JUMAPILI:
29 JUNE 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo la leo linaitwa “Mlinzi wa Mlango”. Mlango ni
sehemu halali ya kuingilia katika
jengo/nyumba/hekalu au sehemu yoyote. Kanuni ya mlango ni kufunga na kufungua. Mtu
anayeingia kwenye jengo/nyumba akipitia dirishani au kutani ujue huyo atakuwa
jambazi/mwizi au ni jasusi.
YOHANA 10:1 ….[ Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi.]…. Kwa desturi, milango inakuwa na walinzi kutokana na kuwepo kwa wezi. Miji mingi kipindi cha Agano la Kale ilijengwa na kuzungushiwa kuta.
YOSHUA 6:1-2 ...[Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. 2 Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake.]…. Yerusalemu vivyo hivyo ni mji uliozungushiwa ukuta na kuwa na malango 12.
Baba (SNP) Dr. Godson Issa Zacharia, akihubiri somo la 'Mlinzi wa Mlango' katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro 29 June 2014. |
YOHANA 10:1 ….[ Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi.]…. Kwa desturi, milango inakuwa na walinzi kutokana na kuwepo kwa wezi. Miji mingi kipindi cha Agano la Kale ilijengwa na kuzungushiwa kuta.
YOSHUA 6:1-2 ...[Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. 2 Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake.]…. Yerusalemu vivyo hivyo ni mji uliozungushiwa ukuta na kuwa na malango 12.
Milango ya kuingilia kwenye makazi ya mji ilikuwa na
WALINZI. Hawa walinzi walikuwa na jukumu
la kudhibti wanaoingia na kutoka kwenye hii miji.
YOSHUA
2:1-3 … [Yoshua, mwana wa
Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza,
akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani
kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko. 2 Mfalme wa Yeriko
akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo
usiku, ili kuipeleleza nchi. 3 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu,
akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako,
maana wamekuja ili kuipeleleza nchi. 4 Yule mwanamke akawatwaa wale watu
wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua
walikotoka; 5 ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa giza, watu
wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi, maana mtawapata. 6
Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua ya kitani,
aliyokuwa ameyatandika juu ya dari.7 Basi hao watu wakawafuata kwa njia iendayo
Yordani mpaka vivukoni; na mara wale watu waliowafuatia walipokwisha kutoka,
wakalifunga lango. 8 Tena kabla hawajalala akawaendea juu darini,].
Samsoni naye aliwahi kuingia katika mji wa Gaza na walinzi wa mji wakataka
kumzuia.
WAAMUZI
16:1-3….[Samsoni akaenda
Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa,
ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha,
penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka
mapambazuko, ndipo tutamwua. 3 Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane,
akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake
miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata
kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.]…. Kuingia kwenye
malango, kutategemea ni mlinzi yupi umemkuta mlangoni. Wachawi na waganga wa
kienyeji huweka walinzi vile vile kwenye vyanzo
MWANZO
19:1-2..[
1 Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa
amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama
kifudifudi. 2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa
mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema
mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.]… Hapa ni bahati tu kwamba Lutu alikuwepo mlangoni. Kama angekuwepo mlinzi mwingine, malaika hawa wangezuiliwa kuingia. Kumbe basi,
wewe kupata nafasi ya kuingia mahali Fulani inateegemea aina ya walinzi walioko
mlangoni.
MAOMBI: Mji wa Morogoro na walinzi wako
wa kiroho tunawavamia kwa Jina la Yesu.
WALINZI
WA MLANGO NI AKINA NANI?
Hawa ni
mashetani ambao wanakuwa ndani ya mtu. Je, uliwahi kujiuliza swali, kwanini
katika nyingi ya vituo vya kuwekea mafuta utawakuta watu unaohisi machizi
(vichaa) wanasimama kuanzia asubuhi hadi jioni? Hao usidhani ni machizi/vichaa,
ni walinzi (watch towers). Kila ofiis,
shule, kijiji, kata, wilaya, mkoa, nchi,
familia au ukoo wapo walinzi wa kiroho. Ndiyo maana, ni rahisi sana kuona watu wakizuia waliookoka
kufanya maombi kwa mgonjwa kwa kisingizio kuwa ‘huyu siyo wa dini yetu’. Badala yake ni rahisi kwa mgonjwa huyo
kupelekwa kwa mganga wa kienyeji, na kupatiwa Baraka zote na hata kuchangiwa
fedha za kufanya safari hiyo.
MASHETANI HAWA WALINZI WAKO
WA AINA MBILI:-
1. Wapo wale wanaokaa ndani ya mtu
ili kumlinda mtu aendelee kukaa katika
taabu uliyo nayo. Mfano, endepo mtu ni
mgonjwa wa ugonjwa Fulani, mashetani
haya hukaa ndani yake na kuhakikisha kuwa ugonjwa huu hauondoki. Nyakati
nyingine,mgonjwa anakuwa na hali mbaya
sana, lakini unapotaka kumuombea anakataa
kabisa. Hata ukifanikiwa kumshawishi aje kanisani atakuwa na visingizio lukuki,
ili asifike. Hii ni dalili ya walinzi kuwepo ndani ya mtu huyo na kumzuia
asipate uponyaji.
