Sunday, June 22, 2014

SOMO: KIWANDA CHA KUIUNDA KESHO YANGU NINACHO - Na: Pastor Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)

JUMAPILI: 22 JUNE 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

Utangulizi: Somo letu  linaitwa “Kiwanda Cha Kuiunda Kesho Yangu Ninacho”. Ukiwa unacho kiwanda una vyote na huwezi kukwama. Kwa mfano, endapo watanzania wakiamua kuzichoma moto gari zote aina ya Toyota,  siyo kwamba utakuwa mwisho wa bidhaa za Toyota kuwepo duniani kwani bado kiwanda chenyewe kipo Japan na kinazalisha bidhaa zake kama kawaida.


MITHALI 6:2…..[Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,]… Kumbe kinywa chaweza kugeuka na kuwa mtego unaoweza kunasa. Maneno yatokayo kinywani yana uwezo wa kutega mtego. Kila mmoja anacho  kinywa chake. Hapana kiungo kingine katika mwanadamu chenye uwezo wa kutoa maneno zaidi ya kinywa. Ili mtu aapate Baraka au laana hapa duniani, lazima kiwepo kinywa cha kuyafanya hayo. Kinywa ndico kiwanda chcenye uwezo wa kutengeneza maisha, kazi, ndoa, uumbaji wa aina zote n,k. mungu aliumba vyote kwa kutumia kinywa. Utaona imo nguvu katika kinywa. Watu wengi wamejisahau wanafananisha kinywa na viungo vingine kama mkono,  mguu n.k.




MWANZO 1:3...[Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.], 


MWANZO 1:6...[Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.], 


MWANZO 1:9...[Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.], 


MWANZO 1:14-15...[Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka.15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.], 


MWANZO 1:20...[Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.], 


MWANZO 1:24...[Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo], 


MWANZO 1:26...[Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.], 


Mungu alitamka na kila alichotamka kikawa hivyo. Mungu alisema,ikawa…. Alisema tena, ikawa. Akasema tena,  ikawa………………. Kesho yako imeunganishwa sana na kinywa chako.  Yamkini maisha uliyo nayo leo ni matokeo ya kinywa chako, au kinywa cha mtu mwingine aliyenena kukuhusu wewe. Uwakilishi wa wananchi Bungeni hufanywa na Wabuge, na kile wanachokijadili hugeuka na kuwa sheria ya kupindisha kesho yako.


2 NYAKATI 18:19-22… [Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramothgileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 20 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? 21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo. 22 Basi sasa, angalia, Bwana ametia pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa; naye Bwana amenena mabaya juu yako.]... Uwe makini  sana na kuwakilishwa. Mungu alikuwa na uwezo wa kumuua Ahabu. Lakini kumbuka kuwa Mungu haui. Mashetani yapo tayari kufanya hivyo. Kwa kinywa cha Manabii, ufalme wa Ahabu ulikoma kabisa. Hebu jiulize! Huyo anayekuwakilisha kwenye serikali  ya  mtaa, bungeni, wilayani n.k. Je, anakuwakilisha kiukweli kama Bwana anavyotaka? Hawa wawakilishi wetu huvamiwa na mapepo yanayowalazimsha kutamka mambo ya kuzimu.


MAOMBI: Kwa Jina la Yesu,  ninalzaimasha vinywa vya wawakilishi wangu, naviteka, naamuru malaika w Bwana alazimishe hivyo vinywa viyataje yaliiiyo mema kwa ajili ya kesho yangu, name nakiteka kwa Jina la Yesu.


NINI KINATOKEA UNAPOSEMA WEWE?
Jirani sana na kinywa chako kuna wasajili wa maneno. Hawa wasajili wanashikilia faili kabisa ili kunukuu yale unayotamka. Wasajili wa manenoni wa rohoni na si rahi kuwaona kwa macho. Wapo wasajili  wa aina mbili: Malaika wa Mungu na Malaika wa Shetani (Mapepo).

