JUMAPILI: 17 AUGUST 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Kutoka Kushoto: AP Amos, SNP Dr. Godosn na RP Mwandambo wote wakimsifu Bwana Yesu katika ibada ya Jumapili 17/08/2014, Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro. |
MAOMBI: Kila mchoiro waliyonichorea
ninaifuta na kuitegua kwa Jina la Yesu.
Katika maisha hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya
(coincidence). Kwanza ijulikane kwamba uovu ulioratibiwa, hufanywa na watu
mahiri, wachawi waliobobea. Yamkini ipo michoro imeshachorwa kwa ajili yako ila wewe hujui.
Majeshi ya Bwana Yesu katika kusifu kwenye ibada ya Jumapili 17/08/2014, Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro. |
MATENDO 23:12-16 ..[Kulipopambauka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo. 13 Na hao walioapiana hivyo walipata zaidi ya watu arobaini. 14 Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo. 15 Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia. 16 Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari.]….. Kitendo cha kufunga ni kitendo cha kuongeza nguvu za rohoni. Pamoja na uovu huo, walidhamiria kuongeza nguvu za kiroho, ingawa ni za uovu. Walifanya huo mfungo ili watu wasiwashtukie, bali waonekane ni watu wa dini.
MATENDO
23:20-21 ..[Akasema Wayahudi
wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana
kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi. 21 Basi wewe usikubali;
kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala
wasinywe hata watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakiitazamia ahadi kwako.]…
Uovu huu ukikupata siyo wa ghafla. Wapo wasimamizi
wa huo uovu ulioratibiwa. Ukiona kuna mafanikio yakitokea kwenye mazishi,
harusi, tatizo, taabu, kifo n.k. ujue kuna mratibu wa mambo hayo. Hakuna
shughuli inayofanikwa bila kuwepo kwa mtu wa kuratibu hayo mafanikio.
Leo tunamtangazia yeyote aliyeratibu matatizo katika
maisha yako akuachie kwa Jina la Yesu.
MAOMBI: Waratibu wote, wachawi, wasoma
nyotaa nawafyeka kwa Jina laYesu.mratibu yeoyote anayeratibu kuanguka kwangu
nakuponda kwa Jina la yesu. Ewe mratibu joka uliyetuma unirudishe shimoni, au
unirudishe Misri, nakuponda kwa Jina la yesu. Ninaamuru waratibu owte, waratibu
wa familia, waratibu wa ndoa, awaraibut
waukoo, waratibu waliotumwa wakusimamie wewe katika dhiki yako, ninaamuru
wakuachie leo kwa Jina la yesu. Amen.
Unaona Paulo alikuwa ni mtu kama wewe lakini wakawepo watu zaidi ya
40 wakawa wamepanga kumuua. Ndivyo hivyo hata leo, yawezekana wapi watu wengi
wanaoratibu shida kwa ajili ya maisha yako.
Asingekuwepo mtu wa kutoa ile taarifa ya ule uovu ulioratibiwa, leo hii tusingekuwa tunamfahamu Paulo. Leo lazima tufute michoro yote iliyochorwa kwa
ajili yako kwa Jina la yesu.
Walipotaka kumuangusha Danieli, walikaa kikao na
wakachora mchoro wa uovu. Kazi ya kuratibu uovu siyo ya mtu mmoja.
MAOMBI: Michoro ya kifo, michoro ya kushindwa, michoro ya hasira, michoro ya kupoteza ngooka kwa Jina la yesu. Aliyeniandalia
taabu hii ninayoiptia, namponda kwa Jina la Yesu. Kila uovu ulioratibiwa, naupiga kwa Jina la Yesu. Yeyote aliyenitega
mtego, nakufyeka kwa Jina la Yesu. Amen.
NAMNA GANI WAWEZA KUUSHINDA UOVU
ULIORATIBIWA?
Endapo upo mradi au mratibu, na kasha huyo mratibu akaondolwa, huo mardi hukoma kuendelea. Mfano, endapo mradi
ulianzishwa na raisi fulan, pale akeshatoka madarakani mradi huo huinia shakani
kuendelea, na mara nyingi huisha. Mchoro ukeshachorwa wanaluwepo
wasimamizi wa ujenzi wa kufanya sawasawa
na huo mchoro. Mfano: Mchoro wa kumfanya mtu apate ajali, mchoro wa kumfanya mtu apinde miguu, mchoro wa kumfanya mtu akataliwe.
MAOMBI: Mratibu wa uovu, kwenye ndoa, biashara, familia, nakuponda katika Jina la Yesu.
Kutoka Kushoto: SNP Dr. Godosn akisikiliza ushuhuda wa familia ya Tumaini kutoka Iringa tarehe 17/08/2014, katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro. |
MWANZO 11:1-9 …[Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. 3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. 5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.]… Tunaona jinsi wanadamu walivyomuasi Mungu wazi wazi. Mungu alikuwa hapo awali alishaagiza wanadamu wazaane na kuijaza nchi yote, lakini hawa wanadamu wakagoma kutawanyika juu ya nchi kama ambavyo Mungu aliagiza. Kawaida ya wachawi wote, wanakuwa na lugha moja. Leo ni siku ya kuwachafulia lugha zao kwa Jina la Yesu. Usemi wao uchafuliwe kwa Jina la Yesu. Amen
MP Onesmo (suti nyeupe) akiimba kumsifu Bwana Yesu katika ibada ya Jumapili 17/08/2014, Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro. |
Mungu tayari
aliashakuandalia mchoro mzuri kwa
maisha yako. Hata hivyo, watu waovu huweza kuja na kuiba mchoro
wa Mungu kwa maisha yako, na kinachotokea ni kuwa, mchoro
bandia huletwa, na wasimamizi wake hupewa
kazi ya kusimamia mchoro bandia wa maisha yako. Wapo wengi waliotumwa
kuhakikisha kuwa haufanikiwi. Leo ni siku ya kuwachafulia usemi, wote
waliokubaliana kinyume na maisha yangu kwa Jina la Yesu.
==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713
45 95 45)==