UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI: 18 OCTOBER 2015 –
Na: STEVEN
NAMPUNJU (RP)
&
DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Kabla ya kufahamu undani wa kafara ya utawala, je kafara ni kitu gani? Kafara
ni kitu kinachotolewa kwa Mungu au kwa mizimu kama sadaka, kwa ajili ya
kuepukana na balaa fulani. Baadhi ya watu wasiomjua Mungu, mara nyingi huenda kwa wazee wao vijijini ili kutoa kafara ili kupata jambo fulani. Kafara huambatana na KUMWAGA DAMU. Kafara haihusiani na
kutoa sadaka ya ndizi, matunda au chochote kile
kisichokuwa na damu. Makundi
makubwa ya Damu zinapomwagwa: (1) Damu hunena mema au (2) Damu hunena
mabaya.
Vipo
vitu kama vitatu hivi vya kujifunza kuhusiana na damu:
1. Damu inao uwezo wa kutoa sauti:
Damu iliyomwagika mahali popoteinaweza kupaza sauti na wengine wakaitafsiri
sauti hiyo.
2. Damu inaweza kuomboleza:
Kupitia damu yamtu au mnyama, damu
yaweza kutoa sauti ya kuomboleza kwa uchungu wa kumwagika kwake.
3. Mungu ana uwezo wakuisikia sauti inayopazwa na Damu na kuweza kutoa tafsiri
yake: Mfano: MWANZO
4:9-10….[Bwana akamwambia
Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu
yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka
katika ardhi.]… Kaini alijua yale mauaji aliyofmfanyia ndugu
yake ni siri. Mungu lakini aliweza kuisikia sauti ya damu ya Habili na kutoa
tafsiri yake. Tafsiri hii inaweza kuleta
madhara kwa mtu fulani anayeishi.
Imeandikwa katika 2KORINTHO 4:4….[ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini,
isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.]…
Wapo watu wanaweza kumwaga damu kwa malengo yao hapa duniani. Ni kwa sababu mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao. Kumbe
mungu wa dunia hii anaweza kupofusha
fikra za wasiaoamini, na hivyo kuficha ile
nuru ya injili ili isiwazukie.
Imeandikwa katika WALAWI 17:14…[Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai
wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo
yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye
yote atakatiliwa mbali.]… Kumbe basi ndani ya damu ndipo uhai ulipo. Kafara inapotolewa ni sawa na kuutoa uhai wa
kile kilichotolewa.
MADHARA
YA UMWAGAJI DAMU YA MWANADAMU
·
Amwagae
damu ya mwanadamu, damu yake nayo
itamwagwa: Imeandikwa katika MWANZO 9:6…[Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu,
maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.].
·
Hatima
ya mtu inaweza kubadilishwa kwa kmwaga
damu ya mwanadamu:
Maana yake, damu ya mtu mmoja ikimwagwa,
hata hatima ya mtu huyo au taifa lake
inaweza kubatilishwa.
Imeandikwa katika MWANZO4:1-12….[Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa
Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. 2 Akaongeza akamzaa ndugu
yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. 3
Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye
akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana
akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka
yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6 Bwana akamwambia
Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama
ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea
mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. 8 Kaini akamwambia
Habili nduguye, [Twende uwandani]*. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini
akamwinukia Habili nduguye, akamwua 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili
ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya
nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa,
umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu
yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro
na mtu asiye na kikao duniani.]… Jina la Kaini lilikuwa na
tafsiri ya “mtoto atokaye kwa Bwana”.
Hatima ya Kaini ilibadilishwa kwa sababu hii ya kumuua ndugu yake, badala ya
kuwa mtu wa kutulia ikambidi awe mtoro na
mtu asiye na makazi. Unapomuona mtu leo
hii, ni mtoro katika maisha yake, ujue
kuna sadaka ya damu ilimwagwa kwa ajili
yake wakati fulani akiwa anajua au bila yeye kujua. Utoro waweza kuwa kwenye biashara, kwamba kila akifanya
biashara yake mji huu anaacha na kuanza
kitu kingine kipya, na au kuhamia mji mwingine kuanzisha kitu
kingine kipya bila mafanikio yapatiakanayo kwa kukaa mahali pamoja na kutulia.
MIFANO
YA WATAWALA WALIOAWAHI KUTOA KAFARA
1.
HIELI
MBETHELI
Hieli Mbetheli aliwatoa kafara wanae wawili
kwa nyakati tofauti ili mambo ya ufalme/utawala wake yaende vizuri. Imeandikwa
katika YOSHUA 6:26…[Naye Yoshua akawaapisha kiapo
wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na
kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa
kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake
mwanamume aliye mdogo.]…
1WAFALME
16:34….[Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake
kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa
kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa
Yoshua mwana wa Nuni.]…Inawezekana mfalme aliambiwa kuhusu
katazo la Yoshua, lakini kwa kutaka nguvu ya uongozi wake, akaona aendele tu
kutoa kafara za wanae wawili ili kudumisha
utawala wake.
