Tuesday, September 13, 2016

KUBOMOA VIWANDA VYA UHARIBIFU


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH

UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO

JUMAPILI:  11/09/ 2016


Na: PASTOR DR GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)





Viwanda ni majengo ambayo ndani yake kuna mashine na mitambo ya kutengeneza bidhaa mbali mbali.

Kuna viwanda ambavyo vinapika uharibifu

Hivi sio viwanda vya kawaida,ni viwanda ambavyo vinapika uharibifu kwenye maisha ya mtu ,kazi ya mtu ,biashara ya mtu katika ulimwengu wa roho

kila unachokiona leo kiwe kizuri au kibaya iwe ni kazi uliyoianza,iwe ni biashara na mengine  yote unayoyaona  kwenye maisha yako yawe mazuri au mabaya yameanzia kwenye ulimwengu wa  roho ,Kila unachokiona mwilini  kimeanzia rohoni ,iwe mafanikio,Baraka n.k yameundwa kwenye ulimwengu wa  roho ,tunataka leo tukifuatilie hicho kiwanda na tukibomoe kwa jina la Yesu.

Kuna ulimwengu  wa aina mbili

1. Ulimwengu wa  roho

2. Ulimwengu wa mwili
Umati wa Watendakazi Ufufuo na Uzima Morogoro

Ulimwengu wa roho maana yake ni ulimwengu usioonekana kwa macho ya mwilini. Ulimwengu wa roho pia umegawanyika mara mbili yaani ulimwengu wa  roho wa kishetani ,na ulimwengu wa  roho wa kimungu

Lolote linalokupata leo hata kama uliota katika ndoto yote hayo yamekupata yameanzia rohoni.Kuna viwanda ambavyo vinazalisha magonjwa,mateso,shida, leo tunakifuatilia  pale kilipo tunakiharibu.Kuna mfalme mmoja kwenye Biblia aliandaa sanamu na kuwataka watu wote wa mji ule  waisujudie ile sanamu,lakini wakatokea vijana watatu  Meshack ,Shadrack na Abednego  wakaweka msimamo kwa Mungu wao wakakataa kuisujudia ile sanamu ndipo walipoitwa kwa mfalme lakini walikataa kuiabudu ile  sanamu .

Imeandikwa katika Danieli 3:29-30

Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila ya watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.

 Kisha mfalme akawakuza Shadraka, na Meshaki, na Abednego, katika wilaya ya Babeli.

Jaa maana yake ni vitu vilivyokusanywa pamoja,ili tubomoe hivyo viwanda tunahitaji tuwe na silaha,na ukitaka ushinde ni kuhakikisha vile viwanda tunavifunga,kwenye maisha ili viwanda vibomolewe kuna mchakato kwanza wanafunga wanaweka alama ya  x  kuonyesha kwamba hakitakiwi eneo hilo .Leo tunageuka kuwa greda la kiroho tutavivunja viwanda vyote kwa jina la Yesu.

Imeandikwa katika Yeremia 1:10

angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu,

  na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Imeandikwa katika Waefeso 1:20

aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

Yapo mashetani,majini,majoka yanayotenda kazi katika viwanda hivyo katika ulimwengu wa roho na yanahakikisha maisha yako yanaharibika.

Imeandikwa katika Waefeso 2:6

Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

Imeandikwa katika Waefeso 3:10

ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;

Kwenye ulimwengu wa roho kuna viwanda vinatengenezwa na baadae vinadhihirika katika mwili.

Imeandikwa katika Waefeso 6:12

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


Kwenye ulimwengu wa roho kuna wafalme wanaotengeneza viwanda ,kuna mamlaka zinazotengeneza uharibifu ,wanatengeneza virus,bacteri kwa ajili ya kuleta magonjwa kwa watu,ni mashetani wanatengeneza vitu baadae wanaviachilia kwa watu ili viwapate.Kila unachokiona leo duniani  kimetengenezwa rohoni,kukataliwa ,mateso ,matatizo yote unayoyaona  yanawapata wanadamu yote  yametengenezwa rohoni .Ugonjwa wa Ukimwi unaouona unamaliza watu leo umetengenezwa rohoni,kuna dr mmoja anaitwa Robert Charles Gallo ni mzungu alishatamka mwenyewe na kusema yeye mwenyewe aliutengeneza ukimwi mnamo mwaka 1984.  Mwaka 1962 ndipo alipoanza kutengeneza tafiti hizi , akaandika kabisa hatimiliki ya ukimwi . leo lazima tusimame kama shujaa wa Bwana tutavivunja viwanda vyote vilivyotengeneza taabu na mateso katika maisha yetu.panakuwepo na kikundi cha watu kuna technician huko ndani,kuna messenger  wanakaa na wanaplani wanaanza kutengeneza kiwanda.

