JUMAPILI
(PASAKA): 20 APRIL 2014 - UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
Na:
Pastor Godson Issa Zacharia (Snp)
SNP Dr. Godson Issa Zacharia akihubiri leo 20 April 2014 siku ya Pasaka (Ufufuo na Uzima Morogoro). |
SOMO: NGUVU YA KABURI LA KRISTO LILILO WAZI
Utangulizi: Nguvu ya Kaburi la Kristo lililo wazi ni nguvu pekee tunayoipata kutoka kwa Yesu kupitia mauti yake. Hakuna yeyote aitwaye
Mungu hapa duniani (iwe ni mungu wa Wajapani, Marekani, Ulaya n.k) aliyewahi kufa na kufufuka zaidi ya Yesu
Kristo. Ndiyo maana wakristo hatuendi kuhiji mahali popote duniani kwa sababu
Yesu Kristo hayumo kaburini. Ukiona Mkristo anaenda kuhiji, ujue huyo siyo Mkrsito bali ni “Mkristu”.
Mkristo hujigamba kwa sababu Yesu hayumo
kaburini. Hivyo ipo nguvu iliyopo
katika kaburi wazi la Yesu.
Kazi ya Kaburi ni kushikilia na haliruhusu kuachiliwa. Shetani anapomfunga mtu anatuma walinzi kabisa kumdhibiti huyo mtu ili asifunguliwe au kuachiliwa. Ndiyo maana kaburi la Yesu Kristo liliwekwa walinzi ili kumzuia Yesu asifufuke. Hata hivyo, hawa
walinzi wanapozinduka usingizini, ndiposa hulipana pesa ili kueneza uongo kwamba Yesu hakufufuka‼! Ndani ya ufufuo wa
Yesu, mawakala wa shetani (yaani waganga, wachawi, wasoma nyota n.k) huzimia kwanza.
Emmanuel Nkwabi (a.k.a Firigisi) akimwimbia Bwana Yesu siku ya Pasaka 20 April 2014 katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro |
LUKA 9:7-8….. [Na Herode mfalme akasikia habari za yote
yaliyotendeka, akafadhaika kwa sababu watu wengine walisema ya kwamba Yohana
amefufuka katika wafu, 8 na wengine ya kwamba Eliya ametokea, na wengine ya
kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka. 9 Lakini Herode
akasema, Yohana nilimkata kichwa; basi ni nani huyu ambaye ninasikia mambo haya
juu yake? Akataka kumwona.]…
Kumbe ndiyo maana ISAYA 42:22 Biblia inaasema hapana asemaye RUDISHA …. [Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]…
Kumbe ndiyo maana ISAYA 42:22 Biblia inaasema hapana asemaye RUDISHA …. [Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]…
Herode na wachukuaji wenzake
wanaingiwa na hofu sana wanaposikia wale waliowachukua misukule/ Waliowakata vichwa n.k. wanarudi.
MAOMBI:
Mtu yeyeote aliyekata kichwa maendeleo yangu/maisha yangu, leo kwa damu ya
Yesu Nakufyeka. Kwa nguvu ya msalaba, yeyote aliyemeza biashara/kazi/mume/masomo
nasema ACHILIA‼ Yeyote aliyemeza maisha yangu NATOROKA‼ kwa damu ya Yesu kila
shetani na malaika wa kuzimu, nawaagiza leo kwa jina la Yesu ACHILIA, nasababisha tetemeko
la nguvu ya msalaba, Herode na wenzake walionitega mimi wafyekwe.
Pasaka ni siku ya kutoroka. Kuna mahali
upo sasa ambapo siyo sehemu sahihi. Hata gari moja ulililo nalo, usiridhike siyo
sahihi kuwa na moja tu. Kuna mahali ambapo waganga na wachawi katika maisha
yako wamekuweka. Na yamkini watu wanakuambia uvumilie‼ Huu siyo wakati wa
kuvumilia, ni wakati wa kuhama. Wana wa
Israeli walikaa utumwani Misri kwa miaka 400, na ilipofika siku kama ya leo walihamishwa kutoka utumwani.
Yalikuwepo masharti ya Mwanakondoo wa Pasaka. Mwanakondoo huyu hakuwa na doa, nayo ni ishara ya Bwana Yesu Kristo ambaye hakuwa na dhambi yoyote.
KUTOKA
12:11 … [Tena
mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na
fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana.]…
KUTOKA
12:43-45 …. [Bwana akawaambia Musa na Haruni, Amri ya pasaka ni hii; mtu mgeni asimle; 44 lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri, ndipo hapo atamla pasaka. 45 Akaaye kwenu hali ya ugeni, na mtumishi aliyeajiriwa, wasimle pasaka.]… Mgeni
anayeongelewa hapa ni mtu ambaye
hajampa Yesu maisha yake.
Baadhi ya Majeshi ya Bwana Ufufuo na Uzima Morogoro siku ya Pasaka 20 April 2014 |
Siku ya Pasaka ni ya Kushangilia Ushindi, kama ambavyo Majeshi ya Bwana Morogoro yanavyofanya hapa. |
==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==