Imeandikwa katika 2WAFALME 3:4-10…[Basi Mesha, mfalme wa Moabu, alikuwa mfuga kondoo; naye alikuwa akimlipa
mfalme wa Israeli sufu ya wanakondoo elfu mia, na ya kondoo waume elfu mia. 5
Lakini ikawa, Ahabu alipokufa, mfalme wa Moabu akamwasi mfalme wa Israeli. 6
Akatoka wakati ule ule mfalme Yoramu katika Samaria, akawahesabu Israeli wote.
7 Akaenda akatuma kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akasema, Mfalme wa Moabu
ameniasi; je! Utakwenda pamoja nami tupigane na Moabu? Akasema, Nitakwenda;
mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi zangu ni kama farasi
zako. 8 Akauliza, Njia ipi tuiendee? Akajibu, Njia ya jangwa la Edomu. 9 Basi
mfalme wa Israeli akaenda, na mfalme wa Yuda, na mfalme wa Edomu; wakazunguka
mwendo wa siku saba; wala hapakuwa na maji kwa jeshi, wala kwa wanyama
waliowafuata. 10 Mfalme wa Israeli akasema, Ole wetu! Kwani Bwana amewakutanisha
hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.]…Kule jangwani
wanajeshi walikuwa hawana maji ya kunywa.
Imeandikwa katika 2WAFALME 3:4-11-17…[Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hapana hapa nabii wa Bwana, ili
tumwulize Bwana kwa yeye? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema,
Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake
Eliya. 12 Yehoshafati akasema, Neno la Bwana analo huyu. Basi mfalme wa
Israeli, na Yehoshafati, na mfalme wa Edomu, wakamshukia. 13 Elisha akamwambia
mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii
wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa Bwana
amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu. 14 Elisha akasema,
Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama
singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana
nawe. 15 Ila sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga,
mkono wa Bwana ukamjia juu yake. 16 Akasema, Bwana asema hivi, Fanyeni bonde
hili lijae mahandaki. 17 Kwa kuwa Bwana asema hivi, Hamutauona upepo, wala
hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji;
nanyi mtakunywa, ninyi, na ng'ombe zenu, na wanyama wenu. 18 Na jambo
hili ni jepesi machoni pa Bwana; pia atawatia Wamoabi mikononi mwenu. 19 Nanyi
mtapiga kila mji wenye boma, na kila mji ulio mzuri, na kila mti mwema
mtaukata, na chemchemi zote za maji
mtaziziba, na kila mahali palipo pema mtapaharibu kwa mawe. 20 Ikawa asubuhi,
wakati wa kutoa sadaka ya unga, tazama, maji yakaja kwa njia ya Edomu, hata
nchi ikajaa maji..]… Unapokuwa na changamoto za maisha usiwaendee
waganga wa kienyeji, bali umfuate mtumishi wa Bwana. Elisha aliwajibu waandae
mahandaki ili watu wakae ndani yake na wakitoka tu mle washambulie adui zao.
Ili ushinde unapaswa uandae mahandaki (siyo moja) na ambayo ni kama vile wanamaombi,
vikundi na ministries mbalimbali kanisani. Hata hivyo, maji ya mafuriko haya
yatakuja kutoka chini kuelekea juu kinyume na kanuni za dunia hii. Walio kwenye handaki wanakuwa
na nia moja ya ushindi.
2.
MFALME
WA MOABU
Huyu mfalme waMoabu pia aliwahi kutoa kafara ya
watawala ili aendelee kudumu madarakani. Imeandikwa katika 2WAFALME 3:21-27…[Basi Wamoabi wote waliposikia ya kuwa wafalme hao wamekwea ili kupigana
nao, walijikusanya pamoja, wote wawezao kuvaa silaha, na wenye umri zaidi,
wakasimama mpakani. 22 Wakaamka asubuhi na mapema, na hilo jua likametameta juu
ya maji, na Wamoabi wakayaona yale maji yaliyowaelekea kuwa ni mekundu kama
damu. 23 Wakasema, Ndiyo damu hii; bila shaka hao wafalme wameharibika,
wamepigana kila mtu na mwenziwe; basi sasa, enyi Wamoabi, nyara hizo! 24 Hata
walipokuja matuoni kwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata
wakakimbia mbele yao; wakaendelea wakiwapigapiga Wamoabi hata kwao. 25
Wakaibomoa ile miji; wakatupa katika kila mahali palipo pema kila mtu jiwe
lake, wakapajaza; wakaziziba chemchemi zote za maji, wakaikata miti yote iliyo mizuri;
mpaka katika Kirharesethi tu wakayasaza mawe yake; ila wenye kombeo
wakauzunguka wakaupiga. 26 Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa
vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata
kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 27 Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza,
yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya
ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda
nchi yao wenyewe.]…Ilikuweppo hasira kuu juu ya Israeli baada ya
mwana wa kwanza wa mfalme wa Moabu kutolewakafara ukutani. Mashetani yalipandwa
na hasira baada ya kupokea damu hii.