ZABURI 24:7-10….[Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango
ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.8 Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana
mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita.9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.10 Ni
nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu].
MAOMBI: Kwa jina la Yesu, ninawatangazia enyi walinzi mliokaa mfano wa malango ya
milele, muinue vichwa vyenu kwa sababu Bwana mwenye nguvu amekuja, kwa Jina la
Yesu.
2. Walinzi wanaokufungia usiingie
katika mlango wako wa Baraka. Wanajenga ngome kukuzuia. Kila mahali penye Baraka,
upo mlango wa kuingia katika Baraka hiyo. Wakati mwingine mtu
akiwa tayari kwenye uchumba, hutokea mahusiano kuvunjika ili kufanya
hiyo ndoa isitokee. Hawa ndio wanaozuia watoto wako wasisome. Hawa ndio walinzi
wanaozuia hata mishahara ya watu kupanda. Hali uliyo nay oleo siyo mpango wa
Mungu, kwa sababu Bwana anataka usonge mbele kwa ushindi kwa Jina la Yesu.
MAOMBI: Kwa jina la Yesu enyi walinzi mnaonilinda nisiingie kwenye Baraka zangu,
nawafyeka kwa Jina la Yesu. Ninakataa kulindwa na majini, na mapepo na
mashetani, nakataa kwa Jina la Yesu.
MATHAYO 8:28-30…. [Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu
wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu
asiweze kuipitia njia ile. 29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini
nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? 30 Basi,
kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. 31 Wale pepo wakamsihi,
wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe. 32
Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote
wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini. 33 Lakini wachungaji
walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye
pepo pia. 34 Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona,
walimsihi aondoke mipakani mwao.]…
LUKA 8:26-33…[Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. 27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu
mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani,
ila makaburini. 28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake,
akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi
usinitese. 29 Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana
amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na
pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. 30
Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo
wengi wamemwingia. 31 Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. 32 Basi, hapo
palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa
kuwaingia wale. Akawapa ruhusa. 33 Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe,
nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji.]…
MARKO 5:1-9 …[Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.2 Na
alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini,
mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye
yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4 kwa sababu alikuwa
amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na
kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5
Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele
na kujikatakata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio,
akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu,
Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu
amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani?
Akamjibu, Jina langu ni Legioni, a kwa kuwa tu wengi.]..
Kwa sababu ya Yesu, walinzi wa mji
huu walitii amri wakaondoka ndani ya huyu mtu na kuingia ndani ya nguruwe. Unapwaona
walinzi wa maisha yako, usihangaike kugombana nao. Hii ni kwa sababu
kushindana kwetu siyo juu ya damu na nyama.
MAOMBI: Leo ninatoroka katikati ya walinzi wanaonilinda kwenye ngome zao, kwa
Jina la Yesu.
NAMNA TATU ZA KUWANG’OA WALINZI:
1. Kuwapiga walinzi wawe kama wafu. Pindi
akijaamka baadae acute wewe ulishaondoka zamani. MATHAYO 27:62-66 … [Hata siku ya
pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo
wakamkusanyikia Pilato, 63 wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja
alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka. 64 Basi amuru
kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake
wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho
utapita ule wa kwanza. 65 Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde
salama kadiri mjuavyo. 66 Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile
jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.]…. Shida unayoiona
maishani mwako, wapo walinzi waliokwisha weka muhuri na kuhakikisha hauondokoi
kwenye hiyo shida milele. Aliyenilinda, leo azimike na afe kabisa kwa Jina la
Yesu.
2. Kuwapiga walinzi na kung’oa malango yao kabisa. Aina hii huitwa Samson
Style. Njia hii ya Samson aliitumia kwa kung’oa malango na kuruhusu uwazi
ili hata wale wengine waliokuwa wamezuia wapite. Hii itasababisha hata ndugu
zako, wanaukoo n.k. kuweza kupita salama.
Hata hivyo upo uwezekano wa malango mengine kujengwa baada ya hili lango
kung’olewa. Na ndiyo maana ili kuzuia hali hii
isitokee,aina ya tatu ya kuwaondoa walinzi wanaozuia Baraka za maisha
yetu.
3. Kubomoa ngome yote na malango
yake. Hii huitwa Joshua style. Aina hii
ni ya kuzunguka ukuta na kuubomoa wote ili kwamba asipatikane mtu wa kuujenga
ukuta huo tena milele na milele kwa Jina la Yesu.
==Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713
45 95 45)==