Monday, August 29, 2016

SOMO: MIKATABA YA KISHETANI


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH

UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO

JUMAPILI - 28  AUGUST  2016.




Na: STEVEN NAMPUNJU (RP)



AGANO / au MKATABA ni mapatano au makubaliano yanayokuwepo kati ya mtu na mtu au kikundi na kikundi,  Ndani ya mkataba kunakua na makubalioano. Kwenye mkataba kuna malengo , kama ajira au kazi. Lengo la mkataba ndilo litanifanya niusaini mkataba.Pindi tu Unaposaini mkataba   kuna wajibu ambao unatakiwa uutende. Kila Mikataba una malengo yaliokusudiwa  katika mkataba huo.


RP Steven Nampunju akifundisha kuhuusu "Mikataba ya Kishetani" Ufufuo na Uzima Morogoro 28/8/2016


Kuna mikataba ya aina mbili:-

  •  Mkataba wa wazi
  •  Mkataba wa siri



 Mikataba hiyo inapokuwa inasainiwa   inakuwa imebeba malengo tofauti tofauti.

Kuna mikataba ya maandishi  na kuna mikataba ya maneno Ipo mikataba inahitaji maandishi na mashahidi  kadha  wa kadha. Ukijua mkataba utajua kazi ya mtu , ukisaini mkataba utajua wajibu wa mtu katika maisha yake ya kila siku  Ndani ya ule mkataba kuna majukumua mbayo unatakiwa utende na kuna vitu ambavyo hautakiwi kutenda.


Mungu aliwahi kufanya mikataba na watu mbalimbali katika Biblia:



Imeandikwa katika MWANZO 6:13-19

(Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia. 14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami. 15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake. 16 Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu. 17 Na tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa. 18 Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe. 19 Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke.)



Mungu anamwambia Nuhu  Kila chenye mwili mwisho wake ulikuwa umekaribia. Kisha Mungu akamwambia Nuhu aandae "mkataba  wa safina" ili watakao kuwa ndani ya safina tu ndio watakao kuwa wamepona, na watu wakawa wanamcheka sana Nuhu. Kumbe hao watu walikuwa hawajui kuwa  Nuhu alikuwa ameongea na Mungu.  Mchana wa leo Mungu anataka kuongea na wewe uweke mkataba wa kumtumikia yeye. Mchana  huu jaza mkataba na Bwana.



 Mfano wa pili Mungu aliwahi kufanya mkataba wa maneno na Ibrahimu



Imeandikwa katika MWANZO 12:1-5

(Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. 4 Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani. 5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.)



Mtu mwingine ambaye Mungu alifanya nae mkataba wa maneno ni Abrahamu. Alikuwa anafanya shughuli zake za kawaida za ufugaji. Mungu akamwambia atoke.  Kumbe mkataba unaweza ukakuhamisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hata katika kazi za kawaida za serekali au kampuni mfanyakazi anaweza kuhamishwa kutoka kituo kimoja hadi kituo kingine. Hatima uliyonayo leo ni kutokana na mkataba  uliousaini wewe kipindi Fulani cha maisha yako.


Matatizo yanayompata mtu ni kutokana na  yeye kuvunja mkataba  bila njia sahihi za kufanya hivyo. Ndani ya mkataba ndipo kuna ulinzi. Kutokana na mkataba mtu unaweza ukahamishwa kutoka sehemu  moja kwenda sehemu nyingine.  Mungu wetu huwa anatunza maagano na anapenda maagano.


Vijana wa Showers of Glory wa Ufufuo na Uzima Morogoro wakiimba na kucheza mbele za Bwana 28/8/2016



Imeandikwa katika MWANZO 6:18

(Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe.)

Hapa tunaona jinsi Mungu alivyofanya mkataba na Nuhu mkataba huo  unahusisha  watoto wa Nuhu, wajukuu wa Nuhu, wakwe wa Nuhu, na mifugo ya Nuhu. Kumbe basi, Mtu mmoja kwenye familia anaweza akasaini mkataba na  mkataba huo  ukapelekea  familia nzima ikaingia kwenye matatizo.  Watu waliokuwa juu yako wamejaza mkataba gani kukuhusu? Yumkini kuna mkataba ambao umejazwa na ambao wewe unatembea na ule mkataba, yale yanayokupata leo yanatokana mkataba wa siri  uliojaza  na ndiyo unatesekea hadi leo.



Imeandikwa katika MWANZO 15:18-21

18 Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati, 19 Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni, 20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai, 21 na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.)



Mungu anaweka mkataba na Ibrahimu kabla hajapata mtoto wala kufika nchi anayotakiwa kwenda. Ni kweli leo hauna kazi lakini Mungu anaona hatima yako ilivyo, na anaiona  kazi yako, na mafanikio yako pia. Isaka alizaliwa baada ya agano kufanyika.  Kabla hujazaliwa Mungu alishafanya mkataba tayari. Mkataba unaweza  kupelekea mtu  ukabadilisha jina lako, kama katika ule Mkataba ambao Mungu aliusaini na Abrahamu.


Mungu alisaini na Samsoni kabla ya kuzaliwa. Lengo lilikuwa kuja kuwaangamiza  wafilisti.  Malaika alikuja kumwambia Manoa  kuwa asije akaharibu mkataba, hivyo asinywe kilevi wala chochote ambacho ni najisi wala uchafu wowote.  Leo umeharibu mkataba wa mtoto wako kwa kunywa pombe tangu akiwa tumboni, au kwa kumpeleka kwa waganga!!!! Ndiyo  maana leo hii mtoto huyo darasani amekuwa haelewi chochote!!!.