MADHARA
YA KAFARA ZITOLEWAZO
1.
Mungu
kutozisikia sauti za watu wanapoomba.
Imeandikwa katika MIKA 3:1-4…[Nikasema, Tafadhali sikieni, enyi vichwa vya Yakobo,
mnaoitawala nyumba ya Israeli. Je! Haiwapasi ninyi kujua hukumu? 2 Ninyi
mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na
nyama mifupani mwao. 3 Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi
zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa
chunguni, na kama nyama sufuriani.4 Ndipo watakapomwomba Bwana, asiwaitikie;
naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa
matendo yao.]… Watawala wanapoomba, Mungu hazisikii sauti
zao. Endapo haki haitendeki, Mungu atauficha uso wake kwako. Kafara zinazotolewa kwa mungu asiye
Mungu muumba mbingu na nchi,
2. Kiongozi anayekuwakilisha wewe ana
uhusiano mkubwa na hatima
yako
na kila kitu ulicho nacho. Mkumbuke Ayubu jinsi ambavyo watoto na
familia yake, mali zake, na mifugo yake vilivyolindwa na Bwana. Maana yake
ni kuwa, hatima ya vyote itategemeana na
mahusiano yaliyopo kati ya kiongozi wako
na Mungu.
3.
Kiongozi
anayetoa kafara kwa mashetani, anawaunganisha watu na mashetani.
Imeandikwa katika 1KORINTHO 10:20-21…[Sivyo, lakini vitu vile
wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi
kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha
mashetani.21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya
mashetani.]…. Mungu
tunayemtumikia hapokei kafara za wanyama au za wanadamu. Kwenye familia
au taifa, jambo likitokea na ukamuona mmojawapo wa watu anachukua wanyama
kuchinja ujue mtu huyo anataka kuwaunganisha ninyi na madhabahu za kuzimu.
Imeandikwa katika WAEBRANIA 12:24…[na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema
kuliko ile ya Habili.]… Yesu ni mjumbe wa Agano Jipya. Damu ya
Yesu inanena mema, lakini pia zipo damu
zinazonena mabaya. Leo tutaomba kwa ajili ya taifa letu, ili kama zipo
damu zilizomwagwa kwa ajili ya kuharibu maisha ya watanzania, tuzikatae kwa
Jina la Yesu.
UKIRI
Kuanzia leo, na kuanzia sasa, ewe kuhani, ewe
mtawala uliyemwaga damu mahali popote ili unitawale, leo nakukataa kwa Jina
la Yesu. Kila nguvu ya utawala wako ulizowekeza ili kunitawala leo najitoa
kwenye utawala wako, naitoa na familia yangu na taifa langu kwenye kafara
zako kwa Damu ya Yesu. Amen.
|
Kumbuka damu zinapomwagwa hupindisha hatima za watu.
Yamkini ni damu za watu au wanyama zilizomwagwa ili kukuvuta nyuma usisonge
mbele. Leo tuikate mikono yote ya
mashetani inayokuvuta urudi nyuma kwa
Damu ya Mwanakondoo Yesu Kristo.
Kama ilivyokuwa kwa Zakaria, baba wa Yohana
Mbatizaji aliyebisha sana kuhusu kuzaliwa kwa Yohana na kisha badala yake akaupata
ububu, vivyo hivyo kiongozi au mtu
yeyote Tanzania anayetaka kutoa
matamko ya kuhatarisha amani na uchaguzi mkuu mwaka huu, kuanzia wiki
hii kinywa chake kitiwe ububu kama kile kinywa cha Zakaria kwa Jina la Yesu. Amen. Wapo wanadamu pia wanaotamka
maneno mabaya juu ya maisha yako.
Wiki hii ni wiki ya kufunga midomo.
Ikiwa upo katikati yetu na hujamwamini Yesu, haya yote
tunayoenda kuyaomba siku hii kingyume na kafara za watawala hayatakusaidia.
Yesu akija kwako anakupa uzima tena wa milele.
=== © Information & Media Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa
Zacharia
(Glory of Christ
(Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545