Imeandikwa katika Yohana 10:10

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Kazi ya Mungu sio kuharibu ni kubariki,bali shetani kazi yake ni kuua, kuchinja, na kuharibu

Imeandikwa katika Ayubu 1:19

Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.

 Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu.

 Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.

 Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao.

Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.

 Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.

 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.  Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure?

 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.

 Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.

 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.

 Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,

 mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao;

 mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.

 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.

 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.

Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa;

 mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.

Mungu anaweza kukuwekea kingo,hapa tunaona jinsi shetani alivyojihudhurisha kwenye kikao mbinguni na kuomba ruhusa  kuyaharibu mafanikio  ya Ayubu, Mungu alikua akijadili na shetani bila Ayubu kujua,baada ya shetani kuruhusiwa akageuka akawa kiwanda katika ulimwengu wa roho,akaanza kutengeneza matukio  katika ulimwengu wa mwili. Ayubu  alikua mtumishi wa Bwana mwenye kila kitu watoto ,mali n.k . lakini ni  kikao kilikaliwa na  kiwanda kikatengeneza uharibifu,shetani akiruhusiwa matatizo yanakuja mtiririko,matukio yanaanza kutokea lakini yanakua yametokea kiwandani,wewe unawaza ni matukio ya kawaida tu lakini yametokea kiwandani.

Ukianza kusoma kitabu cha Ayubu ule mstari wa kumi na tatu utaanza kuona matukio yanaanza kutokea kwa Ayubu jozi za ng,ombe,punda,kondoo na watoto wake wote waliteketea kabisa hakikupona hata kimoja .Kuna watu wanaweza kuja kwako leo kukuletea taarifa wengine sio watu wametokea viwandani,wametumwa kukuletea taarifa za matukio ya uharibifu,ni kweli wamekuletea taarifa mbaya zikakuvunja moyo lakini leo Bwana anakuja na taarifa njema ya mbinguni ,taarifa ya ushindi ya kukomboa maisha yako. Kuna viwanda  vinavyotengeneza  matatizo ya familia  utashangaa kizazi chenu wote mnakua na matatizo ya kufanana . Wewe utaona ni matukio ya kawaida kumbe kuna kiwanda cha rohoni kinachotengeneza matatizo hayo,tunamuona Ayubu ambaye shetani amegusa maisha yake na baadaye akamletea taarifa mbaya lakini hakumkufuru Bwana

Hatua za kukiteketeza viwanda katika ulimwengu wa  roho

1.Kwanza unavifunga

2.Unampiga mbunifu,mchoraji na mjenga kiwanda

3.Unakivunja

Yeremia 51:22-23

na kwa wewe nitawavunjavunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunjavunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunjavunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;

 na kwa wewe nitamvunjavunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunjavunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunjavunja maliwali na maakida.

Bwana amekufanya wewe kuwa rungu ,ingia katika ulimwengu wa  roho bomoa  viwanda vyote ambavyo vimeshikilia maisha yako,familia yako,ukoo wako,kazi yako ,huduma yako,bomoa na kuwateketeza wamiliki wa viwanda ili wasiweze kujenga viwanda hivyo tena




UKIRI:

Katika jina la Yesu kristo ninakifuatilia kiwanda kilicholeta mateso,magonjwa kwenye maisha yangu,napiga viwanda vyote ,viwanda vya wachawi naitikisa misingi naikabili misingi ambayo majini wameitumia ili kuzalisha magonjwa kwenye maisha yangu,naifunga kuzimu yote ambayo imezalisha taabu kwenye maisha yangu.Ninawaachisha kazi watenda kazi wote mnaofanya kazi kwenye viwanda ,ninawafyeka wote achia maisha yangu,nateketeza viwanda vyote vilivyozalisha uharibifu katika maisha,naharibu kiwanda chenu hamtatenda kazi,nakifuata kiwanda cha mateso ,kiwanda cha utasa,kiwanda cha magonjwa leo naviteketeza kwa jina la Yesu. Amen







©MEDIA &  INFORMATION MINISTRY


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH,


KANISA LA UFUFUO NA UZIMA

MKUNDI – MOROGORO (TANZANIA)

TEL: +255765979866

           +255713459545
Share:
Powered by Blogger.

Pages