JUMAPILI: 01 NOVEMBER 2015 –
UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
Na: STEVEN
NAMPUNJU (RP)
&
DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Dunia na vyote vilivyomo ndani yake vinaunda kitu kiitwacho ‘Ulimwengu’. Mkuu
wa ulimwengu huu ni yule mwenye madaraka juu ya ulimwengu huu: upate nini;
uishi vipi; ule nini‼!; n.k. Huyo ndiye
mwenye mamlaka ya kuamua usome wapi, ule nini, uishi vipi‼. Kumbuka Mungu
anaheshimu mamlaka. Zipo mamlaka zimewekwa lakini zinasimamia matatizo ya watu.
Kwenye YOHANA 12:31 imeandikwa…[Sasa hukumu ya ulimwengu huu
ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.]…Na pia imeandikwa
katika 2KORITNHO 4:4… [ambao ndani yao mungu wa dunia
hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake
Kristo aliye sura yake Mungu.]….Yupo ‘mungu’ wa dunia hii, anayeweza
kupofusha fikra za watu. Huyu tena anayo mamlaka.
Kwenye LUKA
4:1-12 Yesu alikuwa anajaribiwa. Imeandikwa [Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka
Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, 2 akijaribiwa na
Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. 3
Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. 4
Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. 5 Akampandisha
juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi
akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi
mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu
yote yatakuwa yako. 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu
wako, umwabudu yeye peke yake. 9 Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya
kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; 10 kwa
maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba, Mikononi
mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12 Yesu akajibu
akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.]…. Huyu mwenye
mamlaka anamwambia Yesu mambo haya. Huyu anayetoa kwa wale anaopenda leo ni
siku ya kumkamata na kufutilia mbali kwa
Jina la Yesu. Kutokana na uhitaji wa mtu, mkuu wa ulimwengu huu anayo majina mengi. Mungu wetu anaitwa “Nipo ambaye nipo”.
Kwamba ukiwa na kiu, yeye Mungu ni kisima cha maji ya uzima, ukiwa na njaa yeye
ni chakula cha uzima
Majina ya mkuu wa ulimwengu huu nayo ni mengi pia;
Mifano ya majina yake nikama vile:-
1. NYOKA WA ZAMANI:
kama ilivyoandikwa katika UFUNUO 12:7..[Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake
wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;]…
Yesu pia anafananishwa na nyoka wa shaba aliyeinuliwa jangwani kipindi kile cha Musa.
2. BABA WA UWONGO: Imeandikwa katika YOHANA 8:41-43...[Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi
hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu. 42 Yesu
akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka
kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye
aliyenituma. 43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi
kulisikia neno langu. 44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu
ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa
hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa
sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. 45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli,
hamnisadiki.]…. Endapo yupo mtu asiyetaka kumsikiliza Yesu
Krsito, maana yake siyo wa uzao wa Ibrahimu.
3. MWIZI:
Imeandikwakatika YOHANA 10:10…[Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na
uzima, kisha wawe nao tele.]… Mkuu wa ulimwengu hapa anaitwa mwizi kutokana na
kazi ya wizi anayoifanya.
4. MUUAJI TOKA MWANZO: Imeasndikwa 1YOHANA 3:8-12…[atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda
dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili
azivunje kazi za Ibilisi.9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa
sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu
amezaliwa kutokana na Mungu. 10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na
watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye
asiyempenda ndugu yake. 11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo,
kwamba tupendane sisi kwa sisi; 12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu,
akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake
yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.]… Muasisi wa
mauaji ni shetani ambaye ndiye mkuu wa ulimwengu huu.
5. MSHTAKI WA NDUGU:
Imeandikwa katika UFUNUO 12:10…[Nikasikia sauti kuu mbinguni,
ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya
Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye
mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.]… Mkuu wa ulimwengu huu
unamtambua kutokana na kazi zake. Ili uweze kuzishiinda hila za ibilisi
nikuzijua hila zake. Imeandikwa katika MAOMBOLEZO 3:31-33…[Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana
ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo
wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.]…. Siyo kusudi
la Bwana kumhuzunisha mtu yeyote. Uonapo huzuni au mateso yameandama maisha yako, usimhusihse Mungu
bali ujue huo ni mpango wa Mkuu wa
Ulimwengu huu (shetani).
UMUHIMU
WA KUMTUPA NJE MKUU WA ULIMWENGU
·
AMESHIKA
VIPAWA NA KUZUIA HATIMA YA MTU: Mfano wa kwanza: MARKO 5:1-10…[Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. 2 Na
alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini,
mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye
yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4 kwa sababu alikuwa
amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunjavunja
zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na sikuzote,
usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na
kujikatakata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio,
akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu,
Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu
amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani?
