (malaika) na viumbe wachafu (mashetani) ndiyo maana shetani anaitwa mungu wa dunia hii kwa sababu vitu vyote vipo chini ya himaya yake.

RP Adriano ndani ya Nyumba Ya Ufufuo na Uzima - Morogoro leo 10.08.2014

LUKA 4:1-13...[ 1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, 2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. 3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. 4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. 5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. 9 Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; 10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba, Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 13 Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.]…. Shetani  alishajua Yesu amkeaa muda wa siku 40 katika mfungo bila kula, hivoy nikimletea wazo la mkate, ni dhahiri atakubali kula,  na akeshakula utamkaba tumboni na atakufa tu. Ni vizuri kukumbuka kuwa Biblia inasema “Nchi na vyote viijazazvyo ni mali ya Bwana”. Ndiyo maana hata leo wapo watu ambao huenda kwa wataalam/ waganga wa  kienyeji na kupewa uwezo huo kwa kufuata masharti fulani fulani ili wapate utajiri.


Hautakiwi kutamani mali za watu wengine kwa sababu baadhi ya hizi  mali hutokea kwa yule muovu shetani. Yesu hakumbishia shetani alipokuwa amemwambia kuwa “vyote vipo mikononi mwangu” kwa sababu Yesu anajua kuwa ule uwezo wa kumiliki wa binadanu ulitoweka pale bustanini Edeni alipodanganywa na shetani. Yesu hakutishwa na mali. Shetani  humpa mtu mali kama chambo ili mwishowe ammeze. Ulimwengu huu unaongozwa kwa njia za mali. Shetani alidhani kuwa kwa kuwa amezoea kuwadanganya wengine kwa kutumia mali, basi hata Yesu ni kama wale wale. “Yesu si kama wale” wanaotamani mali za ulimwengu huu. Shetani anaumiliki  ulimwengu kwa njia nyingi ikiwemo 'kutumia mali'.


YOHANA 12:31…[Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.]…Kumbuka kuna ulimwengu unaoonekana na ulimwengu usioonekana.  Ule ulimwengu usioonekana ndio unaosababisha “matukio”. Mfano: mtu na mke waliokubaliana kuoana baada ya muda mrefu wa mahusiano na makubaliano,  wanaanza kugombana na hata kuachana.  Ukiona hivyo ujue kuna viumbe wa rohoni wametumwa ili kuleta hayo “matukio”.
Majeshi ya Bwana ya Ufufuo na Uzima Morogoro
wakimsikiliza kwa makini RP Adriano leo 10.08.2014.



====

MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, Kila kiumbe kilichokaa ndani na kuniwekea dosari yoyote toka kwa Jina la Yesu.
====

Viumbe wengine huweza kukaa katika moyo wa mtu.  Utamkuta mtu  anakuwa analipuka tu kwa hasira,  kumbe ni pepo tu amekaa katika moyo wa huyo mtu. Leo ni siku ya kumtoa huyo pepo katika moyo wa mtu kwa Jina la Yesu.


MAOMBI: Achia  moyo wangu, kwa Jina la Yesu. Nayafungua maisha yangu yaliyofungwa, kwa Jina la Yesu. Kila kamba iliyofungwa katika maisha yangu, .. Ewe joka uliyegeuka ukawa uvimbe, niachie kwa Jina la Yesu. Achia biashara yangu kwa Jina la Yesu. Kila msingi uliojengwa ili usababishe matatizo, leo naubomoa kwa Jina la Yesu. Imeandikwa "Na ishara hizi zitaambatana na wale waaaminio, na kwa Jina langu watatoa pepo", ....Ewe pepo mchafu nakuamauru kuanzia sasa toka,  toka,  kwa Jina la Yesu, naliondoa giza katika maisha yangu, giza kwenye biashara, giza katika elimu, giza katika ndoa, naliondoa toka,  kwa Jina la Yesu, kuanzia leo maisha yangu yafunguliwe kwa Jina la Yesu.


Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomjua Yesu. Hakuna mtu anakuwa kwenye mamlaka ambapo hakuna nguvu iliyomuweka hapo!!. Ukimuona mtu yeyote  (Mkurugenzi, waziri n.k) amekaa kwenye kiti chake,  ujue ipo ‘nguvu ya rohoni’ iliyomweka mahali pale. Unakumbuka kipindi kile  Yesu alipopelekwa kuhukumiwa, Pilato alianza kumdhihaki Yesu,  lakini Yesu akamwambia ‘kama siyo Baba yangu wa mbinguni aliyekuweka hapo usingekuwa kiongozi kwa nafasi hiyo’.


WARUMI 10:9-10…[Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.]… Unapokiri ni kwa “kinywa chako”.  Siyo kwa kinywa cha mchungaji  wako. Unapokiri kitu unapokea kitu. Ndiyo maana ni  lazima ukiri kuwa "sitakufa" na itakuwa hivyo ulivyosema.
======

MAOMBI: Mimi ninayesema kuanzia sasa maisha yangu yatakuwa sawasawa na yalivoypangwa kwa Jina la Yesu. Nakiri kuwa ‘Nitaoa nitaolewa/nitaoa, nitasoma, nitafanikiwa’ kwa Jina la Yesu. Kila maneno niliyotamkiwa, maneno niliyotamka binafsi, leoNayabatilisha.  Nayatengua maneno hayo. Sitakuwa maskini kwa Jina la Yesu. Mimi ni tajiri kuanzia leo. Maneno yaliyosemwa kabla sijazaliwa, nayafuta maneno hayo kwa Jina la Yesu, maneno ya ndugu, maneno ya ukoo nayafuta kwa Jina la Yesu.
======

Unapoona biashara yako haiendi ujue kuna nguvu nyuma ya hilo tatizo. Waweza kuwa unafanya biashara ya kandambili,  lakini wateja wanakuona kuwa unauza mihogo. Ndiyo maana kwa wale wafanya mazingaumbwe, huweza kugeuza macho ya watu na hivyo kuonekana kama vile 'mkuki umeingizwa kichwani mwao, na kutokea masikioni'. Kumbe kinachoonekana hapo siyo kweli, bali ni  macho ya watu yamegeuzwa na kuyafanya yaone hivyo jinsi yanavyoona upotofu huo.
=====

MAOMBI: Leo nafungua leso kwa Jina la Yesu. Sanda nilizofungwa mikononi na miguuni mwangu, nazifungua kwa Damu ya Yesu. Niachie niende, niachie nikue, navuka mstari wenu mlioniwekea kwa Damu ya Yesu. Leo ninaamka kutoka usingizini mlikonilaza kwa Jina la  Yesu. Naamka kifedha, naamka kihuduma kwa Jina la Yesu.
=====


==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==

==(Cellphone: (+255) 713 45 95 45)==
Share:
Powered by Blogger.

Pages