GLORY OF
CHRIST TANZANIA CHURCH,
UFUFUO NA
UZIMA MOROGORO
JUMAPILI 04
SEPTEMBA 2016.
NA: STEVEN
NAMMPUNJU (RP)
Swali la kujiuliza: Sadaka ni ni kitu gani? Sadaka ni kitu chochote atoacho mtu kwa 'mungu yeyote yule' ili
huyo mtu atendewe kitu fulani. Katika Biblia hata shetani anaitwa “mungu wa dunia hii” (1KOR
4:4…(ambao ndani yao mungu wa dunia hii
amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake
Kristo aliye sura yake Mungu.)). Mtu atoavyo sadaka, lengo kubwa ni ili
atendewe kitu fulani na “mungu” wake. Sadaka ni kama agano lifanyalo kazi kati
ya mtu na mungu. Biblia inaonesha pia kuwa Mungu aliwahi kuitoa sadaka kama ilivyoandikwa
katika YOHANA 3:16… (Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.). Mungu kwa
kuupenda ulimwengu aliamua kumtoa mwanae wa pekee, kama ishara kuwa anaupenda
ulimwengu huu. Lengo la Mungu kumtoa mwanae wa pekee ilikuwa ni kuunusuru
ulimwengun usipotee. Kwa hiyo kila sadaka inayotolewa inakuwa na malengo.
Ibrahimu vivyo hivyo alipotokewa na Mungu, aliambiwa amtoe
sadaka mwanae wa pekee Isaka. Hata hivyo Mungu alimpatia mbadala wa mwanae kwa
kumletea Ibrahimu mwanakondoo aliyefnyika sadaka pale madhabahuni badalaya
Isaka. Nuhu aliwawahi kutoa sadaka na Mungu
akaipokea.
1. Sadaka
inao uwezo wa kuongea hata kama aliyeitoa ameshakufa.
Sadaka ina nguvu ndani mwake.
WAEBRANIA 11:4…(Kwa
imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo
alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo,
ijapokuwa amekufa, angali akinena.). Ijapokuwa biashara imekufa tayari,
au kazi imeshakufa tayari, lakini sadaka yako itaendelea kuongea kwa Jina la
Yesu. Sadaka inaweza kumfanya mtu aongee.
2.
Sadaka ina uwezo wa kubadilisha
historia ya mtu.
Mtu ambaye alitakiwa ashinde lakini ikitolewa sadaka kwa wasiofaa, mtu huyo
atashindwa tu.
MATENDO
9:36-40
… (Na
mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi
(yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37
Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya
kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie
kuja kwetu. 39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu
orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu
na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa
nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena,
Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua,
akaketi.).. Kilio hakiwezi kuiondoa taabu, na ndiyo maana Petro
akawatoa nje wale waliokuwa wakilia. Kupitia sadaka, historia ya Dorkas
inabadilika kutoka kwa aliyekufa hadi kwa aliyefufuka.
3. Sadaka
inaweza kumfunga mtu.
Imeandikwa katika MATHAYO
23:18…(Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa
sadaka iliyo juu yake, amejifunga.). Kumbe kuapa tu siyo tatizo, ila
tatizo lipo endapo kuapa huko kunaendana na sadaka.
Imeandikwa katika UFUNUO
2:14….(Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu
washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya
Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.).
Kumbe hapa sasa tunajifunza kuwa zipo sadaka zinazotolewa kwa sanamu (mashetani).
Katika 1WAKORINTHO 10:20
Imeandikwa…..(Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala
si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea
kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.). Sadaka huleta uhsirika
katya mtaoaji na Sadaka inakuwa na malengo mbalimbali. Shetani anaweza kupokea
sadaka ili kuharibu maisha ya mtu. Imeandikwa katika YOHANA 10:10.. (Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.). Mwivi huyu ni
shetani. Lengo la kwanza ni kuiba, na akiona huyu mtu hafai
kuibiwa anaingia kutekeleza lengo la pili
ambalo ni kuchinja. Shetani akiona kuchinja hawezi ataamua
kuharibu tu. Kwa upande wa Mungu wetu,Yeye pia hupokea sadaka za watakatifu
wake, na humfanya mtu anayemtolea sadaka
hizo kwa uaminifu afanikiwe.
Kama wewe hujaokoka, leo ni vyema kumkabidhi Bwana Yesu maisha
yako ili kuweza kumpinga shetani na wale watoa sadaka kwa mashetani kwa
kuitumia Damu ya Yesu.
© Media and Information Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima Mkundi - Morogoro)
Tel: +25571765979866 / +255713459545
|