Akamjibu, Jina langu ni Legioni, a kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi sana
asiwapeleke nje ya nchi ile.]….
Mkuu wa ulimwengu huu hupaenda kuzuia watu wasivae nguo. Uonapo watu
wanavaa nguo fupi sana, na pengine za nusu uchi, ujue mkuu wa ulimwengu huu
yupo kazini. Kumbe uonapo mtu hakai
nyumbani, ni kazi za mkuu wa ulimwengu huu. Huyu kijana alipaswa awe mhubiri wa injili lakini mkuu wa ulimwengu huu
akamzuia ili asiione nuru ya injili maishani
mwake. Aliyepaswa afanikiwe anarudi
nyuma.
UKIRI
Ewe mkuu wa ulimwengu uliyenizuia nisifanikiwe,
leo kwa Jina la Yesu nakukataa, ninakutupa
nje, ewe mkuu wa ulimwengu huu, achia maisha yangu katika Jina la Yesu. Amen
|
·
ANAWEZA
KUKUZUIA: 1 YOHANA
3:8… [atendaye dhambi ni
wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana
wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.]… Yesu
alikuja duniani ili kuvunja kazi za ibilisi. Wapo watu ambao wanayo mamlaka juu
ya maisha yako. Mwenye mamlaka huyu
anaweza kuzuia uinuke kwa kiwango
gani, au uwe mtu wa aina gani‼
·
ANAWEZA
KUTUMIA CHOCHOTE: Mkuu wa ulimwengu huu anaweza kutumia
wanyama au vitu (mfano: paka, panya, nazi n.k.). Yesu pia aliwahi kutumia
mamlaka yake kuwatuma Petro Baharini wakavue samaki, na ndani ya samaki yule wa
kwanza akawaambia wataokota humo fedha itakayotosha kulipia kodi kwa Petro na
Yesu.
UKIRI
Ninashinda
kazi zako, na utawala wako kwa Damu ya Yesu, niachie katika Jina la Yesu.
Amen
|
Yamkini wewe
unanga’ng’ania kuolewa au kupata kazi kumbe wakati hup huo hujamtoa nje mkuu wa
ulimwengu huu anayekuzuia usivipate hivi vyote.
Imeandikwa katika YOHANA 14:30..[Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa
ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.]… Ewe Mkuu wa Ulimwengu
huu, huna kitu kwangu. Leo
ninakunyang’anya vyote vinavyonihusu katika Jina la Yesu.
Leo tuiambie bahari iliyokamata fedha zetu/ afya
zetu/ndoa zetu/biashara zetu, iachie kwa Jina la Yesu. Leo tuilazimishe bahari
iliyomeza samaki ambao ndani yao kuna fedha na vitu vyetu, iachie kwa Jina la Yesu.
Ili upate itategemea ukaribu wako na mwenye mamlaka.
Ili ufanikiwe sana, inabidi uunde
ukaribu sana na mwenye mamlaka. Maana yake, ukaribu wako na mwenye mamlaka utakufanya upate unachokitaka. Maana yake, ukiwa
karibu sana na Mungu au ukijenga ukaribu wako na shetani ndivyo utakavyopata
unavyotaka kutoka kwa mwenye mamlaka
husika. Wakati mwingine mchawi mmoja anaweza kumuumbua mchawi mwingine,na
hii ni kutokana na ukaribu alio nao na yule mwenye mamlaka (kwa jinsi anavyotoa
kafara kubwa n.k).
Mkuu wa ulimwengu huu lazima atupwe nje. Shetani hahitaji
majadiliano kama ya wanasiasa, hapana! Shetani anapigwa tu‼ Mkuu wa
Ulimwengu huu ana uwezo wakubadilisha tabia. Pengine ulikuwa na mume, leo hii
humpendi tena.
UKIRI
Katika Jina la Yesu, Imeandikwa “nimepewa mamlaka ya
kukanyaga nyoka na nge na kazi zote za
yule muovu wala hazitanidhuru”, wewe mkuu wa ulimwengu ninakutupa nje kwa Jina la Yesu. Amen.
|
Haipaswi mtu kuwa vuguvugu. Siri kubwa ni kumgeukia
Yesu Kristo, kwa kuwa mkuu wa ulimwengu huu
hana kitu kwetu. Leo wewe ambaye hujaokoka ni wakati mzuri ukafanya
maamuzi ya kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako kwa
kuokoka.
=== © Information & Media Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa
Zacharia
(Glory of Christ
(Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545