1.      Malaika wa Mungu:
Huandika neno lolote la uhai unalotamka. Kwa mfano,  unaposemanimepona,  hawa hulichukua hilo neno hadi msalabani ambapo kwa kupigwa kwa Yesu sisi wote tumepona. Ukisema nitakuwa tajiri, idara maalumu ya vifaa, hawa humwendea Yesu na kumwambia imeandikwa ulikufa maskini ili sisi tuwe tajiri.

2.      Malaika wa Shetani.

UFUNUO 12:7-12 … [Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.]… Kwa hiyo malaika Mikaeli anao malaika zake na Yule Joka naye ana malaika zake. Kwa hiyo katika kinywa chako,   wapo wawakilishi wa pande zote mbili kwa ajili  ya  kusajili maneno ya kinywa chako.


JE, ITAKUWA JE KUSEMA WASAJILI WOTE WAWILI WAPO WAKATI MTU HUYO YUPO KANISANI LEO?

ZEKARIA 3:1… [Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.]….

ZABURI 1:1...[Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki;Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.]… Ukikaa penye baraza la wenye mizaha, maana yake na wewe utatamkka maneno ya mizaha. Wala usisimame na
Utaona kuwa, hata umaskini wa nchi ya Tanzania unatokana na maneno ya yaanayotamkwa na viongozi wetu. Tanzania siyo maskini. Tumezungukwa na madini ya kila aina. Madini kama Tanzanite hayapatikani nchi nyingine yoyote. Lakini maneno ya ‘umaskini wetu, umaskini wetu’ yanayotamkwa na vionngozi wan chi hii husajiliwa na mashetani na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa maskini.

MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, leo  ninakataa maneno yalizalishwa na kinywa changu, viongozi wangu, ndugu zangu na wawakilishi wangu, Nakataa kwa Jina la Yesu.
Kinywa ni kiwanda cha kutengeneza kesho  yako. Ni lazma kukitumia kiwanda kwa mambo ya uzima. Mungu alitupa kuchagua kati ya uzima na mauti.


KUMBUKUMBU 30:15… [Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;]….


KUMBUKUMBU 30:19… [Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako]…. Usipochagua jinsi ya kutumia kiwanda chako,kitafungwa au watakikodi watu wengine kukitumia. Endapo ulikuwa mwimbaji kanisanai naukamuacha Bwana, Lusifa atakikodi kinywa chako na ndiposa mtu huyu huanza kuimba nyimbo za kishetani.


MAOMBI: Nakataa kwa Jina la Yesu, Enyi Wasajili mliosajili magonjwa niliyotamka, mliosajili laana nilizotamka, niachieni kwa Jina la Yesu.


HESABU 22:6 …[Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga,   niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.]…. Balaam upande mmoja anaoekana kama Mtumishi wa Mungu, upande mwingine, kinywa chake kiliazimwa ili  kulaani wana wa Mungu (Israeli). Wale watu walimpa sadaka ya uganga ili Balaam awalaani wana wa Israeli. Kuna mtu umeitwa uwe mwimbaji, au  Mwinjilisti na umeanza taratibu kugeuka. Usipotumia kiwanda chako kama Bwana atakavyo kitafungwa, na pindi  kifungwapo, kitazimwa na wageni wakitumia kwa kazi za kuzimu.


HESABU 14:26-28…. [Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 27 Je! Nichukuane na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hata lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo. 28 Waambieni, Kama niishivyo, asema Bwana, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;]… yamkini kweli watu waliwahi  kusema “wewe huwezi kufanikiwa, wewe hutaolewa, wewe utakuwa maskini” n.k. Kumbuka imeandikwa “Maskini na aseme ni tajiri, aliye dhaifu na aseme nina afya"


MAOMBI: Leo ninaagiza, kwa damu ya Yesu, kinywa changu ni kiwanda cha kuitengeneza kesho yangu. Leo ninakifungua kiwanda changu kilichofungwa, leo ninamfukuza anayetumia kinywa niharibikiwe, au ili mimi nisifanikiwe,  ninamfukuza huyo mpangaji kwa Jina la Yesu.


Leo hii Bwana anataka awapige walioazima kinywa chako na  ambao wamepindisha maisha yako.



==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==

==(Cellphone:  (+255) 713 45 95 45)==
Share:
Powered by Blogger.

Pages