Mfano mwingine Mungu aliweka mkataba na zakaria ya kwamba mkewe Elizabeth atachukua mimba nae  atamzaa mtoto mwanaume na jina lake atamwita Yohana.

LUKA 1:8-17,

LUKA 57-66.


Usikubali leo kuzuiliwa kwa sababu mkataba wako unakuruhusu kufanya kazi. Ipo mikataba ya kishetani lengo ni kumuangamiza mtu na kuharibu maisha yake. Kuna watu walifanya mikataba na kuzimu inayowatesa hadi leo. Watu wengine mliota ndoto mtu anakupa sarafu ya shilingi mia mia mbili kumbe ni mkataba ulitengenezewa inayomtesa hadi leo, na wengine ulikwenda kwa mganga wa kienyeji akakuchanja chale ile damu ikabaki kwa mganga wa kienyeji ikafanyika mkataba. Nguvu ya kufanya kazi katika maisha ya mtu ipo ndani ya mkataba. Kuna hatari ya kutokujua mkataba. Mungu alimpa Musa amri kumi ambazo wana wa Israeli walitakiwa kuzifuata, kama mkataba wao.


Petro alimuuliza Yesu Kristo kuwa "sisi tumeacha kila kitu je tutapata nini", utaona kwamba alitaka kujua  hatima ya mkataba wake.  Inawezekana leo umekuwa na changamoto ulizonazo , shida ulizonazo kutokana na mikataba waliyosaini watu waliotutangulia



 IPO MIKATABA YA KISHETANI,

Ambapo shetani anakutesa kutokana na mikataba ambayo walisaini watu waliotutangulia.



Imeandikwa katika 2Wafalme3:26-27

26 Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 27 Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.


Sehemu ya Umati wa Watendakazi wa Ufufuo na Uzima Morogoro wakifuatilia kwa makini mafundisho, kwa kuandika.


Yesu yupo na anataka apenye kwenye kila mkataba aokoe maisha yako  Kuna watu wapo kwenye mikataba ambayo inawatesa unaweza ukasaini mkataba  na unamtesa, unaweza ukasaini kwa njia ya ndoto, kwa waganga wa kienyeji.Kifungo cha mkataba ni hatari sana huwezi kutoka mpaka umalize mkataba. Na kuna hatari kubwa sana ya  kuvunja mkataba bila utaratibu. Mkataba una mashatri mengi sana  ambayo  yanamfunga mtu.  Leo lazima tufanye mkataba na Bwana , ili ufanikiwe lazima uwe na mkataba.  Ijapokuwa Yusuph aliuzwa utumwani na wana  wa Israeli walienda utumwani miaka mia nne  lakini Bwana akawatetea , Ni kwasababu Mungu alikumbuka agano lake , wakati wakiwa njiani wakakutana na wayebusi ,waamaleki , wahiti, wahivi, wakaangamia wote kwasababu ya mkataba wake na Ibrahimu na Musa. Ipo mikataba ya kishetani ambapo shetani anafanya mkataba na mtu mmoja mmoja, au unafanya mkataba na taifa. Hasara ulizokuwa nazo leo zimetokana  na kuvunja mikataba bila utaratibu.



Watendakazi wakiombea watu waliofungwa na "Mkiataba  ya Kishetani"  na kuwaweka huru kw Jina la Yesu 
Jumapili 28/8/2016 - katika Bonde la Maono Mkundi (Myumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro)


Kuna watu leo wamefungwa na mikataba wasisaidiwe tena, wasije wakaolewa kabisa, wasifanikiwe tena.





Shida ulizokuwa nazo ni matokeo ya mikataba Fulani, sasa utaona unakuwa na wasimamizi ndani yake ambao ni majini, mapepo, mashetani, mawakala ambao wanazuia mtu asisonge mbele. Kuna mikataba ya msimu, ni mikataba ambayo unakuta mtu anakuwa na shida au matatizo kwa kipindi fulani,kama ni magonjwa basi mtu huyu anakua mgonjwa kwa kipindi kifupi baadaye anapona,baada ya miezi kadhaa ugonjwa unamrudia tena.

Ila pia kuna mikataba ya mda mrefu,mtu anapatwa na shida inakua ni ya kudumu,kama ni mateso yanakua juu ya maisha yake yote hadi atakapokufa.



UKIRI
Leo ninaamuru wachawi wote walioandaa mkataba nikasaaini katika ndoto leo mniachilie kwa jina la Yesu,mikataba yote ya siri iliyosainiwa kwa siri iwe ni kwa waganga wa kienyeji leo naifuta kwa jina la Yesu,kuanzia leo ninawakabili wasimamizi wa mikataba leo mniachilie ,mikataba yote iliyosainiwa kwenye ulimwengu war oho ya kutumikia mizimu naiharibu leo kwa damu ya Yesu ,naishambulia mikataba ya maneno,mikataba ya chale ,nashambulia misingi yenu mikataba ya kifo naishambulia leo,ninateka kila nguvu ya mikataba inayotesa maisha yangu,navunja mikataba yote iliyopelekea nishindwe ,iliyofunga maisha yangu kwa jina la Yesu.




Share:
Powered by Blogger.

Pages